WABUNGE wanapendekeza sheria kali kwa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wakiendesha uchaguzi katika vituo ambavyo havijaidhinishwa rasmi.
Maafisa hao wataweza kutozwa faini ya Sh2 milioni au kifungo cha miaka mitano jela, au adhabu zote mbili wakipatikana na hatia.
Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makosa ya Uchaguzi wa mwaka 2024, ambao unatarajiwa kujadiliwa katika hatua ya kamati katika Bunge la Kitaifa wiki hii.
Mswada huo unalenga kuimarisha uadilifu wa uchaguzi kwa kuhakikisha matokeo yanayotangazwa na maafisa wa IEBC yanatoka vituo vilivyoidhinishwa rasmi kupitia tangazo la serikali.
Kwa sasa, kuendesha uchaguzi katika kituo kisichoidhinishwa hakujatajwa kama kosa la uchaguzi chini ya sheria inayotumika kwa sasa.
Mswada huo unapendekeza kurekebisha kifungu cha sita cha Sheria ya Makosa ya Uchaguzi ili kuingiza kosa hilo pamoja na makosa mengine yanayohusiana na kutangaza na kubadilisha matokeo.
Pia, maafisa wa IEBC watakaochelewesha bila sababu kutangaza matokeo ya uchaguzi au kubadilisha kimakusudi matokeo yaliyokwisha kutangazwa watakuwa wakitenda kosa la uchaguzi.
Mswada huo uliofadhiliwa kwa pamoja na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot (Kericho), na mwenzake wa Wachache, Stewart Madzayo (Kilifi), ulitokana na mapendekezo ya Kamati ya Mdahalo wa Kitaifa (Nadco).
Ripoti ya Nadco iliidhinishwa na Bunge mnamo Februari 2024, baada ya mazungumzo ya pande mbili yaliyolenga kupunguza joto la kisiasa kufuatia maandamano yaliyosababisha vifo baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022 kupingwa na kiongozi wa wakati huo wa Azimio, Raila Odinga.
Seneti iliidhinisha mswada huo Novemba 19, 2024, kabla ya kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa, ambako ulisomwa kwa mara ya kwanza Desemba 3, 2024.
Katika uchaguzi mkuu wa 2022, IEBC iliidhinisha vituo 46,232 vya kupigia kura, ikilinganishwa na vituo 40,883 katika uchaguzi wa 2017.
Hata hivyo, kesi iliyopinga matokeo ya urais ya 2017 ilidai kuwa vituo visivyoidhinishwa vilianzishwa kinyume cha sheria katika Kaunti ya Mandera na kusimamiwa na maafisa ambao hawakuwa wameteuliwa rasmi.
Vilevile, kesi iliyopinga ushindi wa urais wa 2022 ilielezea hitilafu katika upeperushaji wa matokeo, ikidai kuwa matokeo kutoka zaidi ya vituo 11,000 ambavyo havikuwa vimeidhinishwa yalijumuishwa katika hesabu ya mwisho.
Kanuni za Uchaguzi za mwaka 2022 zinahitaji IEBC kutangaza rasmi vituo vya kupigia kura, maeneo yake na nambari zinazovitambulisha.
Faini ya Sh2m, jela miaka mitano kwa kuendesha uchaguzi nje ya vituo rasmi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…