Washindi CRDB kutembelea hifadhi ya Serengeti

Habari Leo
Published: Apr 10, 2025 10:25:53 EAT   |  Travel

WASHINDI wa Benki ya CRDB kupitia kampeni ya “Tembo Card ni Shwaa ” wanakwenda Hifadhi ya Taifa ya…

The post Washindi CRDB kutembelea hifadhi ya Serengeti appeared first on HabariLeo.

WASHINDI wa Benki ya CRDB kupitia kampeni ya “Tembo Card ni Shwaa ” wanakwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuona wanyama mbalimbali akiwemo Simba kwa muda wa siku tatu.

Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Cosmas Saadat wakati wa mapokezi ya washindi hao tisa kutoka mikoa mbalimbali ya nchi ikiwemo mkoa wa Njombe, Iringa,Dar es Salaam, Kilimanjaro na nk ambao wanakwenda.

Washindi hao wa Tembo Card ni shwaa wamepata mapokezi mkoani Arusha ambao ni lango la utalii kupitia benki hiyo kisha kuendelea na safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujionea wanyama na vivutio vingine via utalii

“Nyie ni mfano halisi wa kadi yetu ya tembo card na awamu ya pili itahusisha washindi wengine kwenda kutembea nje ya nchi kwa kuchanja shwaa kupitia kadi hiyo na awamu ya tatu mshindi atapewa gari jipya aina ya Ford Ranger yenye ziro kilomita”

Alisema kampeni hiyo inaawamu tatu ya kwanza washindi away ya kwanza wanaenda kuona wanyama mbalimbali ikiwemo Simba katika Hifadhi ya Serengeti.

Naye mmoja kati ya washindi hao, Ponsiano Kanijo Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Mkwawa aliishukuru benki hiyo kwa kuja kampeni hiyo kwani anatumia benki hiyo na familia yake katika kupata huduma mbalimbali

“Tusibebe fedha kadi zetu za benki zinalipia kila kitu popote ulipo hivyo tusibebe fedha mkononi tutumie kadi za benki kupata huduma”

  1. Wakati huo huo,Jackson Julius kutoka kitengo cha biashara cha kadi kutoka benki hiyo alitoa rai kwa wateja wa benki hiyo kutumia kadi kufanya malipo kwa kadi ili waweze kupata ushindi.

The post Washindi CRDB kutembelea hifadhi ya Serengeti appeared first on HabariLeo.