Kigoma yaanza kutekeleza mpango utalii tiba

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji huduma za afya ambapo kwa sasa…
The post Kigoma yaanza kutekeleza mpango utalii tiba appeared first on HabariLeo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji huduma za afya ambapo kwa sasa Mkoa wa Kigoma umeanza kutekeleza mpango wa serikali wa huduma za tiba kuwa sehemu ya utalii.
Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Jamal Tamim amesema hayo katika hafla ya futari ya jioni iliyoandaliwa na Taasisi ya Jai Tanzania iliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kigoma Maweni ambapo viongozi wa CCM, serikali na dini waliohudhuria.
Tamim amesema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeimarisha huduma kwa kiasi kikubwa katika hospitali hiyo ikiwemo vipimo na vifaa vya uchunguzi hali inayofanya hospitali hiyo kupokea idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu kupata huduma hospitalini hapo.
Amesema kuwa amani iliyopo Tanzania ndiyo sababu kubwa ya kuimarishwa kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za tiba na utekelezaji wa miradi mikubwa ambayo imeifanya Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo huku akiipongeza Taasisi ya Jai Tanzania kwa moyo wake wa kusaidia huduma za afya nchini.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kigoma Maweni Dk.Stanley Binagi.
Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Jai Tanzania, Gwanko Kamana amesema wamekuwa wakitoa msaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwemo kusaidia gharama za watu wasio na uwezo wa matibabu ambapo katika hospitali hiyo wametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya milioni 87.
Katibu wa Taasisi ya Jai Tanzania Gwanko kamana.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dk. Stanley Binagi amesema kuwa hospitali imeimarisha utoaji huduma kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na mashine mbalimbali za upimaji magonjwa ikiwemo CT Scan hivyo kuvutia watu wengi kupata huduma hapo.
Sambamba na hilo alisema kuwa hospitali imekuwa ikibeba gharama za wagonjwa wasio na uwezo wa kulipa gharama za matibabu ambapo kwa mwaka hospitali hiyo inqtoa misamaha ya matibabu kwa wagonjwa wasio na uwezo inayogharimu zaidi ya milioni 150 wakiwemo waomba hifadhi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
The post Kigoma yaanza kutekeleza mpango utalii tiba appeared first on HabariLeo.