Mataifa 200 kushiriki jukwaa utalii wa vyakula

Habari Leo
Published: Apr 22, 2025 13:43:10 EAT   |  Travel

WASHIRIKI  zaidi ya 300 kutoka mataifa 200 wanatarajia kushiriki Jukwaa la Pili la Utalii wa Vyakula ambavyo vinatajwa…

The post Mataifa 200 kushiriki jukwaa utalii wa vyakula appeared first on HabariLeo.

WASHIRIKI  zaidi ya 300 kutoka mataifa 200 wanatarajia kushiriki Jukwaa la Pili la Utalii wa Vyakula ambavyo vinatajwa kuchagiza masoko ya vyakula na uchimu wa nchi kupitia ubunifu wa vyakula vya asili.

Aidha jukwaa hilo linatarajia kufunguliwa kesho na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria wakiwemo viongozi wa ngazi za juu katika sekta ya utaliu na ukarimu, watumishi wa serikali na wataalam wa chakula.

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana wakati akiongea na wanaahabari juu ya maandalizi ya jukwaa hilo linalofanyika leo Aprili 23 hadi 25 Arusha.

Amesema mkutano huo unahusisha matukio mbalimbali ikiwemo maonesho ya mapishi ikiwashirikisha wapishi wa mashuhuri na vipaji vya ndani, kuonja aina tofauti za vyakula na vinywaji, mijadala ya jopo na mawasilisho itakayoainisha fursa mpya katika utalii wa vyakula na jinsi unavyoweza kunufaisha uchumi na jumuiya za wenyeji.

Amesema jukwaa hilo ni muhimu kwa nchi yaTanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniania(UN Tourism) Kanda ya Afrika kwalengo la kukuza maendeleo yakiuchumi kupitia sekta ya vyakula vya utalii wa vyakula

The post Mataifa 200 kushiriki jukwaa utalii wa vyakula appeared first on HabariLeo.