Tanzania mwenyeji tuzo za World Travel

Habari Leo
Published: Apr 14, 2025 13:08:35 EAT   |  Travel

TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa tuzo za kimataifa za utalii ‘World Travel’ na hafla ya kutangaza washindi wa…

The post Tanzania mwenyeji tuzo za World Travel appeared first on HabariLeo.

TANZANIA imechaguliwa kuwa mwenyeji wa tuzo za kimataifa za utalii ‘World Travel’ na hafla ya kutangaza washindi wa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi itakayofanyika Juni 28, 2025 Dar es Salaam chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Aprili 14,2025, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Ephraim Mafuru amesema tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1993 na Kampuni ya World Luxury Media Group kwa lengo la kutambua, kuthamini na kusherehekea mchango wa wadau katika sekta ya Utalii na Ukarimu duniani.

Amesema wadau wanaotambuliwa ni mashirika ya ndege, watoa huduma za malazi, vivutio vya utalii, wakala wa biashara za utalii, vivutio vya utaliii, mamlaka za usimamizi na utangazaji wa utaliima wadau wengine na zimekuwa chachu ya ubunifu, ushindani na kuboresha viwango vya huduma.

“Heshima hii ya kuwa mwenyeji wa tuzo hizi ni matokeo ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake wa kutangaza sekta ya utalii,”amesema.

Amewahimiza Watanzania kushiriki kikamilifu kupigia kura vivutio hivyo ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia na kuweza kuwapokea wageni kutoka zaidi ya nchi 30 wanaotarajiwa kushiriki wakiwemo wawekezaji, wanahabari wa kimataifa na wadau mbalimbali.

Mafuru amesema Tanzania imetajwa katika vipengele zaidi ya 15 ikiwemo nchi inayoongoza kwa Utalii Afrika, Bodi bora ya Utalii Afrika, Bodi ya Utalii Tanzania, Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika Ngorongoro, Mlima unaoongoza Afrika – Mlima Kilimanjaro.

Pia, Hifadhi Bora ya Taifa Barani Afrika Serengeti. Hifadhi za Kitulo, Nyerere, Udzungwa, Mahale, Arusha Tarangire na nyingine zimetajwa katika vipengele vingine kulingana na ubora wake, Uwanja Bora wa Ndege Barani Afrika – Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bandari Bora Barani Afrika Bandari ya Dar es Salaam, Fukwe Bora Africa: Zanzibar.

“Hivyo ni baadhi tu ya vipengele ambayo vivutio vyetu vimetajwa pia kampuni za watoa huduma za usafiri, malazi na waongoza watalii nchini nazo zimetajwa katika makundi ya tuzo hizi,”amesema.

The post Tanzania mwenyeji tuzo za World Travel appeared first on HabariLeo.