RAIS William Ruto jana alimrejelea Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kama kiongozi msaliti ambaye alimgeuka na kupuuza maelewano ya kila mmoja wao kuongoza kwa mihula miwili baada ya kuchukua uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2013.
“Nilikuunga mkono katika uchaguzi wa 2013 na 2017, ukatangaza kuwa ungehudumu kwa miaka 10 kisha uniunge mkono kwa miaka 10 mingine. Lakini ulinidanganya. Wewe nimtu asiyekuwa na shukrani hata kidogo,” akasema Rais Ruto.
Alikuwa akiongea katika ngome yake ya kisiasa, Kaunti ya Uasin Gishu ambapo aliwataka wafuasi wake kumpa kura milioni moja zaidi katika uchaguzi wa 2027.
Bw Kenyatta na Rais Ruto walihudumu pamoja kama rais na naibu rais kuanzia 2013 hadi 2022, lakini uhusiano wao ulidorora Uhuru alipomuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa 2022.
“Wale ambao wanalalamika kuhusu Uhuru wanafaa waniulize. Huyo jamaa ni mkora. Kama alinihadaa, mimi mwenye nilimpigia kura na kumfanyia kampeni, fikiria vile atamalizana na hao haraka sana,” akaongeza.
Ziara ya jana ilijumuisha uzinduzi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika kaunti za Uasin Gishu na Nandi, huku Rais akitumia fursa hiyo kuimarisha ushawishi wake katika ngome yake.
Pia alionekana kuanzisha kauli-mbiu mpya ya chama chake cha UDA akitumia maneno “Usawa ni Sawa” pamoja na kaulimbiu ya “Kazi ni Kazi”.
Katika kituo cha Kaptumo, Kaunti ya Nandi, aliwaambia wafuasi wake: “Ninaposema UDA, ninyi mnajibu ‘Usawa ni Sawa’. Ninaposema ‘Usawa ni Sawa’, ninyi mnajibu ‘Mbele Pamoja’”.
Kaulimbiu hiyo inajiri wakati Rais anajaribu kutumia miradi ya maendeleo kuimarisha nafasi yake ya kisiasa, hasa katika maeneo ambayo amekuwa akipata uungwaji mkono mkubwa.
Katika Kaunti ya Nandi, Rais aliwaomba wakazi wamwongezee kura milioni moja kwa zile za awali na kuwataka vijana wanaostahili kupata vitambulisho vya taifa wajiandikishe kuwa wapigakura.
“Urais unapatikana kupitia kura, na kama watu wangu, sitaki mnivunje moyo. Ninahitaji kura milioni moja zaidi kutoka kwenu,” akasema.
Alitetea rekodi ya serikali yake, akisema imetekeleza ahadi zake katika sekta nyingi na iko tayari kwa uchaguzi mkuu.
“Tumezitimiza ahadi zetu na kufanikisha mengi katika karibu sekta zote ili kuboresha maisha ya Wakenya. Rekodi yetu ya kuchapa kazi inajidhihirisha,” akasema, akiwashutumu wapinzani kwa kukosa manifesto na mipango madhubuti.
Katika uzinduzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Moiben, Uasin Gishu, Rais Ruto alisema wapinzani wake hawatamshinda hata wakiungana.
Alitetea pia ushirikiano wa serikali ya Kenya Kwanza na ODM, akisema utadumu hata baada ya uchaguzi wa 2027.
“Serikali Jumuishi na washirika wetu wa ODM tutaendelea kuwepo hata baada ya 2027. Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha usawa kwa Wakenya wote,” alisema.
Ziara hiyo pia ilifichua tofauti za kisiasa miongoni mwa viongozi wa eneo hilo huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia.
Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago aliwaonya wanasiasa dhidi ya kutumia ziara ya Rais kulipiza kisasi au kuwafedhehesha wapinzani wao.
Gavana Jonathan Bii alihimiza umoja huku akitaka ofisi yake iheshimiwe kama mwenyeji wa Rais. Viongozi hao waliwataka wakazi kumuunga mkono Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena.
Kiongozi wa Wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot alisema Uhuru anapaswa kuipa serikali ya sasa nafasi ya kuongoza, huku Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen akimtaka Rais kuzingatia maendeleo na umoja wa kitaifa.
Ziara hiyo itafikia kilele katika sherehe za Mashujaa Day Oktoba 20, zitakazoandaliwa kwa pamoja na kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet.
Elgeyo Marakwet itaandaa mashindano ya riadha, Nandi fainali za voliboli, huku Uasin Gishu ikiandaa fainali za soka.
Rais aliambatanisha ujumbe wake wa kisiasa na miradi ya miundombinu, umeme, nyumba za gharama nafuu na elimu ya ufundi.
Katika Kaunti ya Nandi, alitangaza uwekezaji wa Sh20 bilioni kujenga kilomita 350 za barabara.
Kwenye maeneo ya kilimo cha majanichai Nandi, wakulima wanaohudumiwa na viwanda vya Chebut na Kaptumo walipokea bonasi ya Sh12.50 kwa kila kilo ya chai msimu huu. Dkt Ruto aliwataka wakulima kuchagua wakurugenzi wenye uwezo wa kusimamia viwanda hivyo ili kuhakikisha wanapata mapato bora.
“Bonasi za chai hutegemea jinsi wakurugenzi wanavyosimamia viwanda. Nawahimiza kuchagua viongozi wenye uwezo watakaohakikisha mnapata mapato bora,” akasema.
Alifichua kuwa serikali ilikuwa imetoa Sh850 milioni kusaidia wakulima wadogo wa majanichai katika eneo hilo.
Ruto ampapura Uhuru, asema hawezi kuaminika

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…