WAFANYABIASHARA Homa Bay wanatarajia kuvuna pakubwa huku kaunti hiyo ikiwa mwenyeji wa Sherehe za Madaraka Dei mnamo Juni 1.
Usimamizi wa hoteli kadhaa ulithibitisha kuwa utakuwa makao ya wageni mashuhuri na itakuwa vigumu kupata nafasi ya kuwasitiri watu wengine wa kawaida.
Wikendi, baadhi ya hoteli zilikuwa zimejaa na waliokuwa wakitafuta nafasi waliambiwa wasake makao kwingine. Hoteli ya hadhi ya Cold Spring yenye uwezo wa kuwapa makao wageni 70 tayari imejaa kwa kuwa vyumba vyake vimelipiwa na vitatumika na wageni watakaohudhuria sherehe za Madaraka.
Usimamizi wa Cold Spring uliambia Taifa Leo kwa wateja wao ni maafisa kutoka ubalozi mbalimbali. Meneja wa hoteli hiyo Dickson Osore alisema wageni wengi watawasili hotelini humo Mei 31 kisha kuondoka Juni 1.
Kwa mujibu wa Bw Osore, chumba cha mwisho kililipiwa wiki iliyopita.
“Wengine watakwepo hadi baada ya Juni 1. Lakini kwa sasa vyumba vyote 70 vimelipiwa,” akasema Bw Osore huku akisema wanalenga kutumia sherehe hizo kuvumisha hoteli yao.
“Sherehe hizi zitakuwa silaha ya kuvumisha hoteli zetu Homa Bay na sekta ya utalii. Huwa tuna huduma bora na tunawaalika wageni wote hata baada ya sherehe za Madaraka,” akaongeza.
Homa Bay pia itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Ugatuzi mnamo Agosti mwaka huu, lile la uchumi samawati na Maadhimsho ya Siku ya Chakula Duniani.
Hoteli nyingine ambazo zimejaa Homa Bay ni Golden Ray, Twin Towers na Tausi.
Homa Bay yaanza kuvuna hoteli zikijaa kuelekea sherehe za Madaraka

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
TravelMiss World Kufungua Milango ya Utalii
ZANZIBAR imeendelea kujitokeza kama moja ya vivutio muhimu vya utalii nchini, safari hii ikipokea ugeni wa Miss World 2026, Joheirry Molla aliyewasili visiwani humo Novemba 19, 2026, akiwa ameambatana na warembo kutoka mabara sita.
TravelAskari Tanapa, TFS mbaroni mauaji ya wabeba mkaa
KAGERA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia askari 13, wakiwemo wa wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), askari wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na askari mgambo, kwa tuhuma za mauaji ya watu wanne yaliyotokea Kijiji cha Kanyamika, Kata ya Karambi, Tarafa ya Kimwani, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Taarifa…
TravelNgorongoro scoops continental gong
ACCRA: THE Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has won the Excellence in Sustainable Tourism and Conservation Management Award at the Africa Business Forum & Awards 2026. The award recognises Ngorongoro’s contribution to biodiversity conservation, sustainable tourism development and the protection of its outstanding natural and cultural heritage. The awards ceremony was held in Accra, Ghana,…
TravelDk Kijaji: Mashindano makubwa gofu Afrika kufanyika Serengeti
MARA; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji, amesema Uwanja wa Gofu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti utawezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya gofu ya Afrika na kimataifa, hatua inayotarajiwa kuongeza idadi ya watalii, mapato na kuitangaza nchi kupitia utalii wa michezo. Akizungumza leo Oktoba 18, 2026, wakati wa uzinduzi wa…