DAR-ES-SALAAM : MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Utalii Ephraim Mafuru akitoa salaam za ukaribisho kwa wageni wa ndani na nje ya Nchi waliofika kwenye Hafla ya Tuzo za 32 za Utalii Duniani kwa ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi zinazofanya usiku huu kwenye hotel ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.
DAR ES SALAAM: Jopo la watalii kutoka Al Wakra Qatar Academy ya nchini Qatar limewasili Tanzania kwa safari yao ya kitaaluma inayoambatana na kupanda Mlima Kilimanjaro. Ujumbe huo unajumuisha Mlezi wa Wanafunzi, Abdirahman Hussien Handule, wanafunzi sita, mwalimu mmoja na mzazi mmoja kama mwakilishi. “Safari hii ya ajabu ni sehemu ya dhamira pana ya chuo…
GHUBA ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma ni hifadhi ya bahari iliyoanzishwa Julai 2000 chini ya Sheria Namba 29 ya Hifadhi za Bahari ya Mwaka 1994 ikiwa na eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 650. Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Dk Redfred Ngowo anasema eneo la kilometa 420 kati ya hizo ni bahari…
ZANZIBAR; Mkutano wa hivi karibuni wa AviaDev Africa 2025, umekuwa mkutano wenye mafanikio makubwa katika sekta ya usafiri wa anga. Mkutano huo uliosimamiwa na Kampuni ya Showtime ya Zanzibar, ulileta pamoja zaidi ya washiriki 500, ikiwa ni pamoja na wawakilishi kutoka kampuni 36 za ndege na mamlaka za utalii kutoka nchi 46, wote wakitafuta kujenga…
DAR ES SA SALAAM; Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Tuzo za 32 za Kimataifa za Utalii kwa Ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Juni 28 mwaka huu. Akizungumza kuhusu tuzo hizo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru alisema hizo ndiyo tuzo kubwa zaidi za…
JUHUDI za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujenga sekta moja ya utalii itakayoifanya Kanda nzima kuwa kitovu cha utalii zimezaa matunda kutokana na maonesho ya Karibu-Kilifair 2025. Maonesho haya makubwa zaidi ya utalii Afrika Mashariki, yanaendelea sasa, yakileta pamoja wajasiriamali zaidi ya 500 kutoka nchi 15 na washiriki wa nje ya nchi zaidi ya 1,000.…
“GUGU Karoti ni tishio kwa uoto wa asili, malisho ya mifugo na maisha ya wanyamapori. Kwa msingi huo, ushirikiano wa jamii ni silaha kuu dhidi ya mmea huu vamizi.” Ofisa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Gregory Mtega anasema hayo wakati akitoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha…
TANZANIA imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi wakiwamo wanyamapori ambao wamekuwa sehemu ya vivutio vya utalii nchini na kuliingizia taifa mabilioni ya fedha za kigeni kutokana na watalii wa ndani na nje ya nchi. Wanyamapori hao wamekuwa wakipatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi hususani katika hifadhi za taifa, lakini pia katika mapori ya akiba na maeneo…
WASHIKADAU wa sekta ya utalii katika Kaunti ya Lamu, wamelalamika kuhusu bango linalotangaza kusakwa kwa mshukiwa sugu wa ugaidi, Abdullahi Banati, lililoezekwa Mokowe. Wadau hao walieleza hofu kuwa, bango hilo linawatia wasiwasi wageni wanaotaka kuzuru Lamu kwani wanaona ni kama hakuna usalama. Bango hilo lililoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na Kisomali, linawarai wananchi wenye taarifa zozote kumhusu Banati waarifu polisi ili akamatwe. Serikali ya Amerika ilikuwa imetenga zawadi ya Sh1.3 bilioni kwa yeyote atakayesaidia kumkamata mshukiwa huyo sugu wa ugaidi. Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Lamu (LTA), Bi Fridah Njeri, aliishinikiza serikali kupitia wizara husika kuliondoa bango hilo. Kulingana naye, sekta hiyo kwa sasa iko chini, ambapo inatimiza kati ya asilimia 35 hadi 40 pekee na hivyo basi hatua yoyote ya kutia hofu wageni inaleta hasara. “Nimepokea malalamishi kutoka kwa wamiliki wa hoteli, hasa maeneo ya Mokowe kwamba wageni karibu 50 waliokuwa wamepanga kukodisha vyumba pale, walikatiza mipango yao punde walipofika na kuona tangazo la gaidi huyo likiwa limetundikwa kwenye bango kubwa. Hatutaki wageni wetu kufikiria kuwa sisi tumemficha huyo gaidi au Lamu si salama. Ni vyema bango liondolewe kuiokoa sekta hii muhimu,” akasema Bi Njeri. Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii na Maendeleo kwenye manispaa ya Lamu, Bw Abdallah Fadhil, alisema hajafurahishwa na hatua hiyo. [caption id="attachment_173191" align="alignnone" width="2560"] Picha za bango la gaidi wa kimataifa anayetafutwa, Abdullahi Banati lililotundikwa eneo la Mokowe Jeti, Lamu. Bango hilo limewachukiza wadau wa utalii wakiwashinikiza wahusika kuliondoa wakidai linafurusha watalii.Picha|Kalume Kazungu[/caption] Alieleza kuwa, eneo hilo tayari limekuwa na matatizo ya muda mrefu kuhusiana na utovu wa usalama unaochangiwa na al-Shabaab ila utulivu umeshuhudiwa kwa muda mrefu sasa. “Ilitosha wao wamtangaze gaidi kwenye redio, magazeti, televisheni na hata mitandaoni. Kutuwekea bango hilo Lamu kunaleta uoga kwa wengi kama kwamba Lamu ina uhusiano na gaidi. Bango liondolewe mara moja,” akasema Bw Fadhil. Alieleza masikitiko yake kwamba tangu Januari mwaka huu, sekta ya utalii imekuwa ikifanya vibaya. “Hoteli na gesti nyingi zimekuwa zikipokea idadi ndogo ya wageni wanaokodi vyumba. Utapata wageni hawafiki hata asilimia 20 ilhali hoteli na gesti nyingine zikikosa kupata chochote. Lazima tuitunze hii sekta yetu ya utalii kwa kuhakikisha ni matangazo mazuri pekee yanapeperushwa. Hili la gaidi limeudhi wengi,” akasema Bw Fadhil. Wadau hao wameamua kutuma wajumbe kukutana na Waziri wa Usalama, Bw Kipchumba Murkomen na mwenzake wa Utalii, Bi Rebecca Miano, ili kujadiliana kuhusu hatima ya bango hilo. Hata hivyo, Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Wesley Koech, alisema hajafahamu kuwepo kwa bango hilo Mokowe.Bw Koech aliahidi kufuatilia ili ibainike ni nani aliyeweka bango hilo.
“Mikindani ni moja ya miji mikongwe inayopatikana katika pwani ya Afrika Mashariki, yenyewe tunaizungumzia hata kabla ya ujio wa wageni. “Hapa tunazungumzia miaka mingi iliyopita, wakati wa jamii za Kiafrika kabla ya ukoloni. Hapo, tunazungumzia chini ya miaka 200 kabla ya Kristo.” Ndivyo mazungumzo yanavyoanza baina ya HabariLEO na Meneja Mafunzo katika Hoteli ya Mafunzo…
WAFANYABIASHARA Homa Bay wanatarajia kuvuna pakubwa huku kaunti hiyo ikiwa mwenyeji wa Sherehe za Madaraka Dei mnamo Juni 1. Usimamizi wa hoteli kadhaa ulithibitisha kuwa utakuwa makao ya wageni mashuhuri na itakuwa vigumu kupata nafasi ya kuwasitiri watu wengine wa kawaida. Wikendi, baadhi ya hoteli zilikuwa zimejaa na waliokuwa wakitafuta nafasi waliambiwa wasake makao kwingine. Hoteli ya hadhi ya Cold Spring yenye uwezo wa kuwapa makao wageni 70 tayari imejaa kwa kuwa vyumba vyake vimelipiwa na vitatumika na wageni watakaohudhuria sherehe za Madaraka. Usimamizi wa Cold Spring uliambia Taifa Leo kwa wateja wao ni maafisa kutoka ubalozi mbalimbali. Meneja wa hoteli hiyo Dickson Osore alisema wageni wengi watawasili hotelini humo Mei 31 kisha kuondoka Juni 1. Kwa mujibu wa Bw Osore, chumba cha mwisho kililipiwa wiki iliyopita. “Wengine watakwepo hadi baada ya Juni 1. Lakini kwa sasa vyumba vyote 70 vimelipiwa,” akasema Bw Osore huku akisema wanalenga kutumia sherehe hizo kuvumisha hoteli yao. “Sherehe hizi zitakuwa silaha ya kuvumisha hoteli zetu Homa Bay na sekta ya utalii. Huwa tuna huduma bora na tunawaalika wageni wote hata baada ya sherehe za Madaraka,” akaongeza. Homa Bay pia itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Ugatuzi mnamo Agosti mwaka huu, lile la uchumi samawati na Maadhimsho ya Siku ya Chakula Duniani. Hoteli nyingine ambazo zimejaa Homa Bay ni Golden Ray, Twin Towers na Tausi.
KATIKA safari ya ndoa au mahusiano ya kudumu, wanawake mara nyingi hujifunza mbinu nyingi za kutunza nyumba, kulea watoto, au hata kufanya kazi kwa bidii. Lakini kuna kipengele kimoja muhimu kinachopuuzwa na wengi- sanaa yakupanga mume. Hili halihitaji ujanja au hadaa. Linahitaji hekima, heshima, na mapenzi ambayo hujenga uhusiano imara na wa kuridhisha pande zote mbili. “Kupanga mume kunamaanisha kumfahamu, kumthamini, na kumgusa kwa njia ambazo humfanya kuwa karibu nawe kimwili, kihisia, na kiakili,” asema mtaalamu wa mahusiano na mshauri wa wanandoa, Veriane Kiruki Ngono, asema, si haki tu ya ndoa, bali ni njia ya mawasiliano ya kina kati ya wanandoa. “Wakati mwingine, mwanamume huhitaji tu kuguswa ili apone kiakili. Kumpa mapenzi kwa hiari, kwa joto la upendo na bila masharti, kunamweka katika hali ya utulivu na furaha. Usisubiri aanzishe kila mara – unapoanza wewe, anakuheshimu zaidi,” aeleza. Hakuna mwanaume anayetaka kurudi nyumbani na kukaribishwa kwa lawama, kelele au mashambulizi ya maneno. Nyumba iwe hifadhi yake ya amani, mahali ambapo anahisi salama na anapenda kurudi. Mazungumzo ya busara, subira na hekima ni silaha kubwa ya mwanamke mwerevu. Kiruki asema kama vile wanawake hupenda kuulizwa walivyolala au jinsi siku yao ilivyokuwa, vivyo hivyo waume nao wanahitaji hilo. “Maswali madogo kama, “Ulikula vizuri?” au “Kazi iliendaje leo?” yanamaanisha mengi zaidi ya unavyodhani,” asema. Kulingana na wataalam, mwanaume mwenye mawazo huwa na wakati mgumu kupanga mambo yake. Msaada mdogo kama kumsaidia kupanga mavazi, kupanga ratiba yake au kumkumbusha ahadi fulani kunaweza kumwondolea mzigo mkubwa wa akili. “Unamjua kwa undani – changamoto zake, maamuzi yake magumu, na ndoto zake. Sala zako ni silaha ya nguvu. Mwombee kwa moyo, na mwambie unamwombea. Hili linamgusa hata kama hakuonyeshi mara moja,” asema mshauri wa masuala ya ndoa Kenn Kiambi. “Usimwache mumeo abebe mzigo wa kifedha peke yake. Kama unaweza kuchangia, fanya hivyo. Kama si kwa pesa, basi kwa kupunguza gharama zisizo za lazima, kusaidia kupanga bajeti, au kuwa mbunifu kwenye matumizi ya familia,” aeleza. Mwanaume pia hupitia vipindi anavyojiona kuwa hafai au kuchoka. “Katika kipindi kama hiki, mthibitishe kwa maneno yenye heshima na mapenzi: ‘Najivunia kuwa na wewe’, ‘Ninaamini unaweza’. Haya ni mafuta ya moyo wake,” asema Kiambi. Anasema uaminifu si wa kimwili tu – bali pia wa hisia. “Epuka siri zisizokuwa na maana, zungumza kwa uwazi na mume wako, na mpe amani ya moyo. Usaliti ni sumu inayovunja kabisa uaminifu na usalama wa moyo wa mwanaume,” aeleza. Mwanaume anapopata nafasi ya kuzungumza, asema Kiruki, huwa ni fursa ya dhahabu. Hivyo, usimkatize, usimchekelee, na usitumie udhaifu wake dhidi yake baadaye. Kuwa ngome yake ya usiri na faraja. “Na usipuuze nguvu ya tabasamu lako. Ni dawa ya uchovu wake, ni alama ya kukaribishwa nyumbani, na ni mwanga wa moyo wake. Tabasamu linaweza kubadilisha siku nzima kuwa nzuri,” ashauri. Busu si kwa wapenzi wapya tu. Katika ndoa, busu ni muhuri wa upendo unaoendelea. Mbusu asubuhi, kabla ya kulala, wakati wa shukrani – kila mara kuna nafasi ya kuonyesha upendo bila maneno. Mambo mapya huleta msisimko katika uhusiano. Tembeeni sehemu mpya, pikeni pamoja, angalieni sinema, chokozaneni, chekeni hadi mjilize. Hii huimarisha uhusiano na kuongeza ukaribu wenu. Kupanga mume, asema Kiambi, si sawa na kumbadilisha, bali ni kumwezesha kuwa bora zaidi kwa msaada wako. Ni kumpenda kwa vitendo, kwa hekima na kwa moyo wa kweli. Katika dunia yenye msukosuko, kuwa kimbilio lake .na atakuwa ngome yako.
DODOMA: The Ministry of Natural Resources and Tourism has outlined ten (10) strategies to address the challenges posed by dangerous and destructive wildlife for the fiscal year 2025/2026. One of the strategies by the ministry is the procurement of two (2) helicopters through conservation institutions TANAPA (Tanzania National Parks) and NCAA (Ngorongoro Conservation Area Authority).…
AKIWA Dodoma Mei 17, 2025 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana alitoa taarifa kuhusu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Nyuki Dunia. Akasema maadhimisho hayo ni sehemu ya uzingatiwaji wa Azimio la Bazara Kuu la Umoja wa Mataifa kutambua umuhimu na mchango wa nyuki katika maisha ya…
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Peter Ulanga amesema katika miaka mitano ijayo anaiona ATCL ikiwa sehemu ya ukuaji wa uchumi na mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii. Pia, Ulanga amesema katika muda huo anaiona ATCL itakuwa na uwezo wa kuunganisha bara la Afrika na Ulaya. Amesema hayo alipozungumza katika kipindi cha…
NINGEPENDA tutafakari kwa pamoja uwezekano wa kuwa na siku zijazo zilizo bora zaidi katika uhusiano kati ya Marekani na Tanzania ambapo tutakuwa tumejenga ustawi mkubwa kwa mataifa yetu yote mawili. Katika siku njema zijazo, safari za ndege za moja kwa moja zitaiunganisha Marekani na Tanzania, zikisafirisha mamia ya maelfu ya watalii wa Kimarekani kila mwaka…
LINDI; Lukwika Lumesule ni moja ya hifadhi za kipekee Tanzania lakini zisizotembelewa na watalii wengi. Naweza kusema ni hifadhi zisizo na umaarufu mkubwa kulinganisha na vivutio vya kipekee vilivyomo ndani yake. Hifadhi hiyo iliyojificha Kusini mwa Tanzania (Kusini Magharibi na Magharibi mwa Wilaya ya Masasi) katika Mkoa wa Lindi, kijiografia inapakana na Hifadhi ya Niassa…
SEKTA ya utalii inaonekana kufufuka baada ya kuandikisha ongezeko la kima cha asilimia 60 la watalii wanawasili nchini tangu 2022, kulingana na takwimu kutoka kwa Wizara ya Utalii. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa watalii 2.4 milioni walitembelea Kenya mnamo 2024, ikilinganishwa na watalii 1.5 milioni waliowasili 2022. Akizungumzia takwimu hizo kutoka kwa wizara yake, Waziri wa Utalii Rebecca Miano alisema ongezeko hilo la idadi ya watalii limewezesha mapato kutoka kwa sekta hiyo kupanda hadi Sh452 bilioni, kutoka Sh268 bilioni miaka miwili iliyopita. “Kwa muda mrefu watalii wamekuwa wakizuru fuo na mbuga za wanyama pekee licha ya uwepo wa vivutio vingine vya watalii kote nchini. Kwa mfano watalii wanaweza kuzuru maeneo ya kispoti, kitamaduni, kilimo na kiafya,” Bi Miano akasema. Alieleza kuwa ongezeko la idadi ya watalii wanaozuru nchini limechangia Sh509 bilioni kwa utajiri wa nchini, ambao ni asilimia 2.6 ya mchango wa sekta hiyo unaokadiriwa kuwa ya thamani ya Sh1 trilioni. Vile vile, data zinaonyesha kuwa idadi ya wanaoajiriwa imepanda katika sekta hiyo, huku ikikadiriwa kuzalisha nafasi 1.5 milioni 2024 kutoka nafasi 1.1 milioni mnamo 2022. Waziri Miano alisema katika juhudi za kupunguza utegemezi kwa watalii wanaozuru fuo na mbuga za wanyama, wizara yake imekuwa ikipanua maeneo mapya ya kuvutia watalii. Aidha, alitambua kwamba shughuli za michezo kama vile mashindano ya Magical Kenya Open, Kip Keino Classic na mbio za magari za Naivasha WRC Rally zimeondokea kuvutia idadi kubwa ya watalii. “Hafla za kitamaduni kama Tamasha ya Jamii za Maa na Tamasha ya Rusinga pia zinaendelea kuwa vituo kwa watalii,” Bi Miano akaeleza. Isitoshe, utalii wa makongamano umevutia katika miaka ya hivi karibuni ambapo Kenya ilikuwa mwenyeji wa mikutano, makongamano na maonyesha 643, 595 yaliyovutia idadi kubwa ya wageni kutoka mataifa ya kigeni mnamo 2024. Idadi hii inawakilisha ongezeko la asilimia 12.5 ikilinganishwa na mwaka wa 2022. Wizara ya Utalii pia imekuwa ikivumisha utalii wa humu nchini, hasa baada ya janga la Covid-19 lililoshuhudiwa kati ya miaka ya 2020 na 2021. Inafanya hivyo kupitia kampeni kama vile “Tembea Kenya” inayohusisha kupunguzwa kwa ada ya kuingia mbuga za wanyamapori na kupunguzwa kwa ada za usafiri kwa watu wa familia moja. Kampeni hizo zimechangia idadi ya watalii wa humu nchini wanaokodisha wanalala kwenye mikahawa kupanda hadi zaidi ya 5.1 milioni mnamo 2024.
DODOMA: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Nyuki Dunia yanayofanyika kuanzia leo uwanja wa Chinangali jijini Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana ametoa taarifa hiyo leo Mei 17, 2025 na kuongeza kuwa maadhimisho hayo ni uzingatiwaji wa Azimio la Bazara Kuu la Umoja wa…
MWAKA 2022 wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tanzania, The Royal Tour jijini Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan alisema, “Tangu kutengenezwa kwa fi lamu hii Sekta ya utalii imeanza kukua tena baada ya wadau wengi duniani kutuunga mkono.” “Ni ushauri wangu sasa na sisi kama taifa tuanze kujipanga kwa kufanya marekebisho mbalimbali ikiwa…
POLO aliyekuwa akimezea mate demu mmoja aliingia baridi mwanadada huyo alipomwambia wazi kuwa anapenda pesa sana. Jamaa alikuwa akirushia demu mistari ya mapenzi na siku moja binti akampa miadi wakutane katika hoteli moja. Walipokuwa wakipiga gumzo wakiendelea kuteremsha vinywaji, demu alisema yeye anapenda pesa sana na anaweza kufanya chochote kuzipata. “Siwezi kuacha pesa. Ninaweza kufanya chochote mradi tu nizipate kisha nishughulikie athari zinazofuata baada ya kuziweka mfukoni,” demu alisema. Jamaa alipomdadisi zaidi, demu alishikilia kuwa hawezi kuvumilia mwanamume bila pesa. “Hii ndiyo sababu siwezi kujifunga kwa mwanamume mmoja kwa kuwa akiishiwa lazima nitamtema niende kwa aliye nazo,” demu alisema na jamaa akaamua kuachana naye.
ARUSHA: MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais, Philip Mpango ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa mfuko huo katika kufanikisha Mkutano Mkuu wa 12 wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi (TAPSEA) uliofanyika Arusha. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Utawala PSSSF, Fatma Chondo…
MKUTANO wa Tatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na sekta ya umma na binafsi katika utalii unaendelea jijini Arusha ukiwa na lengo la kujadili maendeleo ya sekta ya utalii nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utalii. Mkutano huo pia ni mwendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu…
DODOMA: Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya utalii ili ichangie kikamilifu uchumi na maendeleo ya taifa. Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa wizara hiyo kuhusu majadiliano baina ya sekta ya umma na binafsi katika utalii uliofanyika leo…
NGORONGORO: THE Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism, Commissioner of Police Benedict Wakulyamba, has praised the visit of delegates from the 14th Lusaka Governing Council to the Ngorongoro Crater Conservation Area, describing it as a great success. He noted that the delegates had the rare opportunity to see Africa’s “Big…
Pori hilo ambalo ni Urithi wa Utamaduni wa Dunia, liko chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Kanda ya Kusini Mashariki. Katika mazungumzo na HabariLEO Ikwiriri wilayani Rufiji, Ofisa Utalii Hifadhi ya Wanyamapori Selous, Stephano Lukumay anasema, “Ingawa hili ni Pori la Akiba la Selous, sisi tunapenda kuliita Hifadhi ya Wanyamapori…
“HIFADHI ya Ngorongoro ni eneo la kipekee duniani lenye hadhi tatu zinazotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).” Inasema taarifa ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA, Dk Elirehema Doriye kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na…
WAKAZI wa kisiwa cha Lamu wamefurahishwa na hatua ya serikali ya kaunti ya Lamu ya kuwajengea vibaraza vinavyobembea kimpango ndani ya Bahari Hindi. Vibaraza hivyo vimejengwa kwa kutundikwa kwenye ngome ya kukinga maji ya Bahari Hindi kufikia makazi ya binadamu na biashara, hasa mbele ya mji wa kale wa Lamu. Kimtazamo, vibaraza hivyo viko ndani ya Bahari Hindi, japo vinabembea kwa juu, hivyo kuwapa wageni, watalii na wenyeji furaha na utamu wa aina yake wanapobarizi. Wenyeji, wageni na watalii waliozungumza na Taifa Leo kisiwani Lamu hawakuficha furaha yao kufuatia ujenzi wa vibaraza hivyo. Bi Halima Omar, mkazi wa mtaa wa Mkomani, anasema kila anapozidiwa na joto nyumbani, yeye huteremka na kujibanza kwenye mojawapo ya vibaraza hivyo ili kupata hewa safi kutoka baharini. “Tangu vijengwe, hivi vibaraza vimetuwezesha kupata upepo mwanana wa moja kwa moja kutoka baharini. Yaani tunapokaa vibarazani tunajihisi kana kwamba tuko ndani ya mashua au boti katikati ya Bahari Hindi tukipunga hewa. Twashukuru kaunti kuibuka na mpango huu,” akasema Bi Omar. Bw Jeremiah Oluoch, mtalii wa ndani kwa ndani kutoka Nyanza, anasema tangu alipozuru mji wa kale wa Lamu wiki moja iliyopita amekuwa mpenzi wa kubarizi kwenye vibaraza hivyo. [caption id="attachment_171465" align="alignnone" width="2560"] Vibaraza vilivyojengwa na serikali ya Kaunti ya Lamu kuwapa wenyeji, wageni na watalii nafasi ya kubarizi kupunga hewa ndani ya bahari mjini Lamu. Picha|Kalume Kazungu[/caption] Anasema punde anapokaa vibarazani yeye huitalii bahari na mji wa kale wa Lamu kiurahisi. “Kaunti ilifikiria sana kabla ya kuja na mradi kuu wa vibaraza. Kama mgeni wa eneo hili, nimefurahia si haba. Nikikaa kwenye vibaraza hupata fursa nzuri ya kutalii mandhari ya Bahari Hindi na pia mji wenyewe wa kale. Waongeze hivi vibaraza kwani ni vichache mno,” akasema Bw Oluoch. Baadhi ya wenyeji, watalii na wageni pia wameshuhudiwa wakiweka meza, viti au hata kutandika mikeka kwenye vibaraza hivyo, hasa nyakati za magharibi ilmuradi wajivinjari pale. [caption id="attachment_171466" align="alignnone" width="2560"] Vibaraza vilivyojengwa na serikali ya Kaunti ya Lamu kuwapa wenyeji, wageni na watalii nafasi ya kubarizi kupunga hewa ndani ya bahari mjini Lamu. Picha|Kalume Kazungu[/caption] Bw Omar Bunu anasema vibaraza hivyo vimekuwa msaada, hasa kwao kama wazee wa Lamu kwani mara nyingi wamekuwa wakikusanyika hapo na kujadiliana masuala muhimu ya kuuendeleza mji wao. “Utatupata sisi wazee tukipiga gumzo kwenye vibaraza hivyo, si kupitisha muda tu bali kugusia masuala muhimu ya kuuendesha mji wetu wa kale. Vibaraza hivi vimetupa nafasi nzuri ya kupumzika, kukutanika, kutangamana na kutagusana na wengine. Ni fahari yetu,” akasema Bw Bunu. Mji wa kale wa Lamu ni kivutio kikuu cha watalii wanaozuru kaunti hiyo kila mwaka. Mnamo 2001, Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliuorodhesha mji huo kuwa miongoni mwa maeneo yanayotambuliwa zaidi ulimwenguni kwa kuhifadhi ukale wake, yaani Unesco World Heritage Site.
MTWAPA MJINI JOMBI wa hapa alilazimika kujipikia asilale njaa mkewe alipomhadaa alikuwa amechelewa kazini ilhali alikuwa amelalia kifua cha mpango wake wa kando katika hoteli moja Mombasa. Jamaa alikuwa akisubiri mkewe afike aandae chajio alipopata arafa kutoka kwa demu akimjulisha kwamba, alikuwa amechelewa kazini. Demu alisema alipokuwa akimtumia jamaa arafa hiyo alikuwa amelala katika kifua cha dume wakijiandaa kurushana roho. “Alikuwa mpango wangu wa kando wa kwanza na alinipandisha mizuka nikalazimika kumhadaa mume wangu. Nilifika nyumbani saa sita usiku na nikapata amepika na kula,” demu alifunguka katika ukurasa mmoja wa mtandao wa kijamii ambao akina dada huzungumzia uzoefu wa maisha ya ndoa. *** Nilikutema kwa kulaza damu, demu aambia ex KIRIBWET, TRANSMARA Kipusa wa hapa alijuta kuitikia ombi la mpenzi wake wa awali la kumtaka amwambie ukweli kuhusu sababu ya kumtema. Duru zinaarifu wawili hao walishiriki uhusiano wa kimahaba kwa muda mrefu kabla ya kipusa kumtaka jamaa ajaribu bahati kwingine. Kipusa hakumfichulia polo sababu ya kumrusha nje lakini jamaa hakukoma kumlilia amwambie alivyokosa. Ndiposa hatimaye kipusa alimchoma jombi kwa ukweli kuwa yeye ni goigoi kwenye tendo la ndoa. NA KIPNGENO CHERUIYOT
Tragedy struck weekend during what was meant to be a joyous occasion, as a Lagos hotelier, Otunba Kunle Akinyele, suddenly slumped and died during his wife’s 60th birthday thanksgiving service. The thanksgiving ceremony, held in honour of Deaconess Catherine Adejoke Akinyele, it was gathered, took place at Christ Apostolic Church, Oke-Iyanu, Odemuyiwa District Headquarters, in […]
MIILI ya vijana wawili kati ya watatu walioripotiwa kutoweka baharini eneo la Shella, Kaunti ya Lamu, ilipatikana Jumatatu ikielea karibu na ufuo huo huo wa Shella. Akithibitisha taarifa hizo, Meneja wa Kituo cha Kukabiliana na Majanga ya Dharura Lamu (EOC), Iftakhar Majid, alisema miili hiyo ilipatikana kufuatia operesheni inayoendelea ya kuwasaka waliotoweka wakati wakiogelea baharini ufuoni Shella mnamo Jumapili jioni. Bw Majid alisema kwa sasa operesheni bado inaendelea ili kuusaka mwili wa tatu. Vijana hao walikuwa miongoni mwa kundi la wana-rika 30 waliokuwa wamezuru Lamu kutoka eneo la Hongwe, tarafa ya Mpeketoni kwa shughuli za kikanisa. Baada ya kukamilisha shughuli zao za kanisa mapema Jumapili, waliandamana hadi ufuo wa Shella ili kujivinjari kwa kuogelea. Hali ilibadilika ghafla pale watatu waliokuwa miongoni mwa makumi ya walioogelea waliposhindwa nguvu, hivyo kutoweka baharini. “EOC ilipokea simu kutoka kwa msamaria mwema aliyetufahamisha kilichokuwa kikiendelea Shella. Ilikuwa majira ya saa 12 unusu hivi jioni ya Jumapili. Tulifika eneo husika na kuanzisha msako mara moja lakini tulikatiza operesheni katikati baada ya giza kusheheni kwani usiku ulikuwa umewadia,” akasema Bw Majid. Operesheni ya kusaka miili ya watatu hao hata hivyo ilirejelewa Jumatatu asubuhi, hivyo kupelekea kuopolewa kwa miwili ambayo ni ya mwanaume na mwanamke. Operesheni inaendelezwa na maafisa wa kituo cha EOC Lamu kwa ushirikiano na Kenya Coast Guard Service (KCGS), Shirika la Msalaba Mwekundu nchini na wapiga mbizi wa kujitolea. “Kwa sasa operesheni bado inaendelea kuusaka mwili wa tatu na wa mwisho. Ningeshauri watalii, wageni na wenyeji kuwa makini wanapoogelea kwenye fuo zetu. Baadhi ya fukwe, ikiwemo Shella, ni hatari kwa usalama wao kwani zimesheheni vidimbwi vya kina kirefu,” akasema Bw Majid. Pia aliwataka wavuvi na mabaharia wengine kuwa makini na kutii maonyo ya kila mara yanayotolewa na ofisi yake na ile ya Idara ya Hali ya hewa kuhusiana na hali ilivyo baharini. Si mara ya kwanza watu kufa maji wakati wakiogelea kwenye ufukwe wa Shella, Lamu. Julai 2018, mwanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo na Kiufundi (TVET) ya Lamu, Juma Mohamed, alikufa maji wakati akiogelea Shella. Novemba 2018, kijana wa miaka 25 kwa jina Joseph Kitsao, pia alikufa maji akiogelea kwenye ufukwe wa Shella. Wenzake wawili waliokolewa na wapiga mbizi wa kujitolea waliokuwa karibu wakati wa tukio. Mbali na Shella, sehemu zingine zinazotambuliwa kuwa hatari kwa kuogelea na hata kuvuka ukisafiri kwenye Bahari Hindi, Kaunti ya Lamu ni vivuko vya Mkanda, Manda Bruno, Mlango wa Kipungani, vyote vikipatikana Lamu Magharibi. Vingine ni Mlango wa Tanu huko Mkokoni, Mlango wa Ali upatikanao Kiwayu na Mlango wa Bomani ulioko Kiunga, vyote vikiwa Lamu Mashariki.
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Tuzo za Kimataifa za Utaili zijulikanazo kama World Travel Awards katika hafla ya kutangaza washindi wa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi. Hafla hiyo ya kutangaza washindi wa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi ‘Africa & Indian Ocean Gala Ceremony’ itafanyika […]
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Benki ya CRDB imetangaza washindi sita wa kampeni ya ‘Tembo Card Shwaa’ ambao watasafiri kwenda kutalii katika mbuga ya Serengeti mkoani Mara. Washindi hao ambao watasafiri wakiwa na wenza wao wamepatikana kupitia droo iliyochezwa Aprili 3,2025 ikiwa ni awamu ya kwanza ya Kampeni ya ‘Tembo Card Shwaa’. Meneja Mwandamizi Kitengo […]
Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kung’ara katika ulingo wa mawasiliano na uhusiano wa umma baada ya kushinda Tuzo ya Ubora ya Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania (PRST) kwa mwaka 2024 kupitia kampeni yake bunifu ya “Merry & Wild: Ngorongoro Awaits.” Kampeni hiyo, iliyolenga kuhamasisha utalii wa ndani wakati wa msimu […]
DAKTARI na mtaalamu wa afya Dkt Myro Figura ametahadharisha dhidi ya kupiga busu wanaume wenye ndevu, akisema hatua hiyo inaweza kukusababishia maambukizi na mwasho kwa ngozi. Kutokana na hilo amewataka wanaume au wanawake wanaobusu wanaume wenye ndevu wajihadhari kwa sababu hiyo ni njia moja ya kujiletea maradhi. “Kupiga busu mwanamume mwenye ndevu kunaweza kukusababishia maradhi. Iwapo ndevu zenyewe si safi huwa ni hifadhi ya bakteria, na wakati wa kupiga busu vijidudu hivyo hatari vikitagusana na ngozi basi huleta upele wa malengelenge (impetigo kwa Kimombo),” asema Dkt Figura. Impetigo ni ugonjwa ambao unasambaa kwa urahisi. Huanza kwa ngozi kuwa na uvimbe kisha kutoa uchafu mwekundu. Mara nyingi uchafu huo ambao ni majimaji si rahisi kutambuliwa kwa watu wenye ngozi nyeusi au rangi kahawia. “Uvimbe ukipasuka huacha vidonda vidogo na husambaa sehemu mbalimbali za mwili. Kibaya zaidi ni kuwa aliyeathirika hujikuna sana na kuhisi uchungu kutokana na mwasho,” aongeza mtaalamu huyo katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la habari la Daily Mail nchini Uingereza. Tiba ya maambukizi haya ya bakteria ni kupaka mafuta yenye kemikali ya hydrogen peroxide ama kumeza tembe za kukabiliana na bakteria mwilini. Ushauri wa daktari utafaa kumaliza bakteria hizi, ila cha mno ni kwa wanaume kuhakikisha kuwa ndevu zao ni safi na pia nywele zilizo sehemu zingine za uso zinaoshwa. Kufutia utafiti huo wa Dkt Figura na video aliyochapisha mitandaoni, wanawake wengi walimuunga mkono na hata kudakia suala hilo kama kisababu cha wao kuepuka wanaume wenye kidevu. Wengine walishangaa kwamba wanaume huwaoshi ndevu zao mara kwa mara, huku wale ambao midume yao ina kidevu wakiapa kuwafuatilia ili kuhakikisha wanaosha nywele hizo kisawasawa.
SEKTA ya utalii inatazamiwa kukua mwaka huu na kuletea nchi zaidi ya Sh560 bilioni kufuatia kuwasili kwa maelfu ya wageni kupitia meli na ndege licha ya wasiwasi kuhusu usalama. Waziri wa Utalii, Rebecca Miano, alihakikishia watalii wanaotembelea Kenya kuhusu usalama wao, huku Amerika ikitoa onyo kwa raia wanaozuru Kenya kuepuka baadhi ya sehemu. Waziri Miano anasema serikali imeweka mikakati kuhakikisha usalama wa wageni katika mpango wake wa mwaka wa kuvutia angalau wageni milioni 3. “Tunataka kuwahakikishia wageni wetu kwamba wanaweza kutembea kwa uhuru, wajihisi salama, na mikakati ya kutosha imewekwa ili kuhakikisha usalama wao,” alisema Waziri Miano. Jumanne wiki jana, Amerik ilitangaza baadhi ya maeneo ya pwani na kaskazini mwa Kenya kuwa hatari na kuonya raia wake kutoyatembelea. Hata hivyo, Miano alisema serikali imeweka mipango kuhakikisha usalama wa watalii Pwani, ambayo inachangia takriban asilimia 50 ya mapato ya sekta ya utalii. Alisema kwamba inakadiriwa watalii wa kimataifa mwaka huu watakuwa 3 milioni na idadi inatarajiwa kuongezeka hadi 5 milioni katika miaka miwili ijayo. Mwaka 2024, sekta ya utalii ya Kenya iliimarika kwa kasi, huku mapato ya utalii yakiongezeka kwa asilimia 19.79 hadi Sh452.20 bilioni. Mapato kutoka watalii wa kigeni yaliongezeka kutoka Sh377.49 bilioni mwaka 2023, hadi Sh452.20 bilioni mwaka 2024. Kenya ilikaribisha watalii 2.4 milioni wa kimataifa mwaka 2024, ongezeko la asilimia 15 kutoka milioni 2.09 mwaka 2023. Ukuaji huu unahusishwa na juhudi za masoko ya kimkakati, utoaji wa bidhaa mbalimbali za utalii, na kuanzishwa kwa safari mpya za ndege. Serikali inajikita katika kuboresha majukwaa ya kidijitali na kuboresha uzoefu wa wageni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
By Ozioruva Aliu BENIN CITY – THE Business and Hotelier Stakeholders’ Forum (BHSF) in Edo State has expressed reservations over the recent increase and implementation of the consumer tax, describing it as a “devastating blow” to businesses already struggling to stay afloat. In a press release, the group’s Chairman and Secretary Chief Dr. Omogiade Edokpolo, […]