A total of 667,040 candidates are expected to sit Tanzania’s Form Four national examinations from October 19 to November 6, 2026, as the National Examinations Council of Tanzania (Necta) steps up security measures to ensure a safe and fair examination period.
Thousands of university applicants who missed out on admission in the first two rounds have been given a final seven-day opportunity to secure undergraduate places for the 2026/27 academic year. The Tanzania Commission for Universities (TCU) opened the third and final admission window, running from October 3 to 9, for applicants to apply to institutions with available vacancies. TCU Executive Secretary Prof Charles Kihampa said the extension followed requests from applicants who had not secured places and universities that still had vacancies. “After completing the two admission rounds, the commission received requests from some applicants who were unsuccessful in securing admission in the previous rounds, as well as universities that still have vacancies and requested more time to continue admitting students,” he said. He urged applicants who had not applied or failed to secure admission in the second round to use the final window to apply to programmes with available places. Universities have been directed to publicise their remaining vacancies. Under the new schedule, universities will submit names of applicants admitted in the third round to TCU on October 13 and 14, with successful applicants expected to be announced on October 17. Applicants selected by more than one university in the third round will have from October 17 to 19 to confirm their preferred institution. The same period applies to those who failed to confirm admission in earlier rounds. Applicants who secured admission to more than one university in the second round, as well as those who failed to confirm their first-round admission, have also been given until October 19 to complete the process. Confirmation requires a special identification number sent via text message or email using the contact details provided during application. “Those who do not receive the confirmation number on time should access the admission systems of the respective universities and request that the number be sent to them,” Prof Kihampa said. TCU said applicants must complete confirmation through the same accounts used for their original applications. The commission has also published the list of applicants admitted to more than one university on its website. Prof Kihampa said applicants experiencing confirmation difficulties should contact the respective universities, which have been directed to resolve such cases in accordance with established procedures. “All higher learning institutions have been instructed to receive reports from applicants experiencing difficulties with admission confirmation and work towards resolving them promptly,” he said.
HakiElimu Executive Director Mary Ndaro urged the fellows to use the programme to build the confidence, networks and skills needed to participate meaningfully in national affairs.
As the Tanzania Commission for Universities (TCU) wraps up the first round of undergraduate admissions for the 2026/2027 academic year, a massive logistical and financial bottleneck has emerged.
As the Tanzania Commission for Universities (TCU) wraps up the first round of undergraduate admissions for the 2026/2027 academic year, a massive logistical and financial bottleneck has emerged.
Thousands of students have another opportunity to secure university places after the Tanzania Commission for Universities (TCU) opened the second round of undergraduate admissions for the 2026/27 academic year.
As universities increasingly turn to digital platforms to expand access to higher education, experts have warned that the rapid growth of online learning could undermine public confidence in academic qualifications unless institutions strengthen their internal quality assurance systems. The warning emerged during a Tanzania Commission for Universities (TCU) consultative workshop in Tanga on August 22, 2026. The meeting brought together vice-chancellors, deputy vice-chancellors, principals, and senior academic leaders from across the country to discuss emerging trends in higher education. Held alongside National Education, Skills and Innovation Week under the theme: Responding to Emerging Trends and Advancing Excellence in University Education, the forum highlighted online and transnational education as key areas requiring urgent intervention. Director of Academic and Institutional Audits at the Zimbabwe Council for Higher Education (ZIMCHE), Dr Hardson Kwandayi, noted that online learning is expanding rapidly across Africa, driven by digital transformation, internationalisation, and demand for flexible study modes. However, he warned that this rapid growth poses significant risks to universities and regulators, spanning academic integrity, inadequate infrastructure, degree recognition, and the proliferation of fraudulent providers. "Traditional quality assurance systems are no longer sufficient for online education, as they were designed mainly for campus-based institutions and often fail to evaluate digital learning environments adequately," said Dr Kwandayi. While online learning removes geographical barriers, supports self-paced study, and fosters international collaboration, Dr Kwandayi stressed that these benefits depend entirely on robust institutional frameworks. Unlike conventional contact learning, digital delivery exposes students to unstable internet connections, high data costs, limited peer interaction, and weak academic support. Universities also struggle to deliver practical laboratory training online, while digital assessments heighten risks of plagiarism, impersonation, contract cheating, and unauthorized AI tool usage. Unchecked poor-quality providers threaten to erode public trust across the entire higher education ecosystem. Dr Kwandayi urged institutions to collaborate closely with quality assurance agencies rather than relying solely on external regulation. TCU's regulatory response In response, the TCU is tightening frameworks governing internal quality standards. TCU executive secretary, Prof Charles Kihampa, told delegates that the regulator has adopted resolutions to strengthen institutional Quality Assurance Units, enforce regulatory compliance, and improve academic governance. Key measures include embedding quality assurance into strategic planning, acting on audit recommendations, and enforcing approved student intake limits through the Universities Information Management System. "The Commission already maintains specific guidelines covering online and blended delivery modes, alongside programme benchmarks and the University Qualifications Framework," said Prof Kihampa. He added that all programmes must undergo accreditation via the online Programme Management System, which also functions as a public database of accredited curricula. Beyond compliance Regional Project Coordinator for the East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP), Dr Cosam Joseph, argued that institutions must look beyond basic regulatory requirements. "Compliance alone is no longer sufficient to ensure institutions remain relevant, innovative, and globally competitive," said Dr Joseph, urging university leaders to reposition quality assurance as a driver of continuous improvement, evidence-based decision-making, and institutional excellence.
A total of 734 farmers from 17 Agricultural Marketing Cooperative Societies have successfully completed training under the Elimu Tija initiative, a programme spearheaded by the Kilombero Community Charitable Trust in collaboration with Kilombero Sugar Company Limited
WAZAZI wawili wamewasilisha kesi mahakamani kutaka Wizara ya Elimu izuiwe kukamilisha uteuzi wa wanafunzi wa Gredi 10 katika shule za sekondari, wakidai mfumo wa kusimamia habari za elimu Kenya ( KEMIS) una hitilafu zinazowanyima wanafunzi nafasi ya kuchagua shule wanazotaka. Mabw Omwenga Ongegu na John Ominde wanasema mfumo huo unaonyesha shule 1,000 pekee kwa kila mseto wa masomo, hata pale ambapo shule nyingi zaidi zinatoa mseto huo nchini. Pia wanadai kuwa baadhi ya miseto ya masomo haina shule zilizoorodheshwa. Katika ombi lao, Ongegu alisema miseto 26 ya masomo imeathiriwa na idadi ya shule hizo 1,000, hali inayoficha taasisi nyingine zinazotoa masomo hayo. Kwa mfano, mseto wa ST1048 unaojumuisha Baiolojia, Kemia na Fizikia katika mkondo wa Sayansi, Tekonolojia na Hisbati (STEM) una shule 10,515 zinazodaiwa kuutoa nchini, lakini mfumo unaonyesha shule 1,000 pekee. Hii ina maana kuwa wanafunzi wanaona takriban asilimia 9.51 pekee ya shule zinazopatikana kwa mseto huo. Walalamishi pia wanasema kuwa kati ya mIseto 418 iliyoorodheshwa kwenye mfumo, 28 haina shule yoyote iliyoonyeshwa, huku 303 ikiwa na shule 94 au chini ya hapo. Wanasema kasoro hizo zinazuia wanafunzi na wazazi kupata taarifa sahihi kabla ya kufanya maamuzi yatakayoathiri masomo yao ya baadaye. “Hii haiwezi kuachwa bila kurekebishwa hadi wanafunzi watakapofika wakati wa kuomba nafasi za shahada na diploma kupitia KUCCPS,” sehemu ya kesi inasema. Pia walalamishi wameibua wasiwasi kuhusu jinsi masomo ya Gredi 10 yatakavyoathiri nafasi za kujiunga na vyuo vikuu. Wanasema hakuna ufafanuzi wa kutosha kuhusu jinsi somo la Community Service Learning litakavyoathiri wanafunzi kujiunga na kozi mbalimbali. Wanataka mahakama itangaze kuwa kuonyesha orodha zisizokamilika bila kutoa tahadhari kunakiuka haki za wanafunzi. Pia wanataka wizara iamriwe kufungua tena mfumo huo ili wanafunzi warekebishe uchaguzi wao baada ya kupewa taarifa kamili kuhusu shule na mseto wa masomo. Wamependekeza mfumo ufunguliwe tena baada ya mitihani ya tathmini ya Gredi 9 kuanza Oktoba 26, ili kuepusha kuwaongezea watahiniwa shinikizo. Mfumo wa KEMIS ulifunguliwa Agosti 24, 2026, na muda wa kuchagua shule uliongezwa hadi Septemba 15.
LONGIDO: NAIBU Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, Dk. Stephen Kiruswa, amekabidhi mashine ya kunakili na kuchapisha nyaraka pamoja na kompyuta kwa Shule ya Msingi Lesing’ita, vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni tatu, ili kupunguza gharama za shule katika uchapishaji wa karatasi za mazoezi, mitihani na shughuli nyingine za…
By Edwin Philip, Lafia The Nasarawa State Government has reiterated its commitment to tackling gender-based violence through the implementation of the Violence Against Persons (Prohibition) Law, enacted in the state in January 2021. The Commissioner for Women Affairs and Social Development, Rebecca Adamu Kwaji, gave the assurance on Wednesday at a two-day workshop on bridging […]
MWANZA; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesogeza huduma karibu na wananchi jijini Mwanza kupitia kambi maalumu iitwayo ‘Viwango Clinic’, ili kufikisha elimu kuhusu ubora wa bidhaa mbalimbali za chakula na vipodozi. Kambi hiyo ya siku tano ilianza Jumatatu Oktoba 19, 2026 na itamalizika Ijumaa Oktoba 23, 2025 inafanyika katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza,…
A total of 667,040 candidates are expected to sit Tanzania’s Form Four national examinations from October 19 to November 6, 2026, as the National Examinations Council of Tanzania (Necta) steps up security measures to ensure a safe and fair examination period.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuhakikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ufundi ya Mkuranga unakamilika mapema ili wanafunzi waanze kusoma ifikapo Januari 2027. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, alitoa maagizo hayo jana wakati akikagua ujenzi wa shule…
IRINGA: Ujenzi wa maabara za kisasa, hosteli, maktaba na majengo ya kitaaluma wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 30.4 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) unatarajiwa kuongeza uwezo wa chuo hicho kuandaa walimu wenye ujuzi unaohitajika katika sekta ya elimu. Aidha, Serikali imeweka msisitizo katika usimamizi wa fedha na ukamilishaji wa miradi kwa…
ZAIDI ya watahiniwa milioni 3.6 wanaojiandaa kufanya mitihani na tathmini za kitaifa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha shuleni na tishio la mgomo wa walimu wanaosimamia na kusahihisha mitihani. Watahiniwa 1,048,355 wa Mtihani wa Kitaifa cha Kidato cha Nne (KCSE) walifanya maandalizi ya mwisho mnamo Alhamisi, huku mitihani ya utendaji ikipangwa kuanza Jumatatu, Oktoba 19, 2026. Mitihani mikuu itafanyika kuanzia Novemba 2 hadi 20. Wakati huo huo, watahiniwa wa Tathmini ya Elimu ya Msingi (KPSEA) na Tathmini ya Elimu ya Sekondari ya Chini (KJSEA) wanatarajiwa kufanya mitihani yao baadaye mwezi huu. Hata hivyo, maandalizi yamekumbwa na mgogoro wa malipo baada ya Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (Kuppet) kuwataka wanachama wake kususia usimamizi, uangalizi na usahihishaji wa mitihani hadi malalamishi yao yatakaposhughulikiwa. Katibu Mkuu wa Kuppet, Akello Misori, anataka wasimamizi walipwe angalau Sh4,000 kwa siku na walimu wanaosahihisha karatasi za mitihani walipwe angalau Sh100 kwa kila karatasi. Kwa sasa, wasimamizi hulipwa kati ya Sh630 na Sh680 kwa siku, huku malipo ya kusahihisha karatasi yakianzia Sh35 hadi Sh75. Hali hiyo imewafanya walimu wakuu kutaka mkutano wa dharura kati ya Muungano wa Kitaifa wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili (KESSHA), Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) na Kuppet ili kutafuta suluhu kabla ya mitihani kuanza. Mwenyekiti wa KESSHA, Willy Kuria, alisema malalamishi ya walimu yana msingi, lakini kususia mitihani kutawaathiri zaidi ya watahiniwa milioni moja wa KCSE. “Tunahitaji mkutano kutatua masuala haya. Badala ya mgomo, tunaweza kukubaliana jinsi ya kuendesha mitihani,” akasema. Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC, David Njengere, alisema viwango vya malipo ya wasimamizi wa vituo, wasimamizi na walimu wanaosahihisha mitihani hupitiwa kila baada ya miaka minne na vinatarajiwa kufanyiwa marekebisho mwaka ujao. Mbali na mgogoro huo, shule zinakabiliwa na uhaba wa fedha za kununua vifaa vya maabara na mahitaji mengine ya mitihani ya vitendo. KESSHA inasema shule za sekondari za umma zimekosa Sh5,787 kwa kila mwanafunzi katika mgao wa mwaka huu, hali inayozilazimisha baadhi kukopa kutoka kwa wasambazaji. Serikali inapaswa kutoa Sh22,244 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka, lakini mgao uliopokelewa umekuwa chini ya kiwango hicho. Katika hatua nyingine, maafisa wa elimu na usalama wamesema mipango imewekwa kuhakikisha watahiniwa wanalindwa na mitihani inafanyika bila udanganyifu. Katika Kaunti ya Nakuru, watahiniwa 48,038 wanatarajiwa kufanya mitihani katika vituo 485. KESSHA imesisitiza kuwa mazungumzo ya haraka ni muhimu ili kulinda uadilifu wa mitihani na kuhakikisha wanafunzi hawaadhibiwi kutokana na mizozo kati ya walimu na serikali.
TANGA: WAKALA wa Mbegu za Kilimo (ASA) umehamasisha wakulima kutumia mbegu bora zinazolingana na mazingira yao na zinazoweza kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi, ili kuongeza tija na kuimarisha usalama wa chakula nchini. Elimu hiyo imetolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika mkoani Tanga, ambapo wananchi waliotembelea banda la ASA wamepata fursa ya…
IRINGA: MIRADI ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 71.46 katika sekta ya elimu ya juu na usafiri wa anga inatarajiwa kukaguliwa na Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Iringa, Oktoba 18, mwaka huu. Miradi hiyo inahusisha uwekezaji wa Sh Bilioni 30.4 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)…
MWANZA; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amezindua Shule ya Msingi Butiriti iliyopo wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makonda amesisitiza umuhimu wa elimu katika kupambana na umaskini na kuimarisha maendeleo ya jamii. Makonda amempongeza Rais wa Dk Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu, akisema…
HATIMA ya usimamizi wa mitihani ya kitaifa ya mwaka huu iko mashakani baada ya Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Kati (Kuppet) kusisitiza kuwa wanachama wake hawatashiriki katika shughuli za mitihani hadi malalamishi yao yatatuliwe. Tishio hilo linajiri siku chache kabla ya wanafunzi kufanya mazoezi ya mwisho ya mitihani ya Cheti cha Elimu ya Sekondari nchini (KCSE), yanayotarajiwa kuanza Ijumaa, Oktoba 16. Mitihani hiyo itaanza rasmi Oktoba 19, huku wiki ya kwanza ikitengwa kwa mitihani ya Kifaransa, Kijerumani, Kiarabu, Lugha ya Ishara ya Kenya na Muziki. Mitihani ya masomo mengine inayohusisha idadi kubwa ya watahiniwa itaanza Novemba 2 na kukamilika Novemba 20. Katika azimio lililotolewa baada ya mkutano wa Baraza la Kitaifa la Uongozi, Kuppet ilielezea wasiwasi kuhusu jinsi Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (Knec) linavyoshughulikia malalamishi ya walimu wanaohusika na usimamizi wa mitihani. Katibu mkuu wa Kuppet, Bw Akelo Misori, alisema chama hicho huo kimewaagiza wanachama wake kujiondoa katika shughuli zote za mitihani za Knec hadi baraza hilo litakapotoa hakikisho la kuboresha masharti ya kazi na malipo ya wasimamizi wa mitihani. “Tunaomba wanachama wetu wasishiriki katika mitihani yote inayoendeshwa na Knec. Wasipotoa hakikisho la kuboresha masharti ya kazi na malipo ya watahini, tunatahadharisha baraza hilo kuwa mwaka 2026 hautakuwa wa kawaida. Tutahakikisha usimamizi wa mitihani unavurugika mwaka mzima,” alisema. Mgogoro huo unahusu malipo ya walimu wanaohusika na usimamizi wa vituo, kusimamia watahiniwa, kupeana mitihani na kusahihisha karatasi za mitihani, miongoni mwa majukumu mengine.
DAR ES SALAAM: Wizara ya Nishati na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) zimekutana kujadili mikakati ya kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma kuhusu miradi ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia inayotekelezwa nchini. Majadiliano hayo yaliyofanyika Oktoba 13, 2026 katika Ofisi za PURA Jijini Dar es Salaam yalihudhuriwa na…
KIGOMA: Wazazi na walezi mkoani Kigoma wametakiwa kusimamia elimu, malezi na ndoto za watoto wa kike badala ya kuwapeleka kwenye ndoa za utotoni kwa watu wenye umri mkubwa sawa na baba au babu zao kwa lengo la kupata mali. Kaimu Afisa Elimu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Fausta Akaro, alisema hayo akimwakilisha Katibu Tawala…
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema Chuo Kikuu cha Kikanda cha Usafiri kwa Njia ya Maji (RMU) kinatarajiwa kujengwa Tanzania ili kuwa kitovu cha elimu, mafunzo, utafiti na ubunifu katika sekta ya usafiri wa majini kwa nchi wanachama wa Shirika la Bahari la Kanda ya Mashariki, Kusini na Kaskazini mwa Afrika…
DAR ES SALAAM: Wataalamu wa afya wameonya kuhusu arthritis, kundi la magonjwa zaidi ya 100 yanayoweza kushambulia viungo vya mwili na kusababisha ulemavu ikiwa hayatagunduliwa na kutibiwa mapema. Arthritis si ugonjwa mmoja, bali ni jina linalotumika kuelezea magonjwa mbalimbali yanayoathiri viungo na wakati mwingine sehemu nyingine za mwili. Profesa Francis Furia, Mhadhiri wa Chuo Kikuu…
DAR ES SALAAM: WALIMU nchini wametakiwa kutambuliwa na kupongezwa kwa mchango wao katika malezi na utoaji wa elimu kwa watoto, huku wakihimizwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa Shule ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Eugenia…
RUKWA:Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) kimetakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika tafiti, ubunifu na matumizi ya teknolojia zinazolenga kutatua changamoto za maendeleo nchini, ili kiwe kinara wa sayansi na teknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema hayo Oktoba 11, 2026, alipotembelea Kampasi ya…
Unguja. Ujenzi wa Shule ya Kimataifa ya GEMS Zanzibar katika eneo la mradi wa Infinity Hills unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Ujenzi huo ni hatua kubwa katika kupanua fursa za elimu visiwani humo kupitia shule iliyobuniwa maalum kuhudumia hadi wanafunzi 1,500. Uwezo wa shule hiyo umeongezwa kutoka lengo la awali la wanafunzi 1,100 baada ya tathmini…
Kwa vijana wengi, ni wazazi wao waliowachagulia kanisa walikokulia. Huko ndiko walikohudhuria shule ya Jumapili, kujifunza Biblia, kupata marafiki na kushiriki shughuli za kidini. Hata hivyo, wanapokua na kuanza kujitafutia mwelekeo wa maisha, baadhi hujiuliza ikiwa makanisa hayo bado yanakidhi mahitaji yao ya kiroho. Kwa Hillary Agidho, safari hiyo ilianza katika familia iliyokuwa na madhehebu mawili. Baba yake ni Muanglikana, huku mama yake akiwa Mkatoliki. Akiwa mtoto, alihudhuria shule ya Jumapili katika Kanisa la Anglikana, ingawa wakati mwingine aliandamana na mama yake katika ibada za Kikatoliki. Baadaye, alijiunga na shule ya wavulana iliyofadhiliwa na Waanglikana na kujihusisha zaidi na huduma za kanisa. Hata hivyo, akiwa chuo kikuu, alikutana na huduma mbalimbali za Kipentekoste, ambako alishiriki katika uinjilisti. Alivutiwa na makanisa hayo yalivyoendesha ibada na hatimaye, baada ya kuomba na kutafakari, alijiunga na Kanisa la PEFA mwaka 2024 alipohamia Nairobi. “Nilitaka mazingira ambayo yangenisaidia kukua kiroho na kutumia vipawa nilivyokuwa nimekuza kupitia huduma,” anasema. Ingawa baadhi ya jamaa na marafiki walishangazwa na uamuzi wake wa kuacha kanisa la familia, wazazi wake walimwelewa na kuamini angefanya uamuzi unaofaa. Kwa Joan Omondi, mabadiliko yalianza alipokuwa shule ya upili. Alikulia katika Kanisa la Nomiya, kanisa la Kikristo la jamii ya Waluo, ambako alishiriki shule ya Jumapili na masomo ya Biblia. Siku moja alihudhuria ibada ya Muungano wa Kikristo (CU) na kuvutiwa na nyimbo na waumini walivyoshiriki ibada. Anasema uzoefu huo ulimsaidia kutambua kuwa alitaka kujenga uhusiano wake binafsi na Mungu badala ya kuendelea na kanisa kwa sababu tu familia yake ilikuwa hapo. Hata hivyo, baba yake mwanzoni alitatizika kukubali uamuzi huo, akiamini familia inapaswa kuabudu pamoja. Joan anasema baada ya muda wazazi wake walielewa kuwa hakuwa akiwakataa wala kupuuza malezi yao. Badala yake, alikuwa akitafuta nafasi ya kukua kiroho. Ashon Musya naye aliamua kutafuta kanisa jingine baada ya kuhisi kuwa vijana hawakupewa nafasi ya kutosha kushiriki shughuli za kanisa alilokuwa akihudhuria. Alikulia katika Kanisa Katoliki kabla ya mama yake kuhamia Maranatha Faith Assembly, kanisa la Kipentekoste. Baadaye, alivutiwa na huduma za vijana na akaanza kuhudhuria CITAM Valley Road baada ya kualikwa na jirani. Anasema alifurahishwa na mafundisho ya Biblia, ushauri wa kiroho na ufuatiliaji wa karibu aliopata. “Ukikosa kuhudhuria ibada Jumapili mbili, kuna mtu anayekupigia simu kuuliza kilichotokea,” anasema. Musya anaongeza kuwa kukua kwake kiroho kuliboresha hata uhusiano wake na wazazi wake, kwani walianza kushiriki zaidi katika mazungumzo kuhusu Biblia na maombi. Kwa vijana hao watatu, kuhama makanisa hakukumaanisha kuacha imani waliyojifunza utotoni, bali kutafuta mazingira yanayowasaidia kuimarisha uhusiano wao na Mungu. Wanawahimiza vijana wanaopitia hali kama hiyo kuomba mwongozo wa Mungu, kutafakari kwa makini na kutafuta kanisa linalowapa nafasi ya kujifunza, kuhudumiana na kukua kiroho.
IRINGA: WAZAZI na walezi wametakiwa kutambua kuwa mafanikio ya watoto hayaishii katika kupata elimu darasani, bali yanategemea pia malezi yanayojenga maadili, nidhamu na uwajibikaji katika jamii. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Mount Komaguru, Dk Yahaya Msigwa, wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuunganisha elimu na malezi…
Ofisa miradi ya jamii wa Vodacom Tanzania Foundation, Deborah Kaluzi (kulia) akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Makumbusho, Yasini Shehaghilo (kushoto). Hafla hiyo ni sehemu ya mpango wa kusaidia shule mbalimbali unaotekelezwa kupitia msafara wa Nyerere Cycling Tour 2026. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Archie…
KONDOA, DODOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, mkoani Dodoma, Said Majaliwa kwa kuwa serikali tayari imetumia takribani Sh milioni 154 kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Amelazimika kufafanua hilo wakati akikanusha taarifa zilizodai kuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Hurumbi, iliyopo Kata ya Selia, wanasoma wanatumia miundombinu chakavu. Majaliwa alisema hayo hivi karibuni…
DAR ES SALAAM: Kisukari cha mimba kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mama na mtoto iwapo hakitagundulika na kudhibitiwa mapema, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Amani Idris Kikula, amesema. Kikula amesema hali hiyo hutokea pale mwili wa mama mjamzito unaposhindwa kutumia na kudhibiti kiwango cha sukari ipasavyo, hali inayohusishwa…
WANAFUNZI wa shule za kutwa ndio wanaobeba mzigo mkubwa wa ada haramu, huku karibu theluthi mbili wakitumwa nyumbani au kuzuiwa kuingia darasani wazazi wanaposhindwa kulipa, utafiti mpya umebaini. Utafiti wa Elimu Bora Working Group (EBWG) ulionyesha kuwa asilimia 64.9 ya wanafunzi wa shule za kutwa wamewahi kufukuzwa au kuzuiwa kuingia darasani kwa sababu ya ada hizo, ikilinganishwa na asilimia 40.5 katika shule za bweni. Bw Chris Owalla wa EBWG alisema sera ya serikali ya elimu ya sekondari bila malipo imeshindwa kuwasaidia watoto wanaohitaji msaada zaidi. “Sera ya elimu ya sekondari bila malipo haifanyi kazi kwa sababu watoto wa shule za kutwa ndio wanaoteseka zaidi,” alisema. Utafiti huo uliowahusisha wazazi, walezi 388 katika kaunti 11 ulibaini kuwa shule za umma zinatoza ada haramu za kati ya Sh15,000 na Sh20,000 kwa shule za kutwa, huku za bweni zikitoza hadi Sh60,000. Baadhi ya ada hizo hutajwa kuwa za chakula cha mchana, masomo ya ziada, maendeleo ya shule, ICT, shughuli za chama cha wazazi na walimu(PTA) na masomo ya likizo. Utafiti huo ulionyesha kuwa mzigo huo huwa mkubwa zaidi kwa familia maskini. Asilimia 61.3 ya familia zinazopata chini ya Sh10,000 kwa mwezi zilisema watoto wao wamewahi kufukuzwa shule, ikilinganishwa na asilimia 23.1 ya familia zinazopata kati ya Sh30,001 na Sh60,000. Bw Cornelius Oduor wa EBWG alisema asilimia 61.6 ya waliohojiwa walisema ada hizo ni ngumu au wasizoweza kumudu huku karibu asilimia 37 wakisema wamewahi kukopa au kuuza mali ili kuzilipia. Utafiti pia ulionyesha kuwa asilimia 87.4 ya wazazi hawajawahi kulalamika kuhusu ada hizo kwa kuhofia watoto wao kuadhibiwa. EBWG sasa inataka Wizara ya Elimu kufanya ukaguzi wa kitaifa wa ada katika shule zote za umma, kuwaadhibu wanaotoza zisizoidhinishwa na kuwarejeshea wazazi fedha walizolipa kinyume cha sheria.
HALI ya wasiwasi ilizuka nje ya Kanisa la Redeemed Gospel, Buruburu jijini Nairobi, Jumapili baada ya mamia ya vijana kuandamana wakitaka haki itendeke kwa mwanamke aliyenaswa kwenye video akidhulumiwa na wenzake. Katika video ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, mwanamke huyo anaonekana akishambuliwa na kuzuiwa kutoka kwenye chumba na wasichana wanne. Tukio hilo liliwakasirisha Wakenya wengi, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakidai mmoja wa wasichana wanaodaiwa kumshambulia mwanamke huyo ni mshirika wa kawaida wa kanisa la Burubuviru. Hata hivyo, mchungaji wa kanisa hilo, Felix Kavoli, alipuuzilia mbali madai kwamba yeye ni baba wa mmoja wa wasichana hao. “Waambieni watu wa mitandao ya kijamii kwamba wamekosea, wameelewa vibaya na wanakuja mahali pasipofaa. Sina binti anayesoma katika Chuo Kikuu cha Riara. Binti zangu ni watu wazima na wanafanya kazi, na majina yao yanajulikana. Sina mtoto anayesoma katika Chuo Kikuu cha Riara,” akasema Mchungaji Kavoli. Mchungaji huyo pia aliwaambia waandamanaji wa Gen-Z kwamba tukio hilo la madai ya unyanyasaji halikutokea kanisani na hivyo hawakupaswa kusababisha vurugu huko. “Halimhusu Mchungaji Kavoli na lilifanyika huko nje. Kwa nini shetani analipinga kanisa?” akauliza. Polisi walizunguka kanisa hilo baada ya maandamano, huku maafisa wa kukabiliana na ghasia wakitumwa eneo hilo wakati waandamanaji wakitaka haki kwa mwathiriwa. “Tuko hapa kudai haki kwa Jahenda (anayedaiwa kuwa mwathiriwa). Kwa nini kanisa linaunga mkono hili?” akasema mmoja. Wengine waliitaka kanisa lichukue hatua dhidi ya wasichana wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo. “Haki kwa Jahenda. Haki daima. Amani, amani, amani,” kijana mwengine alisema. Jumamosi, Chuo Kikuu cha Riara kilithibitisha kuwa baadhi ya watu wanaoonekana kwenye video hiyo ni wanafunzi wake na kulaani tukio hilo, kikisema hatua zitachukuliwa. “Tumeona video ambayo imesambazwa mtandaoni ikionyesha wasichana kadhaa wakimtishia na kumshambulia mwanamke mwengine katika eneo linaloonekana kuwa choo cha umma. Chuo Kikuu cha Riara kinalaani vikali vitendo vya unyanyasaji, vitisho, maonevu, au utovu wa nidhamu,” akasema Makamu Mkuu wa Chuo hicho katika taarifa. Chuo hicho kiliongeza kuwa ingawa tukio hilo linalodaiwa lilitokea nje ya chuo, tabia hiyo ilikiuka moja kwa moja maadili ya taasisi hiyo na kanuni za maadili ya wanafunzi. “Uongozi wa chuo umeanza uchunguzi wa ndani kuhusu suala hilo kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Wanafunzi na sera za taasisi, na tumejitolea kushirikiana na kitengo cha uchunguzi, “Chuo Kikuu cha Riara kinaendelea kujitolea kudumisha elimu iliyo salama, yenye heshima na inayowajibika, kama ambavyo tumekuwa tukifanya,” ikasema taarifa hiyo.
KUPATA maarifa ya vitabu na kwenda shule ni kitu kizuri sana na kwa vyovyote vile, kadri ya uwezo wako, jitahidi kupata au kujiendeleza kielimu. Elimu haina umri uwe mtoto, kijana au umepevuka kiumri, unachohitaji tu ni motisha na moyo wa kujituma. Elimu humwezesha mtu kuchanganua, kutathmini mambo, kupanua mawazo na kuwa na mtazamo tofauti kabisa, kwa njia chanya, kuhusu masuala anuai. Hukupa ujasiri wa aina yake kudadisi mambo na kuuliza maswali mazito kuhusu masuala nyeti. Hatahivyo, uhalisia unaopuuzwa mara kwa mara ni kwamba elimu ya vitabu haitakufunza kila kitu. Kwenda shule ni muhimu kwa sababu kutakuwezesha kutangamana ma watu mbalimbali. Lakini elimu pekee haitoshi kukupa ujuzi wa kukabili maisha. Kando na maarifa ya kitabu, umuhimu wa kuwa na maarifa kihisia na maarifa kijamii hauwezi ukasisitizwa vya kutosha. Maarifa haya hukuwezesha kujielewa na kujithamini kwanza kama mtu binafsi ili uweze kutangamana na binadamu wenzako iwe ni jamaa wa familia, majirani, marafiki, wafanyakazi wenza na jamii kwa jumla. Ni maarifa haya yanayokuwezesha kung’amua wakati wa kuzungumza au kukaa kimya, kukaa au kuondoka, kukubali, au kukataa jambo fulani licha ya ushawishi au shinikizo kutoka kwa wanarika au marafiki. Hukuwezesha kuamua ama kuendeleza au kukatiza mahusiano,kuchapisha picha au la. Matukio tunayoshuhudia katika siku za majuzi kuhusu vijana wa shule yanadhihirisha uhalisia wa kutisha kuhusu kuwepo pengo la maarifa kihisia na kijamii. Katika kipindi cha miezi miwili, video zimesambazwa mitandaoni zikiwaonyesha mabinti katika hali za kutatanisha ambazo bila shaka wataishia kujilaumu na kujutoa maisha yao yote. Video nilizokumbana nazo kuhusu mwanafunzi wachuo kikuu mojawapo nchini katika tamasha ya burudani kuwakaribisha wanafunzi wapya. Binti huyo anayeonekana mlevi asiyejifahamu alirekodiwa akijamiiana hadharani na mvulana wakiwa wamezingirwa na wanafunzi wenzao. Katika video nyingine ilimwonyesha binti mchanga aliyelewa chakari akivuliwa nguo na kupapaswa uchi wake katika tamasha ya burudani iliyofurika watu. Katika jamii iliyojaa visa tele kuhusu tishio zinazowakabili wanawake na wasichana, matukio hayo yanazua wasiwasi kuhusu uwajibikaji binafsi wa mabinti kuhusu usalama wao.
DODOMA: THE Tanzania Commission for Universities (TCU) has opened the third and final round of undergraduate admissions for the 2026/2027 academic year, giving prospective students another opportunity to secure places in degree programmes with available vacancies. The admission window runs from October 3 to 9, 2026, following the completion of the first and second admission…
MOROGORO; WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema michezo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu na mazingira, kwani wanapoweza kuona na kunufaika na rasilimali hizo. Makonda, amesema hayo Oktoba 3, 2026 wakati wa ziara yake eneo la mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026…
Thousands of university applicants who missed out on admission in the first two rounds have been given a final seven-day opportunity to secure undergraduate places for the 2026/27 academic year. The Tanzania Commission for Universities (TCU) opened the third and final admission window, running from October 3 to 9, for applicants to apply to institutions with available vacancies. TCU Executive Secretary Prof Charles Kihampa said the extension followed requests from applicants who had not secured places and universities that still had vacancies. “After completing the two admission rounds, the commission received requests from some applicants who were unsuccessful in securing admission in the previous rounds, as well as universities that still have vacancies and requested more time to continue admitting students,” he said. He urged applicants who had not applied or failed to secure admission in the second round to use the final window to apply to programmes with available places. Universities have been directed to publicise their remaining vacancies. Under the new schedule, universities will submit names of applicants admitted in the third round to TCU on October 13 and 14, with successful applicants expected to be announced on October 17. Applicants selected by more than one university in the third round will have from October 17 to 19 to confirm their preferred institution. The same period applies to those who failed to confirm admission in earlier rounds. Applicants who secured admission to more than one university in the second round, as well as those who failed to confirm their first-round admission, have also been given until October 19 to complete the process. Confirmation requires a special identification number sent via text message or email using the contact details provided during application. “Those who do not receive the confirmation number on time should access the admission systems of the respective universities and request that the number be sent to them,” Prof Kihampa said. TCU said applicants must complete confirmation through the same accounts used for their original applications. The commission has also published the list of applicants admitted to more than one university on its website. Prof Kihampa said applicants experiencing confirmation difficulties should contact the respective universities, which have been directed to resolve such cases in accordance with established procedures. “All higher learning institutions have been instructed to receive reports from applicants experiencing difficulties with admission confirmation and work towards resolving them promptly,” he said.
GEITA; Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ipo katika mazungumzo na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Buckreef (BGC) ya Katoro, Geita, kwa lengo la kukuza ushirikiano utakaoandaa nguvu kazi mahiri kwa ajili ya sekta ya madini. Akizungumza katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo Oktoba 1, 2026, Meneja wa…
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amezindua rasmi Mwongozo wa Kuchopeka Elimu ya Fedha katika Mitaala ya Elimu ya Juu, Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania, ukiwa na lengo la kuwezesha wanafunzi na wahitimu kufanya maamuzi sahihi na yenye uwajibikaji kuhusu fedha. Akizungumza wakati wa…
MGONJWA anapoingia hospitalini hupokea matibabu akiamini dawa alizopewa ni salama na zenye ubora unaostahili. Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya dawa zenye kasoro huingia katika mfumo wa afya na kuwafikia wagonjwa kabla ya dosari zake kugunduliwa. Mwaka huu pekee, Bodi ya Dawa na Sumu Kenya (PPB) imetoa maagizo 16 ya kuondoa sokoni dawa na bidhaa za matibabu zinazoshukiwa kuwa na matatizo ya ubora. Dawa hizo zimehusisha za kugadisha, vifaa vya pumu, dawa za tumbo na bidhaa nyingine muhimu zinazotumiwa hospitalini kila siku. Mkurugenzi Mkuu wa PPB, Dkt Ahmed Mohamed, amesema ongezeko la visa vya kuondolewa kwa dawa sokoni linaonyesha kuwa mifumo ya ufuatiliaji imeimarika na sasa inafanikiwa kugundua matatizo ambayo hapo awali yangeweza kupita bila kugunduliwa. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, changamoto inaanzia katika hatua mbalimbali za mfumo wa ugavi wa dawa. Baadhi ya dosari hutokana na utengenezaji katika viwanda vya nje ya nchi, huku nyingine zikisababishwa na hali mbaya ya uhifadhi au usafirishaji wa dawa kabla hazijamfikia mgonjwa. Dawa nyingi zilizoondolewa sokoni mwaka huu zilitengenezwa katika nchi za kigeni, hasa India. Kampuni kadhaa zilihusishwa na matatizo kama kubadilika kwa rangi ya dawa, kushindwa kufikia viwango vya kemikali vinavyohitajika au kuwepo kwa hitilafu zinazoweza kuhatarisha afya ya watumiaji. Mfamasia wa viwandani katika Hospitali ya Mafunzo, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTTRH), Dkt Lonary Ngetich, anasema dawa zinazotengenezwa Kenya mara nyingi huondolewa sokoni kutokana na hitilafu zinazoonekana kwa macho kama uchafu. Kinyume chake, dawa nyingi za nje huonyesha matatizo ya kemikali yanayoweza kugunduliwa tu kupitia maabara. Anasema hata dawa inayotoka kiwandani ikiwa katika hali nzuri inaweza kuharibika kutokana na joto kali, unyevunyevu au uhifadhi usiofaa wakati wa usafirishaji na usambazaji. Madhara ya dawa hizo kwa wagonjwa yanaweza kuwa makubwa. Dawa zisizo na kiwango sahihi cha kemikali zinaweza kusababisha ugonjwa kuendelea kuenea, viungo vya mwili kutofanya kazi au hata kifo. Aidha, matumizi ya dawa hafifu yanaweza kuongeza tatizo la dawa, ambapo bakteria na vimelea hujenga uwezo dhidi ya dawa. Ingawa PPB ina mifumo ya kupokea ripoti kutoka kwa wahudumu wa afya na wananchi, wataalamu wanaonya kuwa mara nyingi dosari hugunduliwa baada ya wagonjwa tayari kutumia dawa hizo. Ili kudhibiti hali hiyo, serikali inatekeleza Mpango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Dawa Hafifu na Bandia. Mpango huo unalenga kuimarisha usimamizi wa mfumo wa ugavi, kuboresha ufuatiliaji wa soko na kuhakikisha ni dawa salama pekee zinawafikia Wakenya. Kulingana na takwimu za PPB, visa vya dawa zenye kasoro vilivyoripotiwa viliongezeka kutoka 42 mwaka 2021 hadi 85 mwaka 2023 kabla ya kupungua katika miaka iliyofuata. Aidha, bidhaa bandia zilianza kugunduliwa mwaka 2023. Hata hivyo, kiwango halisi cha wagonjwa walioathiriwa na dawa hizo bado hakijabainishwa rasmi.
WADAU wa elimu wanataka riba inayotozwa kwenye mikopo ya wanafunzi ifutiliwe mbali ili kupunguza mzigo wa madeni na kuwarahisishia njia ya kurejesha hela walizokopeshwa. Baraza la Elimu la Waislamu limependekeza kuondolewa kwa kipengele kinachotoza riba katika Mswada wa Ufadhili wa Elimu ya Juu na Vyuo vya Kadri, 2026, unaojadiliwa na Kamati ya Elimu katika Bunge la Kitaifa. Baraza hilo limeitaka Kamati hiyo kufuta Kifungu kinachoweka riba kwenye mikopo, pamoja na kile kinachogusia muda wa kurejesha mikopo. “Aliyekopeshwa arudishe kiasi alichokopa na ikiwa kuna ada ya usimamizi ya kutozwa basi kuwe na mjadala kuhusu kiasi hicho,” akasema Said Abdalla, mwanachama wa baraza hilo. Alikuwa akiongea mbele ya kamati hiyo wakati wa kikao cha kupokea maoni ya umma kilichoongozwa na mbunge wa Mandera Kusini Abdul Haro. Kwa sasa, mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi inatozwa riba ya asilimia nne kwa mwaka kwa deni linalodaiwa, pamoja na ada ya Sh1,000 ya kila mwaka ya kusimamia akaunti ya mikopo. Wanafunzi wengi wanaoomba mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) hutoka familia maskini na hutegemea fedha hizo kugharimia karo, malazi na matumizi ya kila siku. Hadi Juni 2025, idadi ya waliokiuka masharti ya kulipa mikopo ilikuwa 256,000, kabla ya kuongezeka kwa karibu asilimia 50 hadi 380,530 kwa kipindi cha miezi mitano. Wadau wanasema kuondolewa kwa riba kunaweza kuwapa walionufaika nafasi nzuri zaidi ya kurejesha mikopo yao bila mzigo wa madeni kuendelea kuongezeka. Muungano wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET) pia umeeleza wasiwasi kuhusu mfumo unaopendekezwa wa ufadhili, ukisema hazina hiyo haijitegemei. Katibu Mkuu wa KUPPET Akello Misori alisema hali hiyo inaweza kufanya mgao wa kila mwaka usiwe wa uhakika na kuwaacha wanafunzi wanaoendelea na masomo bila fedha za kukamilisha kozi . “Hakuna hakikisho kwamba wanafunzi wanaoendelea na masomo watapata ufadhili hadi watakapokamilisha masomo yao,” akasema Bw Misori. Vuguvugu la Elimu Bora (EBWG) nalo limeitaka serikali kutoa ufadhili kamili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, ikijumuisha karo, malazi, chakula, vifaa vya mafunzona usafiri. Kundi hilo pia limependekeza ufadhili utolewe kupitia ruzuku, ufadhili wa masomo na mikopo, kutegemea mahitaji ya mwanafunzi na aina ya gharama inayohusika. Mwakilishi wa EBWG Mohamed Farah alisema kila mwanafunzi anayekubaliwa katika taasisi ya umma iliyoidhinishwa, anapaswa kupata msaada wa kutosha kugharamia masomo kwa muda wote yuko chuoni. “Ufadhili kamili unamaanisha kugharamia karo, malazi, masomo, usafiri, afya, mafunzo ya kazi, utafiti na gharama nyingine muhimu,” akasema. Mshauri wa sera na mikakati katika EBWG, Boaz Waruku naye alisema Helb inafaa kutoa ruzuku, ufadhili wa masomo au mikopo kulingana na mahitaji ya mwanafunzi.
TABORA: TOBACCO farmers in Tabora have complained that buying companies purchased much of last season’s crop below the official indicative price, leaving many growers facing losses amid rising production costs. The complaints were raised during a one-day Special General Meeting of the Western Tobacco Cooperative Union (WETCU), where farmers from various districts called for stronger…
MISSENYI: Vitendo vya uchomaji moto misitu, mashamba na maeneo ya malisho vimeendelea kuleta hofu na simanzi kwa wawekezaji na wananchi katika Wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera, huku wadau wakihimiza kuongezwa kwa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya uchomaji moto. Mwekezaji wa shamba la kilimo cha kahawa na migomba la Bwikaranyange Investment Ltd, lililopo Kata ya…
SHINYANGA: MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu umetenga na kutumia Sh bilioni 2 kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kurejesha faida kwa jamii (CSR), ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, shule za msingi na sekondari pamoja na Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,…
WADAU wa elimu wanataka mabadiliko makubwa katika Mswada wa Elimu ya Msingi wa 2026, ikiwemo kuimarishwa kwa ushiriki wa wazazi, mfumo wa elimu wa 2-6-3-3 kukitwa katika sheria na serikali kubeba kikamilifu gharama ya elimu ya msingi. Mswada huo unapendekeza kuchukua nafasi ya sheria iliyopo kuhusu elimu ya msingi na unahusu usimamizi wa shule, ufadhili, ustawi wa wanafunzi, walimu, ubora wa elimu na data za elimu. Katika mapendekezo yao kwa Bunge kuhusu miswada ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu, Uteuzi na Ufadhili wa Wanafunzi ya 2026, wadau pia wanataka wazazi wapewe mamlaka zaidi kisheria na mfumo wa usimamizi wa vifaa vya kufunza ufanyiwe mabadiliko. Kundi la Elimu Bora Working Group (EBWG) limehoji sababu za kuwasilisha miswada hiyo kabla ya sera mpya ya kitaifa ya elimu kuidhinishwa. Kundi hilo linataka mfumo wa 2-6-3-3 — miaka miwili ya elimu ya chekechea, sita ya msingi, mitatu ya sekondari msingi na mitatu ya sekondari pevu — uwekwe wazi kwenye sheria. Linasema kuacha mfumo huo uamuliwe kupitia kanuni kunaweza kupatia serikali ijayo nafasi ya kubadilisha mfumo wa elimu bila kuhitaji sheria mpya. EBWG pia inataka vigezo vya kuwaweka wanafunzi katika mikondo ya shule ya upili viwekwe wazi, ikiwemo matokeo, maslahi, uwezo na hatua za kuwasaidia wanafunzi kutoka makundi yaliyotengwa. Kuhusu ufadhili, kundi hilo linataka serikali iwajibike kikamilifu kugharamia miundomsingi, vifaa vya kufunza, chakula, usafi na mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu. Linasema mianya inayoruhusu shule kutoza “ada za ziada” inaweza kutumiwa kurejesha ada kwa jina jingine. Chama cha Kitaifa cha Wazazi (NPA) nacho kinataka kitambuliwe kikamilifu kisheria na kupewa uwezo wa kumiliki mali, kuajiri wafanyakazi, kuendesha akaunti na kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake. NPA pia kinataka miundo yake ya uwakilishi kuanzia shuleni hadi kitaifa ihifadhiwe na neno PTA libadilishwe kuwa Parents Associations. Shirika la Education Stakeholders Association of Kenya (ESAK) limependekeza pia lipewe nafasi ya kuteua mwakilishi katika kila Bodi kati ya 47 za Elimu za Kaunti. ESAK linasema wadau wengi wa elimu wameachwa nje ya bodi hizo licha ya kuwa na mchango muhimu katika usimamizi wa elimu ya msingi. Kuhusu elimu ya juu, EBWG inataka serikali iwafadhili kikamilifu wanafunzi na wanafunzi wa mafunzo ya ufundi, huku ufadhili huo ukijumuisha karo, malazi, chakula, vifaa, usafiri, afya na utafiti. Pia linataka mikopo, ruzuku, ufadhili wa masomo na basari zitofautishwe wazi na wanafunzi waendelee kupata ufadhili hadi watakapokamilisha masomo yao.
DODOMA: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima, amewataka wanawake kutafuta elimu na kujiimarisha kiuchumi, ili waweze kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika familia na malezi ya watoto. Dk Gwajima amesema wanawake wanapaswa kuweka mkazo katika kupata elimu na kujenga uwezo wa kiuchumi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu…
MWANZA; Serikali imeongeza bajeti ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu hadi Sh 1.06 trilioni kwa mwaka wa masomo 2026/2027, fedha zinazotarajiwa kuwezesha wanafunzi wasiopungua 292,463. Hayo yamesemwa leo Septemba 23 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dk Bill Kiwia, wakati akizungumza katika kikao…
DAR ES SALAAM: Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sant’Anna School of Advanced Studies (Scuola) cha Italia, kinaendesha mafunzo maalumu kwa Mahakimu Wakazi na Waendesha Mashtaka kwa lengo la kuwaongezea uwezo wa kushughulikia kwa ufanisi mashauri ya uhalifu unaohusu wanyamapori na maliasili. Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa…
LINDI; Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwa karibu na wajasiriamali wadogo nchini kwa kutoa elimu kuhusu viwango na ubora wa bidhaa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kuzalisha bidhaa salama, zenye ubora na zinazoweza kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi. TBS imetoa elimu hiyo katika Maonesho ya Madini na Fursa…
DAR ES SALAAM: THE National Examinations Council of Tanzania (NECTA) has announced that pupils currently in Standard Five and Standard Six will complete primary education in 2027 under changes being implemented in line with the country’s revised education framework. According to a statement issued by NECTA, the changes are being implemented in accordance with the…
KATAVI; Udumavu kwa watoto mkoani Katavi hauchangiwi na sababu moja pekee. Ushahidi kutoka kwa wazazi, wataalamu wa afya na viongozi unaonesha mchanganyiko wa hali ya kiuchumi ya kaya, uelewa wa lishe, namna chakula kinachozalishwa kinavyotumika, pamoja na imani na mitazamo kuhusu chakula na malezi ya watoto. Kwa mujibu wa Tanzania Demographic and Health Survey and…
BAADHI huchukulia kuumwa na tumbo mara kwa mara, kupata kiungulia, tumbo kujaa gesi au kushiba haraka kama jambo la kawaida tu. Matatizo kama hayo yanapotokea, mtu atakimbia katika duka la kuuza dawa na kununua tembe mbili au tatu ili kutuliza mambo.Lakini baada ya muda, maumivu yanarudi. Kwa wengine, hali hii inaweza kuendelea kwa miezi bila mtu kufikiria kwamba huenda kuna tatizo kubwa zaidi. Hii ni moja ya sababu zinazofanya saratani ya tumbo kugunduliwa ikiwa imefika hatua hatari, wataalamu wa afya wanaonya. Dkt Joseph Abuodha, mtaalam wa saratani katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, anasema tatizo kubwa ni kuchelewa kwa utambuzi. “Swali kubwa ni kwa nini idadi ya vifo iwe kubwa hivi? Ni kwa sababu tatizo hugunduliwa ikiwa imechelewa,” anasema. Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) zinaonyesha kuwa vifo vinavyokadiriwa kutokana na saratani ya tumbo duniani viliongezeka kutoka 642,000 mwaka 2024 hadi 654,000 mwaka 2025. Wanaume ndio waathiriwa wakubwa wa aina hiyo ya saratani huku vifo miongoni mwao vikiongezeka kutoka 419,000 hadi 426,000 katika kipindi hicho. Nchini Kenya, vifo vinavyohusishwa na saratani hii miongoni mwa wanaume viliongezeka kutoka 565 mwaka 2024 hadi 586 mwaka 2025, huku vile vya wanawake vikiongezeka kutoka 488 hadi 505. Dalili zinazoweza kupuuzwa Kinachofanya saratani ya tumbo kuwa ngumu kugundua mapema ni kwamba dalili zake za mwanzo zinaweza kufanana na matatizo ya kawaida ya tumbo. Mtu anaweza kuhisi maumivu au usumbufu tumboni, tumbo kujaa gesi, kiungulia, gesi nyingi au dalili anazozihusisha na vidonda vya tumbo. “Unaweza kuwa na maumivu ya tumbo, tumbo kujaa au dalili kama za vidonda vya tumbo. Pia kunaweza kuwa na asidi nyingi tumboni,” anasema Dkt Abuodha. Hii ndiyo sababu mtu anaweza kutumia dawa za kupunguza asidi au kutibiwa bila kufikiria zaidi. Tatizo ni pale dalili zinapoendelea kurudi licha ya matibabu. Dkt Abuodha anasema wagonjwa wengi wanaofika hospitalini wakiwa tayari wamegunduliwa kuwa na saratani huwa waliwahi kufika hospitalini hapo awali. “Mara nyingi tunakuta wagonjwa waliokuja kwetu na kupatikana wanaugua saratani ya tumbo waliwahi kufika hospitalini kwa wakati fulani kwa sababu ya tatizo hilo,” anasema. Kwa hiyo, si kila maumivu ya tumbo yanamaanisha mtu ana saratani. Hata hivyo, daktari huyo anasema kuwa maumivu yanayodumu, kubadilika au kurudi mara kwa mara hayafai kupuuzwa. Dalili nyingine ambayo watu wengi wanaweza kuipuuza ni kushiba haraka. Kwa mfano, mtu ambaye alikuwa akila sahani nzima ya ugali, nyama na mboga bila shida anaweza kuanza kushiba baada ya kula nusu ya chakula alichopakuliwa. “Ukiwa ulikuwa unaweza kula sahani nzima ya ugali miezi sita iliyopita lakini sasa unashiba baada ya kula kidogo, huenda ni kwa sababu tumbo haliwezi kutekeleza wajibu wake kama kawaida,” anaeleza Dkt Abuodha. Hali hii inaweza kuambatana na kupungua uzito bila mtu kukusudia. Mtu anaweza kuendelea kula lakini mwili ukaendelea kupungua uzito. Dalili nyingine inayopaswa kuangaliwa ni kinyesi kuwa cheusi, hali ambayo inaweza kuashiria kutokwa na damu tumboni. Kutapika damu au kuona damu kwenye kinyesi pia kunahitaji mtu kutafuta matibabu haraka. Kwa mtu anayesumbuliwa na kiungulia au vidonda vya tumbo, huenda matibabu ya kawaida yakasaidia. Lakini ikiwa dalili zinaendelea licha ya matibabu yanayofaa, Dkt Abuodha anasema ni wakati wa uchunguzi zaidi. “Baada ya vipindi kadhaa vya matibabu, ikiwa hujapona, unahitaji kufanyiwa vipimo vinavyojulikana kama endoscopy,” anasema. Vipimo hivyo humwezesha daktari kuangalia ndani ya tumbo kwa kutumia kifaa maalumu. Ikiwa kuna sehemu inayotia shaka, sampuli ya tishu inaweza kuchukuliwa na kufanyiwa uchunguzi kwenye maabara. Uchunguzi huo wa tishu, unaojulikana kama histology, ndio njia muhimu zaidi ya kuthibitisha saratani ya tumbo. Vipimo vingine kama CT scan au PET scan hutumika zaidi baada ya saratani kuthibitishwa ili kujua imeenea kwa kiwango gani na kusaidia kupanga matibabu. Jambo jingine linalofanya saratani ya tumbo kuwa hatari ni kwamba katika hatua zake za mwanzo huenda mtu asiwe na dalili zozote zinazoonekana. Mtu anaweza kuwa na tatizo la hapa na pale tumboni na baadaye kuwa sawa. Katika baadhi ya visa, saratani hugunduliwa kwa bahati wakati mtu anafanyiwa kipimo kingine. Kwa mfano, mtu anaweza kufanyiwa CT scan kutokana na maumivu ya tumbo na daktari akaona mabadiliko kwenye tumbo yanayohitaji uchunguzi zaidi. Dkt Abuodha anaeleza kuwa eneo ambalo saratani imejitokeza pia huathiri dalili. Tumbo lina sehemu ya juu ambako chakula huingia kutoka kwenye umio na sehemu ya chini ambako chakula hupita kuelekea kwenye utumbo. Saratani ikijitokeza karibu na mojawapo ya sehemu hizi, hata uvimbe mdogo unaweza kuzuia chakula kupita vizuri. Mtu anaweza kuhisi kama chakula kimekwama au hakipiti vizuri. Lakini saratani inapokuwa katikati ya tumbo, dalili za mwanzo zinaweza kuwa za kawaida zaidi kama kujaa tumbo, kiungulia na maumivu yasiyo makali. Maambukizi ya muda mrefu ya bakteria aina ya H. pylori ni miongoni mwa mambo yanayohusishwa na baadhi ya aina za saratani ya tumbo. Watu walio na vidonda vya muda mrefu wanapaswa kufuatiliwa kulingana na hali zao. Dkt Abuodha anasema mtu ambaye dalili zake zimebadilika au amepata tatizo jipya anapaswa kurudi hospitalini. “Changamoto ni kutambua wakati dalili za kawaida zimechukua muda mrefu na zinahitaji uchunguzi zaidi,” anasema. Umri pia ni sababu muhimu “Kadri mtu anavyozidi kuzeeka, ndivyo uwezekano wa kupata ugonjwa huu unavyoongezeka,” anasema. Uvutaji sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi pia umehusishwa na hatari ya saratani ya tumbo. Daktari pia anashauri watu kuwa waangalifu kuhusu tabia za ulaji, hasa vyakula vinavyosababisha usumbufu wa tumbo vinapoliwa mara kwa mara. Hata hivyo, si kila mtu anayepata saratani ya tumbo huwa na historia ya familia ya ugonjwa huo. Dkt Abuodha anasema chini ya asilimia tano ya visa vinaweza kuhusishwa moja kwa moja na sababu za kijenetiki. Kwa nini wanaume wanaathirika zaidi? Kwa ujumla, wanaume huathirika zaidi na saratani ya tumbo kuliko wanawake. Dkt Abuodha anasema takriban wanaume wawili hupata saratani hii kwa kila mwanamke mmoja. Anaeleza kuwa wanaume wanaweza kuwa na baadhi ya vihatarishi zaidi, huku pia wakichelewa kutafuta huduma za afya wanapopata dalili. “Wanaume wanapopata maumivu, si rahisi kwao kutafuta huduma za afya,” anasema. Hii inaweza kufanya ugonjwa ugunduliwe ukiwa umechelewa. Ingawa mtu anapaswa kuwajibika kwa afya yake, kuchelewa kugundua saratani haimaanishi kila mara kuwa ni sababu ya mgonjwa kupuuza dalili. Kuna pia changamoto katika mfumo wa afya Baadhi ya wagonjwa wanaweza kuchelewa kupewa rufaa au kutumwa kwa mtaalamu anayefaa, huku gharama na upatikanaji wa vipimo kama endoscopy ukiwa kikwazo kwa wengine. Dkt Abuodha anasema wagonjwa walio na dalili zinazotia shaka wanapaswa kuelekezwa upesi kwa mtaalam ili uchunguzi unaofaa ufanywe. Anashauri kula chakula kilichopikwa vizuri, kupunguza vyakula vilivyosindikwa na kuzingatia ubora wa chakula badala ya wingi pekee. Mazoezi ya mwili na kudhibiti uzito pia ni muhimu kwa afya kwa ujumla. Anashauri pia kupunguza au kuacha kabisa uvutaji sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi. Kwa mtu anayepata usumbufu baada ya kula vyakula vyenye viungo vingi au vyakula vya moto sana, ni vyema kuwa mwangalifu na kutafuta ushauri wa daktari ikiwa hali hiyo inaendelea. Muhimu zaidi, anasema mtu anayesumbuliwa na dalili za tumbo kwa muda mrefu hapaswi kujitibu.
ARUSHA: MORE than 400 children took part in the third Elimu Yetu Bonanza in Arusha, an initiative aimed at identifying, nurturing and promoting young sporting talent by providing street-based players with a platform to develop their skills and pursue opportunities at regional, national and international levels. The annual event, organised by Elimu Yetu Development Organisation,…
Amos Kasaramba is the Director of Elimu Yetu Development Organization, which organizes the annual youth recruitment sports bonanza said for the first time also the traditional board game, known as Bao, which is largely played by elderly persons has been included.
IRINGA: JUMLA ya wanafunzi 873 na walimu 43 wa shule ya Sekondari Kalenga iliyopo katika katika Halmashauri ya Iringa wanatarajiwa kunufaika baada ya kampuni ya Helios Towers kuzindua maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shule hiyo. Mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 30 umezinduliwa katika shule hiyo leo, Septemba 15,…
DAR ES SALAAM: Msafara wa Baiskeli wa Nyerere Cycling Tour mwaka huu unatarajiwa kutoa madawati 1,000 kwa shule 10, kukarabati madarasa 40 na kujenga madarasa mapya 10, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini. Msafara huo wenye urefu wa kilomita 1,500 hadi Butiama, utafanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 14,…
HakiElimu Executive Director Mary Ndaro urged the fellows to use the programme to build the confidence, networks and skills needed to participate meaningfully in national affairs.