MTWAPA MJINI
JOMBI wa hapa alilazimika kujipikia asilale njaa mkewe alipomhadaa alikuwa amechelewa kazini ilhali alikuwa amelalia kifua cha mpango wake wa kando katika hoteli moja Mombasa.
Jamaa alikuwa akisubiri mkewe afike aandae chajio alipopata arafa kutoka kwa demu akimjulisha kwamba, alikuwa amechelewa kazini.
Demu alisema alipokuwa akimtumia jamaa arafa hiyo alikuwa amelala katika kifua cha dume wakijiandaa kurushana roho.
“Alikuwa mpango wangu wa kando wa kwanza na alinipandisha mizuka nikalazimika kumhadaa mume wangu. Nilifika nyumbani saa sita usiku na nikapata amepika na kula,” demu alifunguka katika ukurasa mmoja wa mtandao wa kijamii ambao akina dada huzungumzia uzoefu wa maisha ya ndoa.
***
Nilikutema kwa kulaza damu, demu aambia ex
KIRIBWET, TRANSMARA
Kipusa wa hapa alijuta kuitikia ombi la mpenzi wake wa awali la kumtaka amwambie ukweli kuhusu sababu ya kumtema.
Duru zinaarifu wawili hao walishiriki uhusiano wa kimahaba kwa muda mrefu kabla ya kipusa kumtaka jamaa ajaribu bahati kwingine.
Kipusa hakumfichulia polo sababu ya kumrusha nje lakini jamaa hakukoma kumlilia amwambie alivyokosa.
Ndiposa hatimaye kipusa alimchoma jombi kwa ukweli kuwa yeye ni goigoi kwenye tendo la ndoa.
NA KIPNGENO CHERUIYOT
Kalameni ajiandalia mlo mke akitulia kwenye kifua cha mpango wa kando hotelini
MTWAPA MJINI JOMBI wa hapa alilazimika kujipikia asilale njaa mkewe alipomhadaa alikuwa amechelewa kazini ilhali alikuwa amelalia kifua cha mpango wake wa kando katika hoteli moja Mombasa. Jamaa alikuwa akisubiri mkewe afike aandae chajio alipopata arafa kutoka kwa demu akimjulisha kwamba, alikuwa amechelewa kazini. Demu alisema alipokuwa akimtumia jamaa arafa hiyo alikuwa amelala katika kifua cha dume wakijiandaa kurushana roho. “Alikuwa mpango wangu wa kando wa kwanza na alinipandisha mizuka nikalazimika kumhadaa mume wangu. Nilifika nyumbani saa sita usiku na nikapata amepika na kula,” demu alifunguka katika ukurasa mmoja wa mtandao wa kijamii ambao akina dada huzungumzia uzoefu wa maisha ya ndoa. *** Nilikutema kwa kulaza damu, demu aambia ex KIRIBWET, TRANSMARA Kipusa wa hapa alijuta kuitikia ombi la mpenzi wake wa awali la kumtaka amwambie ukweli kuhusu sababu ya kumtema. Duru zinaarifu wawili hao walishiriki uhusiano wa kimahaba kwa muda mrefu kabla ya kipusa kumtaka jamaa ajaribu bahati kwingine. Kipusa hakumfichulia polo sababu ya kumrusha nje lakini jamaa hakukoma kumlilia amwambie alivyokosa. Ndiposa hatimaye kipusa alimchoma jombi kwa ukweli kuwa yeye ni goigoi kwenye tendo la ndoa. NA KIPNGENO CHERUIYOT

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…