UCHUNGUZI kuhusu ajali ya helikopta ya uokoaji iliyotokea katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) umeanza kwa lengo la kubaini chanzo cha ajali hiyo iliyotokea juzi na kusababisha vifo vya watu watano. The post Uchunguzi waanza helikopta iliyoua watano Kilimanjaro first appeared on HabariLeo.
MWAKA unapoelekea kuisha, msisimko wa sherehe unaendelea kutanda kote nchini wengi wakilazimika kujimudu licha ya uchumi mgumu, hali ya anga isiyotabirika pamoja na ubabe wa kisiasa. Maelfu ya Wakenya wamechagua kudumisha desturi ya kujiunga na jamaa zao vijijini kwa sikukuu kama miaka ya nyuma japo mara hii hali ngumu ya maisha inaonekana kuwalemea wengi. Magharibi, eneo ambalo yamkini ndilo linalokumbatia sana sikukuu ya Krisimasi kwa Wakenya, aghalabu hushuhudia ongezeko la wasafiri wenye hamu ya kuungana na familia zao. Kamishina wa Eneo la Nyanza Flora Mworoa, alisema vikosi vya usalama vimeshirikiana na Shirika la Wanyamapori (KWS) kuimarisha usalama katika sekta ya utalii. Vikosi vya usalama vilevile vinashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) kuhakikisha madereva wanazingatia sheria za trafiki ili kuzuia ajali. Kulingana na ripoti iliyotolewa majuzi na Huduma ya Polisi nchini, sehemu hatari Magharibi mwa Kenya zinajumuisha barabara za Mbale–Vihiga, Kakamega–Chavakali, Kakamega–Kisumu–Ilesi, Museno, Kakamega–Mumias Road, Makunga, na barabara kuu ya Kakamega–Webuye–Lubao. Eneo la Nyanza itabidi usalama umakinikiwe zaidi barabara za Awasi–Ahero Kiboswa–Kisumu, Oyugis–Kisumu, Migori–Kakrao, Makutano ya Daraja Mbili–Bondo na barabara ya Oyugis–Katitu. Jiji la Kisumu limeweka kando usingizi na kugeuka sherehe waziwazi ambapo muziki unafuatana na baruti hewani huku kila jioni ikiahidi kumbukumbu mpya za ngoma ambazo wakazi wanaita “sherehe baada ya sherehe (party after party).” Katika eneo la Pwani, wamiliki hoteli walikiri kupokea zaidi ya asilimia 80 ya wageni katika majengo yao, wakitumai kwamba idadi hiyo itafikia asilimia 90–100 kufikia Krismasi na Mwaka Mpya. Msimamizi wa Hoteli ya Malindi Ocean Beach Resort and Spa, Maureen Obunga, alisema karibu nusu ya wageni inajumuisha Wakenya kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Mkuu wa Majeshi, Charles Kahariri alizuru Msitu wa Boni, Lamu, kushiriki tamasha za mapema za Krismasi na Mwaka mpya huku wanajeshi wakitumwa kukabiliana na magaidi wa Al-Shabaab. Doria za kiusalama zimezidishwa Bonde la Ufa huku Kamanda wa eneo hilo, Dkt Abdi Hassan, akiwahimiza waendeshaji magari kuzingatia sheria za usalama barabarani. Hoteli kubwa kadhaa Naivasha na Nakuru zimeandikisha idadi kubwa ya wageni kabla ya Krismasi zikiripoti takriban asilimia 96, Naivasha, na kati ya asilimia 80-90, Nakuru. “Tunatarajia biashara bora zaidi ikilinganishwa na mwaka jana, na hicho ni kitu tunajivunia,” alisema Mwenyekiti wa Muungano wa Utalii Nakuru, David Mwangi.
HANGZHOU, China TUKIO la kushangaza na la aibu lilishuhudiwa katika mji huu baada ya jombi kunaswa kwenye video akining’inia kwenye roshani ya hoteli akiwa amevaa boksa pekee. Inasemekana mwanaume huyo alikuwa akijaribu kutoroka kupitia dirisha ili asionekane baada ya kudaiwa kufumaniwa akila uroda chumbani na mke wa mtu. Walioshuhudia walisema mwanaume huyo aliteleza na kujikuta akining’inia juu ya roshani ya hoteli, akishindwa kupanda wala kushuka. Video za tukio hilo zilisambaa kwa kasi mitandaoni na kusababisha kicheko na kejeli kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Hatimaye, maafisa wa zimamoto waliingilia kati na kumshusha salama. Polisi walisema hakuna aliyekamatwa, lakini tukio hilo limeacha maswali mengi kuhusu uhusiano wa siri na maamuzi hatari yanayochukuliwa baada ya kufumaniwa katika michepuko.
WAGENI wanaozuru maeneo ya Pwani kwa ajili ya likizo za Desemba wametakiwa kufuata masharti ya kiusalama ufukweni ili kuepusha majanga. Wakuu wa usalama wamesisitiza hitaji la kila mmoja kuheshimu kanuni ya kuondoka baharini ifikapo saa kumi na mbili jioni, ambayo huwa ni hatua ya kudhibiti visa vya ukosefu wa usalama na watu kuzama majini. Katika Kaunti ya Kilifi, Kamishna wa Kaunti, Bw David Wanyonyi, alionya kuwa, mawimbi ya bahari huwa makali zaidi na yasiyotabirika wakati wa usiku, hali inayowaweka hatarini watu wanaotembelea fukwe. Aliongeza kuwa, kufungwa kwa fukwe mapema kutasaidia pia kuwalinda wakazi dhidi ya vitendo vya uhalifu ambavyo hutokea kutokana na mikusanyiko mikubwa ya watu. Huko Mombasa, Kamishna wa Kaunti, Mohamed Noor, alisema kikosi cha Shirika la Kuhifadhi Wanyamapori nchini (KWS) kimetumwa kusaidia Polisi wa Utalii na Machifu ili kuhakikisha usalama wa watu wanaotembelea fukwe. “Saa kumi na mbili jioni, tutapiga filimbi kuhakikisha waogeleaji wote wanatoka ufukweni. Hatutaki mtu yeyote azame baharini au kujeruhiwa. Tumezielekeza pia hoteli kuhakikisha zina waokoaji wa majini, ili kuhakikisha hakuna anayefariki au kujeruhiwa kwenye mabwawa ya kuogelea,” akasema Bw Noor. Vilevile, Bw Noor alisema usalama umeimarishwa katika maeneo yote ya Mombasa, ambayo inashuhudia ongezeko la watalii wa ndani na wa kimataifa. Kamishna huyo aliwapongeza maafisa wa polisi kwa kuwakamata washukiwa 36 wa uhalifu katika Kaunti Ndogo ya Kisauni mapema Ijumaa asubuhi. “Tutaendelea kukaza kamba ili kuhakikisha hakuna mtu atakayejitokeza kuwahangaisha watu hapa Mombasa, si wageni pekee bali hata wakazi,” alihakikisha. Gavana wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro, aliitaka serikali ya kitaifa kuharakisha upanuzi wa barabara ya Mombasa–Malindi na Uwanja wa Ndege wa Malindi ili kuvutia watalii zaidi katika kaunti hiyo. “Mwaka jana pekee, Kilifi ilipokea zaidi ya watalii 500,000 wa ndani na wa kimataifa, idadi inayozidi wakazi wa miji ya Malindi na Kilifi. Hili ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na idadi ya watalii waliorekodiwa mwaka uliotangulia,” alisema. Aliongeza kuwa, kaunti hiyo inaibuka kama kitovu bora cha utalii wa mikutano, na asilimia 40 ya watalii waliotembelea kaunti hiyo walikuja kwa ajili ya mikutano. Wote walikuwa wakizungumza wakati wa sherehe za Jamhuri katika kaunti zao. Kwingineko, Kamanda wa Polisi wa Trafiki eneo la Pwani, Bw George Kashimiri, alisema idadi ya maafisa wa trafiki imeongezwa barabarani ili kuimarisha utekelezaji wa sheria. Alisema alama za barabarani zinazoonyesha kiwango cha mwendo kinachoruhusiwa zimeekwa jijini Mombasa, na yeyote atakayepitisha viwango vinavyohitajika atakamatwa. “Sheria hii inawahusu madereva wa magari yote. Kwa kuwa idadi ya wageni inaongezeka, tumepeleka maafisa wa ziada. Katika maeneo yenye taa za trafiki tumepunguza idadi ya polisi na kuwapeleka katika maeneo yasiyo na taa. Tuna maafisa wa kutosha kusimamia Mombasa nzima. Pia tumeanza kutumia kifaa cha kupima kiwango cha ulevi wa pombe (Alco-blow) na tutaendelea nacho katika msimu wote wa sherehe,” alieleza. Afisa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama na Uchukuzi (NTSA), Bw Douglas Nyagwoka, alisema wiki iliyopita, madereva 23 wa mabasi ya kampuni moja Mombasa walisimamishwa kazi kwa kuendesha kwa kasi, na vifaa vyao vya kudhibiti mwendo vilisaidia maafisa husika kuwafuatilia. “Kampeni hii itasaidia pakubwa. Magari yasiyo na vifaa vya kudhibiti mwendo huwa na athari kubwa zaidi yanapopata ajali. Pia tunafanya kazi na polisi wa trafiki kukabiliana na mwendo kasi katika eneo la Dongo Kundu,” akasema. Naibu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Matatu Salim Bates, aliwataka waendeshaji wa vyombo vya usafiri wa umma kuwa waangalifu na kuwasihi wasimamizi wa sekta hiyo kuimarisha usimamizi.
KILIMANJARO: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande amewataka wahitimu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, kuzingatia uadilifu, uzalendo na unyenyekevu wakati wa kuhudumia wananchi na kulinda rasilimali za wanyamapori. Lengo kuongeza thamani katika maendeleo ya ukuaji wa sekta ya utalii kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla. Chande ametoa wito … The post Chande awafunda wahitimu chuo cha wanyamapori first appeared on HabariLeo.
MBUNGE wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Dk Yannick Ndoinyo ameahidi kufuatilia kujua kwa nini mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6 unasuasua kukamilika kwa zaidi ya miaka saba sasa. Ndoinyo amekutana na kilio cha wakazi wa jimbo hilo maeneo ya Yasi, Mdito, Olorien, Magaiduru, Tinaga, Ngarwa, Mgongo na Mageri katika … The post Kero ya maji yamkera Mbunge Ngorongoro first appeared on HabariLeo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuongeza ushirikiano ili Zanzibar na Tanzania kunufaika zaidi na tuzo na fursa za kimataifa. The post Rais Mwinyi apokea Tuzo ‘Africa’s Best Corporate Retreat 2025’ first appeared on HabariLeo.
MOROGORO: John Jackson, a Tanzanian living abroad, decided to make the most of his vacation back home by heading to the iconic Mikumi National Park because nothing beats reconnecting with the wild beauty of Tanzania. While exploring the park, he struck up conversations with fellow travelers, and their feedback was powerful and consistent. Tanzania is … The post Tanzania: A safari destination that captures hearts and calls you back first appeared on Daily News.
ARUSHA: NGORONGORO Conservation has proudly celebrated the 64th anniversary of Tanzania’s independence with pride as one of the country’s pillars of tourism. The Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) Commissioner, Mr Abdul-Razaq Badru, hailed the Conservation Area’s commitment in maintaining its status as one of the world’s most significant sites for conservation and tourism. Delivering his Independence … The post Ngorongoro proudly preserves its pride as it marks 64 years of independence first appeared on Daily News.
WENGI hawajui thamani ya vifuu vya nazi. Vifuu hivyo, mara nyingi huchukuliwa na wengi kama taka zinazochafua mazingira. Hata hivyo, MacDonald Ngala, 36, kutoka eneo la Mariakani, Kilifi, huvitumia vifuu hivyo pamoja na sehemu nyinginezo za nazi kuzitengeneza bidhaa zenye thamani. Huzitengeneza bidhaa kama vile maua ya kurembesha maskani, mbali na bidhaa nyinginezo kutokana na vifuu hivyo, na kuwauzia wateja kutoka maeneo mbalimbali katika eneo la Pwani ya Kenya. Hutengeneza kobe, maua, samaki, glasi za kunywea mvinyo, vikombe, majagi, vifaa vya kuweka sabuni, na kadhalika. [caption id="attachment_181816" align="alignnone" width="1920"] MacDonald akionyesha bidhaa anazozitengeneza katika eneo la Mariakani. PICHA/PETER CHANGTOEK[/caption] Anadokeza kuwa, amekuwa akizitengeneza bidhaa hizo kwa muda wa miaka minne. “Siku moja nilipata vifuu vya nazi vikiwa vimetupwa na vimeliwa na mchwa. Nikachukua; nikaangalia, nikaona vimeliwa na mchwa hadi vimebakishwa, nikaona hicho ni kitu kigumu sana,” asema MacDonald. Anaongeza kuwa, baada ya kuvitazama vifuu hivyo kwa muda, akawa na shauku moyoni ya kutengeneza bidhaa kutokana navyo. “Nimegundua kuwa, kumbe huu mti wa mnazi una thamani kubwa,” asema, akiongeza kuwa, alianza kuvitengeneza viti vya ajabu kutokana sehemu fulani ya minazi, kisha akaanza kuvitumia vifuu kuvitengeneza vipuli. Alipoanza kuzitengeneza bidhaa zake, watu walikuwa wakienda kuziangalia tu, na hawakuwa wakizinunua, ikabidi ahamishe shughuli hiyo hadi eneo jingine lililoko mjini Mariakani. “Kuna shirika fulani ambalo lilikuwa limenichukua katika maonyesho katika Uga wa Mkomani. Liliona kuwa ninaongeza thamani kwa mti wa mnazi. Nikaona kuwa kumbe kifuu kinatengeneza makaa na kuna mafuta ambayo yanatengenezwa kutoka kwa nazi. Nilikuwa nikitumia nazi vibaya kwa sababu nilikuwa nikinunua nazi halafu ninakata na kuwagawia watu,” asema. Anaongeza kwamba kuna mashine ambayo anahitajika kuwa nayo ili kuanza kuzitumia nazi kuyatengeneza mafuta. “Nazi moja inaweza kutengeneza pesa nyingi sana,” asema MacDonald, akiongeza kuwa, hupata malighafi kutoka sehemu tofauti tofauti, kama vile katika hoteli na kutoka kwa watu binafsi, ambapo hununua kwa bei nafuu. [caption id="attachment_181815" align="alignnone" width="1920"] Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na MacDonald. PICHA/PETER CHANGTOEK[/caption] Anafichua kuwa alikisoma kitabu kilichoandikwa na Irene Mureithi kinachoitwa Celebrate the Hard Times kilichomtia moyo, ndiposa akaamua kukitumia kipaji chake vyema kuzitengeneza bidhaa aina ainati kutokana na sehemu tofauti tofauti za mnazi. “Niligundua kuwa, ukitambua kipawa chako, mambo huwa rahisi kuliko kukaa. Nikawa ninafunza shule fulani wanafunzi jinsi ya kugundua talanta zao. Nikasoma kitabu kingine cha Robert Asewe kutoka Uganda,” asema, akiongeza kuwa baada ya kuvisoma vitabu hivyo, akawa na motisha zaidi. Huuza bidhaa zake kwa bei tofauti tofauti. “Huuza yale maua meupe kwa Sh2,000, kila moja, la njano ni Sh1,800, na kuna yale ya Sh1,500. Huuza jozi moja ya vipuli kwa Sh200,” afichua MacDonald, ambaye pia huuza mkufu mmoja kwa Sh350, na bangili kwa Sh250 kila moja.
NGORONGORO: A newlywed couple, Sebastien and Pauline, have fulfilled their longtime dream by picking Tanzania for their honeymoon. The couple who always desired to go on a safari in Tanzania killed two birds with one stone by turning the trip into both a tour of the country and a honeymoon to celebrate their two-month-old marriage. … The post Ngorongoro spellbinds French-Canadian honeymoon first appeared on Daily News.
KATAVI; Watu watatu wamekamatwa na askari wa maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo haramu cha bangi ndani ya eneo la hifadhi ya misitu ya Kijiji cha Kapanga. Watuhumiwa hao wawili ni wanaume na mmoja ni bibi mwenye umri wa miaka 65, lakini majina yao hayakutajwa kwa … The post Bibi matatani kilimo cha bangi first appeared on HabariLeo.
SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuongeza nguvu katika utafiti na masoko ya bidhaa za utalii ili kufikia lengo la kuileta Tanzania kwenye idadi ya watalii milioni nane, kama ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030. The post Dk. Kijaji: Boresheni Masoko ya Utalii first appeared on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: ILI kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka nchini na kufikia milioni nane kwa miaka mitano, Bodi ya Utalii Tanzania imetakiwa kutumia fursa ya Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya Mataifa Afrika (AFCON 2027) ili kujitangaza zaidi na kuongeza idadi ya watalii nchini. Agizo hilo limetolewa leo Novemba 26, 2025 na Waziri wa Maliasili … The post ‘TTB tumieni AFCON 2027 kuongeza watalii’ first appeared on HabariLeo.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amefanya ukaguzi wa ukarabati mkubwa unaoendelea katika Hoteli ya Mikumi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, hatua inayolenga kuongeza viwango vya huduma za utalii na ushindani wa hifadhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi. The post Dk. Kijaji aagiza ukarabati wa Hoteli Mikumi first appeared on HabariLeo.
MOROGORO: WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji ameagiza Uongozi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuongeza ubunifu wa hali ya juu ili kuchangia kwa kasi kufikia malengo ya Serikali ya kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia milioni 8 ifikapo mwaka 2030. Dk Kijaji ametoa wito huo jijini Morogoro alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya … The post Waziri Kijaji aitaka Tanapa kuongeza ubunifu first appeared on HabariLeo.
SAFARI ya watalii kuelekea Maasai Mara ilikatizwa ghafla jana asubuhi baada ya ndege ndogo ya kampuni ya Mombasa Air Safari, iliyokuwa imebeba abiria 11 akiwemo rubani, kuanguka katika msitu wa Nyando, eneo la Matuga, Kaunti ya Kwale, na kulipuka moto. Ndege hiyo aina ya Caravan, yenye nambari za usajili 5Y-CCA, iliondoka Uwanja wa Ndege wa Diani saa mbili na dakika ishirini na tano asubuhi, ikielekea Kambi ya Kichwa Tembo katika Hifadhi ya Maasai Mara, Kaunti ya Narok. Kambi hiyo ya kifahari ni maarufu kwa mandhari yake mazuri na ukaribu wake na njia za uhamaji wa nyumbu. Abiria waliokuwa wamepanga mapumziko ya kifahari walikuwa ni watalii wanane kutoka Hungary, wawili kutoka Ujerumani, na rubani mmoja Mkenya. Kwa masikitiko, wote waliangamia. Walioshuhudia walisema ajali hiyo ilitokea mvua kubwa ilipokuwa ikinyesha na kusababisha ukungu mzito uliopunguza mwonekano. Bw Hamadi Garashi, mkazi wa eneo hilo, alisema waliposikia mlipuko mkubwa, walikimbia eneo la tukio na kukuta moto mkubwa ukiwaka. “Tuliposikia mlipuko, tulikimbia tukadhani ni radi. Tulipofika, tuliona moto mkubwa na mabaki ya ndege. Tulimjulisha afisa wa kijiji ambaye aliarifu maafisa wengine wa serikali,” alisema Bw Garashi. Mkazi mwingine, Bw Makopa Sazu, alisema hali ya hewa ilikuwa mbaya kiasi kwamba ilikuwa vigumu hata kuona ardhini. “Niliposikia mlio, nilikimbia na kufika eneo la ajali. Nilikuta moto mkubwa na sehemu za miili zikiwa zimezagaa,” alisema. Mvua kubwa ilitatiza juhudi za uokoaji katika kijiji cha Nyando, huku magari ya dharura yakitatizika kufika eneo la ajali kutokana na matope na miinuko eneo hilo. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (KCAA) kupitia Mkurugenzi Mkuu wake, Emile Arao,ilithibitisha ajali hiyo, ikisema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo chake. [caption id="attachment_179915" align="alignnone" width="300"] Ndege iliyobeba watalii baada ya kuanguka na kulipuka. Picha | Kevin Odit.[/caption] Waziri wa Uchukuzi, Davis Chirchir, alisema ndege hiyo ilipoteza mawasiliano ya rada na mnara wa udhibiti wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mombasa muda mfupi kabla ya kuanguka. “Wote waliokuwa kwenye ndege walipoteza maisha. Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege (AAID) imetumwa eneo la tukio kufanya uchunguzi wa kina,” alisema Waziri. Mwenyekiti wa Mombasa Air Safari, Bw John Cleave, alithibitisha kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea Maasai Mara, na kwamba hakuna aliyenusurika. Aliongeza kuwa kampuni hiyo imeunda kikosi kutoa ushauri na kuratibu shughuli za mazishi. Gavana wa Kwale, Bi Fatuma Achani, alituma rambirambi kwa familia za marehemu na kuwaonya madereva kuwa waangalifu wakati huu wa mvua kubwa. Ajali hiyo ilijiri saa chache baada ya watu watano kufariki Jumatatu usiku katika ajali ya barabarani iliyotokea mjini Keroka, mpakani mwa kaunti za Kisii na Nyamira. Ajali hiyo ilihusisha trela lililokuwa lilitoka Nyangusu na waendeshaji wa pikipiki. Kulingana na kamanda wa trafiki wa Masaba Kaskazini Peter Chege, dereva wa trela hiyo anasemekana kukosa kulidhibiti lilipokuwa likiteremka sehemu ya barabara ya Ichuni-Keroka. Baada ya lori hilo kukosa mwelekeo, lilibingiria barabarani na kuwaangukia wanabodaboda watatu walikuwa kando kando mwa barabara wakingoja wateja katika solo Hilo. Mkuu huyo wa trafiki aliongeza kuwa dereva wa trela hiyo naye pia alipoteza maisha yake na mtu mwingine aliyekuwa naye humo ndani. "Inashukiwa kuwa dereva wa trela alishindwa kulidhibiti. Lakini tumeanzisha uchunguzi kujua ni nini kilienda vibaya," Bw Chege aliwambia Taifa Leo kwa simu. Afisa huyo wa polisi aliwataka madereva wa magari kuwa waangalifu wanapoteremka sehemu hiyo ya barabara kwa kuwa ina sifa mbaya ya kusababisha ajali. "Eneo hilo ni hatari. Tunawaomba madereva kuwa waangalifu kila wanapofika eneo hilo haswa wakati huu ambapo tunashuhudia mvua kubwa," Bw Chege alisema. Ajali ya Keroka iliongeza idadi ya ajali za barabarani zilizoshuhudiwa kote nchini wiki hii, ambapo ripoti zinaonyesha kuwa watu 17 wamepoteza maisha katika kipindi cha saa 72
ARUSHA: Mgombea ubunge wa Jimbo la Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yanick Ndoinyo, ametoa wito kwa wananchi wa kata zote 28 za jimbo hilo kuhakikisha wanajitoa kwenda kupiga kura lengo ni kutimiza wajibu wao wa kikatiba. Akizungumza katika kikao cha kufunga kampeni za CCM ngazi ya Wilaya ya Ngorongoro, kilichofanyika katika kata ya Oldonyo … The post Mgombea ubunge Ngorongoro ahamasisha amani kesho first appeared on HabariLeo.
ARUSHA: MSIMAMIZI wa uchaguzi katika Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Emmanuel Mchome amesema katika jimbo hilo waliojiandikisha kupiga kura ni 175,068 Mchome amesema kuwa wapiga kura hao watapiga kura katika vituo 550 vilivyotengwa kwa ajili ya kupiga kura na vituo hivyo vitafunguliwa kuanzia saa 1 asubuhi na vitafungwa majira ya saa 10 jioni. Alisema kutokana … The post Wapiga kura 175, 068 kupiga kura Ngorongoro first appeared on HabariLeo.
DODOMA: Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha (MNRT SACCOS LTD) kilicho chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kimefanikiwa kutoa mikopo kwa wanachama wake zaidi ya Sh bilioni 1.2 kwa mwaka kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na … The post MNRT Saccos yatoa Sh bil 1.2 ya mikopo mwaka mmoja first appeared on HabariLeo.
KARATU: A NEW chapter in Tanzania’s heritage unfolds under the wide skies of Karatu, Arusha. On 16 October 2025, the Vice President of the United Republic of Tanzania, Dr Philip Isdor Mpango, inaugurated the Urithi Geo-Museum, a modern sanctuary that celebrates and preserves the geological and cultural legacy of the Ngorongoro-Lengai UNESCO Global Geopark. This … The post Ngorongoro-Lengai Geopark: Where earth tells its stories first appeared on Daily News.
Sometimes, all it takes for men to bond is a glass of bourbon or a shared passion for a football team. For Italian friends Paolo Paolini and Fabio Santoni, it was their mutual love for hiking that cemented their friendship. When Paolini arrived in Tanzania in August 2024, he discovered that Fabio had already climbed Mount Meru. Soon after, they began planning to conquer Mount Kilimanjaro together. By February 2025, their plan had taken shape, and they contacted a specialist company to organise the climb. Paolini, an active man who keeps himself in good physical form, intensified his training regimen. His preparation included playing football twice a week and paddling every weekend. “The days I didn’t spend on the pitch, I was in the gym, following a specific programme prepared by Nino, one of my elder sons,” he said. Beyond physical readiness, Paolini found mental preparation to be even more crucial. As it is impossible to simulate the high altitude or predict how the body will react at over 4,000 metres above sea level, he said, “Mentally, I was going through different scenarios, focusing on reaching the summit, but none of these scenarios had the option of failure.” Scaling the world’s highest free-standing mountain demands both respect and awareness of the challenge that lies ahead. Paolini was born in Switzerland, and at the age of three, his father placed him on skis and told him to follow. “I grew up near the Swiss Alps and also in my region in Italy—Friuli-Venezia-Giulia, in the north-eastern part close to Austria and Slovenia—which has beautiful landscapes and mountains. I would say that I just love everything that has to do with mountains,” he said. Hiking, to him, is deeply sentimental—it means spending quality time with family and friends. While Kilimanjaro was a significant challenge, Paolini regarded it as a “normal” hike for someone raised among snowy peaks. “To me, hiking means relaxing, enjoying nature, and recovering from the usual stress—and, if possible, rewarding myself with delicious food and an ice-cold beer afterwards,” he added with a laugh. Nevertheless, climbing Kilimanjaro allows no comfort. “No shower, very little contact with family and friends for seven days. But more or less, you are prepared for it,” he noted. For him, the most challenging part was not knowing whether mountain sickness would affect him. “There are many possible symptoms, some of which can be severe,” he said. “Luckily, I only had headaches on the second and third day.” During the final 150-metre stretch from Stella Point to Uhuru Peak, Paolini struggled slightly with shortness of breath, but adrenaline—and the sight of the summit so close—pushed him through the final steps. “I feel blessed and proud to have reached the top of Africa with my buddies, and especially with my son Luis,” he said. He proved to himself that with the right physical and mental preparation, one can go beyond their limits. “But I think, in general, my biggest life challenge is to give a proper education to our children and do everything I can to see them happy,” he reflected. Paolini finds time for holidays whenever schedules align. “It’s all about time management,” he said, adding that compromises with his wife and family make it possible. Married for 25 years, he knows his spouse very well, and they both understand each other’s needs. He cherishes their alone time together. “For example, a fixed point in our daily schedule is the coffee we take together every single day when I return from work. It’s just 30 minutes, but this time belongs only to us. Or the daily walks with our dogs every morning at 6.00 a.m. This early morning exercise and chat are good for our bodies and souls,” he elaborated. For Santoni, climbing Kilimanjaro was an adventurous goal he set before moving to Tanzania for work. “I was thinking with my wife about reaching the summit of this huge and famous mountain before starting work in Tanzania,” he recalled. When he first met Paolini at an event in Dar es Salaam, they quickly realised they shared the same ambition. To prepare, Santoni walked several times over medium distances—between 12 and 14 kilometres—along the seaside promenades in Dar es Salaam. He also ran outdoors for about 10 kilometres once or twice a week and trained on the treadmill at the gym. His passion for trekking began years earlier in Italy when he explored routes in the Tuscan Apennines with friends. He realised that reaching mountain summits gave him a profound sense of freedom, and the grandeur of nature always rewarded him with a special gift each time he reached the top. During his Kilimanjaro ascent, Santoni encountered difficult moments due to the altitude. The most challenging part, he said, was climbing at night as they neared Stella Point (5,756 metres). “I started feeling dizzy, my legs were very weak, and I was breathing heavily. It was a kind of mountain sickness, as climbers call it,” he said. Despite his struggle, he persevered. Slowly but surely—polepole, as Tanzanian guides often advise—he reached the summit. “My greatest strength during the ascent was my mind and soul,” he said. Santoni does not view the climb as a conquest of Africa’s highest mountain but rather as overcoming a personal challenge. He pushed his body and endurance to the limit in conditions he had never experienced before, especially at such altitude. To him, travel is never a waste of money or time. “It’s one of the best investments you can make in yourself. I will never stop travelling,” he said. Having moved to Tanzania more than a year ago, this is Santoni’s first time in Africa. Initially, everything was very different from Italy and Europe, but he soon grew fond of life in Dar es Salaam. “The view of the sea—the Indian Ocean—makes me feel good and peaceful,” he said. Since his arrival, he has visited Arusha, Iringa, Moshi, Morogoro, and Zanzibar. “I’ve been on exciting safaris to Serengeti, Tarangire, Ngorongoro, Mikumi, and Ruaha. I also climbed Mount Meru,” he said proudly. These travels have revealed to him that Tanzania is an extraordinary and vast country, blessed with abundant nature and wildlife. “People here are always smiley and friendly,” he observed. Such experiences have taught him that happiness often comes from simplicity. “People can live in an easy way and still be happy,” he said. However, being far from home sometimes leaves him nostalgic. “Being abroad for work offers great opportunities, but there are also things about normal life in your home country that you miss—like being with your family or friends,” he admitted. “My remedy is to play padel as much as possible,” he added with a grin. Above all, he recommends a Tanzanian safari to anyone seeking an unforgettable encounter with nature. “I would definitely tell my friends and family to come, because it’s an amazing experience with nature and animals that you’ll never forget,” he said. “Even though I’ve just started going on safari here, I think Tanzania is one of the best places in Africa to experience wildlife, beautiful landscapes, and excellent service from expert and knowledgeable guides,” he affirmed.
MNAMO Aprili 2023, Bi Bishara Abdinoor aliingiwa na hofu alipomwona mwanae wa kiume amerejea nyumbani akimbeba mtoto wa duma. Tineja huyo alikuwa ameshinda mchana kutwa akilisha ng’ombe katika kijiji chao cha Kursi kinachopakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Sabuli, alipompata mnyama huyo mdogo akiwa ametelekezwa na mamake. Mama Abdinoor hakuwa na ufahamu kuwa ni hatia kuwa na mnyama wa porini bila leseni kutoka kwa Shirika la Wanyamapori Nchini (KWS) na hatari ambayo mwanawe aliwaletea kwa kumleta nyumbani mtoto wa duma. “Nilitaka kumtupa mtoto huyo wa duma kwa hofu kwamba mamake angefuatilia harufu yake na aje kumchukua. Lakini mwanangu aliniomba nimruhusu amlishe kabla ya kumruhusu arejee mwituni,” akaelezea kwenye mawasiliano ya simu na Taifa Leo Dijitali. Mahojiano hayo yalikuwa yamepangwa na Naibu Mkurugenzi anayesimamia eneo la Uhifadhi la Kaskazini Bakari Chongwa, ambapo Bi Abdinoor aliongea kupitia mkalimani. “Mwanangu alimlisha mtoto huyo wa duma kwa chakula ambacho tuliandaa jioni hiyo; mchele kwa kitoweo cha nyama. Aidha, alimtengenezea kizimba cha kulala,” akaeleza. Lakini familia ya Bi Abdinoor iliogopa kuwa duma huyo akiwa mkubwa angeanza kula mifugo wao, haswa mbuzi, kando na kuwashambulia watu. Na hata baada ya kumrejesha msituni, alirejea nyumbani kwa Bi Abdinoort kila wakati, kwani alionekana kupenda chakula kilichopikwa. “Baada ya miezi kadhaa tuliingiliana na mnyama huyo wa mwituni, alipenda watu na angetambua kila mtu katika familia yetu. Sasa tulianza kumfunga chini ya kivuli cha mti huku tukimlisha kwa hofu kwamba angewashambulia watu,” akasema. Siku moja Afisa wa KWS anayesimamia Kaunti ya Wajir Rashid Jumale alialikwa katika redio moja inayopeperusha matangazo kwa lugha yamama, ambapo alihimiza wanajamii kuripoti visa vya wanyamapori kuingia katika makazi ya watu na hapo ndio familia iliwasiliana na KWS. Baada ya kusikiza ushauri huo, Bw Abdinoor alituma ujumbe kwa KWS kwamba wanafuga duma ambaye walimwokoa kutoka msitu. Bw Chongwa alimshukuru mwanamke huyo kwa kutumza mwana duma huyo sawa na mbwa au paka wake.Maafisa KWS walimchukua mnyama huyo na kumsafirisha hadi hifadhi ya Nairobi Safari Walk, ambako anatunzwa.
NGORONGORO: FOR a period of 21 years, starting from 1979, the Ngorongoro Conservation Area (NCA) was recognised by the United Nations Educational, Scientific and Cultural Organisation (UNESCO) as a Natural World Heritage site alone, without acknowledging the unique archaeological heritage found within this area. This recognition came only two years after the Government of the … The post Understanding contribution of NCAA on growth of archaeological sector first appeared on Daily News.
ARUSHA: THE Tanzanian Vice President, Dr Philip Mpango, has graced the official opening of the new heritage museum at the Ngorongoro-Lengai Conservation Area worth over 32bn/-. The heritage museum located in Karatu, Arusha Region, has been funded by the Chinese government. Speaking during the launch in Arusha, the VP said that environmental protection and climate change … The post VP inaugurates new heritage museum at Ngorongoro Conservation first appeared on Daily News.
MOROGORO; WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Benhubert ya Kivule, Dar es Salaam, wakiwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Morogoro leo Agosti 11, 2025, ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo utalii.
DUKA la jumla la Quickmart Jumanne lilimsimamisha kazi mmoja wa meneja wake na kuomba msamaha kuhusu tukio la mteja aliyekuwa amenunua maziwa kudhulumiwa. Kupitia taarifa, usimamizi wa supamaketi hiyo ulisema kuwa umemsimamisha kazi meneja wa tawi lake la Buruburu ambaye anatuhumiwa kwa kumpiga mteja, kisa kilichozua ghadhabu za Wakenya. Video iliyosambaa mitandano ilionyesha baadhi ya wateja wakidai kuwa wamewahi kuhangaishwa na meneja huyo. Kutokana na kusambaa kwa video hiyo, kumekuwa na wito kuwa Wakenya wasusie supamaketi hiyo huku wengine wakitaka waheshimiwe na kusaka uwajibikaji kutoka kwa Quickmart. “Tunawapa kipaumbele wateja wetu na heshima kwa kila mteja anayeingia mlango wetu. Tunasikitisha kilichofanyika na kumwomba msamaha mteja aliyeathirika pamoja na yeyote ambaye alikerwa na tukio lenyewe,” ikasema taarifa ya Quickmart. “Punde tu baada ya kufahamishwa kuhusu tukio hilo, tulichukua hatua kwa kumsimamisha mfanyakazi wetu aliyehusika huku tukiendeleza uchunguzi na asasi husika,” ikaongeza taarifa hiyo. Quickmart ilitoa ufafanuzi zaidi kuwa imemfikia mteja aliyedhulumiwa na kumwomba msamaha kisha kuahidi kushirikiana naye wakati wa uchunguzi. Vilevile ilisema inamakinikia kuwa na mazingira maridhawa ya utendakazi kwa wafanyakazi na wateja wake. Kwenye video iliyosambaa mitandaoni, mteja huyo alisimulia kuwa pamoja na ndugu yake, walijijazia maziwa baada ya kukosa mhudumu na wakalipa kisha kupewa risiti. Walipokuwa wakiondoka walikabiliwa kwa nini walijijazia maziwa hayo ambapo vuta ni kuvute ilifuata kisha meneja huyo akachukua risiti yao na kuirarua. Meneja huyo aliwashangaza zaidi kwa kudai wawili hao walikuwa wameiba lita 57 za maziwa kisha kuwazuiliwa kwenye hifadhi ya supamaketi na kuwapiga. “Tuliingiwa na wasiwasi na meneja huyo alituzuilia kisha akaanza kutupiga pamoja na ndugu yangu. Tulipomuuliza kwa nini alikuwa akitupiga, alikataa kujibu,” akasema mteja huyo. Wawili hao kisha walipelekwa Kituo cha polisi cha Buruburu lakini baba yao alikuwa tayari huko na wakawaachiliwa.
Kisiwa cha Lundo ni kisiwa kidogo chenye ukubwa wa hekta 20 kilichoko katikati ya Ziwa Nyasa, takribani mwendo wa dakika 45 kwa boti kutoka mji wa Mbambabay au dakika 10 kutoka Kijiji cha Lipingo, kata ya Lipingo Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Kisiwa hicho mbali ya kuwa kivutio cha utalii wa wanyama na aina nyingi…
Nancy Oketch ni miongoni mwa Wakenya wengi wanaopenda sana mboga za kienyeji. Kila Jumapili baada ya ibada kanisani, huenda sokoni Kibuye na kuchagua kwa uangalifu mboga za majani asilia kupikia familia yake. Hali hii pia ni ya kawaida kwa Dolrose Akinyi, mkazi wa Kisumu, ambaye anasema amekuwa akitegemea mboga hizo kwa muda mrefu, akizinunua kwa wingi siku maalum za soko. “Hapo zamani kulikuwa na siku maalum za soko, kwa hivyo nilikuwa nanunua mboga nyingi za kutosha hadi siku nyingine ya soko,” aeleza. Kutokana na uchungu wa asili wa mboga hizi, wanawake hao wanasema huwa wanazichemsha kwanza kisha kuzikaanga na kitunguu na nyanya kabla ya kuongeza maziwa kama njia ya kuzihifadhi. “Kwa kuwa haziliwi mara moja, huwa nazipasha moto tena kwa kutumia maziwa ili zisiharibike,” asema Bi Akinyi. Anasema aliiga utaratibu huu kutoka kwa mama yake, ambaye naye alifundishwa na mama yake mzazi. “Alot mokuog (mboga zilizochemshwa na kuchachuka) ni nzuri kwa afya na huzuia magonjwa,” anakumbuka alivyofundishwa. Kadri magonjwa ya mtindo wa maisha yanavyoendelea kuongezeka nchini, Wakenya wengi wameanza kugeukia lishe bora ili kuzuia maradhi kama saratani. Mboga za kienyeji ni chaguo maarufu kwa sababu ya virutubisho vyake na faida za kiafya. Mboga hizi ni pamoja na managu, terere, mrenda, saga, kunde na majani ya viazi vitamu. Kulingana na utafiti wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), asilimia 34 ya watu wanaoishi mijini na viunga vya miji nchini Kenya hula mboga hizi. Hata hivyo, wataalamu wa lishe wameelezea wasiwasi wao kuhusu mbinu za kitamaduni za kupika mboga hizi, hasa matumizi ya maziwa, ambayo yanaweza kupunguza kiwango cha virutubisho vinavyopatikana. Mboga hizi huwa na vitamini A, B na C kwa wingi, pamoja na madini ya chuma na pia zina viua sumu vya asili. Lakini kwa sababu ya ladha yake chungu, watu wengi huzichemsha kwa muda mrefu na kumwaga maji kabla ya kukaanga jambo linalopunguza virutubisho. Bi Betty Okundi, Mkurugenzi wa Lishe na Chakula katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, anasema kuwa matumizi ya maziwa hupunguza kwa kiasi kikubwa virutubisho vya mboga hizo. “Maziwa yana madini ambayo hufunga chuma na baadhi ya vitamini katika mboga. Hii hupunguza uwezo wa mwili kuyeyusha virutubisho, hivyo mtumiaji hanufaiki vilivyo,” asema. Bi Okundi anasema kuwa mboga zenye rangi ya kijani kibichi kwa kina huwa na madini ya chuma kwa wingi, jambo linalozifanya kuwa muhimu zaidi kwa wanawake wajawazito. “Tunashauri wanawake wajawazito kula mboga hizi, lakini wengi wao huzipika kwa kutumia maziwa. Mwishowe hurudi hospitalini wakiwa na kiwango cha chini cha hemoglobini,” asema. Onyo hili pia linahusu uji na omena zinapopikwa kwa maziwa kwani maziwa pia hufunga virutubisho vilivyomo kwenye vyakula hivyo. Kutokana na umaarufu na faida za kiafya za mboga hizi, baadhi ya watu wameanza kuzipanda kwenye bustani za nyumbani, huku wengine wakiendelea kununua kutoka sokoni. Baada ya kuvuna au kununua, hatua ya kwanza ni kutenganisha majani na shina gumu, kisha kuosha vizuri kuondoa mchanga na wadudu. Bi Okundi anashauri maji yachemshwe kwanza kabla ya kuweka mboga. “Tumia maji kidogo ya moto yasiyohitajika kumwagwa,” asema. Mboga zikishakatwa vipande vya kati (baada ya kuoshwa, si kabla), zichemshwe kwa dakika 10 hadi 15. “Wengine huzichemsha kisha kuzirushia maji baridi jambo linalosababisha virutubisho kupotea,” anaonya. Baada ya kuchemshwa, zinaweza kukaangwa kwa vitunguu, nyanya na viungo vingine. Caleb Odipo, mpishi katika hoteli moja Kisumu, anasema mikahawa mingi sasa imeacha desturi ya kuchemsha mboga kwa muda mrefu. “Kwanza huchemsha maji, kisha huweka mafuta kidogo, chumvi na vitunguu vilivyokatwa. Kisha huongeza mboga zilizosafishwa na kukatwa,” asema. Baada ya kupika kwa dakika 7 hadi 10, maji yaliyobaki huondolewa na kuhifadhiwa. “Kisha mboga hukanguliwa kwa mafuta kidogo na kumalizia kwa mchuzi wa kuku ili kuongeza ladha,” aongeza. TAFSIRI: BENSON MATHEKA
Juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Tanzania; The Royal Tour, zimeongeza idadi ya Watalii katika Pori la akiba la Selous na kupandisha mapato kufikia bilioni 9.1 kwa mwaka wa fedha 2024/25. Ofisa Mhifadhi daraja la II na Ofisa Utalii Pori la Akiba Selous, Stephano Lukumay aliyabainisha hayo hivi karibuni…
RUVUMA; HIFADHI ya Msitu wa Matogoro iko Kusini Mashariki mwa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, takribani kilometa 15 kutoka Songea mjini. Msitu huu umezungukwa na vijiji vya Ndilima na Litembo kwa upande wa Magharibi na Mahilo na Mpingi kwa upande wa Mashariki. Upande wa Kusini kuna Kijiji cha Lipaya na Matogoro kwa upande wa Kaskazini.…
DIRA ya Taifa ya Maendeleo 2050 imetaja sekta zenye fursa ya mageuzi kiuchumi ikiwemo ya viwanda, kilimo na utalii. Imeeleza kuwa Tanzania inalenga kuwa kitovu cha viwanda chenye ushindani kimataifa ifikapo mwaka 2050 ikitumia ongezeko la idadi ya watu, maendeleo ya kiteknolojia na msingi wake imara wa kilimo, kama nyenzo muhimu. “Ili kufanikisha azma hii,…
ZANZIBAR; Programu ya OCP School Lab (OSL) rasmi ilizindua mpango wake wa kisasa wa upimaji wa udongo wa simu katika hafla yenye nguvu iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip zANZIBAR. Mada kuu katika prpgramu hiyo inasema: “Napima afya ya udongo wangu kwa matumizi sahihi ya mbolea kulingana na zao.” Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika…
MWISHONI mwa wiki Bunge la Jumuiya wa Afrika Mashariki (EALA) lilikutana kujadili na kupitisha ripoti ya kamati za kilimo, maliasili na utalii kuhusu kilimo cha ikolojia katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa mujibu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), kilimo cha ikolojia ni mbinu ya kilimo inayotumia maarifa na kanuni…
TANZANIA imefanikiwa kuwa nchi ya kwanza Afrika kuongeza mapato kupitia sekta ya utalii kwa asilimia 66 ikifuatiwa na Tunisia na Morocco. Imefanikiwa pia kuongeza idadi ya watalii kwa asilimia 50 na kuingia katika orodha ya nchi 20 bora duniani kuwa na ongezeko kubwa la watalii tangu 2019. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja…
PWANI; Sanamu ya Bikira Maria (Mariam), anayesemwa katika vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu na Kurani Tukufu kuwa ni Mama wa Yesu Kristo (Issa bin Mariam), iliyogundulika ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani inatajwa kuwa maajabu mapya yasiyo ya kawaida kwa macho na masikio ya watalii ndani na nje ya Tanzania huku ikiongeza upekee wa…
DODOMA: OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Taasisi ya Ulinzi na Usalama ya Sekta ya Utalii Tanzania (TTSSP) inakusudia kuzindua kitabu cha mkakati za kukuza utalii wa mkoa huo, tukio litakalofanyika Agosti 4, 2025 saa 3:00 asubuhi ukumbi wa Mabeyo Complex Dodoma. Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo na kusainiwa na Mkuu…
THE black sand dunes that occur in the eastern Serengeti Plain near the Olduvai Gorge hominid site within the Ngorongoro Conservation Area in Tanzania are mainly identified as volcanic sand dunes. The migratory dunes, also known as the Shifting Sands, are located at least twelve kilometers north-west of the Museum at Olduvai Gorge and nearly…
NGORONGORO: THE government has launched a national livestock vaccination programme in Ngorongoro, Arusha Region, a key step in its five-year strategy to safeguard animal health across the country. The initiative, led by Minister for Livestock and Fisheries, Dr Ashatu Kijaji, at Mokilal Village, marks a significant push to protect the nation’s valuable livestock. Speaking recently…
Wadau wa sekta ya utalii, mazingira na maendeleo ya jamii wameitaka Serikali na mashirika ya kimataifa kuweka msukumo maalumu kuhakikisha mbio za Great Ruaha Marathon zinapandishwa hadhi na kuwa tukio la kimataifa. Hatua hiyo imeelezwa itasaidia kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kimataifa, kukuza utalii wa ndani na nje, pamoja na kuhamasisha uhifadhi wa maliasili…
Mr Segun Osifeko, Chairman, Hoteliers Association of Nigeria, Epe branch, Lagos State, says hotels within the Eredo, Epe axis have intensified security surveillance systems ahead of the upcoming local government area election in the state.
DUBAI: Wadau wa sekta ya utalii nchini wamehimiza uboreshaji na ubunifu wa vivutio vipya vya kisasa ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa. Aidha, wamesisitizwa kuwa kutegemea vivutio vya asili pekee kama wanyamapori na fukwe hakuwezi kutosha kuipeleka Tanzania kwenye ushindani wa kimataifa wa utalii kwa miaka ijayo. Akizungumza na HabariLEO kutoka…
MWISHONI mwa wiki, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Tuzo za 32 za Utalii duniani 2025 maarufu World Travels Awards Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa tuzo hizo kufanyika nchini tangu zilipoanzishwa mwaka 1993. Habari njema kwa Tanzania ni kwamba imeshinda tuzo 27 kati ya 60 zilizotolewa katika vipengele…
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk, Pindi Chana amesisitiza Mamlaka ya (NCAA ) inapaswa kuongeza jicho katika kuhakikisha wanawake wanafikia nafasi za juu za uongozi katika nafasi mbalimbali. Dk, Chana ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa kuwavisha cheo manaibu kamisha wawili huku makamishna wasaidizi waandamizi watano wakivishwa vyeo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi…
IRINGA: Maandalizi ya msimu wa nne wa Great Ruaha Marathon yanaendelea kwa kasi kubwa huku tukio hilo linalojizolea hadhi ya kimataifa, likitarajiwa kufanyika Julai 5, 2025, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mojawapo ya hifadhi kubwa na za kipekee barani Afrika. Katika kuthibitisha uzito wa tukio hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa…
ARUSHA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) is finalising the development of interactive digital platforms and global payment systems that will enable tourists and visitors to make payments virtually from anywhere in the world. According to NCAA Commissioner, Abdul-Razaq Badru, the new system is designed to streamline payments, allowing tourists to complete transactions conveniently from…
MOROGORO: IN a bold conservation move, Mikumi National Park is set to install surveillance cameras at key entry points in response to the alarming rise in wildlife deaths caused by speeding vehicles. The cameras will be placed at the Doma Village gate and Mikumi Town, where the main highway to Iringa cuts through the park,…
KILOSA: MIKUMI National Park is set to inaugurate a new entrance gate in Kilosa District, strategically located to better serve tourists arriving via the Standard Gauge Railway (SGR). This significant development is expected to dramatically reduce travel time and further invigorate domestic tourism. Park Chief Warden Commissioner Augustine Masesa announced the plan recently, saying the…
For many years, the Tanzania Tourism industry was concentrated in the Northern Circuit where most tourists and awards would find their way to Kilimanjaro, Ngorongoro and the Serengeti, but this time around, the World Travel Awards have flown south.
During the 32nd World Travel Awards Gala Ceremony for Africa and the Indian Ocean, Ngorongoro Conservation Area (NCA) grabbed back the prestigious title.