SEKTA ya meli za kitalii za kimataifa imepata pigo nchini kutokana na kisa cha kwanza cha Ebola nchini, huku kampuni ya MSC Cruises ikisitisha kuajiri mabaharia Wakenya kwenye meli zake.
MSC Cruises, ambayo huajiri mamia ya Wakenya kwenye meli zake, imesema hatua hiyo ya muda itadumu hadi Oktoba 31, ikitaja hali ya hivi karibuni ya afya ya umma nchini.
Katika ujumbe kwa wafanyakazi walioathiriwa, kampuni hiyo ya usafiri wa meli za kitalii, ilisema uamuzi huo ni wa tahadhari huku ikiendelea kufuatilia na kutathmini hali ilivyo.
Kampuni hiyo iliomba radhi kwa kutoa taarifa hiyo katika muda mfupi, lakini ikawahakikishia wafanyakazi walioathiriwa kuwa uamuzi huo hautaathiri ajira zao, mikataba yao ya kazi wala fursa zao za baadaye katika kampuni hiyo.
Ilisema wafanyakazi ambao mipango yao ya kusafiri imeahirishwa watapewa kipaumbele katika kupanga upya safari zao kuanzia Novemba 1, isipokuwa kama kutakuwa na matukio mengine yatakayohitaji hatua za ziada.
Ingawa MSC Cruises haikutaja Ebola moja kwa moja katika taarifa yake, hatua hiyo imezua maswali kuhusu uwezekano wa waajiri wengine wa kimataifa kuchukua hatua kama hizo za tahadhari na athari zake kwa Wakenya wanaotafuta ajira nje ya nchi.
Mwezi Julai, baadhi ya wafanyakazi Wakenya pia walikwama baada ya kampuni hiyo ya meli za kitalii kuahirisha safari za wafanyakazi kutoka Kenya, ingawa hakuna kisa cha Ebola kilichokuwa kimeripotiwa wakati huo.
“Tafadhali fahamuni kuwa kutokana na mlipuko wa Ebola, usimamizi umeamua kuahirisha kuingia kwa wafanyakazi kutoka Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda kwenye meli hadi pale itakapotangazwa vinginevyo,” barua pepe kutoka kwa kampuni hiyo ya meli za kitalii ilisema.
Duru zilisema baadhi ya wafanyakazi kutoka Diani na Mombasa waliokuwa wanatarajiwa kuabiri meli ya kampuni hiyo walikwama.
Mchambuzi wa masuala ya utalii, Bw Mohamed Hersi, alisema sekta hiyo haijapokea ripoti za watalii waliokatiza safari zao nchini kwa sababu ya Ebola.
Hata hivyo, alionya kuwa hali inaweza kubadilika iwapo nchi ambazo Kenya hutegemea sana kwa utalii zitatangaza masharti makali zaidi ya ushauri wa usafiri.
“Hatujapokea taarifa za safari zozote zilizoghairiwa. Yote yatategemea ushauri wa usafiri, hasa kutoka kwa serikali za Uingereza, Marekani na Milki za Kiarabu (UAE),” alisema Bw Hersi, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Pollman’s Tours and Safaris.
Bw Hersi alieleza matumaini kuwa Kenya itaepuka ushauri mkali wa usafiri kwa kuwa kisa cha Ebola kilichoripotiwa kilitoka nje ya nchi na maafisa wa afya wamechukua hatua za kudhibiti hatari.
Kwa upande wake, meneja wa kampuni ya Africa Last Minute Ltd, Bw Abraham Guyo, alionya kuwa kisa hicho kinaweza kudhoofisha imani ya wageni kwa Kenya kama kivutio cha watalii, hasa iwapo wasiwasi wa kimataifa utaongezeka.
Wizara ya Afya ilithibitisha kisa cha kwanza nchini Kenya cha ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo mnamo Oktoba 6.
Mgonjwa huyo, aliyekuwa amesafiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Uganda hadi Nairobi, baadaye alifariki na kuzikwa kwa kuzingatia taratibu za afya ya umma.
Serikali imesisitiza kuwa kisa hicho kilitoka nje ya nchi na imewataka Wakenya kuwa watulivu, kufuata mwongozo rasmi wa afya na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.
Serikali imesema inaongeza ufuatiliaji wa magonjwa na kuimarisha hatua nyingine za afya ya umma ili kuzuia maambukizi zaidi.
Ebola: Pigo kampuni ya meli ikisitisha ajira kwa Wakenya

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…