Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
ZANZIBAR: Chama cha Mawakili Zanzibar (ZLS) na Wizara ya Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi, pamoja na kufanya mapitio na marekebisho ya sheria mbalimbali. Makubaliano hayo yalijadiliwa wakati wajumbe wa Baraza la Uongozi la ZLS walipotembelea ofisi za…
HOFU ya uwezekano wa mlipuko wa Ebola mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia, imepungua baada ya vipimo kuthibitisha kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 aliyefariki hospitalini hakuwa na virusi hivyo. Mwanamke huyo, aliyekuwa akifanya kazi katika duka la kuuza pombe mjini Nanyuki, alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Nanyuki (NTRH). Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Dkt Sammy Kilonzo, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika idara ya dharura saa 11 alfajiri Jumatatu akiwa na dalili za udhaifu wa mwili, homa na kikohozi kikavu kilichokuwa kikijitokeza mara kwa mara. Dkt Kilonzo alisema mwanamke huyo hakuwa na historia ya kusafiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) au Uganda, wala kuwasiliana na mtu aliyekuwa na dalili kama zake. Hata hivyo, katika saa 24 kabla ya kufikishwa hospitalini, alianza kupata shida ya kupumua na kuvuja damu kupitia sehemu za mwili na maeneo yaliyokuwa yamedungwa sindano, hali iliyozua wasiwasi miongoni mwa wahudumu wa afya. Akizungumza na Taifa Leo, Dkt Kilonzo alisema sampuli za mgonjwa zilipelekwa katika Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu nchini (Kemri) Jumatatu jioni kwa uchunguzi. Mwili wake ulihifadhiwa hospitalini huku wodi aliyokuwa amelazwa ikifungwa kwa muda wahudumu wakisubiri matokeo ya vipimo. Mhudumu mmoja wa afya katika hospitali hiyo, aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwanamke huyo huenda alifariki kutokana na upungufu mkubwa wa damu. Dkt Kilonzo alisema hospitali iliruhusu mwili wake kuhamishwa hadi mochari baada ya kupokea matokeo yaliyothibitisha kuwa hakuwa na Ebola. Alisema hospitali ilichukua tahadhari zote muhimu kulinda wahudumu wa afya na kituo hicho wakati wa kumhudumia mgonjwa huyo. Baada ya taarifa hizo kusambaa, shirika la kijamii la Sheria Mashinani liliwataka wakazi wa Nanyuki na maeneo mengine ya Laikipia kutulia na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa. Mwangi Wangai, anayetaka kuwania ubunge wa Laikipia Mashariki, alisema taarifa hizo ziliwatia hofu wakazi, huku baadhi yao wakihoji kilichotokea. Aliitaka serikali kutoa taarifa sahihi na kwa wakati wakati wa dharura za kiafya ili kujenga imani ya wananchi na kuondoa mkanganyiko.
WABUNGE wanapendekeza sheria kali kwa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wakiendesha uchaguzi katika vituo ambavyo havijaidhinishwa rasmi. Maafisa hao wataweza kutozwa faini ya Sh2 milioni au kifungo cha miaka mitano jela, au adhabu zote mbili wakipatikana na hatia. Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Uchaguzi wa mwaka 2024, ambao unatarajiwa kujadiliwa katika hatua ya kamati katika Bunge la Kitaifa wiki hii. Mswada huo unalenga kuimarisha uadilifu wa uchaguzi kwa kuhakikisha matokeo yanayotangazwa na maafisa wa IEBC yanatoka vituo vilivyoidhinishwa rasmi kupitia tangazo la serikali. Kwa sasa, kuendesha uchaguzi katika kituo kisichoidhinishwa hakujatajwa kama kosa la uchaguzi chini ya sheria inayotumika kwa sasa. Mswada huo unapendekeza kurekebisha kifungu cha sita cha Sheria ya Makosa ya Uchaguzi ili kuingiza kosa hilo pamoja na makosa mengine yanayohusiana na kutangaza na kubadilisha matokeo. Pia, maafisa wa IEBC watakaochelewesha bila sababu kutangaza matokeo ya uchaguzi au kubadilisha kimakusudi matokeo yaliyokwisha kutangazwa watakuwa wakitenda kosa la uchaguzi. Mswada huo uliofadhiliwa kwa pamoja na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot (Kericho), na mwenzake wa Wachache, Stewart Madzayo (Kilifi), ulitokana na mapendekezo ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (Nadco). Ripoti ya Nadco iliidhinishwa na Bunge mnamo Februari 2024, baada ya mazungumzo ya pande mbili yaliyolenga kupunguza joto la kisiasa kufuatia maandamano yaliyosababisha vifo baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022 kupingwa na kiongozi wa wakati huo wa Azimio, Raila Odinga. Seneti iliidhinisha mswada huo Novemba 19, 2024, kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa, ambako ulisomwa kwa mara ya kwanza Desemba 3, 2024. Katika uchaguzi mkuu wa 2022, IEBC iliidhinisha vituo 46,232 vya kupigia kura, ikilinganishwa na vituo 40,883 katika uchaguzi wa 2017. Hata hivyo, kesi iliyopinga matokeo ya urais ya 2017 ilidai kuwa vituo visivyoidhinishwa vilianzishwa kinyume cha sheria katika Kaunti ya Mandera na kusimamiwa na maafisa ambao hawakuwa wameteuliwa rasmi. Vilevile, kesi iliyopinga ushindi wa urais wa 2022 ilielezea hitilafu katika upeperushaji wa matokeo, ikidai kuwa matokeo kutoka zaidi ya vituo 11,000 ambavyo havikuwa vimeidhinishwa yalijumuishwa katika hesabu ya mwisho. Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2022 zinahitaji IEBC kutangaza rasmi vituo vya kupigia kura, maeneo yake na nambari zinazovitambulisha.
WIKI baada ya mgonjwa wa Ebola aliyekuwa ameingia Kenya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda kufariki, hakuna kisa kingine kilichothibitishwa nchini kufikia sasa. Wataalamu wa afya wanasema licha ya kutokwepo kwa maambukizi mapya, Kenya italazimika kusubiri siku 21 ndipo itangazwe kuwa huru kutokana na Ebola. “Kila siku inayopita bila dalili inatupa sababu zaidi ya kutumaini kuwa maambukizi ya pili na kuenea kwa virusi ndani ya nchi kumezuiliwa.” Akasema Dkt Ahmed Kalebi, mtaalamu wa magonjwa na mtafiti wa afya ya umma. Wizara ya Afya imesema watu 122 waliokutana na mgonjwa huyo wametambuliwa na kuthibitishwa. Kati yao, 108, sawa na asilimia 88.5, wamewekwa karantini na kufuatiliwa kila siku. Hakuna aliyekuwa amepata dalili kufikia taarifa ya Oktoba 11. Sampuli 293 zimepimwa, lakini ni ya mgonjwa huyo pekee iliyopatikana na virusi. Zaidi ya wasafiri 667,675 wamechunguzwa katika vituo 26 vya kuingia nchini. Profesa Shem Otoi, mtaalamu wa kukabili magonjwa yanayoenea na Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Daystar, naye anasema mchakato wa kuwafuatilia wagonjwa haupaswi kukomeshwa kwa sababu mtu ni mzima. “Wasiwasi mkubwa zaidi ungekuwa tukio tofauti kisa ambacho hakiwezi kuhusishwa na mgonjwa anayejulikana,” alisema. “Sihofu kisa kimoja au viwili vilivyoletwa kutoka nje. Hofu yangu ni maambukizi ya ndani na ikiwa tutafikia siku ya mwisho bila maambukizi ya ndani, basi tutakuwa salama kama nchi,” akaongeza. Mtaalamu huyo aliongeza kuwa Kenya inaweza kuzuia maambukizi ikiwa itawatambua watu wote walio katika hatari, kuwafuatilia na kukatiza kila mnyororo mpya wa maambukizi. Profesa Omu Anzala, mtaalamu wa virusi na mwanachama Jopo la Kupambana na Kuenea kwa Ebola, naye anasema siku 21 zikikamilika ndipo Kenya itakuwa huru dhidi ya maradhi hayo. “Ni baada tu ya siku 21 ndipo unaweza kuthibitisha kuwa kweli hakuna maambukizi mapya,” akasema. Ebola haisambazwi kupitia hewa, bali kwa kugusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa au aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.
CHAMA cha Democracy for Citizens Party (DCP) kinakabiliwa na jaribio la kwanza la umoja wake huku baadhi ya wanaowania tiketi katika uchaguzi wa 2027 wakilaumu kiongozi wake Rigathi Gachagua na maafisa wakuu kwa kupendelea washirika wao. Mvutano huo unazua maswali kuhusu ahadi ya chama hicho ya kuwaruhusu wanachama kuamua wagombeaji wao kupitia kura za mchujo zilizo huru na za haki. Hali hii inajiri huku Bw Gachagua akisema mazungumzo ya kuunda muungano wa upinzani yatasubiri hadi viongozi wa vyama husika waimarishe ngome zao za kisiasa kabla ya kuafikiana kuhusu mgombeaji mmoja wa urais. Akizungumza na wafuasi wake mjini Dracut, Massachusetts, nchini Amerika, Bw Gachagua aliwataka wawe na subira akisisitiza kuwa upinzani haujachelewa kujiandaa kwa uchaguzi wa 2027. “Hatuko nyuma kwa wakati. Tuko ndani ya muda unaofaa. Muungano unaweza kuundwa tu baada ya viongozi wenye ushawishi kuimarisha ngome zao,” alisema. Alipuuza madai kwamba upinzani umegawanyika au unashindwa kupata mgombeaji mmoja wa urais, akiahidi kuwa DCP itajitolea kuhakikisha vyama vinaungana. “Ninaweza kuwahakikishia kuwa mgombeaji tutakayempata atawafurahisha. Wakenya wanataka mshindi wa uchaguzi apatikane katika awamu ya kwanza. Muungano utakuwa muhimu, lakini si wakati huu kwa DCP. Chama changu na mimi tutajitolea kuhakikisha tunapata mgombeaji mmoja,” alisema. Hata hivyo, huku akitoa hakikisho hilo kwa wafuasi wake, malalamishi yalikuwa yakiongezeka ndani ya DCP kuhusu jinsi chama kitakavyowachagua wagombeaji wa viti mbalimbali. Baadhi ya wanaowania tiketi wanamlaumu Bw Gachagua na mwenyekiti wa baraza la watu mashuhuri la chama hicho, Bw Maina Kamanda, kwa kudhoofisha demokrasia ya ndani ambayo DCP ilijivunia wakati wa mchujo kuelekea uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Wanasema kiongozi huyo amekuwa akiwapigia debe wagombeaji anaowapendelea, huku Bw Kamanda akidokeza kuwa baadhi ya washindani wanaweza kunyimwa tiketi hata wakishinda kura za mchujo. Akizungumza katika kituo cha redio cha Inooro FM mnamo Septemba 22, Bw Kamanda alisema chama hakitawapa tiketi baadhi ya wagombeaji licha ya kushinda mchujo. “Hatuwezi kuwaruhusu watu waliokuwa upande wa wanaotusuta waje dakika za mwisho na kuwashinda wale waliosimama imara na chama pamoja na uongozi wake,” alisema, akitaja Kaunti ya Kirinyaga kama mfano wa wanaoweza kunyimwa tiketi kwa misingi ya uaminifu wao. Kauli hiyo imewaudhi baadhi ya wanaowania tiketi, ambao sasa wanataka uongozi utoe hakikisho kwamba mchakato huo utakuwa wa haki, wazi na unaozingatia matakwa ya wanachama. Mvutano huo ni muhimu kwa sababu DCP imekuwa ikitumia kura za mchujo za Ol Kalou kuthibitisha kujitolea kwake kwa demokrasia ya ndani. Katika zoezi la Julai, wanachama 23,763 walipiga kura, sawa na asilimia 32.6 ya wapigakura 72,997 waliojiandikisha katika eneo hilo. Bw Sammy Kamau Ngotho alishinda tiketi ya chama kwa kura 12,947, kabla ya kuibuka mshindi wa uchaguzi mdogo kwa kura 35,440 dhidi ya kura 5,450 za mgombeaji wa United Democratic Alliance (UDA). Bw Gachagua alitaja zoezi hilo kuwa la kihistoria, akisisitiza kuwa DCP haina utaratibu wa kutoa tiketi moja kwa moja bila kura za mchujo na kwamba wananchi ndio wanaopaswa kuamua. Hata hivyo, baadhi ya wagombeaji sasa wanahofia kuwa utaratibu huo hautatumika katika maeneo mengine. Wasiwasi huo uliongezeka wakati wa ziara yake nchini Amerika, ambapo Bw Gachagua aliwaambia wakazi wa Spokane kuwa Bi Wambui Nyutu ndiye atakayekuwa mbunge wa Maragua kupitia DCP. Kauli hiyo ilimkasirisha mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha tiketi ya chama, Bw Jimmy Mbaki, ambaye alisema ilikuwa ishara kuwa matokeo ya kura za mchujo yalikuwa tayari yameamuliwa. “Ni ushahidi gani mwingine ninaohitaji kujua kuwa ninapoteza muda wangu ndani ya DCP?” alisema. Alilinganisha wagombeaji wanaoendelea kuamini mchakato huo na ng’ombe anayeingia mwenyewe kichinjioni licha ya kuwa na nguvu za kupambana. Bw Mbaki alidai kuwa viti vya ubunge vya Maragua, Kigumo na Gatanga tayari vimetengewa wagombeaji wanaopendelewa na Bw Gachagua. “Kura za mchujo za DCP zitakuwa utaratibu wa kutimiza wajibu tu. Wanaodhani kutakuwa na haki wanajidanganya. Tayari natafuta chama kingine,” alisema. Hata hivyo, uongozi wa DCP umepuuzilia mbali madai ya upendeleo, ukisema kila mgombeaji atapata nafasi ya kushindana. Kaimu Katibu mkuu wa chama hicho, Bw John Methu, aliambia gazeti la Taifa Leo kuwa wagombeaji hawapaswi kuchukulia mazungumzo ya kisiasa kama maamuzi rasmi ya chama. “Watu wanapaswa kuepuka kuchukulia mazungumzo ya kisiasa kwa uzito kupita kiasi. Tunafanya mikutano rasmi na wagombeaji na tunachowaambia wote ndicho kitakachotekelezwa,” alisema. Bw Methu alisisitiza kuwa hakuna anayehakikishiwa tiketi, hata Bw Gachagua mwenyewe katika kinyang’anyiro cha urais kupitia chama hicho. Alionya kuwa DCP haitakubali ushindi unaopatikana kupitia udanganyifu, hongo au vurugu. “Hakuna tiketi itakayotolewa kwa ushindi uliopatikana kwa udanganyifu. Hakuna atakayeshinda tiketi kwa kutumia vurugu au hongo,” alisema. Mchambuzi wa siasa Mixson Gitau alisema wagombeaji wanapaswa kuelewa kuwa vyama vinaweza kuzingatia mambo mengine zaidi ya matokeo ya kura za mchujo. Alitaja uaminifu kwa chama, uwezo wa kushinda uchaguzi na uadilifu kama baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuzingatiwa.
…Ministers seek stronger surveillance, responsible antibiotic use By Sola Ogundipe The Federal government has raised the alarm over the growing threat of antimicrobial resistance (AMR), warning that patients are suffering prolonged illnesses, failing to respond to treatment and dying from infections that antibiotics should ordinarily help control. The Coordinating Minister of Health and Social Welfare, […]
SERIKALI ya Kaunti ya Nairobi imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa matumbwitumbwi katika shule, huku wazazi wakishauriwa kuwaweka nyumbani watoto wanaoonyesha dalili za ugonjwa huo hadi watakapopona kabisa. Kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Amerika (CDC), dalili za kawaida za ugonjwa huu ni pamoja na kuvimba kwa taya kunakosababisha maumivu, homa, uchovu, kupoteza hamu ya kula na maumivu ya kichwa. Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema matumbwitumbwi ni ugonjwa wa ghafla unaowaathiri zaidi watoto na vijana, na husababishwa na virusi. WHO inaeleza kuwa ugonjwa huo kwa kawaida huwa mwepesi na unaweza kupona wenyewe baada ya muda. Tofauti na magonjwa mengi ya kuambukiza, binadamu ndio viumbe pekee wanaojulikana kuwa wenyeji wa virusi hivyo. Ugonjwa huenea kupitia kugusana moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa au kwa matone ya majimaji yanayotoka kwenye mfumo wa juu wa upumuaji. Afisa Mkuu wa Afya ya Umma wa kaunti hiyo, Tom Nyakaba, aliambia Taifa Leo kuwa tayari ofisi yake imetuma tahadhari kwa shule, ikizielekeza kuhusu namna ya kuzuia maambukizi zaidi. “Tumeshauri shule kuhakikisha watoto walioambukizwa wanakaa nyumbani,” alisema. Nyakaba alisema hakuna haja ya hofu kwa sasa kwa sababu idadi ya maambukizi bado ni ndogo na wanafunzi walioathirika wanajitenga ili kuzuia kueneza ugonjwa huo. “Tumekuwa na visa vya matumbwitumbwi kwa muda wa miezi miwili iliyopita, lakini vimekuwa vikitokea hapa na pale. Kufikia sasa tumerekodi takriban visa 11, lakini maambukizi ya hivi karibuni ni matatu pekee, yaliyoripotiwa katika shule moja eneo la Lang’ata,” alisema.
The Makinde-Daura Presidential Campaign Organisation has demanded a comprehensive audit of the N15 trillion Lagos-Calabar Coastal Highway project, accusing the Federal Government of raising fresh questions about its planning, procurement and cost following the recent realignment of the route.
DODOMA; Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Samwel M. Maneno amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Alex Malasusa, Ofisini kwake Mtumba jijini, Dodoma, Oktoba 13, 2026. Katika ziara hiyo Askofu Malasusa aliambatana na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki…
DAR ES SALAAM: Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 70 ya usajili, usimamizi na udhibiti wa taasisi za kiraia yatakayofanyika Oktoba 27 hadi 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam. Akizungumza jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema maadhimisho hayo yenye…
KAKAKE marehemu mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili Betty Bayo, amekata kauli na kusema hataifuatilia tena kesi inayochunguza kiini cha kifo cha dada yake. “Sasa nimejiridhisha kwamba dadangu alifariki kutokana na kuugua AMN. Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa kimatatibabu kufanywa kuhusu kiini cha kifo chake. Nimeridhika na sasa nitamwacha dadangu apumzike kwa amani,” alisema ndugu huyo Edward Mbugua. Bayo alifariki mwaka jana, na ghafla familia yake ikazua kesi ikidai kwamba haikuridhishwa na maelezo yaliyotolewa kuhusu kilichopelekea mauti hayo. Mwanadada huyo aliaga dunia katika hospitali kuu ya Kenyatta akipokea matibabu. Uchunguzi wa awali wa kimatibabu ulishindwa kubaini haswa kilichopelekea kifo chake huku kikiwa na taarifa mkanganyiko zilizoibua madai kwamba alifariki kutokana na kansa ya damu. Hali hiyo ilisukuma familia yake kufungua kesi ikitaka uchunguzi wa kina ufanywe huku mamake akidai Bayo hakuwahi kuwa na historia ya ugonjwa huo uliotajwa wa kansa.
MTANGAZAJI wa zamani wa habari kwenye runinga, Esther Arunga, ameondoa rasmi jina la ukoo la Quincy Timberlake, mwanamume ambaye wakati mmoja alimtangaza kwa fahari kuwa mumewe. Miaka 16 baada ya kutumia jina la “Timberlake” wakati wa sakata iliyozua mjadala mkubwa nchini Kenya, sasa amerejelea jina alilokulia. Katika notisi iliyochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali mnamo Oktoba 9, mawakili wake walisema mteja wao, Esther Adongo Arunga, aliyekuwa akijulikana kama Esther Adongo Timberlake, ameachana rasmi na matumizi ya jina hilo la zamani. Waliomba watu wote wamwite Esther Adongo Arunga pekee. Hatua hiyo inafungua ukurasa mwingine katika maisha ya Esther na Quincy, ambao wamehusishwa na kesi za mahakamani katika mabara mawili. Mnamo Machi 2010, Esther alikuwa ametangaza jijini Nairobi kwamba alikuwa amebadilisha jina lake baada ya kufunga ndoa na Quincy. Kabla ya sakata hiyo, Esther alikuwa miongoni mwa watangazaji waliotambulika sana nchini. Alisoma Shule ya Upili ya Kenya High, akafanya kazi Capital FM na KTN, na kushinda tuzo ya Chaguo la Teeniez ya 2008 kama mtangazaji bora miongoni mwa vijana. Alikubaliwa kuwa wakili mnamo 2009. Maisha yake yalibadilika mnamo 2009 alipojiunga na kanisa la Finger of God, lililoanzishwa na mwanamuziki Joseph Hellon. Februari 2010, watatu hao walitangaza kuunda chama cha PlaCenta, siku ambayo Esther alijiuzulu KTN. Baadaye, polisi walivamia nyumba iliyohusishwa na kanisa hilo jijini Nairobi. Esther na Quincy walihamia Australia kutafuta hifadhi ambapoJuni 18, 2014, mwanao wa miaka mitatu, Sinclair, alifariki. Esther alisema mtoto alikuwa ameanguka kwenye ngazi, lakini uchunguzi wa maiti ulionyesha alikufa kutokana na majeraha makubwa yasiyolingana na kuanguka. Mnamo 2019, Esther alikiri kosa la kumsaidia mkosaji na kuhukumiwa kifungo cha miezi 10, lakini akaachiliwa kwa masharti kisha Septemba 2023, Quincy alikiri kosa la kuua bila kukusudia na akahukumiwa miaka 11 gerezani Hata hivyo, muda aliokuwa amekaa rumande kabla ya hukumu ulihesabiwa, hivyo angeweza kukaa gerezani kwa muda usiozidi miaka miwili zaidi. Notisi ya hivi karibuni inaonyesha anwani ya Esther kuwa Nairobi, hali inayozua uwezekano kuwa amerejea nchini.
CHAMA cha National Reconstruction Alliance (NRA), kinachohusishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah, kimeenda mahakamani kupinga uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wa kulegeza baadhi ya masharti ya usalama wa karatasi za kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Chama hicho kinasema hatua hiyo inaweza kurahisisha kughushi, kunakili na kuchezewa kwa karatasi za kura, hivyo kuzua wasiwasi kuhusu uadilifu na uwazi wa uchaguzi ujao. Mahakama Kuu imetangaza kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza IEBC na walalamishi wengine kujibu ndani ya siku saba. Kesi hiyo itatajwa Oktoba 14 kwa maelekezo zaidi. NRA inapinga marekebisho ya zabuni nambari 3, yaliyotolewa Septemba 17, 2026, ambayo tume hiyo ilisema yanalenga kupunguza gharama na muda unaohitajika kununua karatasi za kura na vifaa vingine vya uchaguzi. Mzozo huo unatokana na zabuni iliyotangazwa Agosti 11, 2026, ya kusambaza karatasi za kura na vifaa vingine chini ya mkataba wa miaka mitatu. Hapo awali, zabuni hiyo ilihitaji mifumo mbalimbali ya usalama, ikiwemo michoro maalumu inayozuia kughushi, maandishi madogo yenye taarifa zinazobadilika, misimbo ya QR inayozuia kunakili na nambari za utambulisho zilizochapishwa kwa wino wa rangi mbalimbali. Hata hivyo, marekebisho hayo yanaruhusu matumizi ya wino mweusi pekee kwa nambari za utambulisho, michoro na maandishi yasiyobadilika. NRA inasema IEBC haijatoa ushahidi wa kiufundi unaothibitisha kuwa masharti mapya yatatoa ulinzi sawa au bora kuliko yale ya awali. Chama hicho kinasisitiza kuwa karatasi ya kura si bidhaa ya kawaida ya zabuni, bali ni stakabadhi muhimu inayotumiwa na Wakenya kutekeleza mamlaka yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi. Kinasema gharama na muda mfupi wa ununuzi havipaswi kutumiwa kama sababu ya kupunguza usalama wa uchaguzi bila ushahidi wa kutosha. NRA pia inaonya kuwa udhaifu wowote ukibainika baada ya karatasi kuchapishwa na kusambazwa, huenda ikawa vigumu kurekebisha hali hiyo. Katibu mkuu wa chama hicho, Amemba Magufuli, alisema wanataka uwajibikaji wa mapema kabla ya maamuzi yenye athari kubwa kukumbatiwa. NRA inataka mahakama itupilie mbali mabadiliko hayo, irejeshe masharti ya awali na kuagiza tathmini huru ya kiufundi ili kuhakikisha usalama wa karatasi za kura unalindwa. Hata hivyo, chama hicho hakidai kuwa IEBC inapanga kuendeleza udanganyifu wa uchaguzi au kwamba karatasi za kura tayari zimechezewa.
DAR ES SALAAM: IMAGINE a Tanzania where more families build wealth through investments, more businesses raise capital to expand and more young people understand how to make their money work for them. This future is within reach. In fact, the progress of Tanzania’s capital market suggests that we are moving in the right direction. The…
TANZANIA: TANZANIA’S ambition to become a one trillion US dollars economy by 2050 will depend not only on sound development policies, but also on its ability to mobilise long-term capital, finance productive enterprises and enable citizens to participate in wealth creation and ownership. Dira 2050 presents a historic opportunity to transform the economy, raise living…
NAIBU wa Rais Prof Kithure Kindiki anatumia baraka za wazee waliomteua kuwa msemaji wa eneo la Mlima Kenya kupanua ushawishi wake katika Mlima Kenya Magharibi, ambako utawala wa Rais William Ruto unakabiliwa na upinzani mkali wa kisiasa. Prof Kindiki aliidhinishwa na wazee katika uwanja wa Kirigiti, Kaunti ya Kiambu, Septemba 19, 2026, na mara moja […]
GENEVA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ameunga mkono Dira ya Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Barham Salih, ya “50 kufikia 35”, inayolenga kupunguza kwa nusu idadi ya wakimbizi duniani ifikapo mwaka 2035. Ayoub alitoa kauli hiyo jana, Oktoba 13, 2026, wakati akiongoza…
TABORA: THE government has provided TANESCO with two vehicles worth 463.48m/- to improve its capacity to respond to electricity faults and maintain power infrastructure in Igunga District, Tabora Region. TANESCO Igunga District Manager, Mr Raphael Ambonisye, said the vehicles would help to address transport challenges that had affected the utility’s operations. He said TANESCO Igunga…
IKIWA imesalia chini ya miezi 10 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, upinzani unaendelea kukabiliwa na mashaka kuhusu viongozi wasioaminika ndani ya kambi hiyo, huku mvutano kuhusu mgombea wake wa urais ukiendelea. Mashaka hayo yamezidi baada ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i, kujitokeza kupinga madai yanayotilia shaka uaminifu wao ndani ya upinzani. Hivi majuzi wawili hao wameonekana kushirikiana kisiasa, hali iliyoibua maswali kuhusu mikakati yao kuelekea uchaguzi ujao. Kuingia kwa Bw Nyoro katika kambi ya upinzani kumepokelewa kwa mashaka, hasa na chama cha DCP ambacho kinaendelea kumhusisha na serikali ya sasa. Jumapili, Seneta wa Nyandarua, John Methu, ambaye ni Katibu Mkuu wa DCP, alitilia shaka nia ya Bw Nyoro, akidai kuwa hatua zake za kisiasa zinaweza kumnufaisha Rais William Ruto. Bw Methu alidai kuwa muda mfupi baada ya DCP kushinda uchaguzi mdogo wa Ol Kalou mnamo Julai, watu kutoka serikalini walimwendea na kumpa ofa ya kuanzisha chama chake ili kugawanya upinzani na kudhoofisha ushawishi wa kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua katika Mlima Kenya. Alisema alikataa ofa hiyo iliyohusisha kupewa chama, fedha, vifaa vya kampeni na wagombea, ili kushindana na DCP na kuifanya ionekane kuwa haishirikiani na serikali. Alidai pia kuwa mpango huo ungeweza kumwezesha kuwa mgombea mwenza wa Ruto. Bw Methu alisema Gavana wa Murang’a, Irungu Kang’ata, pia alifikiwa na pendekezo kama hilo, lakini akalikataa. Aliongeza kuwa alimweleza Bw Gachagua kuhusu suala hilo kabla ya kuwasiliana na Bw Nyoro, ambaye alisema alimwonya dhidi ya kuingia katika mtego wa kugawanya kura za Mlima Kenya. Kwa mujibu wa Bw Methu, mbunge huyo wa Kiharu alimwambia kuwa Rais Ruto anahofia umoja wa Mlima Kenya na hataki viongozi wa eneo hilo wawe katika chama kimoja. Bw Methu alidai Bw Nyoro alikuwa amemwahidi kujiunga na DCP baadaye, na hata alikuwa tayari kumpa nafasi yake ya pili baada ya Bw Gachagua. Hata hivyo, alishangazwa na uamuzi wa mbunge huyo kuanzisha chama chake. Bw Nyoro alizindua chama cha People's Party of Kenya (PPK) mnamo Agosti baada ya kujitenga na UDA ya Rais Ruto. Tangu wakati huo, amekuwa akizunguka nchini kukitangaza chama hicho kabla ya uchaguzi wa 2027. Akizungumza na Taifa Leo, Bw Nyoro alikanusha madai ya Bw Methu, akisema hawajawahi kukutana kujadili suala la kujiunga na DCP. “Hatujawahi kukutana kuzungumzia jambo kama hilo. Huo ni upuuzi mtupu na madai ya kitoto,” akasema Bw Nyoro. Alimshutumu Bw Gachagua kwa kuongoza kampeni ya kumchafua, akidai kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakimfikishia ujumbe kutoka kwa Bw Gachagua Amerika ukiwaelekeza jinsi ya kumkosoa. Bw Gachagua mwenyewe amekuwa akiwaonya viongozi wa upinzani kuhusu watu anaodai wamepandikizwa na Rais Ruto katika vyama vyao ili kuvuruga umoja wao. Dkt Matiang’i pia amewahi kupinga madai kwamba anafanya kazi ya kudhoofisha upinzani kutoka ndani. Alisema shutuma hizo ni mbinu ya kukwepa kujadili masuala muhimu. “Watu wanapokosa hoja, huamua kutumia matusi na majina ya kudhalilisha,” akasema mnamo Agosti. Dkt Matiang’i aliteuliwa hivi majuzi kuwa kiongozi wa chama cha Jubilee, akimrithi rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Bw Methu alisema anamwamini kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, akidai wameonyesha msimamo thabiti wa kutaka Rais Ruto aondoke madarakani. Hata hivyo, alionyesha kutokuwa na uhakika kuhusu Dkt Matiang’i, akisema urafiki wake wa kisiasa na Bw Nyoro umeibua maswali kuhusu uaminifu wake.
DAR ES SALAAM: THE Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) plans to raise about 4tri/- through capital markets as it seeks to diversify funding sources and extend higher education financing to more Tanzanian students. The board said the initiative aims to establish a sustainable funding model that does not rely on a single source of…
SHIRIKA la Huduma za Misitu nchini (KFS) jana lilithibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa ndani ya helikopta yake iliyoanguka katika uwanja wa Gofu wa Kericho wako salama, huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha ajali hiyo. Kupitia taarifa, KFS ilisema helikopta hiyo yenye nambari ya usajili 5Y FSK ilikuwa na rubani mmoja na abiria watatu ilipoanguka asubuhi ya Oktoba 12, 2026. “KFS ingependa kuufahamisha umma kuhusu tukio lililohusisha helikopta yake 5Y FSK, lililotokea asubuhi ya Oktoba 12, 2026, katika Klabu ya Kericho. Kulikuwa na watu wanne, rubani mmoja na abiria watatu. Wote wako salama,” ikasema taarifa ya KFS. Shirika hilo liliongeza kuwa eneo la ajali lilikuwa limetengwa huku maandalizi ya uchunguzi yakianza ili kubaini mazingira yaliyopelekea tukio hilo. “Eneo hilo limetengwa, na uchunguzi utaanza kubaini mazingira yaliyozunguka tukio hilo,” ilisema taarifa hiyo. KFS iliwataka wananchi wanaohitaji maelezo zaidi kuwasiliana nayo kupitia barua-pepe yake rasmi; [email protected]. Mashahidi walisema helikopta hiyo ilikuwa imepaa kwa muda mfupi tu kabla ya kuanza kupoteza mwelekeo na kuanguka muda mfupi baada ya kupaa. Watu waliokuwa ndani yake waliokolewa kutoka kwenye mabaki ya helikopta hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Kusini mwa Bonde la Ufa kwa matibabu ya dharura. Polisi walisema vikosi vya dharura na usalama vilikuwa vikichunguza hali hiyo, huku maelezo zaidi yakitarajiwa kutolewa uchunguzi utakapoendelea. Tukio hilo linajiri huku kukiwa na taarifa za ajali nyingine za ndege nchini Kenya katika miezi michache iliyopita.
SEKTA ya meli za kitalii za kimataifa imepata pigo nchini kutokana na kisa cha kwanza cha Ebola nchini, huku kampuni ya MSC Cruises ikisitisha kuajiri mabaharia Wakenya kwenye meli zake. MSC Cruises, ambayo huajiri mamia ya Wakenya kwenye meli zake, imesema hatua hiyo ya muda itadumu hadi Oktoba 31, ikitaja hali ya hivi karibuni ya afya ya umma nchini. Katika ujumbe kwa wafanyakazi walioathiriwa, kampuni hiyo ya usafiri wa meli za kitalii, ilisema uamuzi huo ni wa tahadhari huku ikiendelea kufuatilia na kutathmini hali ilivyo. Kampuni hiyo iliomba radhi kwa kutoa taarifa hiyo katika muda mfupi, lakini ikawahakikishia wafanyakazi walioathiriwa kuwa uamuzi huo hautaathiri ajira zao, mikataba yao ya kazi wala fursa zao za baadaye katika kampuni hiyo. Ilisema wafanyakazi ambao mipango yao ya kusafiri imeahirishwa watapewa kipaumbele katika kupanga upya safari zao kuanzia Novemba 1, isipokuwa kama kutakuwa na matukio mengine yatakayohitaji hatua za ziada. Ingawa MSC Cruises haikutaja Ebola moja kwa moja katika taarifa yake, hatua hiyo imezua maswali kuhusu uwezekano wa waajiri wengine wa kimataifa kuchukua hatua kama hizo za tahadhari na athari zake kwa Wakenya wanaotafuta ajira nje ya nchi. Mwezi Julai, baadhi ya wafanyakazi Wakenya pia walikwama baada ya kampuni hiyo ya meli za kitalii kuahirisha safari za wafanyakazi kutoka Kenya, ingawa hakuna kisa cha Ebola kilichokuwa kimeripotiwa wakati huo. “Tafadhali fahamuni kuwa kutokana na mlipuko wa Ebola, usimamizi umeamua kuahirisha kuingia kwa wafanyakazi kutoka Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda kwenye meli hadi pale itakapotangazwa vinginevyo,” barua pepe kutoka kwa kampuni hiyo ya meli za kitalii ilisema. Duru zilisema baadhi ya wafanyakazi kutoka Diani na Mombasa waliokuwa wanatarajiwa kuabiri meli ya kampuni hiyo walikwama. Mchambuzi wa masuala ya utalii, Bw Mohamed Hersi, alisema sekta hiyo haijapokea ripoti za watalii waliokatiza safari zao nchini kwa sababu ya Ebola. Hata hivyo, alionya kuwa hali inaweza kubadilika iwapo nchi ambazo Kenya hutegemea sana kwa utalii zitatangaza masharti makali zaidi ya ushauri wa usafiri. “Hatujapokea taarifa za safari zozote zilizoghairiwa. Yote yatategemea ushauri wa usafiri, hasa kutoka kwa serikali za Uingereza, Marekani na Milki za Kiarabu (UAE),” alisema Bw Hersi, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Pollman’s Tours and Safaris. Bw Hersi alieleza matumaini kuwa Kenya itaepuka ushauri mkali wa usafiri kwa kuwa kisa cha Ebola kilichoripotiwa kilitoka nje ya nchi na maafisa wa afya wamechukua hatua za kudhibiti hatari. Kwa upande wake, meneja wa kampuni ya Africa Last Minute Ltd, Bw Abraham Guyo, alionya kuwa kisa hicho kinaweza kudhoofisha imani ya wageni kwa Kenya kama kivutio cha watalii, hasa iwapo wasiwasi wa kimataifa utaongezeka. Wizara ya Afya ilithibitisha kisa cha kwanza nchini Kenya cha ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo mnamo Oktoba 6. Mgonjwa huyo, aliyekuwa amesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda hadi Nairobi, baadaye alifariki na kuzikwa kwa kuzingatia taratibu za afya ya umma. Serikali imesisitiza kuwa kisa hicho kilitoka nje ya nchi na imewataka Wakenya kuwa watulivu, kufuata mwongozo rasmi wa afya na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa. Serikali imesema inaongeza ufuatiliaji wa magonjwa na kuimarisha hatua nyingine za afya ya umma ili kuzuia maambukizi zaidi.
RAIS William Ruto jana alimrejelea Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kama kiongozi msaliti ambaye alimgeuka na kupuuza maelewano ya kila mmoja wao kuongoza kwa mihula miwili baada ya kuchukua uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2013. “Nilikuunga mkono katika uchaguzi wa 2013 na 2017, ukatangaza kuwa ungehudumu kwa miaka 10 kisha uniunge mkono kwa miaka 10 mingine. Lakini ulinidanganya. Wewe nimtu asiyekuwa na shukrani hata kidogo,” akasema Rais Ruto. Alikuwa akiongea katika ngome yake ya kisiasa, Kaunti ya Uasin Gishu ambapo aliwataka wafuasi wake kumpa kura milioni moja zaidi katika uchaguzi wa 2027. Bw Kenyatta na Rais Ruto walihudumu pamoja kama rais na naibu rais kuanzia 2013 hadi 2022, lakini uhusiano wao ulidorora Uhuru alipomuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa 2022. “Wale ambao wanalalamika kuhusu Uhuru wanafaa waniulize. Huyo jamaa ni mkora. Kama alinihadaa, mimi mwenye nilimpigia kura na kumfanyia kampeni, fikiria vile atamalizana na hao haraka sana,” akaongeza. Ziara ya jana ilijumuisha uzinduzi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kaunti za Uasin Gishu na Nandi, huku Rais akitumia fursa hiyo kuimarisha ushawishi wake katika ngome yake. Pia alionekana kuanzisha kauli-mbiu mpya ya chama chake cha UDA akitumia maneno “Usawa ni Sawa” pamoja na kaulimbiu ya “Kazi ni Kazi”. Katika kituo cha Kaptumo, Kaunti ya Nandi, aliwaambia wafuasi wake: “Ninaposema UDA, ninyi mnajibu ‘Usawa ni Sawa’. Ninaposema ‘Usawa ni Sawa’, ninyi mnajibu ‘Mbele Pamoja’”. Kaulimbiu hiyo inajiri wakati Rais anajaribu kutumia miradi ya maendeleo kuimarisha nafasi yake ya kisiasa, hasa katika maeneo ambayo amekuwa akipata uungwaji mkono mkubwa. Katika Kaunti ya Nandi, Rais aliwaomba wakazi wamwongezee kura milioni moja kwa zile za awali na kuwataka vijana wanaostahili kupata vitambulisho vya taifa wajiandikishe kuwa wapigakura. “Urais unapatikana kupitia kura, na kama watu wangu, sitaki mnivunje moyo. Ninahitaji kura milioni moja zaidi kutoka kwenu,” akasema. Alitetea rekodi ya serikali yake, akisema imetekeleza ahadi zake katika sekta nyingi na iko tayari kwa uchaguzi mkuu. “Tumezitimiza ahadi zetu na kufanikisha mengi katika karibu sekta zote ili kuboresha maisha ya Wakenya. Rekodi yetu ya kuchapa kazi inajidhihirisha,” akasema, akiwashutumu wapinzani kwa kukosa manifesto na mipango madhubuti. Katika uzinduzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Moiben, Uasin Gishu, Rais Ruto alisema wapinzani wake hawatamshinda hata wakiungana. Alitetea pia ushirikiano wa serikali ya Kenya Kwanza na ODM, akisema utadumu hata baada ya uchaguzi wa 2027. “Serikali Jumuishi na washirika wetu wa ODM tutaendelea kuwepo hata baada ya 2027. Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha usawa kwa Wakenya wote,” alisema. Ziara hiyo pia ilifichua tofauti za kisiasa miongoni mwa viongozi wa eneo hilo huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia. Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago aliwaonya wanasiasa dhidi ya kutumia ziara ya Rais kulipiza kisasi au kuwafedhehesha wapinzani wao. Gavana Jonathan Bii alihimiza umoja huku akitaka ofisi yake iheshimiwe kama mwenyeji wa Rais. Viongozi hao waliwataka wakazi kumuunga mkono Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena. Kiongozi wa Wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot alisema Uhuru anapaswa kuipa serikali ya sasa nafasi ya kuongoza, huku Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen akimtaka Rais kuzingatia maendeleo na umoja wa kitaifa. Ziara hiyo itafikia kilele katika sherehe za Mashujaa Day Oktoba 20, zitakazoandaliwa kwa pamoja na kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet. Elgeyo Marakwet itaandaa mashindano ya riadha, Nandi fainali za voliboli, huku Uasin Gishu ikiandaa fainali za soka. Rais aliambatanisha ujumbe wake wa kisiasa na miradi ya miundombinu, umeme, nyumba za gharama nafuu na elimu ya ufundi. Katika Kaunti ya Nandi, alitangaza uwekezaji wa Sh20 bilioni kujenga kilomita 350 za barabara. Kwenye maeneo ya kilimo cha majanichai Nandi, wakulima wanaohudumiwa na viwanda vya Chebut na Kaptumo walipokea bonasi ya Sh12.50 kwa kila kilo ya chai msimu huu. Dkt Ruto aliwataka wakulima kuchagua wakurugenzi wenye uwezo wa kusimamia viwanda hivyo ili kuhakikisha wanapata mapato bora. “Bonasi za chai hutegemea jinsi wakurugenzi wanavyosimamia viwanda. Nawahimiza kuchagua viongozi wenye uwezo watakaohakikisha mnapata mapato bora,” akasema. Alifichua kuwa serikali ilikuwa imetoa Sh850 milioni kusaidia wakulima wadogo wa majanichai katika eneo hilo.
MFULULIZO wa ajali za helikopta nchini unapaswa kuwaamsha usingizini wenye mamlaka husika. Hatua za dharura zinahitajika ili kuzuia maafa zaidi. Kila mwaka, takribani ajali tano za helikopta huripotiwa nchini, hali inayozua maswali mazito kuhusu usalama wa usafiri huu wa angani na utekelezaji wa sheria zinazousimamia. Ajali ya hivi karibuni iliyohusisha Katibu wa Wizara ya Mazingira, Dkt Festus Ng’eno, na abiria wengine wanne inapaswa kuwa onyo la mwisho kwa serikali. Ingawa waliokuwa ndani ya ndege hiyo walinusurika, rubani alijeruhiwa vibaya huku helikopta hiyo iliyotua katika uwanja wa Kericho Golf Club ikiharibika pakubwa. Kisa hicho hakifai kutazamwa kama tukio moja pekee. Mwezi Agosti, ajali nyingine ya helikopta iliripotiwa Samburu, miezi michache baada ya Mbunge wa Emurua Dikirr, Yohana Ng’eno, kufariki katika ajali ya helikopta mwezi Februari mwaka huu. Matukio haya yanadhihirisha umuhimu wa kuchunguza kwa kina sababu za ajali hizo na kuhakikisha hatua za kuzuia kurudiwa kwa makosa zinachukuliwa. Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba uchunguzi umekuwa ukifanywa na ripoti kutolewa zikiwa na mapendekezo ya kuimarisha usalama wa usafiri wa angani. Hata hivyo, ikiwa mapendekezo hayo hayatekelezwi kikamilifu, uchunguzi ukibaki kuwa shughuli ya kuwasahaulisha waathiriwa na Wakenya kwa jumla maafa hayo tu. Serikali inapaswa kueleza hatua zilizochukuliwa kutokana na ripoti hizo na kwa nini ajali zinaendelea kutokea. Ripoti kadhaa zimebaini kuwa baadhi ya helikopta zinazotumiwa nchini ni kuukuu na zinahitaji kuondolewa kwenye huduma au kufanyiwa marekebisho makubwa. Ikiwa hali hii imethibitishwa na ukaguzi wa kitaalamu, hakuna sababu ya kuruhusu ndege hizo kuendelea kubeba abiria huku zikihatarisha maisha yao. Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) inapaswa kukagua helikopta zote, kuthibitisha ubora wa matengenezo yake na kusimamisha mara moja zile zisizokidhi viwango vya usalama. Aidha, uchunguzi unapaswa kuangazia mafunzo na uzoefu wa marubani, ratiba za matengenezo, hali ya hewa na mifumo ya usimamizi wa safari. Wamiliki na waendeshaji wa helikopta wanaokiuka kanuni wanapaswa kuwajibishwa bila upendeleo. Matokeo ya uchunguzi na utekelezaji wa mapendekezo yake pia yawekwe wazi kwa umma, bila kuathiri taratibu halali za uchunguzi. Serikali haipaswi kusubiri ajali nyingine imeze maisha ya viongozi au raia wasio na hatia ndipo ichukue hatua. Ni wakati mwafaka wa kutekeleza ripoti hizo kwa dhati. Hatua za sasa zitaamua ikiwa usafiri wa helikopta nchini utakuwa salama au utaendelea kuwa chanzo cha hofu na majonzi
More than N267 billion in released basic education intervention funds remained unspent as of August 2026, while over N65 billion in counterpart funding was yet to be accessed by states, the federal government has disclosed, raising fresh concerns over the management of resources meant to improve learning outcomes across the country.
MWANZA: Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, Oktoba 12, 2026, amezindua Shule Mpya ya Awali na Msingi Bugumangala, iliyopo Kijiji cha Bugumangala, Kata ya Nyanguge, Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza. Ujenzi wa shule hiyo umegharimu Sh milioni 430.7 zilizotolewa na Serikali kupitia Programu ya BOOST katika mwaka wa fedha 2025/2026. Mradi…
MWANZA: WAZIRI wa Habari, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapaswa kuhakikisha mradi wa ujenzi, upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Mwanza Kaskazini unakamilika kwa wakati ili kuimarisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo. Makonda amesema hayo leo alipofanya ziara mkoani Mwanza na kutembelea bandari hiyo, ambapo…
DAR ES SALAAM: Jukwaa la Uongozi wa Wanawake ni muhimu katika kujadili namna ya kuhakikisha wanawake wanaopata nafasi za uongozi wanadumu katika nafasi hizo na kuendelea kutumia uzoefu wao kuchangia maendeleo ya jamii hata baada ya kumaliza vipindi vyao vya uongozi, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) Kadari Singo. Akizungumza leo jijini…
DAR ES SALAAM: Tanzania inaangalia nishati ya nyuklia kama chanzo cha muda mrefu cha umeme, huku Urusi ikiibuka kuwa mmoja wa washirika muhimu wanaoweza kusaidia katika teknolojia hiyo. Rais Samia Suluhu Hassan alisema Juni 2026 kuwa Tanzania inaangalia uwezekano wa kutumia mitambo midogo ya nyuklia kuzalisha umeme na kwamba kampuni ya Urusi ya Rosatom tayari…
USHINDANI wa ugavana wa Mombasa katika uchaguzi wa 2027 unatarajiwa kupima uwezo wa vyama vya upinzani kuungana dhidi ya Rais William Ruto ili kudhibiti nyadhifa muhimu za uongozi katika kaunti hiyo. Kiongozi wa Jubilee Party, Fred Matiang’i, ametangaza kuwa chama hicho kitawasilisha wagombea katika nyadhifa zote za uchaguzi katika eneo la Pwani 2027, huku vyama vya upinzani vikiendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuwa na mgombea mmoja wa urais. Hatua hiyo inaiweka Jubilee katika ushindani wa moja kwa moja na Wiper, ambapo Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali, anapanga kuwania ugavana wa Mombasa kupitia tiketi ya chama hicho. Mbunge wa zamani wa Kisauni, Bw Ali Mbogo, pia anawania kiti hicho cha Gavana Abdulswamad Nassir wa ODM kupitia tiketi ya Jubilee. Awali, kinara wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Bw Rigathi Gachagua, alikuwa ametangaza kumuunga mkono Bw Ali, bila kujali iwapo atawania kiti hicho kwa tiketi ya DCP au Wiper. Dkt Matiang’i alisema Jubilee tayari kina watu wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali Pwani, lakini hakutaja baadhi yao kwa sababu bado wanahudumu serikalini akisema huenda wakaandamwa iwapo watatambuliwa kabla ya kujiuzulu. “Tuna wagombea wengi ambao wanataka kuwania viti vya kisiasa kupitia chama chetu katika eneo hili. Tuna wagombea watatu katika kila kiti cha kisiasa huku Pwani, kwa hivyo tutafanya uteuzi ili kumpata mgombea bora zaidi,” alisema. Jubilee pia imekuwa ikiandaa mikutano ya mashinani inapojitayarisha kwa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC). Dkt Matiang’i alichukua uongozi wa chama hicho kutoka kwa Rais mstaafu Bw Kenyatta mwezi uliopita. Alisema Jubilee imewasilisha kanuni zake za uteuzi kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na inajiandaa kufanya uteuzi wa wagombea kote nchini. Dkt Matiang’i pia alitetea uamuzi wake wa kuacha kazi katika Benki ya Dunia na kurejea nchini Kenya, akisema vijana wa Kenya, hasa kizazi cha Gen Z, walimtafuta wakitumia mtandao wa kijamii kabla ya kurejea kwake. “Nilipigiwa simu na vijana wa Gen Z kabla sijarejea hapa kutoka Benki ya Dunia. Jambo hilo lilikuwa kila mahali, kwenye mitandao ya kijamii,” alisema. Alipuuza madai kwamba kurejea kwake katika siasa kulifadhiliwa na Bw Kenyatta. “Hapana. Mkitaka kuuliza kuhusu mfadhili, wafadhili wangu ni wananchi wa Kenya,” alisema. Dkt Matiang’i alijiunga na Benki ya Dunia baada ya kuondoka serikalini 2022 na kurejea Kenya mwaka 2025 na kutangaza azma yake ya kuwania urais. Jubilee imemuidhinisha kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa 2027. Alisema kampeni yake inaungwa mkono na wakenya wa kawaida, wakiwemo wanaochanga fedha kwa ajili ya shughuli zake. “Urais unahitaji fedha nyingi, lakini mnajua kuwa azma yangu ya kuwania urais ni tofauti. Niliitwa kuja kuwatumikia Wakenya. Ni wao wanaofadhili kampeni zangu. Wananichangia fedha kwa ajili ya kampeni zangu, huku wengine wakinipatia fedha za mafuta ya gari,” alisema. Dkt Matiang’i alisema anawania urais kwa sababu anaamini Kenya inahitaji kiongozi mwenye uzoefu katika utumishi wa umma na utaalamu katika kusimamia Idara za serikali. “Nina uzoefu katika utumishi wa umma baada ya kuhudumu katika wizara mbali mbali. Nimefanya kazi kwa karibu na rais wa zamani na ninaamini mimi ndiye mgombea anayefaa zaidi kuchukua uongozi wa nchi hii,” alisema. Alisema atakabiliana na ufisadi, ubadhirifu wa rasilimali za umma, ushuru wa juu, ukosefu wa usalama na siasa za kikabila. Pia alikosoa sera za elimu za utawala wa Kenya Kwanza, hasa mfumo mpya wa ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu, akidai kuwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa kuendeleza masomo kutokana na changamoto za ufadhili.
MGOMBEAJI wa ugavana Nairobi, Askofu Margaret Wanjiru, jana alipigwa jeki baada ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i katika uchaguzi wa 2027. Akizungumza katika ibada ya kanisa la Jesus Is Alive Ministries jijini Nairobi Jumapili, Dkt Matiang’i alisema chama chake kitashirikiana kuhakikisha Askofu Wanjiru anakuwa gavana wa Nairobi. Alimtaka aendelee na kampeni zake, akisema yuko tayari kushirikiana naye kufikia wapiga kura. Askofu Wanjiru, ambaye atawania kiti hicho kupitia chama cha Kenya Moja Movement, alisema ndiye anayefaa kuongoza jiji na akawataka wagombeaji wengine kumuunga mkono ili kumshinda Bw Sakaja, anayetafuta muhula wa pili. Dkt Matiang’i pia alitoa wito kwa viongozi wa upinzani kuungana ili kuunda muungano moja wa kukabiliana na serikali katika uchaguzi mkuu wa 2027. Alikosoa vurugu na fujo katika mikutano ya kisiasa na kanisani, akisema maeneo ya ibada yanapaswa kuheshimiwa. Bi Wanjiru aliishutumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kushindwa kutimiza ahadi za kuboresha maisha na kuunda nafasi za kazi, huku akiahidi kushirikiana na viongozi wenye mawazo sawa ili kuleta mabadiliko ya kisiasa.
DAR ES SALAAM: Africa is becoming increasingly important to the global transition towards cleaner energy, with countries across the continent holding minerals needed for batteries, electric vehicles, renewable-energy systems and other technologies. But for Tanzania, the emerging green-minerals economy raises a critical question: Will the country become a supplier of minerals for industries abroad, or…
MAKAVAZI ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, Kang’o ka Jaramogi, Bondo, yameundwa kuhifadhi historia yake ya kisiasa na mchango wake katika safari ya kidemokrasia Kenya. Muundo wake wa pembe tano unaashiria umuhimu wa nambari tano katika maisha yake ya kisiasa, ukikumbusha kundi la viongozi watano wa ODM lililojulikana kama “Pentagon” wakati wa uchaguzi wa 2007. Ndani, ngazi tano zinaelekea kwenye kaburi lake, huku picha tano za Raila zikipamba kuta. Kaburi limewekwa juu ya jukwaa pana jeusi lenye taa chini yake. Pia kokoto nyeupe zimejaza sehemu zilizo karibu. Jiwe jeusi aina ya granite limeandikwa mojawapo ya kauli zake maarufu: Democracy is the price of freedom — Aluta Continua! ikimaanisha kuwa demokrasia ndiyo gharama ya uhuru na mapambano yanaendelea. Picha za kihistoria zenye mwangaza na michoro ukutani zinaonyesha safari yake ya kisiasa na mchango wake katika maendeleo ya demokrasia nchini. Pia kuna nukuu kutoka hotuba zake, ikiwemo alizotoa katika mkutano wa Azimio la Umoja katika Uwanja wa Kasarani na sherehe za Madaraka Dei za 2020. Ujumbe mmoja unasema: “Kinachofanya taifa kuwa kuu si watu linaowazalisha, bali watu linaowaheshimu.” Taa kubwa ya kuning’inia kwenye kilele cha paa na spika tano za JBL huongeza mwangaza na sauti ndani ya jengo hilo. Maandishi mengine yanaeleza maisha yake tangu alipozaliwa Maseno mnamo 1945, masomo yake, hadi alipoibuka kuwa mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini. Kwa jumla, makavazi hayo si mahali pa mazishi pekee, bali pia ni kumbukumbu ya maisha, misimamo na urithi wa Raila kwa vizazi vijavyo.
TANZANIA: OVER the past week, Tanzania has been confronted with disturbing reports of women losing their lives in violent circumstances. One woman was reportedly shot dead by her husband, another allegedly stabbed by her partner, while reports from Zanzibar concerning the death of a young woman have raised further questions. Different circumstances, different families, but…
WAZIRI wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu, Deborah Barasa, ametetea ukataji miti kwa ajili ya biashara, akipuuzilia mbali malalamishi kuhusu uharibifu wa misitu na kuyataja kama propaganda na siasa. Katika mahojiano na Taifa Leo, Dkt Barasa alisema serikali imejitolea kurejesha misitu huku ikisawazisha uhifadhi na manufaa ya kiuchumi yanayotokana na biashara ya mbao. Alisema utawala wa Rais William Ruto unalenga kurejesha asilimia 30 ya misitu, ikilinganishwa na asilimia 10 iliyolengwa na utawala uliotangulia. Kauli yake inajiri huku video isiyokuwa na tarehe ikisambaa mitandaoni, ikionyesha malori sita meupe yanayoonekana kubeba magogo yakipitia njia nyembamba msituni Kereita, karibu na Kimende, Kaunti ya Kiambu. Haijabainika magogo hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa sababu gani wala ikiwa shughuli hiyo ilikuwa halali. Video hiyo ilizua mjadala kuhusu hali ya misitu nchini na ilitokea siku chache kabla ya Siku ya Mazingira mnamo Jumamosi, ambapo serikali ilizindua kampeni nyingine ya upanzi wa miti. Zaidi ya miti milioni 17 inatarajiwa kupandwa katika kaunti 31 wakati wa msimu wa mvua za Oktoba hadi Disemba. Hata hivyo, ripoti ya Kiuchumi ya 2026 inaonyesha kupungua kwa mashamba mapya chini ya misitu, kuathirika kwa chemichemi za maji na kupanda kwa mauzo ya makaa katika misitu inayosimamiwa na serikali. Hali hii imechochea mashirika ya kiraia kukusanya saini zaidi ya 60,000 kupinga uharibifu wa misitu. Wiki iliyopita, mashirika hayo yaliandamana hadi Wizara ya Mazingira yakitaka kukomeshwa kwa ukataji miti kiholela, uvamizi wa misitu na uharibifu wa maeneo yaliyohifadhiwa. Mashirika hayo pia yalielezea wasiwasi kuhusu miradi katika Msitu wa Imenti na Hifadhi ya Kitaifa ya Nairobi, yakidai kuwa inaathiri maeneo yanayopaswa kulindwa. Yalisema Wakenya 4,642 wamewasilisha kesi mahakamani kutetea hifadhi hiyo. Aidha, yalipinga kuondolewa kwa marufuku ya ukataji miti katika eneo la Mau, mojawapo ya vyanzo vikuu vitano vya maji nchini. Msitu huo ulipoteza robo ya sehemu yenye miti kati ya 1973 na 2013 kutokana na ugawaji wa ardhi, makazi, ukataji miti haramu na uchomaji makaa. Sherie Gakii, mkuu wa kampeni za misitu nchini katika Shirika la Greenpeace Africa, alisema misitu inakabiliwa na vitisho kutokana na maslahi ya kibinafsi na miradi ya serikali. Hata hivyo, Dkt Barasa alisema ekari 150,000 kati ya hekari milioni 2.6 za misitu iliyotangazwa rasmi ndizo zimetengwa kwa matumizi ya kibiashara. Aliongeza kuwa kusitisha ukataji miti kwa biashara kungeathiri ajira na kulazimisha Kenya kuagiza mbao kutoka nje, jambo ambalo lingeongeza gharama kwa wananchi.
TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) inapanga kuongeza zaidi ya vituo 9,000 vya kupigia kura kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027. Kwa sasa pendekezo la IEBC la kuongeza idadi ya wapigakura katika kila kituo kutoka 700 hadi 1,000 linakabiliwa na upinzani katika Bunge la Kitaifa. Stakabadhi rasmi ya IEBC iliyowasilishwa bungeni inaonyesha kuwa vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kuongezeka kutoka 46,229 vilivyotumika katika uchaguzi wa 2022 hadi 55,393. Hii inatokana na lengo la tume kusajili wapigakura wapya milioni 6.3 kabla ya uchaguzi ujao. Hata hivyo, wabunge wanapinga pendekezo la kuongeza idadi ya wapigakura kwa kila kituo, wakitaka idadi ya sasa ya wapigakura 700 idumishwe. Pendekezo hilo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa 2024 liliidhinishwa na Seneti mnamo Disemba 2024, lakini limekumbana na upinzani katika Bunge la Kitaifa. IEBC inakadiria kuhitaji vifaa 59,959 vya kielektroniki vya Kiems kwa shughuli za uchaguzi, vikiwemo vifaa 3,959 vitakavyotengwa kwa mafunzo ya maafisa wa uchaguzi katika maeneobunge. Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, alisema maeneo ya vituo vipya yataamuliwa baada ya zoezi la usajili wa wapigakura kukamilika. “Vituo vipya vitaanzishwa katika maeneo ambako vituo vya sasa vya kupigia kura na usajili wa wapigakura vinazidi wapigakura 700,” akasema Bw Ethekon, akiongeza kuwa umbali na haja ya kusongeza vituo karibu na wapigakura pia zitazingatiwa. Kifungu cha 38A cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza kuwa idadi ya wapigakura katika kila kituo haipaswi kuzidi 700 ili kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa njia huru. Hata hivyo, Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria ya Bunge la Kitaifa inapinga pendekezo la kuongeza idadi hiyo. “Mimi lazima nikiri kuwa tuna tatizo kidogo kuhusu kifungu hiki na vifungu vingine. Tutapendekeza marekebisho wakati mswada huu utakapowasilishwa kusomwa kwa mara ya tatu,” akasema Mbunge wa Tharaka George Murugara, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo. Bw Ethekon alisema tume itahifadhi sajili ya sasa ya wapigakura milioni 22.3 na kuongeza wapya milioni 6.3, na hivyo kufikisha jumla ya milioni 28.63. Mchakato wa kuhakiki na kuthibitisha sajili hiyo utafanywa miezi sita kabla ya uchaguzi wa 2027. IEBC sasa inaachana na matumizi ya takwimu za sensa kuweka malengo ya usajili, ikipendelea takwimu kutoka Idara ya Usajili wa Watu na Idara ya Huduma za Uhamiaji kuhusu vitambulisho vya taifa na pasipoti zilizotolewa. Tume inasema mfumo wa zamani haukuwa sahihi wala rahisi kuthibitishwa, kwa kuwa takwimu za sensa zinajumuisha watu wasiostahili kupiga kura, wakiwemo wasio raia na wakimbizi. Badala yake, IEBC itatumia mfumo wa idadi ya watu wanaostahili kujiandikisha kama wapigakura, kwa kuzingatia barua zinazohitajika kisheria. Katiba, chini ya Ibara ya 83, inahitaji raia kuwa na kitambulisho cha taifa au pasipoti halali ya Kenya ili kusajiliwa kama mpigakura. Ili kufikia lengo lake, tume itaendeleza usajili katika afisi zote 290 za maeneobunge, vituo vya Huduma Center, wadi, taasisi za elimu ya juu na Wakenya wanaoishi ughaibuni. IEBC inasema mikakati hiyo itasaidia kuweka malengo halisi, kutumia rasilimali kwa ufanisi na kuhakikisha Wakenya wengi zaidi wanapata nafasi ya kujiandikisha kupiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
SERIKALI imesema hakuna kisa kipya cha Ebola kilichoripotiwa tangu kuthibitishwa kwa mgonjwa mmoja aliyekuwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo kutoka nje ya nchi. Watu 108 waliotangamana naye bado wamewekwa katika karantini na kufuatiliwa kwa karibu. Waziri wa Afya Aden Duale jana alisema kuwa hakuna hata mmoja kati ya watu hao aliyekuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo kufikia sasa. Mgonjwa huyo, Mkenya aliyekuwa amesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia Uganda, alipatikana na virusi hivyo, akawekwa katika kituo cha kutengwa Oktoba 5 na kufariki siku iliyofuatia. Bw Duale alisema watu 122 waliokuwa na mtagusano na mgonjwa huyo wametambuliwa na kuthibitishwa. Kati yao, 108, sawa na asilimia 88.5, wako karantini na wanafuatiliwa kila siku huku serikali ikiendelea kuwatafuta wengine. Alisema sampuli 293 zilizochukuliwa kutokana na tahadhari 289 za watu waliokuwa wakishukiwa kuwa na ugonjwa huo zilipimwa, lakini ni sampuli moja pekee iliyothibitisha maambukizi. Serikali pia imewapima wasafiri 667,675 katika vituo 26 vya kuingilia nchini, wakiwemo 2,345 katika muda wa saa 24 zilizotangulia. Bw Duale alisema Kenya iliifahamisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu kisa hicho ndani ya saa 24, huku vikosi vya kukabiliana na dharura vikiwa tayari kufanya kazi saa zote. Maabara tano zilizoteuliwa zinapima sampuli, zikiwemo maabara mbili za kuhamishika katika vituo vya mipakani vya Lwakhakha na Busia. Matokeo ya sampuli zilizothibitishwa yanaweza kupatikana ndani ya saa sita hadi 12. Serikali imetenga vitanda 241 vya kutenga wagonjwa katika hospitali tano jijini Nairobi, Eldoret na Mombasa. Aidha, wahudumu 4,917 wa afya wamepata mafunzo ya kukabiliana na Ebola, huku wataalamu 343 wakiwa tayari kwa dharura zozote. Waziri huyo alisema hakuna marufuku ya safari, biashara, usafiri au mikusanyiko ya umma, na hakuna amri ya kutotoka nje iliyowekwa. Viwanja vya ndege, bandari na vituo vya mipakani vinaendelea kufanya kazi kawaida, ingawa uchunguzi wa afya umeimarishwa. Wakati huohuo, maafisa wa afya wameonya kuhusu hatari ya maambukizi katika miji inayohudumia madereva wa malori yanayosafiri kati ya Kenya, Uganda, DRC, Sudan Kusini na Rwanda. Maeneo yanayofuatiliwa ni pamoja na Mai Mahiu, Naivasha, Gilgil, Salgaa, Molo, Londiani, Kericho, Narok na Bomet, pamoja na Timboroa, Eldoret na Kitale. Afisa wa afya ya umma Dkt Reuben Osiemo alisema uchunguzi katika mpaka wa Kenya na Uganda unapaswa kuimarishwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Hata hivyo, maafisa wa afya Nakuru, Bomet na Kericho walisema kaunti zao zimeweka mikakati ya kukabiliana na dharura, ikiwemo kutenga vituo vya wagonjwa na kuwafunza wahudumu wa afya.
FAMILIA ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga inakabiliwa na mtanziko wa kiitifaki huku Rais William Ruto na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta wakitarajiwa kuhudhuria maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila, uwanjani Migwena, eneobunge la Bondo hapo Alhamisi. Viongozi hao wawili wamekuwa wakishambuliana hadharani, hali inayozua hofu kwamba hafla hiyo inaweza kugeuka uwanja wa mzozo wa kisiasa. Taifa imebaini kuwa baadhi ya jamaa wa familia walitaka Bw Kenyatta awe mgeni wa heshima, huku wengine wakipinga pendekezo hilo. Mwaliko wake ulitolewa kwa matarajio kwamba Rais Ruto hangekuwepo baada ya kuzindua makavazi ya Raila mnamo Jumatano. Hata hivyo, Rais Ruto anatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ya Alhamisi. Msemaji wa mawasiliano wa Bw Kenyatta, Kanze Dena-Mararo, naye alisema kuhudhuria kwake “bado hakujathibitishwa” Jamaa wa familia ya Jaramogi alisema baadhi ya jamaa waliambiwa kuwa Bw Kenyatta angekuwa mgeni rasmi. “Hatujui hilo linamwacha Rais William Ruto katika nafasi gani, kwa sababu hakuna anayeweza kuhutubia baada ya Rais katika hafla. Hatujui kama naye atahudhuria,” akasema. Mbunge mmoja wa ODM alisema Bw Kenyatta hawezi kuwa mgeni rasmi katika hafla ambayo rais ambaye yupo madarakani anahudhuria. Mvutano huo unajiri huku familia ikionekana kugawanyika kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa nchi. Raila Junior, anayetaka kuwania kiti cha ubunge cha Kibra, ameunga mkono Serikali Jumuishi na kuidhinisha azma ya Rais Ruto kuwania muhula wa pili. Anashirikiana na ami yake Kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Oginga. Hata hivyo, dada yake Winnie Odinga, mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), na Mwakilishi wa Kike wa Kisumu Ruth Odinga wamekuwa wakikosoa namna ODM inavyoendeshwa baada ya kifo cha Raila. Winnie anatarajiwa kujiunga rasmi na vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ambaye ni kati ya viongozi wa upinzani wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo. Mama Ida Odinga, ambaye ni balozi wa Kenya na Mwakilishi wa Kudumu katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), amesisitiza kuwa mumewe hakuwa na maadui wa kudumu. “Waliokuwa wapinzani wake, wakijua siasa za Kenya, huenda wanamfahamu Raila vizuri kwa sababu mwishowe wote huungana, na mnakaribishwa. Huyo ndiye Raila,” akasema Jumatano wiki jana. Jamaa mwingine wa familia alikiri kuwa kuna mvutano kuhusu mwaliko wa Bw Kenyatta. “Kamati inapaswa kutoa uamuzi wa mwisho. Kuna wanaotaka hafla hiyo iachwe kwa upinzani, lakini kwa kuwa hii ndiyo sherehe kuu, Rais Ruto anatarajiwa kuhudhuria,” akasema. “Unawezaje kumzuia Rais kuhudhuria hafla kwa sababu ya maslahi ya kisiasa? Huu si mkutano wa kisiasa, bali ni hafla ya kuwakutanisha wote waliompenda Baba. Hakuna anayepaswa kuogopa kushiriki jukwaa na mwingine kwa sababu ya uhasama wa kisiasa,” akaongeza. Naibu wa Baraza la Wazee wa Jamii ya Waluo, Ker James Ayaga, alimtaka Dkt Oginga kuhakikisha familia ya Jaramogi ina umoja. “Yote yanayotokea katika familia ya Odinga ni jukumu la Dkt Oginga kama mwana mkubwa wa Jaramogi kuhakikisha anaunganisha familia,” akasema Bw Ayaga. Alimtaka aketi na wanafamilia wote, akiwemo Ida, ili wazungumze kwa sauti moja. Alisema umoja ndio urithi muhimu wa Jaramogi na Raila. Winnie, akizungumza katika hafla ya wiki iliyopita, alisema watu wa misimamo tofauti ya kisiasa, makabila na mataifa jirani wamealikwa kuadhimisha urithi wa babake. “Tunaweza kuwa na misimamo tofauti ya kisiasa na kutokubaliana kuhusu mwelekeo wa nchi yetu, lakini mnakaribishwa hapa. Hakuna anayetakiwa kuacha imani yake mlangoni,” akasema. Aliwataka wanasiasa kutogeuza Oktoba 15 kuwa mashindano ya kisiasa. “Sisi kama familia, tunatoa wito wa kusitishwa kwa mivutano ya kisiasa kwa heshima yake. Tafadhali, Oktoba 15 iwe siku ya kumkumbuka na kusherehekea maisha yake,” alisema. Kwa upande wake, Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Junet Mohammed, alisema kamati inayoongozwa na Prof Adams Oloo ndiyo itasimamia hafla ya Alhamisi, huku ODM ikihusika na mikutano ya chama ya kumuenzi Raila. “Kamati ndiyo inayosimamia kila kitu. Sisi tunasimamia tu shughuli za chama za kusherehekea maisha ya kiongozi wetu aliyeaga dunia,” akasema Prof Oloo jana alisema alikuwa anaingia kikaoni, hivyo mkuu wake wa mawasiliano angetuma taarifa lakini hakuwa amefanya hivyo kufikia wakati wa kuchapisha habari hizi.
By Nwafor Sunday, Online News Editor Peter Obi, the presidential candidate of Nigeria Democratic Congress, NDC, has questioned whether the Federal Government’s 30-day petrol price discount would reduce poverty, unemployment, insecurity and inequality in Nigeria. Obi raised the questions in a statement posted on his X platform on Sunday, describing the initiative as a reactive […]
By Luminous Jannamike ABUJA – The Peoples Democratic Party (PDP) has begun engaging the Independent National Electoral Commission (INEC) over the omission of some of its candidates from the commission’s final list, seeking a resolution in line with electoral laws and guidelines. The development has raised concerns within the party, with affected candidates facing uncertainty […]
Bill Gates on Sunday warned that unregulated artificial intelligence poses a growing threat and predicted an escalation in AI-powered cyberattacks in the coming year.
FASHONI KUFUA au kutofua mavazi kila baada ya kuyavalia na unapaswa kufua nguo zako kila baada ya muda upi, ni suala ambalo limezua mjadala mkali katika siku za majuzi na kuwagawanya wanamitandao. Mdahalo kuhusu ufuaji wa nguo ambao kiini chake ni hoja iliyosema mashine kubwa za dobi zimewashawishi wanajamii kwamba wanahitaji kuosha kila aina ya mavazi yao baada ya kuvalia mara moja tu. Hoja hiyo ilivutia hisia mseto kila mmoja akishikilia kwamba mtindo wake una mantiki zaidi. Kundi moja linasisitiza kwamba ni sawa kurudia kuvaa mavazi hadi mara nne kabla ya kuyaosha hasa iwapo ni jeans, shati na sweta. Wanaounga mkono hoja hii wanasema mradi hukutoka jasho, hukuzimwagilia chochote na hazinuki, hapana haja ya kufua nguo zako kila baada ya kuzivaa. Hawaoni maana ya kusafisha mavazi eti kwa sababu yaligusa mwili kwa saa sita pekee huku wengine wakisema kipimo cha kunusa mavazi kinatosha kuamua ama kufua au kufua nguo zako. Lakini kunao walioshawishika kwamba unapaswa kufua nguo zako kila baada ya kuyavaa. Wanasisitiza kwamba kila unapotoka nje na kutangamana na umma ni sharti uoshe mavazi uliyovalia. Unaweza, hata hivyo, kurudia kuyavaa bila kuyafua unaposhinda ndani ya nyumba bila kutoka mchana kutwa. Kufua ama kutofua nguo zako baada ya kuzivaa kunategemea mahali unamoishi na kiwango cha kutoka jasho. Kwa mfano, ikiwa unaishi sehemu zenye joto ni kawaida kutoka jasho kwa wingi kila wakati hivyo utahitajika kuosha nguo ulizovalia kila baada ya kuzivua na kuvalia nyingine safi ikilinganishwa na wanaoishi sehemu zenye baridi. Ni siri iliyowazi kwamba moja kati ya athari ya kufua nguo kila mara ni kwamba husababisha mavazi yako kunyauka rangi na kuchujuka kirahisi. Katika juhudi za kutatua mdahalo huo na kutoa mwongozi kuhusu jinsi kila vazi linapaswa kufuliwa, wataalam sasa wameingilia kati na kutoa vidokezo muhimu. Aina ya vazi Hukupa mwongozo kuhusu ama kufua au kutofua mavazi husika kila baada ya kuyavaa, wanafafanua wataalam. Mavazi ya ndani Chupi, kanchiri, shimizi, mavazi ya kuogelea, mavazi ya kwenda gym kufanya mazoezi, soksi, yanapaswa kufuliwa kila baada ya kuyavaa mara moja, wanasema wataalam. Haufai kamwe kurudia kuvaa nguo hizi kabla ya kuzisafisha, kuzianika na kuacha zikauke vyema, wanashauri. Nguo za kila siku Mavazi yenye rangi nyeupe, Tshirts, rinda, yanaweza kufuliwa kila baada ya kuvaliwa mara moja au mbili. Hata hivyo, mavazi kama vile fulana, leso, vikoi, buibui, kofia, yanaweza kuvaliwa mara kadhaa kabla ya kuoshwa vizuri ipasavyo. Jeans, Unaweza kuvalia nguo aina ya jeans mara hadi 10 kabla ya kuziosha. Mavazi mengine unayoweza kurudia mara kadhaa kabla ya kufua ni kama vile sweatshirts (mara tano hadi sita) koti na kabuti (mara moja au mbili kwa kila msimu. Hata hivyo, wataalam wanasistiza haja ya kuzingatia usawazishaji hasa kutokana na sababu usafi na masuala ya kiafya. Japo nguo zikifuliwa kila wakati hazitadumu, kwa wanaougua ugonjwa wa ngozi kama vile eczema ni muhimu zaidi kufua nguo zako ili kuzuia mwasho na bakteria.
UJAUZITO NA UZAZI IWAPO mtoto wako anaugua homa isiyoisha hata baada ya kutibiwa, anatatizika kula na kunywa au kushindwa kupumua vizuri, unashauriwa kumpeleka hospitalini atibiwe. Dalili hizi huenda zinaashiria ugonjwa sugu zaidi ambao haufai kupuuzwa, kulingana na Daktari wa watoto Anne Sheehan. Misimu ya vuli na kipupwe huashiria kilele cha kipindi cha maambukizi ya mfumo wa kupitishia hewa kama vile homa ya kawaida (common cold), influenza, RSV na Covid-19. Maradhi haya, anafafanua Dkt Sheehan, aghalabu huanza na dalili zinazofanana sana hivyo ni muhali kuzitofautisha, hasa wakati msimu wa baridi na homa unapoanzia mwishoni mwa kiangazi hivyo kusababisha mizio ya kimsimu. Mtoto anapougua dalili kama vile kukohoa, kutokwa na kamasi na maumivu ya koo, mtanziko unaomkumbuka kila mzazi ni ama kumruhusu aende shule, akae nyumbani ili apate nafuu au ampeleke hospitalini. Dkt Sheehan anafafanua kuwa kumruhusu mtoto kwenda shule akiwa anaugua kunaweza kumfanya akae muda mrefu bila kupata nafuu na kusambaza maambukizi yake kwa wanafunzi wenzake na wahudumu wa shule. “Maambukizi yote haya yanayozuka mara kwa mata yanaweza kusababisha athari sugu kwa baadhi ya wanajamii wa shule – au familia zao – walio na matatizo sugu ya kiafya yanayoweza kuzorotesha hali zao zaidi,” anafafanua Dkt Sheehan katika jarida la The Conversation. Maambukizi mengi ya mfumo wa kupitishia hewa kwa watoto, kwa kawaida yanaweza kudhibitiwa nyumbani, ikiwemo Covid-19, bila haja ya kwenda hospitalini kila wakati mtoto anapokohoa au kutiririkwa na kamasi, anaeleza. Hata hivyo, baadhi ya dalili huenda zikaashiria ugonjwa sugu hivyo hupaswi kuzipuuza katu. Kama mzazi anayemwelewa vyema mtoto wake, ni muhimu kutofautisha iwapo maambukizi ya mafua anayougua mtoto wako ni mafua ya kawaida, flu, RSV au Covid-19, flu, ikizingatiwa kuwa baadhi ya maradhi haya yanaweza kusababisha matatizo sugu kwa baadhi ya watoto. Covid-19 ina tishio la juu zaidi la kusababisha athari sugu na za muda mrefu kiafya, huku aina nyinginezo za mafua zikiwa na athari finyu, anasema mtaalam huyo wa watoto. “Mafua aina ya flu yanaweza kusababisha makali ya ugonjwa na kulazwa hospitalini huku RSV ikiwa na uwezekano wa kuwa hatari zaidi hasa kwa malaika, watoto wachanga na wanaougua matatizo sugu kiafya.”
MITANDAO ya kijamii imefurika jumbe za kutatanisha zinazohusisha wanawake “wakiwaanika” wanawake wenzao kwa wanachoita ‘kuwaibia” wanaume wao. Kila uchao, ni nadra kukosa kukumbana na picha ya mwanamke aliyechapishwa na mwanamke mwenzake akimmiminia cheche za matusi yasiyoweza kutamkika. Sehemu kubwa ya visa hivi vinahusisha wanawake waliopevuka kiumri wenye watoto kadhaa wanaowaanika wenzo wakiwashutumu kwa kusababisha waume zao kuwatekeleza watoto waliozaa nao. Katika juhudi za kulipiza kisasi na kuwafedhehesha wanawake wanaochumbiana na waume zao, baadhi ya wanawake husika hata huambatisha madai kuwa washindani wao wanaugua maradhi ya zinaa wakiwatahadharisha wengine wajiepushe nao. Ajabu ni kwamba, mwanamme ambaye ni mhusika mkuu anayezozaniwa katu hachapishwi wala jina lake kutajwa popote. Katika kisa cha majuzi, mwanamke ambaye ni mama wa watoto saba amemwanika mwanamke anayemtaja kuwa rafikiye wa miaka mingi kwa ‘kuwaibia’ watoto wake baba yao. Katika juhudi bayana za kumwaibisha mshindani wake, anachapisha picha yake na kutaja umri wake kuwa 55 japo anaonekana mchanga. Baadhi ya wanawake wanampa moyo wakimweleza alivyo mrembo kuliko rafikiye aliyegeuka adui huku wakiwalaani marafiki wanawake! Wengine wanakanusha kuwa mwanamme mtu mzima na akili zake timamu anaweza kuibiwa wakimtaka achapishe pia picha ya mwanamme husika wakihoji alifanya hivyo kwa hiari. Matukio haya yanadhihirisha uhalisia wa kutamausha kuhusu wanawake wanavyohiari kupigana, kuchukiana na kulaumiana badala ya badala ya kukabili mhusika mkuu mwanamme anayesababisha masaibu yao. Haihitaji mtaalam au mshauri nasaha kukueleza kuwa mwanamme mwenye akili razini anachagua kwa hiari ama kuchepuka au kuwa mwaminifu kwa mkewe na kutunza watoto waliojaaliwa pamoja. Wanandoa waliofunga pingu za maisha wana mkataba kati yao na endapo yeyote kati yao ataenda kinyume ahadi zao basi ndiye anayepaswa kulaumiwa wala sio mwanamke au mwanamke anayechepuka nao ambao hawafahamu ndewe wala sikio kuhusu ahadi au pandashuka walizopitia. Ni kinaya kisichoelezeka na aibu kwa wanawake katika karne hii kuumbuana na kuwalaani wanawake wenzao huku wakimwacha mwanamme aliyeamua mwenyewe kuvunja mkataba wa ndoa au mahusiano nao kustarehe wakimsawiri kama mhasiriwa wa kuhadaiwa, kupotoshwa na kuibiwa na mwanamke mwenzao.
TANGA; Dereva Ponsiano Taabuya amefariki dunia kufuatia ajali ya barabarani iliyotokana na lori la mizigo kupinduka na kusababisha kifo cha dereva huyo eneo la Muheza–Kibanda, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Kulingana na taarifa kwa umma iliyotolewa leo Oktoba 11, 2026 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ajali hiyo ilitokea Oktoba 10, 2026…
DAR ES SALAAM: BENKI ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Shirikisho la Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Afrika (ACCOSCA) pamoja na Chama Kikuu cha Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) katika kuunga mkono Kongamano la SACCA 2026, linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11 hadi…
DAR ES SALAAM: Baadhi ya mawakili ambao ni wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamefungua shauri la kikatiba katika Mahakama Kuu kupinga mchakato wa kinidhamu dhidi ya Rais wa chama hicho, Boniface Mwabukusi, ambao unaweza kusababisha kuvuliwa uwakili. Mawakili hao wamesema mchakato wa kumfikisha Mwabukusi mbele ya Kamati ya Maadili ya Mawakili unazua maswali…
WANANDOA katika ndoa za kiraia hawalazimiki kusubiri juhudi za upatanisho zikamilike kabla ya kuwasilisha kesi ya kutengana au kuvunja ndoa. Sheria inaruhusu mmoja wa wanandoa kuwasilisha mahakamani kesi ya kutengana au kuvunja ndoa hata kama juhudi za kuwapatanisha bado zinaendelea. Hata hivyo, wanandoa hao lazima wawe wamekaa kwenye ndoa hiyo kwa angalau miaka mitatu kabla ya kuwasilisha ombi la kutengana au kuvunja ndoa. Sheria inaeleza kuwa mtu aliye katika ndoa ya kiraia anaweza kuomba kutengana au kuvunja ndoa kwa misingi maalum. Misingi hiyo ni pamoja na uzinzi wa mchumba wake, ukatili, tabia mbaya kupita kiasi, kutelekezwa na mchumba kwa angalau miaka mitatu au ndoa kuvunjika kabisa kiasi kwamba haiwezi kurekebishwa. Muhimu zaidi ni kwamba sheria haimlazimishi mtu kusubiri hadi juhudi za upatanisho zifanikiwe au zishindikane. Inasema wazi kuwa mtu anaweza kuwasilisha kesi ya kutengana au kuvunja ndoa “licha ya juhudi zozote za kuwapatanisha wanandoa.” Hii ina maana kwamba kuwepo kwa mazungumzo ya kifamilia, usuluhishi au juhudi nyingine za kuokoa ndoa hakumzuii mmoja wa wanandoa kufika mahakamani. Hata hivyo, mahakama yenyewe inaweza kuamua kupeleka mzozo wa ndoa katika mchakato wa upatanisho iwapo wahusika watakubaliana. Pia, kesi ya kuvunja ndoa inaweza kuahirishwa kwa muda usiozidi miezi sita ili mahakama ifanye uchunguzi zaidi au kuwapa wanandoa nafasi nyingine ya kujaribu kusuluhisha tofauti zao. Sheria pia inaeleza mazingira ambayo ndoa inaweza kuchukuliwa kuwa imevunjika kabisa. Mbali na uzinzi na ukatili, ndoa inaweza kuchukuliwa kuwa imevunjika ikiwa mmoja wa wanandoa amempuuza mwenzake kimakusudi kwa angalau miaka miwili kabla ya kesi kuwasilishwa. Kutengana kwa wanandoa kwa angalau miaka miwili, iwe kwa hiari au kwa amri ya mahakama, pia ni sababu inayoweza kuonyesha kuwa ndoa imevunjika. Kutelekezwa kwa angalau miaka mitatu ni msingi mwingine. Aidha, kifungo cha maisha au kifungo cha miaka saba au zaidi kinaweza kuwa sababu ya ndoa kuchukuliwa kuwa imevunjika. Sheria pia inatambua hali ambapo mmoja wa wanandoa anaugua ugonjwa wa akili usiotibika, iwapo madaktari wawili, mmoja akiwa na ujuzi au uzoefu katika taaluma ya magonjwa ya akili, watathibitisha kuwa hali hiyo haiwezi kutibiwa au uwezekano wa kupona ni mdogo. Mahakama pia inaweza kutambua sababu nyingine yoyote inayofaa kulingana na mazingira ya kesi. Kwa hivyo, juhudi za familia, marafiki au wahusika wengine za kuokoa ndoa haziondoi haki ya mmoja wa wanandoa kuwasilisha kesi mahakamani. Badala yake, sheria inaacha milango yote miwili wazi: wanandoa wanaweza kujaribu kusuluhisha tofauti zao, lakini pia mmoja wao anaweza kuamua kufuata mchakato wa kisheria wa kutengana au kuvunja ndoa iwapo masharti yaliyowekwa yametimizwa.
Former Senator Shehu Sani has raised concerns over the South-East’s low voter registration figures, describing the situation as a serious political issue for the region.