CHAMA cha National Reconstruction Alliance (NRA), kinachohusishwa na Seneta wa Busia Okiya Omtatah, kimeenda mahakamani kupinga uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wa kulegeza baadhi ya masharti ya usalama wa karatasi za kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
Chama hicho kinasema hatua hiyo inaweza kurahisisha kughushi, kunakili na kuchezewa kwa karatasi za kura, hivyo kuzua wasiwasi kuhusu uadilifu na uwazi wa uchaguzi ujao.
Mahakama Kuu imetangaza kesi hiyo kuwa ya dharura na kuagiza IEBC na walalamishi wengine kujibu ndani ya siku saba. Kesi hiyo itatajwa Oktoba 14 kwa maelekezo zaidi.
NRA inapinga marekebisho ya zabuni nambari 3, yaliyotolewa Septemba 17, 2026, ambayo tume hiyo ilisema yanalenga kupunguza gharama na muda unaohitajika kununua karatasi za kura na vifaa vingine vya uchaguzi.
Mzozo huo unatokana na zabuni iliyotangazwa Agosti 11, 2026, ya kusambaza karatasi za kura na vifaa vingine chini ya mkataba wa miaka mitatu.
Hapo awali, zabuni hiyo ilihitaji mifumo mbalimbali ya usalama, ikiwemo michoro maalumu inayozuia kughushi, maandishi madogo yenye taarifa zinazobadilika, misimbo ya QR inayozuia kunakili na nambari za utambulisho zilizochapishwa kwa wino wa rangi mbalimbali.
Hata hivyo, marekebisho hayo yanaruhusu matumizi ya wino mweusi pekee kwa nambari za utambulisho, michoro na maandishi yasiyobadilika.
NRA inasema IEBC haijatoa ushahidi wa kiufundi unaothibitisha kuwa masharti mapya yatatoa ulinzi sawa au bora kuliko yale ya awali.
Chama hicho kinasisitiza kuwa karatasi ya kura si bidhaa ya kawaida ya zabuni, bali ni stakabadhi muhimu inayotumiwa na Wakenya kutekeleza mamlaka yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi.
Kinasema gharama na muda mfupi wa ununuzi havipaswi kutumiwa kama sababu ya kupunguza usalama wa uchaguzi bila ushahidi wa kutosha. NRA pia inaonya kuwa udhaifu wowote ukibainika baada ya karatasi kuchapishwa na kusambazwa, huenda ikawa vigumu kurekebisha hali hiyo.
Katibu mkuu wa chama hicho, Amemba Magufuli, alisema wanataka uwajibikaji wa mapema kabla ya maamuzi yenye athari kubwa kukumbatiwa.
NRA inataka mahakama itupilie mbali mabadiliko hayo, irejeshe masharti ya awali na kuagiza tathmini huru ya kiufundi ili kuhakikisha usalama wa karatasi za kura unalindwa.
Hata hivyo, chama hicho hakidai kuwa IEBC inapanga kuendeleza udanganyifu wa uchaguzi au kwamba karatasi za kura tayari zimechezewa.
Omtatah afika kortini kupinga IEBC kulegeza masharti ya usalama wa karatasi za kura

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…