WANANDOA katika ndoa za kiraia hawalazimiki kusubiri juhudi za upatanisho zikamilike kabla ya kuwasilisha kesi ya kutengana au kuvunja ndoa.
Sheria inaruhusu mmoja wa wanandoa kuwasilisha mahakamani kesi ya kutengana au kuvunja ndoa hata kama juhudi za kuwapatanisha bado zinaendelea.
Hata hivyo, wanandoa hao lazima wawe wamekaa kwenye ndoa hiyo kwa angalau miaka mitatu kabla ya kuwasilisha ombi la kutengana au kuvunja ndoa.
Sheria inaeleza kuwa mtu aliye katika ndoa ya kiraia anaweza kuomba kutengana au kuvunja ndoa kwa misingi maalum.
Misingi hiyo ni pamoja na uzinzi wa mchumba wake, ukatili, tabia mbaya kupita kiasi, kutelekezwa na mchumba kwa angalau miaka mitatu au ndoa kuvunjika kabisa kiasi kwamba haiwezi kurekebishwa.
Muhimu zaidi ni kwamba sheria haimlazimishi mtu kusubiri hadi juhudi za upatanisho zifanikiwe au zishindikane.
Inasema wazi kuwa mtu anaweza kuwasilisha kesi ya kutengana au kuvunja ndoa “licha ya juhudi zozote za kuwapatanisha wanandoa.”
Hii ina maana kwamba kuwepo kwa mazungumzo ya kifamilia, usuluhishi au juhudi nyingine za kuokoa ndoa hakumzuii mmoja wa wanandoa kufika mahakamani.
Hata hivyo, mahakama yenyewe inaweza kuamua kupeleka mzozo wa ndoa katika mchakato wa upatanisho iwapo wahusika watakubaliana.
Pia, kesi ya kuvunja ndoa inaweza kuahirishwa kwa muda usiozidi miezi sita ili mahakama ifanye uchunguzi zaidi au kuwapa wanandoa nafasi nyingine ya kujaribu kusuluhisha tofauti zao.
Sheria pia inaeleza mazingira ambayo ndoa inaweza kuchukuliwa kuwa imevunjika kabisa.
Mbali na uzinzi na ukatili, ndoa inaweza kuchukuliwa kuwa imevunjika ikiwa mmoja wa wanandoa amempuuza mwenzake kimakusudi kwa angalau miaka miwili kabla ya kesi kuwasilishwa.
Kutengana kwa wanandoa kwa angalau miaka miwili, iwe kwa hiari au kwa amri ya mahakama, pia ni sababu inayoweza kuonyesha kuwa ndoa imevunjika.
Kutelekezwa kwa angalau miaka mitatu ni msingi mwingine.
Aidha, kifungo cha maisha au kifungo cha miaka saba au zaidi kinaweza kuwa sababu ya ndoa kuchukuliwa kuwa imevunjika.
Sheria pia inatambua hali ambapo mmoja wa wanandoa anaugua ugonjwa wa akili usiotibika, iwapo madaktari wawili, mmoja akiwa na ujuzi au uzoefu katika taaluma ya magonjwa ya akili, watathibitisha kuwa hali hiyo haiwezi kutibiwa au uwezekano wa kupona ni mdogo.
Mahakama pia inaweza kutambua sababu nyingine yoyote inayofaa kulingana na mazingira ya kesi.
Kwa hivyo, juhudi za familia, marafiki au wahusika wengine za kuokoa ndoa haziondoi haki ya mmoja wa wanandoa kuwasilisha kesi mahakamani.
Badala yake, sheria inaacha milango yote miwili wazi: wanandoa wanaweza kujaribu kusuluhisha tofauti zao, lakini pia mmoja wao anaweza kuamua kufuata mchakato wa kisheria wa kutengana au kuvunja ndoa iwapo masharti yaliyowekwa yametimizwa.
SHERIA: Mipango yaatanisho haizuii mtu kuwasilisha kesi ya talaka

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…