News'Reconsider travel': US raises warning level for Kenya over surging Ebola risk
The alert comes as Kenya confirms eight Ebola cases amidst a broader regional outbreak.
Category
Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.

DAR ES SALAAM: STARTUPS have welcomed the government’s plan to introduce a dedicated policy for the sector within six months, saying it could ease longstanding challenges, particularly limited access to finance and regulatory requirements that often burden early-stage businesses. The proposed policy has raised hopes among entrepreneurs that their businesses will receive greater recognition and…

KATIBU Mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutupilia mbali malalamishi dhidi yake kuhusu kauli aliyotoa kuwa hata watu waliokufa wanaweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2027. Omar alisema matamshi hayo aliyotoa Septemba 11 yalikuwa mzaha wa kisiasa uliolenga kuwahamasisha wakazi wa Pwani kujisajili kama wapigakura na kushiriki uchaguzi, wala si wito wa kufanya udanganyifu. Alisema hayo Jumatano akijitetea mbele ya kamati ya IEBC inayoshughulikia ukiukaji wa kanuni za maadili ya uchaguzi katika majengo ya Anniversary Towers, Nairobi. Kupitia mawakili wake Emmanuel Kibet na Adrian Kamotho, Omar aliomba kamati imwachilie huru kwa madai kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa alikiuka kanuni hizo. Hata hivyo, aliomba apewe onyo iwapo atapatikana na hatia. Kibet alisema kauli hiyo ilipaswa kutathminiwa katika muktadha wa hotuba nzima, akisisitiza kuwa Omar alikuwa akiwahimiza wananchi walio na haki ya kupiga kura kujisajili na kuthibitisha taarifa zao kwenye sajili ya wapigakura. “Ni wazi kuwa wakazi wa Pwani hawajajisajili kama wapigakura kwa wingi. Tunaamini kauli yake inapaswa kuangaliwa katika muktadha wake ili maana halisi ijitokeze,” alisema Kibet. Omar alieleza kuwa Mombasa ilikuwa imesajili wapigakura wapya 12,000 hadi 13,000 pekee, licha ya kuwa na takriban watu 200,000 wanaostahili kujisajili. Alisema juhudi zake za kisiasa zimekuwa zikilenga kukabiliana na kutengwa kwa wakazi wa Pwani, akitaja changamoto za kupata vitambulisho na kutambuliwa kama raia. Omar alisisitiza kuwa wanasiasa hutumia tashbihi na kutia chumvi katika hotuba zao ili kufikisha ujumbe, na kwamba matamshi yake hayakupaswa kuchukuliwa kihalisi. Hata hivyo, makamishna wa IEBC walionya kuwa kauli zinazohusisha matumizi ya majina au alama za vidole za watu waliokufa kupiga kura zinaweza kuibua wasiwasi kuhusu uadilifu wa uchaguzi. Mwenyekiti wa kamati, Moses Alutalala Mukhwana, alikanusha madai kuwa IEBC inalenga viongozi wa UDA pekee, akisema kuitwa kwa maafisa kadhaa wa chama hicho mbele ya kamati hakumaanishi kuwa kuna ubaguzi. Alihimiza vyama kuwasilisha malalamishi yao kupitia Kamati ya Ushirikiano wa Vyama vya Kisiasa badala ya kutumia makosa yanayodaiwa kufanywa na wapinzani kuhalalisha mienendo yao. Kamati hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wake Oktoba 27.

Artificial intelligence has found critical security flaws in a major programming language called PHP, with many websites taken offline Thursday as organisations worldwide scramble to fend off would-be hackers.

ZIARA ya siku 10 ya Rais William Ruto katika ngome yake ya kisiasa ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa imefichua ushindani unaozidi kuongezeka ndani ya chama tawala cha UDA huku wanasiasa wakiwania ushawishi wake kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Ziara hiyo iliyohusisha uzinduzi wa miradi ya maendeleo na sherehe za Mashujaa Day, ilidhihirisha makundi yanayojipanga kuwania viti vya magavana, wabunge na nyadhifa nyingine za uchaguzi ujao. Ingawa UDA ina uungwaji mkono mkubwa katika eneo hilo, tofauti za viongozi wanaotaka tiketi ya chama zimeanza kuwa changamoto kwa Rais Ruto, hasa ikizingatiwa kuwa uteuzi wa chama unaweza kuamua hatima ya wengi wao. Mchambuzi wa siasa wa Eldoret, David Kosgei, alisema wagombea wanajitahidi kupata nafasi ya kuzungumza na Rais wakiamini kuwa baraka zake zitawasaidia kupata kura. “Wagombea wote wanatafuta kuteka umakini wa Rais Ruto kwa matumaini kuwa mkakati huo utawasaidia kupata kura,” alisema. Katika kaunti ya Uasin Gishu, ushindani umejikita kati ya makundi yanayohusishwa na Gavana Jonathan Bii Chelilim na Seneta Jackson Mandago. Kambi ya Mandago inajumuisha Katibu katika Wizara ya Utalii Julius Bitok, ambaye anajaribu kwa mara ya tatu kuwania ugavana, Mbunge wa Soy David Kiplagat na Mbunge wa Kesses Isaac Rutto. Kwa upande mwingine, kundi la Gavana Bii inahusishwa na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na washirika wake wa kisiasa. Hata hivyo, ushindani huo hauhusu uchaguzi wa 2027 pekee, bali pia nani atakuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii ya Wakalenjin baada ya Ruto kuondoka kwenye ulingo wa siasa. Mchambuzi Benjamin Kirwa alisema makundi hayo yanaashiria mapambano makubwa yanayoweza kulipuka iwapo viongozi watashindwa kudhibiti tofauti zao. “Mapambano ya kisiasa hayahusu uchaguzi mkuu wa 2027 pekee, bali pia nani atakuwa msemaji wa Wakalenjin baada ya Rais Ruto kuondoka kwenye ulingo wa siasa,” alisema. Mvutano ulionekana wazi zaidi katika kaunti ya West Pokot, ambapo makundi mawili yanapigania ushawishi kuelekea uchaguzi wa ugavana. Kundi la 5G linahusishwa na aliyekuwa gavana John Lonyangapuo, huku kundi la Message likihusishwa na Mbunge wa Sigor David Pkosing. Makundi hayo yanapigania ushawishi ndani ya UDA licha ya viongozi wao kuhusishwa na Kenya Union Party (KUP), ambacho kimehamia upande wa UDA. Kundi la 5G linajumuisha Seneta Murgor, Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong, Mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto, Mwakilishi wa Wanawake Rael Kasiwai, aliyekuwa Mbunge wa Kacheliba Mark Lomunokol na aliyekuwa Katibu wa wizara James Teko. Mrengo wa Messag nao unajumuisha Gavana Simon Kachapin, Mbunge wa Kacheliba Titus Lotee, aliyekuwa Mbunge wa Sigor Philip Rotino, Balozi wa Kenya nchini Zambia Lillian Tomiton, Naibu Gavana Robert Komolle, MCA wa Sekerr Jane Mengich, Naomi Kendagor na Spika wa Bunge la Kaunti Fredrick Kaptui, pamoja na madiwani wengine. Mchambuzi wa siasa Joshua Kosgei alisema kupata tiketi ya UDA na kuungwa mkono na Rais kunaweza kuwa sawa na kushinda uchaguzi katika eneo ambalo chama hicho kina wafuasi wengi. “Kupata tiketi ya UDA katika mchujo na kuvutia umakini wa Rais ni sawa na kushinda uchaguzi katika eneo ambalo UDA ina nguvu. Haya ni mapambano ya kufa au kupona,” alisema. Katika ziara yake, Rais Ruto alilazimika mara kadhaa kuwataka wafuasi wa makundi hasimu kudumisha umoja ili mikutano ya maendeleo isigeuke uwanja wa malumbano ya kisiasa. Pia alikumbana na malalamishi kuhusu utendaji wa baadhi ya viongozi wa maeneo ya Elgeyo Marakwet na Nandi, ambapo wakazi walihoji rekodi zao za maendeleo. Akijaribu kutuliza hali, Rais aliwataka wagombea na wafuasi wao kubaki ndani ya UDA na serikali jumuishi hadi wakati wa kuchagua viongozi utakapofika. “Mnajua la kufanya kwa kura zenu. Subirini wakati huo, kisha mfanye uamuzi wenu. Kwa sasa, tuungane ndani ya UDA na serikali jumuishi,” alisema, huku akisisitiza kaulimbiu mpya ya chama, Usawa ni Sawa. Rais pia aliwataka wapiga kura kuchagua viongozi kwa kuzingatia rekodi zao za maendeleo, sera na ahadi zao badala ya kufuata ushawishi wa kisiasa pekee. Alisema ana imani kuwa serikali yake imefanya mengi katika miaka minne iliyopita na akapuuza uwezekano wa upinzani kumshinda mwaka 2027.

KENYA imeorodheshwa katika nafasi ya 137 duniani katika kupambana na ufisadi, huku ripoti mpya ikionyesha kudhoofika kwa uhuru wa mahakama na baadhi ya haki za kiraia. Ripoti ya mwaka 2025 ya World Justice Project (WJP) Rule of Law Index inapatia Kenya nafasi ya 102 kati ya nchi na maeneo 143 duniani katika utekelezaji wa utawala wa sheria. Alama ya jumla ya Kenya ilishuka kwa chini ya asilimia moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, lakini nchi ilifanya vibaya zaidi katika kipengele cha kupigana na ufisadi, ambapo iliorodheshwa ya 137 duniani na ya 31 kati ya nchi 34 za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kenya pia iliwekwa katika nafasi ya 128 duniani katika kipengele cha usalama na utulivu, hali inayoangazia changamoto za kulinda watu na mali yao. Ripoti hiyo inasema mifumo ya kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka na kuhakikisha taasisi za serikali zinawajibika imeendelea kudhoofika. “Uadilifu wa mifumo ya kuzuia na kusawazisha mamlaka pia umedhoofika pakubwa, ikiwemo nchini Kenya,” ripoti hiyo inasema. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa uhuru wa kutoa maoni, kujieleza, kukusanyika na kujiunga na mashirika umepungua katika baadhi ya nchi, Kenya ikiwa miongoni mwa zilizorekodi kushuka katika vipengele hivyo. Hata hivyo, ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiraia nchini Kenya ulisalia bila mabadiliko makubwa, tofauti na mataifa mengi ambako ushiriki huo ulipungua. Ripoti hiyo pia inaonyesha wasiwasi kuhusu kuingiliwa kwa mifumo ya haki na wanasiasa. Kenya ilishuka katika vipimo vinavyochunguza uwezo wa mahakama kuzuia matumizi mabaya ya mamlaka ya serikali kuu na uhuru wa mifumo ya haki ya kesi za jinai. Licha ya changamoto hizo, Kenya ilifanya vizuri zaidi katika baadhi ya vipengele. Ilishika nafasi ya 69 duniani katika uwazi wa serikali, ya 82 katika haki za madai na ya 87 katika haki za jinai. Uwazi wa serikali ulijumuisha upatikanaji wa taarifa za umma na mifumo inayowawezesha wananchi kuwawajibisha viongozi. Hiki ndicho kilikuwa kipengele kilichopatia Kenya matokeo bora zaidi kati ya vipengele vinane vilivyopimwa. WJP hutumia maoni ya wananchi, wanasheria na wataalamu kutathmini jinsi utawala wa sheria unavyotekelezwa katika maisha ya kila siku, badala ya kutegemea Katiba na sheria pekee. Duniani kote, asilimia 68 ya nchi na maeneo 143 yaliyotathminiwa yalirekodi kushuka kwa viwango vya utawala wa sheria mwaka 2025, ikilinganishwa na asilimia 57 mwaka 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa WJP Alejandro Ponce alisema hali hiyo imegeuka kwa kasi baada ya kushuka kwa viwango hivyo katika miaka iliyotangulia. “Kuharibiwa kwa taratibu za utawala wa sheria kulipungua katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, mwaka huu tunaona mabadiliko makubwa, huku nchi nyingi zaidi zikishuka na chache zikiimarika,” alisema. Denmark iliongoza katika orodha ya kimataifa, ikifuatiwa na Norway, Finland, Sweden na New Zealand, huku Venezuela ikiwa ya mwisho. Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya ilishika nafasi ya 13 kati ya nchi 34, na nafasi ya 15 kati ya nchi 35 zenye uchumi wa kipato cha chini-kati. Matokeo hayo yanaangazia changamoto ya kuhakikisha kuwa haki zilizowekwa katika Katiba zinalindwa, taasisi za umma zinawajibika na mamlaka yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

UPINZANI nchini unaonekana kukabiliwa na changamoto mpya huku viongozi wakipanga mikakati tofauti ya kumwondoa Rais William Ruto mamlakani katika uchaguzi mkuu wa 2027. Mikakati ya kiongozi wa Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, anayeongoza vuguvugu la Linda Mwananchi, inaonekana kuwa na uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa siasa za upinzani. Hata hivyo, ushirikiano huo unaweza kuimarisha umoja au kuchochea makundi pinzani yanayowania uongozi wa nchi. Kwa sasa, upinzani unaonekana kuunda mirengo mitatu ya kisiasa huku viongozi wakitofautiana kuhusu wakati wa kumteua mgombea urais, namna ya kuendesha kampeni na chama kitakachotumiwa katika uchaguzi. Mrengo wa kwanza unahusisha kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Democratic Party of Kenya (DP) Justin Muturi na kiongozi wa Democratic Action Party-Kenya (DAP-K) Eugene Wamalwa. Watatu hao wamekuwa wakifanya mikutano ya pamoja katika miezi ya hivi majuzi. Mrengo wa pili unajumuisha kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i, Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro wa People’s Party of Kenya (PPK) na kiongozi wa People's Liberation Party (PLP) Martha Karua. Watatu hao wameanza kuonekana pamoja katika mikutano ya kisiasa, wakikosoa utawala wa Rais Ruto. Hapo jana viongozi hao walikuwa Nakuru wakieneza ujumbe wa kupinga serikali ya Kenya Kwanza. Kundi la tatu linaweza kuundwa na Gachagua na Sifuna, ambao wameanza mazungumzo kuhusu ushirikiano kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao. Mnamo Jumanne, Sifuna alifanya ziara ya kushtukiza katika makazi ya Gachagua ya Wamunyoro, Nyeri, ambapo walijadili uwezekano wa kuunganisha nguvu zao. “Tulikuwa na mazungumzo ya wazi na ya kujenga kuhusu ukombozi wa nchi yetu na kuunda utawala wa sita,” alisema Gachagua baada ya mkutano huo. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, mshirika wa karibu wa Sifuna, alisema mkutano huo ni ishara kuwa viongozi wa upinzani wanaweza kuungana. “Njia pekee ya kushinda serikali hii ni umoja. Idadi ya wafuasi wanaoungwa mkono na viongozi hao wawili inaonyesha kuwa mshindi wa uchaguzi huu anaweza kupatikana katika duru ya kwanza,” alisema Natembeya, akiongeza kuwa mazungumzo yataendelea ili kutafuta uungwaji mkono kutoka maeneo mengine. Hata hivyo, tofauti kuhusu jinsi ya kuchagua mgombea urais zimezua mashaka kuhusu uwezekano wa viongozi hao kukubaliana. Kalonzo na Muturi wanataka mgombea atangazwe mapema ili upinzani uwe na muda wa kujiandaa. Kwa upande mwingine, Gachagua na Linda Mwananchi wanataka viongozi wajenge kwanza vuguvugu la kitaifa kwa kuunganisha misingi yao ya kisiasa. Muturi alikiri kuwa kujenga muungano si jambo rahisi, lakini akasema viongozi wana nia ya kushinda changamoto zinazowakabili. “Muungano wa kisiasa haujawahi kuwa rahisi popote, na hatutarajii kuwa jambo jepesi hapa Kenya. Tumejitolea kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza,” alisema. Aliongeza kuwa lengo lao ni kumuondoa Ruto madarakani kwa njia ya kidemokrasia na kurejesha utawala unaoheshimu Katiba, utawala bora na sheria. Nyoro pia alikanusha madai kuwa upinzani umegawanyika, akisema viongozi wanatumia njia tofauti kufikia lengo moja. “Hatujagawanyika. Tumeungana kwa lengo la kumuondoa Rais Ruto mamlakani,” alisema. Alisema hawatakimbilia kumtangaza mgombea urais kwa sababu mchakato huo unahitaji kuzingatia mambo mengi. Kwa maoni yake, upinzani ukiungana na kuwasilisha mgombea mmoja, utakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda. Seneta wa Kitui Enoch Wambua, mshirika wa Kalonzo, pia alipuuzilia mbali uwezekano wa makundi hayo kubaki yakiwa tofauti katika uchaguzi ujao. Alisema hivi karibuni Wakenya wataanza kuona mikutano itakayowaleta pamoja viongozi wa Wiper, DCP, Linda Mwananchi, DAP-K, DP na vyama vingine washirika. Lakini Naibu Kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema ukosefu wa kuaminiana, kusalitiana na hila ni baadhi ya vikwazo vinavyoweza kuvuruga mipango ya upinzani. Alisema baadhi ya viongozi wana uwezo wa kuvutia wapiga kura lakini hawana uungwaji mkono wa kutosha kuongoza nchi, huku wengine wakikabiliwa na tatizo la kukosa imani ya wananchi. Mbali na tofauti za kitaifa, ushindani wa kupata ushawishi katika eneo la Mlima Kenya umeongeza mgawanyiko. DCP, Jubilee, PLP, DP, Party of National Unity (PNU) inayoongozwa na Peter Munya na Devolution Empowerment Party (DEP) ya Lenny Kivuti ni miongoni mwa vyama vinavyowania uungwaji mkono katika eneo hilo lenye ushawishi mkubwa katika siasa za nchi. Mvutano umeongezeka tangu Nyoro azindue PPK mnamo Agosti 17 na kuanza kampeni za kujijengea msingi wa kisiasa kote nchini, pamoja na Mlima Kenya. Baadhi ya viongozi wa DCP wamemlaumu Nyoro kuwa “fuko”, madai ambayo yanalenga kuonyesha kuwa anatumiwa kuhujumu upinzani. Seneta wa Nyandarua John Methu hata amekiita chama cha Nyoro “wilibaro ya kijani”, akijaribu kukihusisha na UDA. Nyoro amepuuzilia mbali madai hayo, akisema ni kampeni ya kumchafua yeye na chama chake. “Hatuna muda wa kujibu mashambulizi na uongo wa kitoto. Anayetuma watu hao aseme moja kwa moja, nasi tutajibu ipasavyo,” alisema. Akiwa Kajiado wiki iliyopita, Nyoro alisema wanaomshambulia wanahofia kuongezeka kwa ushawishi wake wa kisiasa. Ushirikiano wake wa hivi karibuni na Matiang’i katika mikutano ya pamoja umeongeza dhana kuwa wawili hao wanaunda mhimili tofauti ndani ya upinzani. Ilivyo kwa sasa, changamoto kubwa inayowakabili viongozi wa upinzani si kupata tu mgombea anayeweza kumshinda Ruto, bali pia kukubaliana kuhusu mchakato wa uteuzi ambao utawafanya wagombea wengine kuunga mkono mshindi bila kuhisi wamesalitiwa au kushindwa kisiasa

By Henry Umoru ABUJA — National Leader of the Nigeria Democratic Congress (NDC), Senator Seriake Dickson, has congratulated the party’s vice-presidential candidate, Dr Rabiu Musa Kwankwaso, on his 70th birthday, describing him as a symbol of visionary leadership and commitment to public service. Dickson, a former governor of Bayelsa State, congratulated Kwankwaso in a goodwill […]

KAMISHNA wa Kaunti ya Trans Nzoia Hussein Allaso amezua mzozo baada ya kuwaamuru maafisa wa serikali ya kitaifa kuacha kumsalimu Gavana George Natembeya, akimlaumu kwa kumkosea heshima Rais William Ruto. Bw Allaso alitoa agizo hilo wakati wa sherehe za Mashujaa Day katika Shule ya Msingi ya Naminit, wadi ya Chepchoina, eneo bunge la Endebes, akisema maafisa hao hawapaswi kumheshimu gavana ambaye, kwa madai yake, hamheshimu Rais. “Kuanzia leo, hakuna anayeruhusiwa kumsalimu gavana kwa sababu ya kumkosea heshima Rais. Sisi pia tutamkosea heshima,” alisema Bw Allaso alipokuwa akiwahutubia machifu. Alisisitiza kuwa maafisa wa serikali ya kitaifa wataendelea kutekeleza majukumu yao bila kutishwa na viongozi wowote. Alisema uzoefu wake wa miaka 30 katika utawala wa mikoa unampa uwezo wa kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa. Agizo hilo limechochea mjadala kuhusu iwapo maafisa wa umma wanapaswa kuonyesha uaminifu kwa Rais binafsi au kuhudumia wananchi kwa kufuata Katiba. Natembeya alijibu vikali, akimtaja Allaso kuwa mtu anayejipendekeza kisiasa na kukosa kuelewa misingi ya utawala wa kikatiba. Gavana huyo alitoa kauli hiyo akiwa nyumbani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri, alipokuwa ameandamana na viongozi wa upinzani. “Uliajiriwa kuhudumu kwa kuzingatia Katiba, si Rais,” alisema Natembeya, akimshutumu kamishna kwa kutenda kana kwamba ni mlinzi binafsi wa Rais. Alionya kuwa maafisa wa umma wanapaswa kupanda vyeo kwa kuonyesha weledi na utendaji bora badala ya kujipendekeza kwa viongozi wa kisiasa. Akirejelea Ibara ya 232 ya Katiba, Natembeya alisema watumishi wa umma wanapaswa kuzingatia maadili ya kazi, uwajibikaji, uwazi na kutopendelea upande wowote wa kisiasa. Mzozo huo umeibuka baada ya ziara ya maendeleo ya Rais Ruto Trans Nzoia, ambako alizindua mradi wa soko la Masinde Muliro. Naibu Gavana Philomena Kapkory aliunga mkono wito wa kuheshimiwa kwa Rais, akisema Trans Nzoia ni kaunti iliyo na jamii mbalimbali ambazo hazipaswi kugawanywa kwa misingi ya siasa. Alisema viongozi wanapaswa kuvumiliana na kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Natembeya alikosa sherehe hizo na badala yake akaandamana na viongozi wa Linda Mwananchi Movement kukutana na Gachagua kujadili uwezekano wa upinzani kuafikiana kuhusu mgombea mmoja wa urais mwaka 2027.

HUDUMA katika kaunti zote 47 huenda zikavurugika baada ya chama cha wafanyakazi wa serikali za kaunti (COGWU) kutishia kuchukua hatua kupinga mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) ya kudhibiti nyongeza za mishahara. Katibu Mkuu wa chama hicho, Roba Duba, alisema mapendekezo ya tume inayoongozwa na Mary Chebukati yatawaathiri wafanyakazi kwa kusababisha kupunguzwa kwa mishahara, kusimamishwa kwa ajira mpya na kuongezeka kwa changamoto kazini. Pendekezo hilo limezua mvutano wakati serikali za kaunti zinakabiliwa na shinikizo la kulipa mishahara na kugharamia huduma muhimu kwa wananchi. “Pendekezo la kuwafuta wafanyakazi, kusimamisha ajira na kuweka masharti makali ya kifedha kwa kisingizio cha kudhibiti matumizi ya mishahara ni uchokozi wa moja kwa moja na tangazo lisilo la kikatiba la vita dhidi ya msingi wa ugatuzi,” alisema Duba katika taarifa. Chama hicho kilionya kuwa hakitakubali hatua zozote zitakazohatarisha ajira na maisha ya wafanyakazi wa kaunti, kikisema maamuzi yanayowahusu lazima yazingatie sheria. “Ugatuzi hauwezi kujengwa kwa kuharibu maisha ya wafanyakazi,” kilisema chama hicho. Mvutano huo umeibuka wiki moja baada ya CRA kukutana na Baraza la Magavana (COG), ambapo magavana walikataa pendekezo la Sh440.8 bilioni kama mgao wa mapato kwa kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2027/28. Magavana walitaka serikali ya kitaifa kuongeza mgao huo kwa Sh100 bilioni, wakisema fedha zaidi zinahitajika ili kaunti ziweze kutekeleza majukumu yake. Katika mkutano huo, CRA iliwataka magavana kuzingatia kupunguza idadi ya wafanyakazi ili kudhibiti matumizi ya mishahara yanayozidi uwezo wa baadhi ya kaunti. Baadhi ya serikali za kaunti zimekuwa zikikopa fedha za muda mfupi ili kulipa mishahara ya kila mwezi. Hata hivyo, COGWU ilisema CRA haina mamlaka ya kikatiba kusimamia wafanyakazi wa kaunti, kuamua masharti ya ajira au kuelekeza kufutwa kwa wafanyakazi. Duba alitaja Kifungu cha 216 cha Katiba ya Kenya, akisema jukumu la CRA ni kutoa mapendekezo kuhusu ugavi wa mapato kati ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti, pamoja na mgao kati ya kaunti zenyewe. Alisema mamlaka ya kuajiri, kuadhibu na kusimamia wafanyakazi yako chini ya Bodi za Utumishi wa Umma za Kaunti (CPSBs). “CRA haina mamlaka ya kisheria ya kupuuza bodi hizi au kuingilia majukumu yake ya kusimamia ajira,” alisema. Chama hicho pia kilitaja Kifungu cha 6(2) cha Katiba, kinachotambua serikali za kitaifa na za kaunti kuwa tofauti lakini zinazotegemeana. Duba alionya kuwa chama kitapinga hatua yoyote itakayotekelezwa na CRA au serikali za kaunti ikiwa itahatarisha ajira za wanachama wake. Aliitaka tume hiyo kuondoa mapendekezo hayo na badala yake kutafuta njia za kuhakikisha kaunti zinapata fedha za kutosha kutekeleza huduma na kuwalipa wafanyakazi mishahara inayostahili. “Wanachama wetu wawe tayari kutetea ajira zao, familia zao na haki zao za kikatiba,” alisema. Kwa sasa, tishio la chama hicho linaongeza presha kwa serikali za kaunti, ambazo zinapaswa kusawazisha matumizi ya mishahara na mahitaji ya wananchi ya huduma bora za afya, barabara na huduma nyingine za umma.

ZANZIBAR: CCM Zanzibar’s Deputy Secretary-General Abdi Mahamoud Abdi has met with a delegation of leaders from the Communist Party of China (CPC) to discuss ways of strengthening relations and development cooperation between the two parties. The meeting, held at the CCM headquarters in Kisiwandui, Zanzibar, focused on leadership, infrastructure, trade, and efforts to promote unity…

LONGIDO: NAIBU Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, Dk. Stephen Kiruswa, ameitaka Kampuni ya Soils for the Future Tanzania kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusu mradi wa hewa ukaa ili kuondoa hofu na dhana kuwa mradi huo una malengo mabaya kwa jamii. Kiruswa alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara…

UJERUMANI: KIUNGO wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joshua Kimmich, amefiwa na baba yake mzazi, Berthold Kimmich, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57, vyanzo mbalimbali vya habari nchini Ujerumani vinaeleza Taarifa za vyombo vya habari vya Ujerumani zilizochapishwa leo, Oktoba 21, 2026, zimeripoti kuwa kifo hicho kimetokea ghafla,…

SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna amekuwa mlengwa wa matamshi makali kutoka kwa viongozi wa serikali ya Kenya Kwanza, huku akizidisha juhudi za kujijenga kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027. Baada ya Rais William Ruto, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi ndiye wa hivi punde kumkosoa Sifuna, akitilia shaka uwezo wa vuguvugu lake la Linda Mwananchi kuongoza taifa. “Wapo wanaokuja na chama ambacho hakijamaliza hata miezi sita, wakidai ndicho kitakachotoa dira. Tusikubali aina hiyo ya pata-potea ya kisiasa,” alisema Bw Mudavadi. Akizungumza katika kanisa la ACK, Jimbo la Kapsabet, Nandi, Jumapili, Bw Mudavadi alisema, “Wanaofikiria kuwa wanaweza kupandishwa juu kwa parachuti na kupewa uongozi nchini Kenya, ninawaambia kuwa parachuti hiyo itakatika wakiwa angani,” akaonya. Kauli hiyo ilijiri siku chache baada ya Rais Ruto kumshambulia Bw Sifuna na washirika wake wa kisiasa. Dkt Ruto amedai Seneta Sifuna na chama chake (The Equitable Party) kuwa hawana mwelekeo, huku akikejeli juhudi zao za kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi. “Mwenyewe hana kitu, chama chake hakina kitu. Halafu anaanza kuwaomba kina mama shilingi kumi kumi. Chama hicho kimekwama kwenye baa,” alisema Rais Ruto. Ingawa Rais amekuwa akiwakosoa pia viongozi wengine wa upinzani, wakiwemo Kalonzo Musyoka, Fred Matiang’i, Rigathi Gachagua na rais mstaafu Uhuru Kenyatta, mashambulizi dhidi ya Bw Sifuna yamejitokeza kwa uwazi zaidi katika siku za hivi karibuni. Bw Sifuna, ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa chama cha ODM, sasa anajaribu kupanua ushawishi wake nje ya chama hicho huku akipigia debe Linda Mwananchi kuwa vuguvugu la kisiasa linalolenga kuleta mabadiliko katika uongozi wa nchi. Akizungumza katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Jesus Teaching Ministry, Donholm, Nairobi, Sifuna alijibu wakosoaji wake kwa kusema kuwa uongozi haupaswi kuamuliwa na umri, utajiri au muda ambao mtu amekuwa katika siasa. “Tutaingia katika nyumba zenu, tutaingia katika maeneo yote ya taifa hili, na kijana ambaye amechaguliwa kwa muhula mmoja pekee kama seneta ataweka historia ya kuwa rais katika taifa hili la Kenya,” alisema Bw Sifuna. Aliongeza kuwa Wakenya hawapaswi kufungwa na dhana kuwa ni lazima mtu awe na umri fulani au kiwango fulani cha utajiri ili aweze kuwa rais. “Watu wamezoea kuwa siasa za Kenya lazima ziendeshwe kwa njia fulani: lazima uwe na umri fulani, lazima uwe na pesa kiasi fulani,” alisema. Aliwataka wafuasi wake kueneza ujumbe wa Linda Mwananchi kote nchini, akieleza kuwa vuguvugu hilo linaweza kuongoza taifa licha ya kuwa limekuwepo kwa muda mfupi. “Rais William Ruto, utaelewa manifesto yetu tu. Ulituambia tukupeleke pole pole, tutakupeleka pole pole lazima kitaeleweka!” alisema Bw Sifuna. Mwanachama wa Linda Mwananchi, Brian Weke pia alimjibu Rais Ruto kwa kugeuza kejeli ya “kutokuwa na kitu” kuwa hoja kuhusu kile anachodai kuwa msimamo wa kiongozi wao dhidi ya ufisadi na dhuluma. “Sifuna ni ‘Bw Kutokuwa na Kitu.’ Hana ufisadi, hana wizi wa mashamba, hajapiga vijana wetu risasi wala kuwanyanyasa Wakenya,” alisema Bw Weke. Katika mjadala huo, mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Prof Tom Namwamba anatathmini kuwa Bw Sifuna anajitokeza kuwa mshindani wa wanasiasa wa muda mrefu, hasa katika eneo la Magharibi mwa Kenya. Kwa mujibu wa Prof Namwamba, kukosa uzoefu mkubwa wa uongozi wa kitaifa si kikwazo kinachomzuia mtu kuwa rais, kwa kuwa uamuzi wa mwisho hufanywa na wapigakura. Alitolea mfano wa rais wa zamani wa Amerika, Barack Obama, aliyehudumu kama seneta wa jimbo la Illinois na baadaye kuchaguliwa kuwa rais mwaka wa 2008. “Ni wananchi wanaochagua. Wakimchagua Sifuna, wakosoaji wake ni nani kupinga uamuzi huo?” alisema Prof Namwamba. Hata hivyo, mfano huo hauondoi changamoto zinazowakabili wanasiasa wanaotaka kujenga uungwaji mkono wa kitaifa, ikiwemo kuunda kikosi, kuimarisha miundo ya chama na kuweka sera zinazoweza kuvutia wapigakura katika maeneo mbalimbali ya nchi. Umaarufu wa Seneta wa Nairobi pia umejitokeza katika tafiti za maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi wa urais wa 2027. Utafiti wa Infotrak wa Julai 2026 ulimweka Rais Ruto mbele kwa asilimia 32, akifuatwa na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa asilimia 13. Seneta Sifuna na aliyekuwa Waziri wa Usalama Fred Matiang’i walishika nafasi moja kwa asilimia 12 kila mmoja. Kwa upande mwingine, utafiti wa Trends and Insights for Africa (TIFA) uliofanywa Juni 2026 ulimpa Rais Ruto asilimia 24 ya uungwaji mkono kitaifa, huku Bw Sifuna akipata asilimia 15. Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 44 ya wafuasi wa ODM waliohojiwa walimtaja Bw Sifuna kuwa chaguo lao la kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho, ikilinganishwa na asilimia 20 waliomtaja Rais Ruto. Kulingana na Prof Namwamba, matokeo hayo yanaonyesha Bw Sifuna ana uungwaji unaostahili kutiliwa mkazo katika mjadala wa kisiasa, ingawa kura za maoni pekee haziwezi kuamua matokeo ya uchaguzi. Changamoto yake ni kugeuza uungwaji huo kuwa mtandao wa kisiasa unaovuka mipaka ya Nairobi na ngome za jadi za ODM, huku akijenga chama chenye uwezo wa kushindana katika maeneo mbalimbali ya nchi. Kadiri uchaguzi wa 2027 unavyokaribia, mvutano kati ya Sifuna na viongozi wa Kenya Kwanza unaendeleza mjadala kuhusu nafasi ya wanasiasa wapya, uzoefu wa uongozi na uwezo wa kujenga uungwaji mkono wa kitaifa katika siasa za Kenya.

MWANA wa mhubiri tata Paul Nthenge Mackenzie, Dan Mackenzie, ameeleza kuridhika kwake na hukumu iliyotolewa dhidi ya baba yake ya kupatikana na hatia ya kuua watoto 190 katika msitu wa Shakahola kati ya Januari 2021 na Septemba 2023. Dan alisema hana sababu ya kuhuzunika kwa sababu ya mtu ambaye mafundisho yake yalimfanya aache shule akiwa Darasa la Saba na kujitafutia riziki kwa kuendesha bodaboda. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, alisema hukumu hiyo imewaletea faraja familia zilizopoteza wapendwa wao katika mkasa huo, akisisitiza kwamba yeye mwenyewe alikuwa miongoni mwa walioathiriwa na mafundisho ya babake alipokuwa mtoto. “Ni faraja kwetu na kwa waathiriwa waliopoteza wapendwa wao Shakahola. Haki imetendeka. Ilikuwa kipindi kigumu kwetu na kwa waathiriwa. Sasa tumepata faraja na tunasubiri hukumu ya adhabu,” alisema. Dan, ambaye amejitenga na mafundisho ya kidini ya babake, alisema hakuhuzunishwa na uamuzi wa Jaji Diana Kavedza kwa sababu hakushiriki katika uhalifu huo. “Sihuzuniki kwamba babangu amepatikana na hatia. Niko sawa na nimetulia kwa sababu sikuhusika. Ana hatia,” alisema katika Mahakama Kuu ya Mombasa, ambako Mackenzie na washtakiwa wenzake 28 walipatikana na hatia katika mashtaka yote 191 ya mauaji. Hukumu hiyo ilimkumbusha Dan masaibu aliyopitia utotoni alipolazimishwa kufunga akiwa na umri wa miaka 12. Kukataa kwake kufunga kulizidisha uhasama kati yake na babake, na hatimaye akalazimika kuacha shule akiwa Darasa la Saba. Baadaye alianza kuendesha bodaboda mjini Malindi, kazi anayoendelea kufanya hadi sasa. “Tulianza kufunga nilipokuwa na umri wa miaka 12. Nilikataa. Babangu alinikatia tamaa na kuniambia nijitegemee. Hivyo ndivyo nilivyoishia kuendesha bodaboda mjini Malindi,” alisema. Dan pia alisimulia jinsi waumini wa kanisa hilo walivyompiga kwa karibu saa tatu kwa kukataa kuhudhuria ibada. Alimtaja Smart Mwakalama, naibu wa Mackenzie, kuwa miongoni mwa waliohusika. “Nimeathiriwa na mambo ambayo babangu amekuwa akifanya huko Shakahola. Ndiyo maana sikuishia msituni, kwa sababu nilikuwa nimechoshwa naye. Nililazimishwa kufunga kwa wiki moja nilipokuwa na umri wa miaka 12. Waumini hao, akiwemo Smart Mwakalama, walinipiga kwa karibu saa tatu ili tu nihudhurie ibada,” alisema. Mwakalama, mwanzilishi mwenza wa kanisa la Good News International Ministries (GNI), alielezwa kuwa mratibu muhimu wa usafirishaji wa wafuasi kutoka tawi la Furunzi mjini Malindi hadi msitu wa Shakahola. Dan alisema alitambua uzito wa yaliyokuwa yakitendeka Shakahola baada ya babake kukamatwa Aprili 2023 na kesi kuanza kusikilizwa mahakamani. “Hapo ndipo nilipogundua kwamba mambo aliyokuwa akitufanyia utotoni ndiyo aliyokuwa akifanya msituni,” alisema. Pia alifurahia kuokolewa kwa ndugu zake watano, dada watatu na wavulana wawili, waliokuwa wakiishi na nyanya yao katika nyumba ya familia eneo la Furunzi tangu Mackenzie alipokamatwa. Dan alisema aliripoti hali yao kwa polisi, hatua iliyosababisha msako na kuokolewa kwao. “Natumai sasa watakuwa na maisha mazuri,” alisema. Wakati wa ziara ya Mahakama Kuu nyumbani kwa Mackenzie mwezi Juni, Dan aliambia mahakama kwamba ndugu zake walikuwa wamezama katika mafundisho ya babake na kwamba misimamo mikali ya kidini ilikuwa imekita mizizi katika familia. Alitoa ushahidi huo katika kesi nyingine inayohusiana na mkasa huo, ambapo Mackenzie na wengine wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji kama uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na vifo vya watu 53 katika kijiji cha Kwa Bi Nzaro. Licha ya matendo ya babake, Dan alisema majirani zake wanaelewa kwamba hakuhusika na uhalifu huo.

…Shinkafi-Bagudu becomes first African to head UICC, raising hopes for improved cancer care across continent By Joseph Erunke, Abuja Nigeria has broken a major barrier in global cancer advocacy as renowned paediatrician and cancer control campaigner, Dr. Zainab Shinkafi-Bagudu, assumes the presidency of the Union for International Cancer Control (UICC), becoming the first African and […]

AMERIKA Jumatatu jioni ilipandisha kiwango cha tahadhari ya usafiri kwa Kenya kutoka hadhi ya pili hadi ya tatu (Level Two hadi Level Three) ikiwasihi raia wake kufikiria upya mipango ya kutembelea nchi hii. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na hatari za kiafya na kiusalama dhidi ya maambukizi ya Ebola. Kupitia taarifa, Wizara ya Masuala ya Nje Amerika ilitaja hatari ya Ebola, uhalifu, utekaji nyara, ugaidi, machafuko ya raia na usalama barabarani kama baadhi ya sababu za tahadhari hiyo. Kenya imethibitisha kisa kingine cha Ebola, na kufanya jumla ya visa kufikia vinane. Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt Patrick Amoth, alisema watu 38 walipimwa Jumapili, ambapo mmoja alipatikana na virusi vya aina ya Bundibugyo. Kisa hicho kilikuwa cha mhudumu wa afya aliyekuwa akiwaangalia wagonjwa.

DODOMA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, amesema matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi na Ukaguzi wa Vyombo vya Moto (MIMIS) yameendelea kuboresha ufanisi wa ukaguzi wa magari na usimamizi wa taarifa katika Jeshi la Polisi. Ayoub amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa za utekelezaji wa MIMIS…

TANZANIA: THE Parliamentary Standing Committee on Infrastructure has invited members of the public and other stakeholders to submit their views on Tanzania’s proposed ratification of the African Union Convention on Cyber Security and Personal Data Protection, 2014. In a statement issued yesterday, the Communication and Public Education Unit of the Parliament of Tanzania said the…

By Chinedu Adonu The Nigerian Medical Association (NMA), Enugu State chapter, has called for improved working conditions and greater attention to doctors’ welfare, warning that medical practitioners risk compromising their own health while caring for patients. The state Chairman of the association, Dr Ortuanya Emeka, made the call in Enugu during a press briefing to […]

KIONGOZI wa DCP, Rigathi Gachagua, jana alirejea nchini kimya kimya baada ya ziara ya miezi miwili Amerika. Katika mkutano wake wa kwanza wa hadhi ya juu baada ya kurejea, Bw Gachagua alikutana na mrengo wa Linda Mwananchi unaoongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, huku juhudi za kupata mgombea mmoja wa urais zikishika kasi. Duru kutoka kwa kambi ya Bw Gachagua zilisema mkutano huo ulikuwa hatua ya makusudi ya kuonyesha umoja kati ya eneo la Mlima Kenya na mrengo wa Linda Mwananchi. “Huu ni wa kwanza katika mfululizo wa mikutano na atakayefuata kukutana naye ni Kalonzo Musyoka, kisha wote watatu watahutubia mkutano wa pamoja wa kisiasa. Kuna jambo linaloendelea kwa makusudi, na yote ni katika juhudi za kuonyesha kuwa upinzani hauwezi kuendelea kukwepa suala la kuwa na mgombea mmoja wa urais,” duru hizo zikaarifu. Bw Gachagua aliandika kwenye mitandao ya kijamii: “Karibuni katika makazi ya Wamunyoro, binamu zangu kutoka Linda Mwananchi. Tunapoungana, mambo makubwa lazima yatokee.” “Jiandaeni kwa mshangao mkubwa kwa sababu mambo yanaendelea chini kwa chini. Hivi karibuni tutakuwa na mgombea mmoja, manifesto ya pamoja na mikakati ya pamoja ya kumkabili rais aliye mamlakani, ambaye ni lazima tumwondoe madarakani kwa njia ya kidemokrasia 2027, akasema Gavana wa Trans Nzoia, Bw George Natembeya kwenye mahojiano na Taifa Leo. Bw Sifuna aliandamana na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi, aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala, Pauline Njoroge, Faith Odhiambo, Reuben Ndolo miongoni mwa viongozi wengine Bw Gachagua sasa atakumbatia jitihada za kuimarisha uungwaji mkono wake eneo la Mlima Kenya, kutatua migogoro ndani ya chama chake na kushawishi upinzani kukubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Gachagua aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mapema jana siku ya Mashujaa, kabla ya kuelekea moja kwa moja nyumbani kwake Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri. Alirejea kimya kimya, tofauti na Agosti 2025, alipokabiliwa na vurugu wakati wa ziara yake ya awali kutoka Amerika. Makundi ya watu wenye silaha yalishambulia msafara wake kwa mawe kwenye Barabara ya Mombasa, na kujeruhi wafuasi wake na kumlazimisha kuahirisha mkutano wa Kamukunji. Safari hii, hakukuwa na msafara mkubwa wala umati wa wafuasi, lakini changamoto za kisiasa zinazomsubiri ni kubwa. Bw Gachagua alikatiza mkutano wa kisiasa wa siku 15 aliokuwa amepanga kufanya katika ranchi yake Texas, Amerika, baada ya siku 10. Alisema wafuasi wake nchini walikuwa wamemhimiza kurejea na kuongoza kampeni za upinzani dhidi ya azma ya Rais William Ruto kuwania muhula wa pili. Katibu Mkuu wa DCP, John Methu, alisema sasa watamakinikia kuimarisha chama, kuandaa wagombeaji wa uchaguzi wa 2027 na kujadiliana kuhusu mgombea mmoja wa urais.

RAIS William Ruto alitumia hotuba yake ya kuadhimisha Mashujaa Dei kusuta vinara wa upinzani wakiongozwa na vuguvugu la Linda Mwananchi ambapo aliwakejeli kwa kutafuta mamlaka bila mpango halisi. Katika ujumbe wake uliorejelea wapinzani wake hasa kinara wa The Equitable Party, Seneta Edwin Sifuna, Rais Ruto alisisitiza kwamba ushindani unapaswa kujikita kwenye sera na mipango thabiti badala ya migawanyiko, ukabila na kushambulia mahasimu. Akizungumza jana katika sherehe zilizofanyika Kipchoge Keino, Eldoret, Rais alionya kuhusu tishio la viongozi wanaojishughulisha kusaka mamlaka bila mpango thabiti akisema huenda wakakosa kuwajibika baadaye. “Kila kiongozi anapaswa kuwa tayari kuwasilisha rekodi na maono thabiti kuhusu wanapotaka kupeleka nchi ikiwemo mpango madhubuti kuhusu jinsi ya kufika hapo,” alisema Rais Ruto. Huku akinukuu kifungu cha Biblia, Rais alihoji kwamba demokrasia na uhuru hauna maana iwapo hautaboresha nafasi za kujiendeleza kiuchumi, kuboresha huduma za umma na maisha ya wanajamii kwa jumla. “Jinsi maandiko yanavyotukumbusha, imani bila matendo imekufa. Vivyo hivyo, uhuru na demokrasia bila maendeleo na ufanisi ni bure,” alisema Rais. “Wajibu wetu si kuhifadhi tu uhuru tuliorithi, bali kuhakikisha unageuka kuwa hadhi, nafasi na maisha bora kwa Wakenya.” Aidha, alitumia hotuba yake kupigia mageuzi kiuchumi yaliyofanikishwa na serikali yake kupitia miradi mikuu kama vile mpango wa nyumba za bei nafuu, afya, kilimo, ujenzi na ukarabati wa miundomsingi. Alitaja ukosefu wa kazi, barabara duni na ukosefu wa huduma za afya miongoni mwa vizingiti vikuu kwa Wakenya akiwakashifu wapinzani wake kwa kupinga miradi ya Kenya Kwanza bila kutoa suluhisho mbadala. “Unapendekeza nini kando na unachopinga? Alihoji. “Kama unatofautiana na nyumba za bei nafuu, eleza Wakenya jinsi utakavyowapa makazi bora na kuunda nafasi za kazi.” “Ikiwa unapinga mageuzi yetu ya huduma za afya, fafanua utakavyohakikisha kwmaba hakuna familia itakayolazimishwa kuchangisha pesa ili kulipa bili ya hospitali.:

RAIS William Ruto alitumia hotuba yake ya Mashujaa Dei kuorodhesha ufanisi wa serikali yake kiuchumi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, akiahidi kupunguza ushuru, kubuni nafasi zaidi za kazi kwa vijana na kuwezesha upatikanaji wa mali na teknolojia huku akitetea rekodi yake kuhusu kilimo, makazi, huduma ya afya na elimu. Akihutubu katika Uwanja wa Kipchoge Keino, jijini Eldoret, Rais alipendekeza kuwaondolea Ushuru wa Mishahara (PAYE) wafanyakazi wanaolipwa Sh32,333 kwa mwezi, kufuta ada ya ushuru inayotozwa biashara za ardhi yenye thamani ya Sh1 milioni au chini ya kiasi hicho. Rais alipendekeza kuondoa asilimia 25 ya ushuru unaotozwa bidhaa za kigeni kwa simu na kuunda nafasi 50,000 mpya za wanagenzi wa kulipwa kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo kuanzia Januari 2027. Alitangaza vilevile mipango ya kuongeza Sh5 bilioni kwenye mfuko wa Hasla Fund kabla ya mwisho wa mwaka, akitaja mikakati hiyo kuwa sehemu ya ajenda ya serikali yake kuhusu maendeleo kuanzia mashinani (BETA), aliyosema inanuiwa kuweka pesa zaidi mifukoni mwa wananchi na kuwaimarisha kiuchumi. Hotuba hiyo vilevile ilijumuisha ujumbe wa kisiasa huku rais akiwasilisha rekodi ya utawala wake kama ushahidi wa maendeleo huku akikiri kuwa Wakenya wana haki ya kudadisi kuhusu maamuzi ya serikali yake na kuitisha huduma bora. “Wananchi wana haki ya kuhoji serikali, kukosoa maamuzi yake na kuitisha yaliyo bora. Ni sharti tusikilize na kuwajibikia ahadi tulizotoa,” akasema Rais. Chini ya mapendekezo mapya, wafanyakazi wanaolipwa Sh32,333 au chini ya kiasi hicho kwa mwezi wataepushiwa PAYE, hivyo kuongeza pesa wanazotia mfukoni iwapo mikakati hiyo itaidhinishwa na kutekelezwa. Kulingana na rekodi rasmi, Kenya ina jumla ya wafanyakazi 3,468,997 walioajiriwa katika sekta rasmi. Mpango wa sasa wa kuepusha PAYE (Sh0 - Sh24,000) unawafaidi Wakenya 1,328,625. Hatua mpya ya kuondoa PAYE itawafaidi Wakenya wengine 362,846 na kufikisha idadi ya walioepushiwa ushuru huo kuwa 1,691,471. Rais alisema pendekezo hilo linadhamiriwa kuzipunguzia mzigo familia zinazotaabika kukidhi mahitaji ya chakula, usafiri na matumizi mengine ya kila siku. Pendekezo hilo limejiri huku Wakenya wakilalamikia kutozwa ushuru kupita kiasi, uwezo wa kumudu bidhaa muhimu na gharama ya maisha. Manufaa yake halisi yatategemea taratibu za sheria na utekelezaji ikiwemo jinsi uepushaji unavyohusiana na vitengo vilivyopo vya ushuru. Kulingana na Rais, thamani ya soko la hisa imeongezeka maradufu kutoka Sh2 trilioni hadi Sh4 trilioni, huku uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja ukipanda. Rais alisema serikali yake imewasajili wakulima milioni 8.9 na kupunguza bei ya mbolea kutoka Sh7,500 kwa mfuko 2022 hadi Sh2,000 chini ya mpango wa mbolea ya bei nafuu. Mifuko zaidi ya milioni 38 ya mbolea ya bei nafuu imesambazwa, alisema, na kuchangia kuongeza uzalishaji. Alitaja kuboreshwa kwa bei katika sekta za kahawa na majanichai akisema bei ya kahawa imepanda kutoka karibu Sh70 hadi kati ya Sh110 na Sh150 kwa kila kilo. Bei ya jumla kwa zao la majanichai imepanda kutoka Sh35 hadi Sh56 kwa kilo. Katika sekta ya maziwa, Rais alitangaza kuwa wakulima watapokea Sh65 kwa kila lita kuanzia mwezi huu pamoja na bonasi ya ziada ya Sh2 kwa kila lita itakayolipwa kila baada ya miezi mitatu. Alisema uzalishaji wa maziwa kitaifa umeongezeka kwa lita bilioni moja, huku bei zinazolipwa wakulima zikipanda kutoka Sh35 hadi Sh60 kwa kila lita kabla ya mabadiliko mapya. Serikali pia ilitoa chanjo kwa zaidi ya mifugo milioni 22 na kupanua bima ya kiangazi kwenye mpango unaolenga wafugaji milioni 1.6 katika kaunti 21, alisema. Kuhusu miundomsingi, Rais alitaja ukarabati wa barabara kuu ya Rironi-Mau Summit, kuendeleza reli ya Standard Gauge (SGR) kuelekea Kisumu na Malaba, na barabara ya Lake Victoria Ring Road. Alitaja mipango ya kukarabati uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta na kuboresha mikondo mikuu ya usafiri akihoji kuwa uwekezaji katika miundomsingi ni muhimu katika kufanikisha ukuaji kiviwanda na sekta ya kibinafsi. Katika huduma ya afya, Rais alisema idadi ya wakenya waliosajiliwa chini ya Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) imeongezeka hadi 33.3 milioni, ikilinganishwa na milioni saba chini ya NHIF iliyovunjiliwa mbali.

…Targets expansion, higher profitability By Emma Ujah, Abuja Bureau Chief Infinity Trust Mortgage Bank Plc is set to raise ₦50 billion in fresh capital to strengthen its financial capacity, expand operations and improve its competitiveness in Nigeria’s mortgage banking industry. The Chairman of the bank, Dr. Nkechi Bibilari, disclosed this after shareholders unanimously approved the […]

…Raise questions over profiling of Igbo youths …Group demands investigation into alleged sponsors of insecurity in South-East By Steve Oko UMUAHIA — The Indigenous People of Biafra (IPOB) has called for a thorough investigation into the abduction of prospective National Youth Service Corps (NYSC) members along the Owerri–Onitsha Expressway in Imo State, following the arraignment […]

MUUGUZI Jacobeth Jeptoo ni miongoni mwa Wakenya 264 waliotunukiwa tuzo za heshima wakati wa sherehe za 63 za Sikukuu ya Mashujaa katika Uwanja wa Kipchoge Keino, Eldoret. Walituzwa kutokana na mchango wao katika ukombozi, demokrasia, elimu, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya taifa. Bi Jeptoo alitambuliwa kwa ujasiri wake wa kuwasaidia manusura wa ajali ya helikopta iliyoua Mbunge wa Emurua, Dikirr Johana Ng’eno na watu wengine watano katika Kaunti ya Nandi mnamo Februari 2026. Muuguzi huyo alikimbilia eneo la ajali Chepkiep, Kaunti Ndogo ya Mosop, akiwa na glavu na kujaribu kuwasaidia waathiriwa licha ya hatari iliyokuwepo.Alipewa sifa kwa ujasiri, huruma na hatua za haraka za kuokoa maisha. Miongoni mwa mashujaa wengine waliotambuliwa ni Waziri Mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga, mwanaharakati wa demokrasia Philomena Mutai Chelagat, mpiganiaji uhuru Pio Gama Pinto, mwanahistoria Prof Bethwell Allan Ogot, mwanasayansi Prof Calestous Juma na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani John Michuki. Raila alitunukiwa heshima baada ya kifo chake kwa mchango wake katika demokrasia ya vyama vingi, mageuzi ya katiba na haki za kijamii. Alipinga utawala wa chama kimoja na kusaidia kupatikana kwa uhuru wa kisiasa. Pia alishiriki katika mageuzi yaliyochangia kupitishwa kwa Katiba ya 2010 alipokuwa Waziri Mkuu kati ya 2008 na 2013. Mashujaa wa ukombozi waliokumbukwa ni Koitalel Arap Samoei, Mekatilili wa Menza, Dedan Kimathi na Field Marshal Muthoni wa Kirima. Rais William Ruto pia aliwakumbuka Mzee Jomo Kenyatta na waliokuwa pamoja naye katika harakati za kupigania uhuru. Katika sekta ya elimu na utafiti, Profesa Ogot alitambuliwa kwa mchango wake katika historia ya Afrika, huku Profesa Juma akiheshimiwa kwa utafiti wake kuhusu sayansi, teknolojia na maendeleo. Bw Michuki alitambuliwa kwa juhudi zake za kuhifadhi mazingira, huku mwanariadha Kipchoge Keino na wanamichezo wengine wakipongezwa kwa kuiwakilisha Kenya kimataifa na kung’aa katika fani zao. Rais Ruto alisema kuwakumbuka mashujaa hakupaswi kuishia kwenye sherehe, bali Wakenya wanapaswa kulinda uhuru, demokrasia na Katiba waliyojitolea kuipigania. Alisisitiza kuwa wajibu wa kizazi cha sasa ni kujenga taifa lenye usawa na fursa kwa kila mwananchi.

Local Yemeni authorities on Tuesday raised the death toll from a Houthi strike a day earlier on a military camp belonging to government forces to 73, as fighting between the foes escalates.

The United States on Tuesday warned its citizens against travel to Kenya, raising its travel advisory after the country reported an eighth Ebola case.

The latest advisory retains warnings over crime, kidnapping, terrorism and unrest, alongside health and road-safety concerns.

Mabadiliko ya kidijitali barani Afrika yanaibua ushindani mpya wa kimkakati kuhusu rasilimali inayozidi kuwa na thamani kubwa duniani: data. Kadiri serikali, benki, kampuni na wananchi wanavyohamishia huduma zao kwenye mifumo ya kidijitali, miundombinu inayohifadhi na kuchakata taarifa za Waafrika inazidi kuwa muhimu kiuchumi na kiusalama. Mjadala huu hauhusu tena upatikanaji wa intaneti pekee. Sasa unahusu…

POLISI jijini Nairobi wanachunguza mauaji yanayoshukiwa ya Faruz Hussein, 21, zaidi ya wiki mbili baada ya tukio hilo kuripotiwa. Mpenziwe anadaiwa kumnyonga kwa kutumia mto (pillow) kabla ya kurekodi tukio hilo na kutuma video kwa familia yake. Video hiyo ilipoibuka mitandaoni, ilizua ghadhabu huku Wakenya wakitaka hatua za haraka zichukuliwe. Kwa mujibu wa familia, Hussein aliuawa baada ya mzozo wa nyumbani. Jamaa zake walipata habari kuhusu tukio hilo baada ya mshukiwa kuwatumia video hizo. Familia hiyo pia inadai kuwa mshukiwa alitishia kumuua dadake mdogo Hussein, mama yao na kaka yake mwenye umri wa miaka 15, akionya kuwa angeangamiza familia nzima. Familia iliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Sunton, Kasarani, Kaunti ya Nairobi, Septemba 30, 2026, chini ya nambari ya OB 37.

Makala hii inaeleza namna uwepo wa kambi za kijeshi za mataifa ya kigeni barani Afrika unavyoibua mjadala kuhusu usalama, uhuru wa mataifa na ushindani wa madola makubwa duniani. Mazingira ya usalama barani Afrika yanazidi kuwa na uwepo wa majeshi ya mataifa mbalimbali ya kigeni, huku serikali zikikabiliwa na changamoto ya kusawazisha mahitaji ya usalama wa…

DAR ES SALAAM; Chama cha Mafundi Rangi na Ujenzi Tanzania (CHAMARAUTA) kimeiomba Serikali na wadau wa sekta ya ujenzi kuwapa mafundi nchini fursa za kushiriki katika miradi mbalimbali ya ujenzi ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao. Mwenyekiti wa CHAMARAUTA, Juma Chakusaga, ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa…

Madini muhimu, nishati, miundombinu, teknolojia, njia za biashara, ushirikiano wa kiusalama na ushawishi wa kisiasa vinazidi kuwa sehemu ya ushindani wa mataifa yenye nguvu kutafuta ushirikiano mpana zaidi barani Afrika. Afrika imekuwa miongoni mwa maeneo muhimu katika ushindani wa kisiasa na kimkakati duniani, huku Marekani, China, Russia na Umoja wa Ulaya wakizidisha jitihada za kujenga…

DAR ES SALAAM: Sera ya muda mrefu ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote inakabiliwa na mtihani mpya wa kijiografia kutokana na kuongezeka kwa ushindani kati ya mataifa yenye nguvu duniani, ikiwamo Marekani, China, Russia, India na mataifa mengine, ambao unazidi kuenea barani Afrika. Badala ya kuchagua upande mmoja wa nguvu za kisiasa duniani, mfumo…

KUGUNDULIWA kwa mamia ya miili katika makaburi ya kina kifupi katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, kuanzia Machi 20, 2023, ulifichua mkasa uliotokana na miaka mingi ya itikadi kali za kidini. Kiini cha mkasa huo kilikuwa mhubiri Paul Mackenzie, aliyeaminisha wafuasi wake kuwa kufunga hadi kufa kungewasaidia kukutana na Yesu. Mackenzie alianzisha kanisa la Good News International (GNI) mnamo 2003 ila likasajiliwa rasmi mnamo 2010. Mnamo 2012, huduma hiyo ilisajili kampuni ya Good News Media (K) Limited, iliyoendesha kituo cha televisheni cha Times TV mjini Malindi. Kwa miaka mingi, shughuli zake ziliibua wasiwasi kuhusu itikadi kali, elimu ya watoto na kukataa matibabu ya kisasa. Wafuasi waliitwa Wateule na kufundishwa kuachana na mali za dunia, huku serikali ikisawiriwa kama adui. Mnamo 2017, Mackenzie alikabiliwa na mashtaka yaliyohusiana na kueneza itikadi kali na kuendesha taasisi ya elimu isiyosajiliwa. Katika kesi moja, aliachiliwa baada ya makubaliano na upande wa mashtaka na kuamriwa kudumisha tabia njema. Katika kesi nyingine, aliachiliwa kwa dhamana na hatimaye akaachiliwa huru mnamo 2021. Mnamo mwaka huo huo, watoto 43 wenye umri wa kati ya mwaka mmoja na 13 waliokolewa kutoka katika majengo ya GNI eneo la Mayungu. Ripoti zilisema baadhi yao walizuiliwa, kunyimwa elimu na kufundishwa dini. Mahakama iliagiza wapate ushauri nasaha na matibabu kabla ya kurejeshwa kwa familia zao. Mnamo 2019, Kamati ya raia wa Mahakama ya Kaunti ya Kilifi ilijadili malalamishi kuhusu kuenezwa kwa itikadi kali kwa watoto kupitia kanisa na televisheni ya Mackenzie. Mamlaka ya Mawasiliano baadaye ilifuta leseni ya Times TV. Mackenzie pia alishtakiwa kwa kusambaza filamu zisizokaguliwa na kuendesha studio bila leseni. Mnamo Novemba 10, 2023, alipatikana na hatia ya makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi sita, lakini akaachiliwa huru kuhusu shtaka la kuchochea watu kukiuka sheria. Wakati huo, baadhi ya wafuasi wake walikuwa wameanza kuhamia Shakahola mnamo 2019, huku idadi ikiongezeka wakati wa janga la Corona. Upande wa mashtaka ulisema walifundishwa kufunga hadi kufa ili waende mbinguni, huku watoto wakitarajiwa kufa kwanza, wakifuatiwa na wanawake kisha wanaume. Mackenzie na washukiwa wenzake 30 baadaye walishtakiwa kwa mauaji ya watoto 191. Wote walikana mashtaka. Mahakama Kuu ya Malindi iliamuru mnamo 2024 mashtaka hayo yapunguzwe yasizidi 12, lakini Mahakama ya Rufaa ilirejesha mashtaka yote 191 Aprili 11, 2025. Kesi ilianza kusikilizwa Agosti mwaka jana baada ya mvutano wa kisheria, na hukumu ikatolewa katika Mahakama Kuu ya Mombasa Jumatatu. Baada ya mkasa huo kufichuliwa, JSC ilisema ingechunguza jinsi kesi za awali za Mackenzie zilivyoshughulikiwa ili kubaini iwapo kulikuwa na mapungufu katika utoaji wa haki. Mkasa wa Shakahola umeibua maswali kuhusu jinsi mamlaka zilivyoshughulikia tahadhari kadhaa za awali na iwapo kuchukuliwa kwa hatua za mapema zingeweza kuzuia vifo hivyo.

DODOMA: THE Parliamentary Standing Committee on Administration, Constitution and Legal Affairs has called for intensified public education on FAIDA Fund to boost participation among public servants, saying greater awareness could help workers grow their savings, improve their financial security and prepare for home ownership. The call follows the fund’s growth in net asset value to…

VYAMA vya kisiasa vinaendelea kuongezeka nchini huku viongozi wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2027, hali inayoibua maswali kuhusu iwapo miungano hiyo inasukumwa na sera au maslahi ya kisiasa. Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) imetoa vyeti kamili vya usajili kwa vyama vingine sita na kufikisha jumla ya vyama vilivyosajiliwa kikamilifu 107. Zaidi ya vyama 30 vingine vina usajili wa muda, ikilinganishwa na vyama 90 vilivyokuwepo kabla ya uchaguzi wa 2022. Wachanganuzi wanasema baadhi ya viongozi wanaanzisha au kupata umiliki wa vyama ili kudhibiti tiketi za uteuzi, kuimarisha nafasi zao katika mazungumzo ya miungano na kupata manufaa ya kifedha. Miongoni mwa vyama vipya ni Mwongozo Mpya Party (MMP), Imarisha Uchumi Party (IUP), United Super Alliance Party (USAP), Forward Kenya Party (FKP), People’s Prosperity Party (PPP) na Freedom and Opportunity Party (FOP). Aliyekuwa Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Eliud Owalo, aliyeanzisha PPP, amesema chama hicho kitalenga urais na pia kusimamisha wagombeaji katika nyadhifa zote za uchaguzi. Msajili wa Vyama vya Kisiasa, John Cox Lorionokou, amevitaka vyama kuzingatia katiba zao na kuhakikisha vijana pamoja na watu wenye ulemavu wanapata nafasi sawa za kushiriki katika shughuli za kisiasa. Vyama vingine vilivyoibuka ni Democracy for the Citizens Party (DCP) kinachohusishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, People’s Renaissance Movement cha Caleb Amisi na United Progressive Movement (UPM) kinachohusishwa na Boni Khalwale. Viongozi wengine waliamua kupata umiliki wa vyama vilivyokuwapo badala ya kuanzisha vipya. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amejipatia The Equitable Party (TEP), huku Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino akijipatia Muungano Party na kukibadilisha jina kuwa Mwananchi Party (TMP). Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amepata People’s Party of Kenya (PPK), huku Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya akihusishwa na United Democratic Party. Umiliki wa chama huwapa viongozi mamlaka ya kisheria ya kusimamia uteuzi wa wagombeaji na kuamua tiketi zitakazotolewa. Vyama pia hukusanya ada za uteuzi, ambazo zinaweza kufikia Sh50,000 kwa kila wadhifa. Aidha, vyama vinaweza kupata fedha kutoka kwa Hazina ya Vyama vya Kisiasa kulingana na matokeo ya uchaguzi. Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa ya 2022 yaliongeza vyama vinavyoweza kunufaika na mgao kutoka kwa hazina hiyo. Asilimia 70 ya fedha hizo hugawanywa kulingana na kura zilizopatikana, asilimia 15 kwa kuzingatia wawakilishi waliochaguliwa kutoka makundi maalumu, huku asilimia 10 ikitegemea idadi ya wawakilishi waliochaguliwa. Asilimia tano hutumiwa na ORPP kwa usimamizi. Vyama pia hupata nafasi za uteuzi katika Bunge la Kitaifa, Seneti na mabunge ya kaunti.

The alert comes as Kenya confirms eight Ebola cases amidst a broader regional outbreak.

SERIKALI za kaunti zinatarajiwa kupokea Sh71.09 bilioni zaidi katika mwaka wa kifedha wa 2026/2027, baada ya Rais William Ruto kutia saini sheria mpya inayolenga kuimarisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. Rais alitia saini Mswada wa Fedha za Ziada kwa Serikali za Kaunti 2026 kuwa sheria katika Ikulu ndogo ya Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, jana kabla ya maadhimisho ya Siku ya Mashujaa leo. Fedha hizo zimeongezeka kwa Sh425.6 milioni kutoka Sh70.67 bilioni zilizotengewa kaunti katika mwaka wa kifedha wa 2025/2026. Sheria hiyo mpya pia inamtaka Waziri wa Hazina ya Kitaifa kuchapisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu fedha zilizohamishiwa kwa serikali za kaunti. Ripoti hizo zinapaswa kutolewa ndani ya siku 30 baada ya kumalizika kwa kila robo mwaka. Mswada huo ulidhaminiwa na Seneta Ali Roba, mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Fedha na Bajeti. Ulichapishwa Machi 16, 2026, na kusomwa kwa mara ya kwanza katika Seneti Aprili 2. Seneti iliupitisha pamoja na marekebisho Juni 17, kabla ya Bunge la Kitaifa kuupitisha pia kwa marekebisho Agosti 4. Seneti ilikubaliana na marekebisho ya Bunge la Kitaifa Oktoba 6, na hivyo kupisha mchakato wa Rais kutia saini mswada huo. Kati ya fedha hizo, Sh56.38 bilioni ni mgao wenye masharti unaofadhiliwa kupitia mikopo na ruzuku kutoka kwa washirika wa maendeleo. Nazo Sh12.73 bilioni zitatokana na mgao wa mapato ya serikali ya kitaifa, huku Sh1.83 bilioni zikitokana na mirabaha ya madini inayostahili kaunti.

MAHAKAMA Kuu jana ilimpata mhubiri matata Paul Mackenzie na washukiwa wenzake 30 na hatia ya kushirikiana, kutekeleza na kudumisha mfungo uliosababisha vifo vya mamia ya watoto na watu wazima katika msitu wa Shakahola, Kilifi. Katika uchambuzi wake wa mashtaka 191 ya mauaji, Jaji Diana Kavedza alisema vifo hivyo vilisababishwa na vitendo na uzembe usio halali wa watu waliotekeleza na kudumisha mfungo huo, badala ya kuwa matokeo yasiyokusudiwa ya shughuli za kidini. “Baada ya kuzingatia ushahidi wote, mahakama hii imebaini kuwa washtakiwa ambao ushiriki wao binafsi umethibitishwa walitenda kwa pamoja utekelezaji wa lengo moja lisilo halali la kuanzisha na kudumisha mfungo uliosababisha vifo vya watu wengi Shakahola,” akasema Jaji Kavedza. Jaji huyo alibaini kuwa ingawa kila mshtakiwa alikuwa na jukumu tofauti, vitendo vyao vilikuwa sehemu ya mpango mmoja wa uhalifu. Hata hivyo, kila mmoja alipaswa kuwajibishwa kwa msingi wa ushahidi unaoonyesha ushiriki wake na nia yake ya kutenda uhalifu. Kabla ya kuchambua mashtaka ya mauaji, mahakama pia ilibainisha kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka uliibua maswali kuhusu uwezekano wa vitendo hivyo kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya binadamu. Jaji Kavedza alikataa hoja kwamba watoto waliofuata maagizo na kuendelea kufunga hadi kufa walikuwa wameamua kufanya hivyo kwa hiari yao wenyewe. Alisema watoto wenye umri wa kati ya miaka sita na 10 hawakuwa na uwezo wa kutafakari kwa kina na kuelewa kuwa kifo ni cha kudumu. Mawazo yao, tabia ya kutenda bila kufikiria na uelewa wao mdogo viliwafanya kuwa rahisi kudanganywa. “Kwa hivyo, inawezekana watoto katika kundi hili, kutokana na msisimko wa shahidi huyu, licha ya kuonekana kama mifupa iliyofunikwa kwa ngozi, waliamini kuwa kifo kinaweza kubatilishwa,” akasema . Alibaini kuwa watoto hao hawangeweza kutoa ruhusa ya hiari, yenye ufahamu na inayokubalika kisheria ya kujinyima chakula hadi kufa. Mahakama ilisema kutokupinga maagizo au kukubali mafundisho hayo hakumaanishi kuwa watoto walikuwa wameamua kufa kwa hiari. Badala yake, mwenendo wao ulipaswa kuangaliwa katika mazingira ya imani za kidini, utegemezi kwa watu wazima, mamlaka ya wazazi, udanganyifu, hofu na shinikizo. “Mahakama imebaini kuwa vifo vilivyosababishwa na njaa vilitokana na vitendo au uzembe usio halali wa wale waliotekeleza mfumo wa mfungo,” akasema Jaji Kavedza. Mashahidi wa upande wa mashtaka walisema kuwa katika mikutano ya maombi chini ya miti Shakahola, Mackenzie aliwaambia wafuasi kuwa Yesu hangekuja kuwaelekeza kufunga hadi kufa ili waende mbinguni. Ushahidi ulionyesha kuwa wazazi waliagizwa kuwanyima watoto wao chakula, kabla ya kuanzishwa kwa mfungo mkavu uliokataza wafuasi kunywa maji. Maagizo hayo yalihusu waumini wote, wakiwemo watoto ambao hawakuwa na uwezo wa kuelewa kikamilifu matokeo yake. Jaji alisema maagizo hayo yalikuwa ya lazima, huku juhudi zikifanywa kuzuia wafuasi kuacha mfungo. Hali hiyo ilikuwa muhimu katika kutathmini nia ya washtakiwa. Alisema maelezo ya kidini yaliyotolewa kuhalalisha mfungo hayangeondoa moja kwa moja nia ya kutenda uhalifu. Mahakama ilipaswa kuchunguza nia ya vitendo hivyo, kwani lengo la kiroho halimaanishi kuwa mtu hawezi kuwa na nia ya kusababisha kifo. Vifo vilivyoendelea kutokea na hali ya wafuasi kudhoofika kimwili pia vilizingatiwa. Mfungo uliendelea licha ya dalili za wazi za madhara yake. Mahakama pia ilichunguza ushahidi kwamba nguvu zilitumiwa kuwalazimisha wafuasi kutii na kuwazuia watu wa nje kuwafikia waliokuwa wakifunga. Njia za kuingia katika baadhi ya makazi zilifungwa kwa matawi na miiba, huku wahanga waliodhoofika kwa njaa wakiachwa bila msaada. Mnamo Machi 23, 2023, shahidi wa upande wa mashtaka aliingia msituni akiwa na waandishi wa habari. Alisema Julius Katana alimtishia, huku mshtakiwa mwingine akimshika shingoni na kumkandamiza chini.Wengine walidaiwa kumpiga na kumsababishia majeraha kichwani na kwenye mbavu. Washukiwa hao wanatarajiwa kurejea mahakamani Novemba 6 kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja kuhusu hukumu watakazopewa. Shahidi mwingine alithibitisha tukio hilo, ambalo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Lango Baya. Upande wa mashtaka pia uliwasilisha ushahidi kuhusu kushambuliwa kwa afisa wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS) aliyeingia msituni. Jaji alisema matukio hayo yalikuwa muhimu katika kutathmini iwapo mfungo ulidumishwa kwa vitisho, vizuizi na vurugu, na kama washukiwa walielewa matokeo ya vitendo vyao. Ushahidi kutoka kwa Msajili wa Mashirika ulionyesha kuwa Mackenzie alikuwa mkuu wa Good News International Ministries, huku mshtakiwa wa pili akiwa katibu. Mashahidi walisema Mackenzie aliongoza mikutano chini ya miti Shakahola na kutoa maagizo kwa waumini. Baada ya kanisa na kituo cha televisheni cha Times Television kufungwa, aliwaambia wafuasi kuwa kanisa lilikuwa likihamia Shakahola, akitaja eneo hilo kama “Kanisa Jangwani”. Mackenzie alihusishwa na maagizo ya kuwalazimisha wafuasi kufunga, huku baadhi ya mashahidi wakieleza kuhusu kupigwa na matumizi ya mijeledi dhidi ya waliopinga. Baada ya kutathmini ushahidi wote, jaji alisema washukiwa ambao ushiriki wao binafsi ulithibitishwa walitenda kwa pamoja kutekeleza na kudumisha mfungo uliosababisha vifo hivyo. “Nimeridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake bila kuacha shaka ya msingi. Kwa hivyo, kila mshtakiwa anapatikana na hatia katika mashtaka yote 191 ya mauaji na anatiwa hatiani kama alivyokuwa ameshtakiwa,” akasema Jaji. Washukiwa hao wanatarajiwa kurejea mahakamani baadaye kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja kuhusu hukumu watakazopatiwa.

By Chioma Obinna As competition in Nigeria’s non-alcoholic beverage market continues to evolve, Maltina, one of the country’s longstanding malt drink brands, has unveiled a refreshed visual identity to mark its 50th anniversary, retaining its familiar taste while introducing redesigned packaging across its product range.The new identity, unveiled by Nigerian Breweries Plc last week, features […]

“The CityBoy Movement, to all of you, you have done something new in Nigeria politics. You did not just gather people; you built a structure, millions of real, verifiable members,” the President said.

MVUTANO kati ya Rais William Ruto na Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya kuhusu kutenga vibanda katika Soko la Masinde Muliro, Kitale, ulichacha jana huku polisi wakitumwa kulinda usalama na wafanyabiashara wakilalamikia kupoteza mapato. Maafisa wenye silaha kutoka Kikosi cha Kukabili Fujo (GSU) na Polisi wa Utawala (AP) walitumwa katikati ya mji wa Kitale, huku baadhi ya barabara zikifungwa na wafanyabiashara kufunga maduka yao kutokana na hofu ya ghasia. Hali ya wasiwasi pia ilizuka katika makao makuu ya kaunti ya Trans Nzoia baada ya polisi kuvuruga mkutano wa maombi uliokuwa ukiendelea. Gavana Natembeya amesema ataomba Seneti na mahakama kuingilia kati kutatua mzozo huo, akisisitiza kuwa suala hilo linahusu ugatuzi na mamlaka ya serikali ya kaunti. “Nataka Seneti iingilie kati na kusaidia kutatua mzozo huu. Seneti iliundwa kuwa mtetezi wa ugatuzi, na sasa ni wakati wa Bunge hilo kuingilia kati,” alisema Natembeya wakati wa ibada ya kanisa Jumapili. Soko hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh800 milioni lilijengwa na serikali ya kaunti kwa usaidizi wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, mchakato wa kugawa vibanda umesababisha mzozo kati ya viongozi wa kitaifa na wale wa kaunti. Rais Ruto amepinga mchakato wa ugavi uliofanywa na serikali ya kaunti na kusema vibanda vilivyosalia vitagawiwa kwa njia ya bahati nasibu. Bw Natembeya, kwa upande wake, amedai kuwa wafanyabiashara kutoka Uganda walipewa vibanda vingi ingawa madai yake hayajathibitishwa. Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara Kenya (KNCCI) katika kaunti hiyo, Titus Kilong’i, alizua maswali kuhusu mamlaka ya kamishina wa kaunti kuhusika katika ugavi wa vibanda. “Je, kamishina wa kaunti ndiye aliyejenga soko hili kiasi cha kuingilia kati na kugawa vibanda? Baada ya kuvigawa, ndiye atakayekusanya mapato? Je, sheria inamruhusu kufanya hivyo?” aliuliza. Bw Kilong’i alisema orodha za mgao ina utata, akidai kuwa jina la mtu mmoja lilionekana hadi mara nane katika orodha tofauti za masoko. “Tunatakiwa kulipa ushuru, lakini kuna mkanganyiko na tunatishwa. Tutawezaje kuendelea kuishi?” akauliza. Mkurugenzi mtendaji wa KNCCI, Antony Masika, alisema wafanyabiashara wameathirika tangu Alhamisi, huku baadhi yao wakikadiria hasara kutokana na biashara kuvurugwa. Mfanyabiashara Belinda Nakhumicha alisema kufungwa kwa maduka na hali ya wasiwasi imewaathiri wafanyabiashara wanaotegemea mapato ya kila siku. Hata hivyo, washirika wa Rais wameunga mkono miradi yake ya maendeleo katika eneo hilo. Aliyekuwa Waziri wa Afya Susan Nakhumicha alisema wakazi wanafurahia hatua za serikali ya kitaifa kuhusu miradi ya maendeleo na kuingilia kati katika kutenga vibanda sokoni humo. “Tunafurahia yale ambayo Rais ametufanyia, ikiwemo ziara yake katika kaunti wiki iliyopita. Sisi kama wakazi wa Trans Nzoia tunamshukuru sana,” akasema

DODOMA: KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Faris Buruhani, amekiomba Chama hicho kuchunguza tuhuma za rushwa zinazodaiwa kuwakabili baadhi ya vijana ili ukweli ubainike na haki itendeke. Buruhani ametoa ombi hilo leo Oktoba 19, 2026 jijini Dodoma alipozungumza na vijana waliojitokeza kumpokea katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM, kufuatia…

IKUNGI, SINGIDA: Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Singida imekuja na mbinu mpya ya kutumia ngoma za asili kuelimisha wananchi madhara ya rushwa na umuhimu wa uadilifu katika jamii. Hayo yamedhihirika wakati wa tamasha la la ngoma za asili lililofanyika katika kata ya Iyumbu, wilayani Ikungi, Singida mwishoni mwa juma ambapo vikundi…

The Christian Association of Nigeria (CAN) has mourned former Delta State Governor, Dr Emmanuel Eweta Uduaghan, praising his commitment to dialogue and confidence-building during a period of heightened political tension in Nigeria.

DODOMA: DISCIPLINE, courage and professionalism in carrying out international peacekeeping duties are among the qualities demonstrated by Tanzania Immigration Department officers who served in the United Nations Interim Force in Lebanon (UNIFIL). Their participation contributed to international efforts to maintain peace and security while representing Tanzania with distinction on the international stage. The commendation was…

SHAMBA la kahawa la Kiganda lenye ukubwa wa hekta 65 eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a, limekuwa la kwanza Barani Afrika kupata cheti cha Rainforest Alliance Regenerative Agriculture Standard baada ya kubadili namna linavyolima kahawa kwa kuzingatia afya ya udongo, uhifadhi wa maji na mazingira. Shamba hilo, lililokodishwa na kusimamiwa na Coffee Management Services (CMS), hutumia mbolea ya mifugo hasa samadi, mabaki ya matawi yaliyopogolewa kama matandazo, mimea inayoongeza Nitrojeni kwenye udongo na mbinu asilia kudhibiti wadudu. Meneja Mkuu wa CMS Martin Ngare anasema Kiganda huzalisha kati ya tani 110 na 120 za kahawa mbichi kwa mwaka, sawa na karibu makontena sita, ambazo nyingi huuzwa Ulaya na Amerika. “Taji na utambuzi huu unajiri wakati mabadiliko ya tabianchi yanaathiri sekta ya kilimo, yakiweka shinikizo kwa uzalishaji wa kahawa kufuatia kuongezeka kwa kiwango cha joto, mvua isiyotabirika na kuongezeka kwa wadudu na magonjwa,” anasema. Anasema kilimo endelevu kinasaidia kufanya shamba kustahimili changamoto hizo huku likidumisha uzalishaji na ubora. “Mjadala ni kuhusu uboreshaji wa afya ya udongo, kuhifadhi maji, kuongeza bioanuwai na kuhakikisha mazingira mazuri kwa wafanyakazi na watu wanaoishi karibu na shamba,” Ngare anaelezea. Kiganda hufanya vipimo vya udongo ili kubaini virutubisho vinavyokosekana kabla ya kutumia mbolea. Mwaka uliopita, 2025, takriban malori 85 ya samadi yaliwekwa shambani ili kuongeza rutuba na kuboresha uwezo wa udongo kustawisha kahawa. Matawi yanayopogolewa (pruned) huachwa ardhini ili kuoza na kurejesha virutubisho. [caption id="attachment_193144" align="aligncenter" width="300"] Paul Kabubi, meneja wa Kiganda Farm Estate, akiweka chokaa (lime) kwenye mkahawa mnamo Agosti 27, 2026, katika eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a. Picha|Sammy Waweru[/caption] Miti kama Albizia, Ngare anasema hutumika kutoa kivuli, kuupa udongo Nitrojeni na kusaidia kuleta virutubisho. Katika uhifadhi wa maji, udongo ulioinuliwa unazunguka mikahawa na husaidia kuelekeza maji kwenye mizizi, baada ya umwagiliaji wa juu kusababisha upotevu mkubwa wa maji wakati joto linapofikia nyuzijoto 33 hadi 35. Udhibiti wa wadudu Kiganda Farm pia umebadilika. Badala ya kunyunyizia dawa shamba lote, wafanyakazi hufuatilia miti ili kubaini maeneo yaliyoathirika. Mbinu za kibayolojia hutumiwa pamoja na maadui wa kahawa kama vile wasps na ladybirds, huku dawa zikitumika kwa miti iliyoathirika pekee. Julius Ng’ang’a, Mkurugenzi Mkuu wa Impact Programmes in East and Southern Africa at the Rainforest Alliance, anasema shamba la Kiganda kutambuliwa Barani Afrika ni hatua muhimu kwa sekta ya kahawa. “Hali ya hewa inabadilika, joto linaongezeka, wadudu magonjwa ya mimea yanaongezeka. Mashamba lazima yabadilike, yabadilishe mifumo yake ya uzalishaji chakula na kukumbatia ile bora na salama kwa afya ya watu,” anasisitiza. Karugu Macharia, Mwenyekiti wa Kenya Coffee Platform, anasema kilimo endelevu si mbinu mpya. “Unapoweka samadi kwenye udongo, unaongeza rutuba na kuufanya uwe hai,” anasema, akiongeza kuwa mbinu hizo zinaweza kutumiwa hata na wakulima wadogo. [caption id="attachment_193145" align="aligncenter" width="300"] Nyasi zilizotandazwa shambani kama matandazo, mojawapo ya teknolojia za kilimo endelevu zinazotumiwa na Kiganda Farm Estate kukuza kahawa katika eneo la Gatanga, Kaunti ya Murang’a, Agosti 27, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Dkt Tony Maritim, Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa, ndio Coffee Research Institute inayohudumu chini ya Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo (KALRO), anasema aina za kahawa zinazostahimili athari za tabianchi kama vile ukame na wadudu zitakuwa muhimu. “Watafiti pia wanatengeneza na kutathmini aina zinazoweza kustawi katika maeneo mapya yanayolimwa kahawa,” anasema. Kahawa inayohimili mikumbo ya tabianchi itasaidia kuongeza kiwango cha uzalishaji ambacho kimeshuka kwa zaidi ya asilimia 100 ikilinganishwa na miaka 30 na 40 iliyopita. Samuel Mwau, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kiufundi na Ushauri katika Coffee Board of Kenya, anadokeza kuwa uzalishaji wa kahawa nchini sasa ni karibu tani 50,000. “Uzalishaji wa kahawa kwa mkulima mdogo, ambao kihistoria ulikuwa kilo moja hadi mbili kwa mti, sasa unafikia kilo tatu na zaidi katika baadhi ya mashamba kufuatia mikahawa inayostahimili athari za tabianchi,” anasema. Mwau anasema wakulima sasa wanapata Sh120 hadi Sh125 kwa kilo, ikilinganishwa na Sh50 hadi Sh60 miaka mitano iliyopita, hali inayochochea kurejea kwa baadhi ya wakulima katika kilimo cha kahawa.

One person has died and 41 others have been hospitalised following suspected food poisoning in Singida Region after they reportedly consumed a traditional meal and a locally prepared drink while working at a private residence. The deceased has been identified as Ridhiwan Ayoub Omari, 13, who died while receiving treatment at Moyo wa Yesu Dispensary in Singida Municipality. According to a police statement, the incident occurred on October 17, 2026, at around 2pm in Unyambwa Ward, where the victims had been invited to perform work at a private home. They were reportedly served makande, a traditional dish made from maize and beans, and togwa, a locally prepared fermented drink, as payment for their work. Singida Regional Police Commander Matride Kuyeko said the victims began experiencing stomach pains and weakness the following morning. “On October 18, 2026, at around 11am, the deceased and 41 other people began experiencing stomach pains and weakness,” she said. Two children were initially taken to Moyo wa Yesu Dispensary in Mangumitongo, while the other 40 victims were referred to Singida Municipal Hospital for further treatment. Police said the condition of those receiving treatment was improving. Two people are being held for questioning as investigators seek to establish the cause of the suspected poisoning and the circumstances under which the food and drink were prepared and consumed. The incident has drawn attention to communal labour arrangements practised in parts of Tanzania, particularly in the central regions, where households mobilise neighbours to assist with agricultural and domestic activities in exchange for food and drinks. Such arrangements are common during cultivation, harvesting, millet threshing, roofing traditional houses and constructing livestock enclosures, with meals and beverages often forming part of the compensation. However, the involvement of children among those affected raises questions about the nature of the work they were invited to perform and the circumstances surrounding the incident. Police had not identified the suspected contaminant or established whether the food or drink caused the illnesses. Medical findings and further investigations will be needed to determine the cause of the incident and whether any criminal responsibility arises.

MVUTANO wa kisiasa kati ya Rais William Ruto na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya umechacha huku washirika wao wakipigana vikali kuhusu miradi ya maendeleo na uchaguzi wa 2027. Bw Natembeya ametaka ufafanuzi kuhusu ufadhili wa miradi iliyotangazwa na Rais, akitishia kuzuia mradi wa hospitali ya Sh1 bilioni huku akipinga kile anachokitaja kuwa serikali ya kitaifa kujipatia sifa kwa miradi ya kaunti. Mvutano huo uliongezeka baada ya Rais kutembelea kaunti hiyo mara kadhaa wiki iliyopita, akimkosoa gavana kuhusu huduma za afya na kuwatambulisha wanasiasa wanaoweza kumpinga katika uchaguzi ujao. Rais alielezea Hospitali ya Rufaa ya Wamalwa Kijana kama hatari kwa wagonjwa, akidai imepewa jina la “Shakahola” kwa sababu wagonjwa wanaoenda kutafuta matibabu humo hawarudi wakiwa hai. “Viongozi wanapaswa kupanga kuhusu afya, wala si mazishi ya wananchi wao,” alisema Dkt Ruto, akitangaza kujenga hospitali mpya ya vitanda 300 ndani ya miezi minane. Hata hivyo, Bw Natembeya amehoji umuhimu wa kujenga hospitali nyingine bila kuweka wazi mipango ya ufadhili, akisema vituo vilivyopo vinapaswa kuimarishwa. Washirika wa Rais, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen na Seneta wa Trans Nzoia Allan Chesang, wamemkosoa gavana na kuahidi kuwarai wapigakura kumwondoa mamlakani 2027. Rais pia aliwatambulisha Mbunge wa Kiminini Kakai Bisau, aliyekuwa mbunge Chris Wamalwa na mwakilishi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Susan Nakhumicha kama viongozi wanaoweza kushindana na Bw Natembeya. Mgogoro mwingine unahusu Uwanja wa Kitale ambao ujenzi wake umekwama. Rais alisema serikali ya kitaifa itachukua jukumu la kuukamilisha. “Ingawa nimejenga viwanja 32 kote nchini, uwanja wenu umekwama kwa miaka mingi. Gavana wenu ameshindwa kuukamilisha, nami nitachukua jukumu la kuumaliza,” akasema Rais. Bw Natembeya alijibu kwamba alikuwa ameidhinisha mazungumzo na maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kenya kuhusu kukamilisha mradi huo kwa fedha za serikali ya kitaifa. Alidai mradi haujaanza kwa sababu amekataa kujipendekeza kisiasa kwa Rais. Kuhusu soko la kisasa la Masinde Muliro mjini Kitale, Dkt Ruto alisema serikali ya kitaifa imetumia karibu Sh1 bilioni kulijenga na akaagiza wafanyabiashara 1,500 walioathiriwa na ujenzi wapewe kipaumbele katika ugawaji wa vibanda. Kila mmoja alipewa Sh10,000 za kuendeleza biashara yake. Bw Natembeya ameapa kufuatilia ugawaji huo ili kuhakikisha wafanyabiashara wa eneo hilo hawabaguliwi na watu kutoka nje. Mvutano umeongezeka zaidi baada ya walinzi wa gavana kuondolewa kwa mara ya pili. Ameitaka Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kueleza sababu za hatua hiyo, akisema usalama ni haki wala si mapendeleo. Gavana amehusisha hatua hiyo na tofauti zake za kisiasa na serikali ya kitaifa, ingawa madai hayo hayajathibitishwa kwa njia huru. Vuta nikuvute ilidhihirika pia katika mazishi ya Afisa Mkuu Msaidizi wa Inspekta Jenerali wa Polisi Lazarus Simiyu Opicho huko Maili Saba ambapo Bw Natembeya na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna walikutana na washirika wa Rais. Kaulimbiu za “Wantam” zilivuruga shughuli na kuzuia baadhi ya viongozi wa upinzani kuhutubia waombolezaji. Baadaye, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya mkutano wa viongozi wa upinzani mjini Kitale. Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisema maafisa wawili walijeruhiwa na magari mawili ya serikali kuharibiwa, huku uchunguzi ukianzishwa.