CAG: Bajeti ndogo imezorotesha kukuza utalii

DODOMA — Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebainisha dosari kubwa katika utekelezaji…
The post CAG: Bajeti ndogo imezorotesha kukuza utalii appeared first on HabariLeo.
DODOMA — Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebainisha dosari kubwa katika utekelezaji wa mipango ya kukuza utalii nchini Tanzania.
Ingawa sekta ya utalii inachukuliwa kama mhimili muhimu wa uchumi wa taifa, Bodi ya Utalii Tanzania ilipokea asilimia 69 tu ya bajeti yake ya mwaka 2023/24, hali iliyosababisha kutoshiriki kwenye maonesho zaidi ya nusu yaliyopangwa—fursa ambazo zingekuwa chachu ya kuongeza watalii na mapato ya serikali.
CAG anataja kuwa kati ya maonesho 212 yaliyopangwa, ni 103 tu (asilimia 48) yaliyofanyika. Hii ni ishara kuwa mikakati imewekwa vizuri kwenye makaratasi lakini utekelezaji wake unakwamishwa na ukosefu wa fedha—kinyume na dhamira ya kitaifa ya kukuza sekta hii muhimu.
Aidha, changamoto ya mtandao wa intaneti katika hifadhi za taifa kama Serengeti, Mikumi na Saadani imeibuliwa kama kikwazo kingine kikubwa. Ucheleweshaji wa kuwasiliana, kutotoa vibali kwa wakati, na taswira mbaya kwa watalii wa kimataifa, yote haya yanapunguza ushindani wa Tanzania katika soko la utalii la dunia.
CAG anashauri Bodi ya Utalii na TANAPA kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha zinatolewa kwa wakati. Serikali ikiwa makini, inaweza kuongeza mara dufu mapato ya utalii ndani ya miaka mitano. Vinginevyo, tutabaki kusubiri watalii bila kuwaonesha ni kwa nini waje Tanzania.
The post CAG: Bajeti ndogo imezorotesha kukuza utalii appeared first on HabariLeo.