FASHONI
KUFUA au kutofua mavazi kila baada ya kuyavalia na unapaswa kufua nguo zako kila baada ya muda upi, ni suala ambalo limezua mjadala mkali katika siku za majuzi na kuwagawanya wanamitandao.
Mdahalo kuhusu ufuaji wa nguo ambao kiini chake ni hoja iliyosema mashine kubwa za dobi zimewashawishi wanajamii kwamba wanahitaji kuosha kila aina ya mavazi yao baada ya kuvalia mara moja tu.
Hoja hiyo ilivutia hisia mseto kila mmoja akishikilia kwamba mtindo wake una mantiki zaidi.
Kundi moja linasisitiza kwamba ni sawa kurudia kuvaa mavazi hadi mara nne kabla ya kuyaosha hasa iwapo ni jeans, shati na sweta.
Wanaounga mkono hoja hii wanasema mradi hukutoka jasho, hukuzimwagilia chochote na hazinuki, hapana haja ya kufua nguo zako kila baada ya kuzivaa.
Hawaoni maana ya kusafisha mavazi eti kwa sababu yaligusa mwili kwa saa sita pekee huku wengine wakisema kipimo cha kunusa mavazi kinatosha kuamua ama kufua au kufua nguo zako.
Lakini kunao walioshawishika kwamba unapaswa kufua nguo zako kila baada ya kuyavaa.
Wanasisitiza kwamba kila unapotoka nje na kutangamana na umma ni sharti uoshe mavazi uliyovalia.
Unaweza, hata hivyo, kurudia kuyavaa bila kuyafua unaposhinda ndani ya nyumba bila kutoka mchana kutwa.
Kufua ama kutofua nguo zako baada ya kuzivaa kunategemea mahali unamoishi na kiwango cha kutoka jasho.
Kwa mfano, ikiwa unaishi sehemu zenye joto ni kawaida kutoka jasho kwa wingi kila wakati hivyo utahitajika kuosha nguo ulizovalia kila baada ya kuzivua na kuvalia nyingine safi ikilinganishwa na wanaoishi sehemu zenye baridi.
Ni siri iliyowazi kwamba moja kati ya athari ya kufua nguo kila mara ni kwamba husababisha mavazi yako kunyauka rangi na kuchujuka kirahisi.
Katika juhudi za kutatua mdahalo huo na kutoa mwongozi kuhusu jinsi kila vazi linapaswa kufuliwa, wataalam sasa wameingilia kati na kutoa vidokezo muhimu.
Aina ya vazi
Hukupa mwongozo kuhusu ama kufua au kutofua mavazi husika kila baada ya kuyavaa, wanafafanua wataalam.
Mavazi ya ndani
Chupi, kanchiri, shimizi, mavazi ya kuogelea, mavazi ya kwenda gym kufanya mazoezi, soksi, yanapaswa kufuliwa kila baada ya kuyavaa mara moja, wanasema wataalam.
Haufai kamwe kurudia kuvaa nguo hizi kabla ya kuzisafisha, kuzianika na kuacha zikauke vyema, wanashauri.
Nguo za kila siku
Mavazi yenye rangi nyeupe, Tshirts, rinda, yanaweza kufuliwa kila baada ya kuvaliwa mara moja au mbili.
Hata hivyo, mavazi kama vile fulana, leso, vikoi, buibui, kofia, yanaweza kuvaliwa mara kadhaa kabla ya kuoshwa vizuri ipasavyo.
Jeans,
Unaweza kuvalia nguo aina ya jeans mara hadi 10 kabla ya kuziosha.
Mavazi mengine unayoweza kurudia mara kadhaa kabla ya kufua ni kama vile sweatshirts (mara tano hadi sita) koti na kabuti (mara moja au mbili kwa kila msimu.
Hata hivyo, wataalam wanasistiza haja ya kuzingatia usawazishaji hasa kutokana na sababu usafi na masuala ya kiafya.
Japo nguo zikifuliwa kila wakati hazitadumu, kwa wanaougua ugonjwa wa ngozi kama vile eczema ni muhimu zaidi kufua nguo zako ili kuzuia mwasho na bakteria.
Je unafaa kufua nguo zako kila baada ya kuzivaa? Vidokezo hivi vitakufaa
FASHONI KUFUA au kutofua mavazi kila baada ya kuyavalia na unapaswa kufua nguo zako kila baada ya muda upi, ni suala ambalo limezua mjadala mkali katika siku za majuzi na kuwagawanya wanamitandao. Mdahalo kuhusu ufuaji wa nguo ambao kiini chake ni hoja iliyosema mashine kubwa za dobi zimewashawishi wanajamii kwamba wanahitaji kuosha kila aina ya mavazi yao baada ya kuvalia mara moja tu. Hoja hiyo ilivutia hisia mseto kila mmoja akishikilia kwamba mtindo wake una mantiki zaidi. Kundi moja linasisitiza kwamba ni sawa kurudia kuvaa mavazi hadi mara nne kabla ya kuyaosha hasa iwapo ni jeans, shati na sweta. Wanaounga mkono hoja hii wanasema mradi hukutoka jasho, hukuzimwagilia chochote na hazinuki, hapana haja ya kufua nguo zako kila baada ya kuzivaa. Hawaoni maana ya kusafisha mavazi eti kwa sababu yaligusa mwili kwa saa sita pekee huku wengine wakisema kipimo cha kunusa mavazi kinatosha kuamua ama kufua au kufua nguo zako. Lakini kunao walioshawishika kwamba unapaswa kufua nguo zako kila baada ya kuyavaa. Wanasisitiza kwamba kila unapotoka nje na kutangamana na umma ni sharti uoshe mavazi uliyovalia. Unaweza, hata hivyo, kurudia kuyavaa bila kuyafua unaposhinda ndani ya nyumba bila kutoka mchana kutwa. Kufua ama kutofua nguo zako baada ya kuzivaa kunategemea mahali unamoishi na kiwango cha kutoka jasho. Kwa mfano, ikiwa unaishi sehemu zenye joto ni kawaida kutoka jasho kwa wingi kila wakati hivyo utahitajika kuosha nguo ulizovalia kila baada ya kuzivua na kuvalia nyingine safi ikilinganishwa na wanaoishi sehemu zenye baridi. Ni siri iliyowazi kwamba moja kati ya athari ya kufua nguo kila mara ni kwamba husababisha mavazi yako kunyauka rangi na kuchujuka kirahisi. Katika juhudi za kutatua mdahalo huo na kutoa mwongozi kuhusu jinsi kila vazi linapaswa kufuliwa, wataalam sasa wameingilia kati na kutoa vidokezo muhimu. Aina ya vazi Hukupa mwongozo kuhusu ama kufua au kutofua mavazi husika kila baada ya kuyavaa, wanafafanua wataalam. Mavazi ya ndani Chupi, kanchiri, shimizi, mavazi ya kuogelea, mavazi ya kwenda gym kufanya mazoezi, soksi, yanapaswa kufuliwa kila baada ya kuyavaa mara moja, wanasema wataalam. Haufai kamwe kurudia kuvaa nguo hizi kabla ya kuzisafisha, kuzianika na kuacha zikauke vyema, wanashauri. Nguo za kila siku Mavazi yenye rangi nyeupe, Tshirts, rinda, yanaweza kufuliwa kila baada ya kuvaliwa mara moja au mbili. Hata hivyo, mavazi kama vile fulana, leso, vikoi, buibui, kofia, yanaweza kuvaliwa mara kadhaa kabla ya kuoshwa vizuri ipasavyo. Jeans, Unaweza kuvalia nguo aina ya jeans mara hadi 10 kabla ya kuziosha. Mavazi mengine unayoweza kurudia mara kadhaa kabla ya kufua ni kama vile sweatshirts (mara tano hadi sita) koti na kabuti (mara moja au mbili kwa kila msimu. Hata hivyo, wataalam wanasistiza haja ya kuzingatia usawazishaji hasa kutokana na sababu usafi na masuala ya kiafya. Japo nguo zikifuliwa kila wakati hazitadumu, kwa wanaougua ugonjwa wa ngozi kama vile eczema ni muhimu zaidi kufua nguo zako ili kuzuia mwasho na bakteria.

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…