TTB yaomba kura za watanzania tuzo za World Travel

DAR ES SALAAM – Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imezindua rasmi kampeni ya “Tanzania Shines 2025”, yenye lengo…
The post TTB yaomba kura za watanzania tuzo za World Travel appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM – Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imezindua rasmi kampeni ya “Tanzania Shines 2025”, yenye lengo la kuhamasisha watanzania kupigia kura vivutio vya utalii vya nchi vilivyoteuliwa kushiriki katika tuzo za kimataifa za World Travel Awards 2025.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa TTB, Vivian Temi amesema kuwa tuzo hizo zimekuwa zikitolewa kwa zaidi ya miaka 30, zikilenga kutambua mafanikio ya wadau wa utalii na ukarimu duniani kote.
Katika mwaka 2024, Tanzania ilifanikiwa kuibuka na tuzo mbalimbali zikiwemo World’s Leading Safari Destination, Africa’s Leading Destination, Africa’s Leading Tourist Board (TTB), Africa’s Leading Tourist Attraction – Mlima Kilimanjaro na Africa’s Leading National Park – Serengeti
Amesema kwa mwaka huu 2025, Tanzania imeteuliwa kushiriki katika vipengele 14 na kuomba Watanzania Kila mmoja kuingia World Travel Awards na kuichagua Tanzania.
Miongoni mwa vipengele inavyowania ni Africa’s Leading Destination, Africa’s Leading National Park – Serengeti, Leading Tourist Attraction – Mlima Kilimanjaro na Ngorongoro, Leading Beach Destination – Zanzibar, Bandari bora Africa Bandari ya Dar es Salaam, Uwanja Bora wa ndege Julius Nyerere Na mbuga nyingine kama Nyerere, Tarangire, Kitulo, Katavi, na Mahale zikiwakilisha katika vipengele vya kipekee.
Pia, kampuni mbalimbali za huduma za utalii kama vile Zara Adventures, Gosheni Safaris, Gran Meliá, na Serena Hotel nazo zimetajwa kuwania tuzo.
“Kwa pamoja, tunapaswa kutumia nafasi hii kuonyesha uzalendo wetu kwa kupiga kura na kuitangaza Tanzania kama nchi ya kipekee kwa vivutio vya asili, utamaduni, na ukarimu,” amesema.
Kampeni ya “Tanzania Shines 2025” itafanyika nchi nzima kwa njia ya redio, televisheni, mitandao ya kijamii, na kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali. Zoezi la kupiga kura kwa ukanda wa Afrika na Bahari ya Hindi linatarajiwa kufungwa Mei 4, 2025.
Katika hatua ya kufurahisha zaidi, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa hafla kubwa ya kutangaza washindi wa kanda hiyo, ijulikanayo kama Africa & Indian Ocean Gala Ceremony, itakayofanyika jijini Dar es Salaam Juni 28,2025.
The post TTB yaomba kura za watanzania tuzo za World Travel appeared first on HabariLeo.