Na Malima Lubasha, Serengeti Kampuni ya Kitalii Nomad Tanzania inayofanya shughuli katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara, imetoa msaada wa Baiskeli 10 zenye thamani ya Sh 2 .0 milioni kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha kwanza wanaotoka kijiji cha Mbirikiri na kusoma Shule ya Sekondari Sedeco kutokana na umbali ulipo ili kuepuka […]
KAUNTI ya Narok ilishindwa kueleza jinsi ilivyotumia Sh8 milioni kuweka alama kwenye masikio ya vifaru 20 weusi katika Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara. Uongozi wa Gavana Patrick Ntutu pia haukuweza kueleza kiasi cha pesa kilichotumika kununua mafuta yaliyotumiwa wakati wa zoezi hilo. Zaidi ya hayo, fomu za uwasilishaji, fomu za toleo la kaunta (S11) na fomu za stakabadhi za kaunta (S13) hazikutolewa ili kuthibitisha matumizi ya Sh901, 000 zaidi kwa ununuzi wa dawa, kulipa mawakala, kununua vifaa vya kuchezea na vifaa vya matibabu. Afisa wa kaunti hiyo pia anamulikwa kwa matumizi ya Sh2, 172, 800 na Sh1, 568, 000 zilizolipwa kwa wafanyikazi wa Idara ya Utalii na Huduma ya Wanyamapori Kenya mtawalia, ambayo haikuwa kwenye Mkataba wa Maelewano na Idara na Huduma. Zaidi ya hayo, kampuni iliyokodishwa kwa utoaji wa huduma za helikopta haikuwa katika orodha ya watoa huduma waliosajiliwa kwa Mtendaji wa Kaunti kwa mwaka unaoangaziwa. "Katika hali hiyo, usahihi na ukamilifu wa kiasi cha matumizi cha Sh8, 141, 800 haukuweza kuthibitishwa," inafichua ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu ya mwaka unaoishia Juni 30, 2014. Katika Kaunti ya Kilifi, huenda Sh44 milioni zilizotumika katika ununuzi wa chakula cha msaada kwa wakimbizi katika kaunti hiyo zimepotea. Kulingana na ripoti hiyo Sh44, 639, 728 zilitumika kulipia msaada wa dharura na usaidizi wa wakimbizi yaliyotolewa kwa kampuni nne kwa ajili ya usambazaji na utoaji wa chakula cha msaada. Hata hivyo, haijulikani ikiwa vifaa husika vilifika kwa walengwa. Katika mwaka unaoangaziwa, jumla ya Sh250, 000, 000 zilitumwa kwa hazina ya dharura, huku kaunti chini ya Gavana Gideon Mung’aro ikiashiria kuwa ilitumia duka kuu kupokea na kusambaza chakula kilichonunuliwa. Hata hivyo, ripoti zilizothibitisha kiasi kilichopokelewa na kutolewa hazikutolewa. Zaidi ya hayo, maelezo ya magari yaliyotumika kusambaza vifaa hivyo hayakutolewa. Kaunti ya Tana River, pia inamulikwa kwa malipo yasiyo ya kawaida ya usafiri wa kigeni na marupurupu ya Sh6 milioni. Kaunti hiyo ililipia gharama za usafiri kutoka nje ya nchi ya Sh26, 503, 679 ambapo Sh6, 395, 500 zilitumika kama wafanyakazi walipokuwa wakihudhuria Jumuiya Trade Investment and Education Exchange Mission nchini Amerika. Kaunti hiyo pia inachunguzwa kuhusu uwezekano wa hasara ya Sh170, 895, 999 iliyotokana na gharama za bima. Kiasi hicho kinajumuisha bima ya matibabu ya wafanyakazi ya Sh149, 999, 999 iliyolipwa mapema bila utaratibu.
Na Mwandishi Wetu, KAMATI Tendaji ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) imeeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri za Wilaya ya Mbarali na Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya. Hayo yamebainishwa leo Jumapili (Machi 16, 2025) Mkoani Mbeya wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati hiyo […]
Na Mwandishi Wetu, KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) ulioanza mwaka 2021-2025 katika Mikoa mitano na Halmashauri za Wilaya saba nchini. Aidha amesema mwitikio chanya wa wananchi […]
Na Mwandishi wetu Tanzania inashiriki katika msafara wa kunadi vivutio vya utalii katika nchi za Ulaya Magharibi ulioanza tarehe 10- 15 machi 2025 ambapo wauzaji na wanunuzi katika sekta ya utalii wanakutana katika msafara huo wenye mawakala zaidi ya 50. Msafara huo unaojulikana kwa jina la “My Tanzania Roadshow 2025 ” na kuratibiwa na kampuni […]
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inatarajia kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato iliyojiwekea kwa mwaka wa fedha 2024/25 la kukusanya shilingi bilioni 230 kwani hadi kufikia Februari 2025, tayari imeshakusanya asilimia 92 ya mapato hayo. Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka hiyo, Dkt. Elirehema Doriye amesema hayo leo […]
Na Hamis Dambaya, Dodoma Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye amesema kuwa mamlaka hiyo imefikia malengo ya ongezeko la watalii na ukusanyaji wa mapato kwa miaka minne mfululizo kutokana na mchango mkubwa wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu […]
Na Mwandishi Wetu Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, wanawake zaidi ya 400 kutoka taasisi za serikali na sekta binafsi wemetembelea hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama wakubwa watano maarufu kama “Big Five”. Akizungumza na wanawake hao baada ya kuwapokea leo tarehe 7 machi, 2025 Kamishina Msaidizi Mwandamizi […]
*Wahamasisha utalii wa ndani Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, wahifadhi wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapaori Tanzania (TAWA) wametembelea Pori la Akiba Wamimbiki lililopo katika Mikoa ya Morogoro na Pwani kwa lengo la kuhamamisha utalii wa ndani. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, iliyofanyika Machi 1, 2025, […]
Marekani na Ukraine zimefikia makubaliano ya kuruhusu upatikanaji wa madini na maliasili nyinginezo za nchi hiyo ya Ulaya, Rais wa Marekani Donald Trump amesema. Akizungumza katika Ikulu ya White House siku ya Jumanne, Trump alithibitisha ripoti za awali kwamba alifikia makubaliano na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuendeleza maliasili ya nchi yake. “Nasikia anakuja Ijumaa. […] The post Trump adai kuwa Zelenskyy yupo mbioni kusaini makubaliano adimu ya rasilimali first appeared on Millard Ayo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema ujio wa Watafiti wa Mimea Vamizi kutoka nchini Cuba waliokuja nchini watasaidia katika kukabili Mimea Vamizi katika Hifadhi ya Taifa Saanane pamoja na Ziwa Viktoria ambayo yamekuwa changamoto katika Shughuli za usafirishaji, Uvuvi na Utalii. Mhe. Mtanda amebainisha hayo Februari 24, 2025 mara baada ya kuipokea […] The post RC Mtanda awapokea watafiti wa mimea vamizi first appeared on Millard Ayo.
RAIS William Ruto ameeleza sababu ya kuchelewa kuhudhuria ibada kuu ya Jumapili katika kanisa la Askofu Wilfred Lai la Jesus Celebration Centre (JCC) mjini Mombasa. Kwa mujibu wa Rais Ruto, alichelewa kutokana na ujumbe Askofu huyo aliokawia kujibu ujumbe mfupi wa WhatsApp aliomtumia usiku wa Jumamosi, na pamoja na majukumu ya asubuhi katika bandari ya Mombasa. "Usiku wa Jumamosi kabla ya kulala, nilimtumia Askofu Lai ujumbe wa WhatsApp nikimfahamisha kuhusu nia yangu ya kuhudhuria ibada ya Jumapili asubuhi. Nilikuwa nimepanga kuhudhuria hafla ya utalii asubuhi hiyo, lakini nikasema sitaenda, bali nitaipa kanisa kipaumbele," alieleza. "Nilihisi moyoni mwangu hitaji la kuja kumsikiliza mtumishi huyu wa Mungu. Hata hivyo, Askofu Lai alijibu ujumbe wangu saa tano asubuhi, wakati ambapo tayari nilikuwa nimehudhuria hafla ya utalii. Ingawa nilichelewa, nilisisitiza kwamba kwa vyovyote vile, lazima nifike JCC. Nilipowasili saa tano asubuhi, aliniarifu kuwa ibada kuu ilikuwa imeisha lakini akasema kuwa kuna ibada ya kifamilia kuanzia saa tisa na nusu mchana," aliongeza. Rais Ruto alisisitiza kuwa alikuwa amedhamiria kuhudhuria ibada hiyo licha ya kufika akiwa amechelewa. "Niliamua moyoni mwangu kwamba lazima nifike JCC na kusikiliza mahubiri. Nilimweleza Askofu kuwa ningeenda kumaliza majukumu yangu kisha nirudi baadaye jioni. Namshukuru Mungu kuwa niliweza kuhudhuria ibada hii. Imekuwa muda mrefu tangu nilipokuja hapa kumsikiliza Askofu Lai," alisema. Kiongozi huyo wa taifa alimshukuru Askofu Lai kwa kuhubiri kwa hekima na kusema ukweli kuhusu hali ya taifa na uongozi wake, huku akiwaomba waumini waendelee kuombea nchi. "Askofu ameongea kwa hekima na ukweli kuhusu taifa letu na uongozi wake. Nimefurahi na kubarikiwa sana. Kama ulivyosema, Askofu, Mungu anaponya taifa na uchumi wetu. Nitakuwa Pwani kwa wiki moja nikisimamia miradi ya maendeleo katika eneo hili. Namshukuru Mungu kwa fursa ya kuwa hapa leo," alisema. Rais Ruto, anayejulikana kuhudhuria ibada za kanisa kila Jumapili asubuhi alikosa kuhudhuria ibada kuu Februari, 23. Kama si kwa ibada ya kifamilia inayofanyika kuanzia saa tisa nchana katika JCC, Rais angekosa kabisa kuhudhuria ibada Jumapili hiyo. Rais alipowasili kanisani siku hiyo asubuhi, alikuta ibada kuu ikiwa imeisha na kulazimika kuondoka kwa muda, lakini baadaye alirejea jioni kueleza sababu ya kuchelewa kwake. Alimshukuru Askofu Lai na kueleza imani yake kuwa kila kitu kitafanyika kulingana na mpango wa Mungu. Alisisitiza kuwa ziara yake Pwani imelenga kuzindua miradi ya maendeleo ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo. "Ninakubaliana nawe, Askofu, kwamba kile ambacho Mungu amepanga hakuna mwanadamu anayeweza kupangua. Hivyo basi, nawaomba muendelee kutuombea," alisema, akishangiliwa na waumini. Rais Ruto, ambaye ameimarisha sifa yake kama 'Mkristo mwaminifu' na kawaida huanza Jumapili zake kwa ibada, alikuwa na asubuhi yenye shughuli nyingi, jambo lililosababisha tukio hilo nadra. Siku yake ilianza katika Bandari ya Mombasa, ambako aliukaribisha rasmi meli ya kifahari ya MS Norwegian Dawn, iliyokuwa na watalii zaidi ya 2,200. Rais alitumia muda wake kuwapokea wageni hao, akisisitiza dhamira ya Kenya ya kupanua sekta ya utalii na kuimarisha sifa yake kama kivutio bora cha watalii. Alieleza kuwa serikali yake itawekeza katika miundomsingi, kutekeleza mikakati madhubuti ya masoko, na kuboresha huduma za utalii ili kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea nchi. Katika hafla hiyo, Rais aliandamana na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, Waziri wa Utalii Rebecca Miano, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (KPA), Kapteni William Ruto, miongoni mwa viongozi wengine. Meli hiyo yenye urefu wa mita 294, inayoongozwa na nahodha Maxim Kyselov, ni miongoni mwa meli ndefu zaidi zilizotia nanga katika bandari ya Mombasa mwaka huu. Baada ya shughuli hiyo bandarini, Rais alielekea JCC, lakini kuchelewa kwake kulishangaza wengi, kwani anajulikana kurauka katika ibada za kanisa. Licha ya kukosa ibada kuu, Rais alitumia muda kuzungumza na baadhi ya waumini waliokuwa bado kanisani baada ya ibada. Pia alipata nafasi ya kuzungumza kwa kifupi na Askofu Lai kabla ya kuendelea na ratiba yake ya siku. Baadaye jioni, alirejea kanisani kumaliza Jumapili yake kwa ibada. Rais Ruto yuko Pwani kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi wa Shule ya Upili ya Kiwegu na mradi wa kuunganisha umeme katika shule hiyo huko Lunga Lunga, Kaunti ya Kwale. Pia, anatarijiwa kuzindua mradi wa kuboresha Kituo cha Afya cha Mkongani hadi hadhi ya hospitali ya Kaunti Ndogo, Kuzindua chumba cha upasuaji na wodi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkongani, Matuga. Rais Ruto pia anatarajiwa kugawa hati miliki za ardhi na kuweka jiwe la msingi kwa mradi wa nyumba za bei nafuu katika eneo la Whitehouse, Ukunda.
Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, imeteketeza ekari 336 za mashamba ya bangi yaliyokuwa ndani ya hifadhi ya Ikome Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma yakiwa yamechanganywa na mazao mengine halali ili kuficha shughuli hiyo haramu. Akizungumza wilayani Kondoa wakati wa […]
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha, amewataka wakazi wa Amboni kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira, akisisitiza umuhimu wa kutunza hifadhi ya Amboni ili iendelee kuwa kivutio chenye hadhi kwa maendeleo endelevu. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Diko la Amboni iliyoandaliwa na Hifadhi ya Ngorongoro, Kubecha alisisitiza kuwa juhudi za kulinda mazingira […] The post DC Tanga awataka wananchi kujiepusha na vitendo vinavyochochea uharibifu wa mazingira first appeared on Millard Ayo.
WASHUKIWA wanne, akiwemo raia wa Amerika na raia wa Pakistani, wameshtakiwa kwa makosa ya kuwapatia Wakenya watano shahada ghushi zikiwemo za uzamivu baada ya mafunzo ya siku tatu pekee katika Hoteli ya White sands. Miongoni mwa shahada ghushi zilizotolewa ni Shahada tatu za Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (Uongozi na Usimamizi) na Shahada mbili za Uzamivu (PhD) katika Uongozi. Washukiwa hao, waliotambuliwa kama Dayis Lawrence Bennett (raia wa Amerika), Farah Akbar (raia wa Pakistani), Ekra Wambui Ndung'u, na Josephine Ndune, walikamatwa na maafisa wa polisi wa kituo cha Bamburi waliovamia hoteli hiyo baada ya kupokea taarifa ya kijasusi. Wanne hao walifikishwa mbele ya Mahakama ya Shanzu Alhamisi na kushtakiwa kwa makosa matano ya uhalifu, ikiwemo kutoa shahada kinyume na Kifungu cha 28(2) na (3), kama kinavyosomwa pamoja na Kifungu cha 28(5) cha Sheria ya Vyuo Vikuu. Kwa mujibu wa karatasi ya mashtaka, washukiwa hao, pamoja na wengine ambao hawakufikishwa mahakamani, walijiwasilisha kama mawakala wa taasisi ya kigeni na kwa njia isiyo halali wakatoa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Uongozi kwa Purity Kimotho Wakuhu na Issack Alio Hassan bila idhini kutoka kwa Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE). Katika mashtaka mengine, walidaiwa kutoa kwa njia isiyo halali Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara katika Uongozi kwa Evely Mila, Sepiso E.L. Nalumango, na Ahmed Noor Hassan bila idhini inayohitajika. Mahakama iliambiwa kuwa, makosa hayo yalifanyika Februari 12, katika Hoteli ya Whitesands, Bamburi. Hata hivyo, washukiwa walikana mashtaka yote walipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Shanzu, Leah Juma.Bennett na Akbar waliomba kupewa dhamana wakidai walikuwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji uangalizi wa mara kwa mara. Kupitia kwa wakili wao, walihakikishia mahakama kuwa hawana nia ya kutoroka na kuwa wako tayari kufuata masharti yote ya mahakama.Kesi hiyo itatajwa tena Februari 18.
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar na Chama cha waongoza watalii Zanzibar (ZATO) Februari 6, 2025 walifanya ziara maalumu (Fam – Trip) katika Hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia Magofu ya Kale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kupanua wigo wa soko la […]
The Zone 2 Police Command in Lagos State on Wednesday paraded a hotelier, simply identified as Macdonald, following his detention over allegations of having unlawful carnal knowledge of a male minor. The Zonal Public Relations Officer (ZPRO), CSP Umma Ayuba, paraded the suspect before newsmen at the Command Headquarters, Onikan, Lagos. Ayuba said that the […]
“Procurement procedures are being made via the Dubai based company NAFFCO FZCO and immediately after they arrive in the country, the motor vehicles will be distributed countrywide including Ngorongoro District".
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Steve Mengele maarufu Steve Nyerere, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mafanikio makubwa ya sekta ya utalii, ikiwemo kufikisha watalii milioni 5.3 na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa. Steve ametoa pongezi hizo Januari […]
The AIG said the hotelier was detained after a 16-year-old secondary school student confessed to his mother that he met the suspect at his hotel located at Bucknor in the Isheri Oshun area of the state.
WADAU wa sekta ya utalii katika Kaunti ya Kwale wameanza kutayarisha Mswada wa Usimamizi wa Fuo za Kwale ili kuhakikisha kuna usalama na usafi kwa madhumuni ya kustawisha sekta hiyo. Wadau hao kwa muda wamekuwa wakilalamikia kero kutoka kwa vijana wanaoendeleza huduma mbalimbali ufuoni, almaarufu kama beach boys, ambapo baadhi yao hudaiwa kujihusisha na uhalifu. “Mara tu tutakapotunga sheria hii, tutakuwa na utaratibu ufukweni,” alisema Mwenyekiti wa Wahudumu wa Utalii Pwani Kusini, Bi Sally Mathenge. Polisi walithibitisha huwa wanapokea ripoti za unyanyasaji wa watalii katika ufuo wa Diani, lakini kesi hizi zimepungua katika miezi michache iliyopita. Kwa mujibu wa Msimamizi wa Polisi wa Kitengo cha Watalii cha Diani, Bw Godfrey Parteneu, visa vya unyanyasaji vimekuwepo. Hata hivyo, alisema maonyo ya mara kwa mara, pamoja na elimu kwa wahudumu wa ufuoni, yamepunguza malalamishi ya watalii. “Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, tumeona kesi hizi zimepungua lakini sio asilimia 100. Tunahakikisha kwamba wahudumu wote walio kando ya ufuo wanajiunga na vikundi vilivyoteuliwa ili kusaidia kufuatilia visa vyovyote vya unyanyasaji na hili limefanya kazi,” alisema Bw Parteneu. Wadau wa utalii sasa wanatumai kuwa mswada unaotungwa ukipitishwa kuwa sheria, utasaidia kudhibiti shughuli za ufuoni kwa kuhakikisha kuna usalama kwa watalii. Afisa Mtendaji wa Chama cha Wahudumu wa Hoteli nchini (KAHC), tawi la Pwani, Dkt Sam Ikwaye, alisema imechukua zaidi ya miaka kumi kuanzisha kanuni za ufuoni. Kulingana naye, mara nyingi mchakato huo huingiliwa na masuala ya siasa. Hii ni kutokana na wanasiasa ambao hutaka kuonekana wanatetea maslahi ya vijana. Dkt Ikwaye alisema takwimu za awali za Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) zilionyesha kuwa watalii 7 kati ya 10 walisema hawakufurahishwa na ziara yao katika Pwani ya Kenya kutokana na usumbufu. “Tunataka kanuni hizi ziwe sehemu ya sheria katika Kaunti ya Kwale. Usimamizi wa ufuo umegatuliwa lakini miaka hii yote hakuna serikali ya kaunti iliyoweka sheria za kulinda fuo ambazo zina jukumu muhimu kwa uchumi wa eneo la Pwani,” alisema. Aliongeza kuwa, hatua hii pia itakuza uwajibikaji kwa baadhi ya wawekezaji ambao wanajulikana kuchafua fuo kwa kutupa taka ovyo. Maoni yake yaliungwa mkono na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Leopard Beach Kioko Musyoki, ambaye alisema wadau walipaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha Diani inaendelea kupigiwa kura kama ufuo bora zaidi barani Afrika. “Wengi wanasema ufuo ni safi lakini ‘beach boys’ huishia kuwa kero,” akasema.
A 16-yr-old secondary school student in Lagos has allegedly ran mad after confessing that he was sexually molested by a popular Lagos hotelier at Bucknor, Isheri Oshun area of the state. The incident, which rattled his parents reportedly started before last Christmas when the student confided in his mother that he had a confession to […]
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema watalii Milion 1,863,108 (1.8) wametwmbelea hifadhi za Taifa ( TANAPA) Kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la watali 244,570 ukilinganisha na mwaka 2022/2023 ambapo watalii 1,618,538 (Mil. 1.6) Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro akieleza mafanikio […] The post Watalii Mil.1.8 watembelea hifadhi za TANAPA mwaka 2023/2024 first appeared on Millard Ayo.
Tanzania na Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa (UN Tourism) zimesaini mkataba wa makubaliano utakaoifanya Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la Pili la Kikanda la Utalii wa Vyakula la Shirika la Umoja wa Mataifa (The 2nd UN Tourism Regional Forum on Gastronomy Tourism for Africa) linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Machi 11 […] The post Tanzania mwenyeji Kongamano la Kimataifa la Utalii wa Vyakula Barani Afrika first appeared on Millard Ayo.
Wadau wa Mazingira na utalii wametakiwa kuwa mabalozi kwa kutunza vivutio vya asili Ili jamii inayowazunguka iige mfano kutoka kwao. Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili iliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Sunset Iringa mjini mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Joachim Nyingo ambae alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema kampeni hii […] The post Wadau wa Mazingira na utalii watakiwa kuwa mabalozi kwa kutunza vivutio vya asili first appeared on Millard Ayo.
Na Mwandishi wetu Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kuongeza ubunifu katika utendaji wao wa kazi wa kila siku ili kuongeza mapato na hivyo kusaidia kuimarisha huduma za uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii. Kamishna Doriye ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo […]
Na Safina Sarwatt, Mtanzania Digital Msimu wa 23 wa mbio maarufu za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025 umezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Salinero, Moshi. Hafla hiyo, iliyojumuisha wadau mbalimbali wa michezo, ilitangaza maandalizi ya mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Februari 23, 2025. Akizungumza kwa niaba ya […]