Tanzania, Niger kukuza biashara, utalii

TANZANIA inatazamia kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na taifa la Niger katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii…
The post Tanzania, Niger kukuza biashara, utalii appeared first on HabariLeo.
TANZANIA inatazamia kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na taifa la Niger katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii kwa manufaa ya nchi zote mbili, Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jakaya Kikwete anaeleza.
Kikwete ameeleza hay oleo Aprili 17, alipokutana na kuzungumza na Rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani katika Ikulu ya Niamey nchini humo.
Akiwasilisha ujumbe maalum wa Rais Samia kwa Serikali ya Niger, Kikwete ameeleza hisia za Rais Samia kufurahishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Niger huku akisisitiza umuhimu wa kukuza uhusiano huo.
Aidha, ameeleza shauku ya Rais Samia kuona nchi za Afrika zikibadilishana uzoefu na ujuzi ili utajili mkubwa wa maliasili uliopo uweze kuvunwa na kuendelezwa kwa faida ya wananchi wa bara hilo.
The post Tanzania, Niger kukuza biashara, utalii appeared first on HabariLeo.