WAZIRI wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu, Deborah Barasa, ametetea ukataji miti kwa ajili ya biashara, akipuuzilia mbali malalamishi kuhusu uharibifu wa misitu na kuyataja kama propaganda na siasa.
Katika mahojiano na Taifa Leo, Dkt Barasa alisema serikali imejitolea kurejesha misitu huku ikisawazisha uhifadhi na manufaa ya kiuchumi yanayotokana na biashara ya mbao.
Alisema utawala wa Rais William Ruto unalenga kurejesha asilimia 30 ya misitu, ikilinganishwa na asilimia 10 iliyolengwa na utawala uliotangulia.
Kauli yake inajiri huku video isiyokuwa na tarehe ikisambaa mitandaoni, ikionyesha malori sita meupe yanayoonekana kubeba magogo yakipitia njia nyembamba msituni Kereita, karibu na Kimende, Kaunti ya Kiambu.
Haijabainika magogo hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa sababu gani wala ikiwa shughuli hiyo ilikuwa halali.
Video hiyo ilizua mjadala kuhusu hali ya misitu nchini na ilitokea siku chache kabla ya Siku ya Mazingira mnamo Jumamosi, ambapo serikali ilizindua kampeni nyingine ya upanzi wa miti.
Zaidi ya miti milioni 17 inatarajiwa kupandwa katika kaunti 31 wakati wa msimu wa mvua za Oktoba hadi Disemba.
Hata hivyo, ripoti ya Kiuchumi ya 2026 inaonyesha kupungua kwa mashamba mapya chini ya misitu, kuathirika kwa chemichemi za maji na kupanda kwa mauzo ya makaa katika misitu inayosimamiwa na serikali.
Hali hii imechochea mashirika ya kiraia kukusanya saini zaidi ya 60,000 kupinga uharibifu wa misitu.
Wiki iliyopita, mashirika hayo yaliandamana hadi Wizara ya Mazingira yakitaka kukomeshwa kwa ukataji miti kiholela, uvamizi wa misitu na uharibifu wa maeneo yaliyohifadhiwa.
Mashirika hayo pia yalielezea wasiwasi kuhusu miradi katika Msitu wa Imenti na Hifadhi ya Kitaifa ya Nairobi, yakidai kuwa inaathiri maeneo yanayopaswa kulindwa. Yalisema Wakenya 4,642 wamewasilisha kesi mahakamani kutetea hifadhi hiyo.
Aidha, yalipinga kuondolewa kwa marufuku ya ukataji miti katika eneo la Mau, mojawapo ya vyanzo vikuu vitano vya maji nchini. Msitu huo ulipoteza robo ya sehemu yenye miti kati ya 1973 na 2013 kutokana na ugawaji wa ardhi, makazi, ukataji miti haramu na uchomaji makaa.
Sherie Gakii, mkuu wa kampeni za misitu nchini katika Shirika la Greenpeace Africa, alisema misitu inakabiliwa na vitisho kutokana na maslahi ya kibinafsi na miradi ya serikali.
Hata hivyo, Dkt Barasa alisema ekari 150,000 kati ya hekari milioni 2.6 za misitu iliyotangazwa rasmi ndizo zimetengwa kwa matumizi ya kibiashara.
Aliongeza kuwa kusitisha ukataji miti kwa biashara kungeathiri ajira na kulazimisha Kenya kuagiza mbao kutoka nje, jambo ambalo lingeongeza gharama kwa wananchi.
Waziri wa mazingira atetea ukataji miti, ataja malalamishi kuwa propaganda

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…