IKIWA imesalia chini ya miezi 10 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, upinzani unaendelea kukabiliwa na mashaka kuhusu viongozi wasioaminika ndani ya kambi hiyo, huku mvutano kuhusu mgombea wake wa urais ukiendelea.
Mashaka hayo yamezidi baada ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro na aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt Fred Matiang’i, kujitokeza kupinga madai yanayotilia shaka uaminifu wao ndani ya upinzani.
Hivi majuzi wawili hao wameonekana kushirikiana kisiasa, hali iliyoibua maswali kuhusu mikakati yao kuelekea uchaguzi ujao.
Kuingia kwa Bw Nyoro katika kambi ya upinzani kumepokelewa kwa mashaka, hasa na chama cha DCP ambacho kinaendelea kumhusisha na serikali ya sasa.
Jumapili, Seneta wa Nyandarua, John Methu, ambaye ni Katibu Mkuu wa DCP, alitilia shaka nia ya Bw Nyoro, akidai kuwa hatua zake za kisiasa zinaweza kumnufaisha Rais William Ruto.
Bw Methu alidai kuwa muda mfupi baada ya DCP kushinda uchaguzi mdogo wa Ol Kalou mnamo Julai, watu kutoka serikalini walimwendea na kumpa ofa ya kuanzisha chama chake ili kugawanya upinzani na kudhoofisha ushawishi wa kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua katika Mlima Kenya.
Alisema alikataa ofa hiyo iliyohusisha kupewa chama, fedha, vifaa vya kampeni na wagombea, ili kushindana na DCP na kuifanya ionekane kuwa haishirikiani na serikali. Alidai pia kuwa mpango huo ungeweza kumwezesha kuwa mgombea mwenza wa Ruto.
Bw Methu alisema Gavana wa Murang’a, Irungu Kang’ata, pia alifikiwa na pendekezo kama hilo, lakini akalikataa.
Aliongeza kuwa alimweleza Bw Gachagua kuhusu suala hilo kabla ya kuwasiliana na Bw Nyoro, ambaye alisema alimwonya dhidi ya kuingia katika mtego wa kugawanya kura za Mlima Kenya.
Kwa mujibu wa Bw Methu, mbunge huyo wa Kiharu alimwambia kuwa Rais Ruto anahofia umoja wa Mlima Kenya na hataki viongozi wa eneo hilo wawe katika chama kimoja.
Bw Methu alidai Bw Nyoro alikuwa amemwahidi kujiunga na DCP baadaye, na hata alikuwa tayari kumpa nafasi yake ya pili baada ya Bw Gachagua. Hata hivyo, alishangazwa na uamuzi wa mbunge huyo kuanzisha chama chake.
Bw Nyoro alizindua chama cha People's Party of Kenya (PPK) mnamo Agosti baada ya kujitenga na UDA ya Rais Ruto. Tangu wakati huo, amekuwa akizunguka nchini kukitangaza chama hicho kabla ya uchaguzi wa 2027.
Akizungumza na Taifa Leo, Bw Nyoro alikanusha madai ya Bw Methu, akisema hawajawahi kukutana kujadili suala la kujiunga na DCP. “Hatujawahi kukutana kuzungumzia jambo kama hilo. Huo ni upuuzi mtupu na madai ya kitoto,” akasema Bw Nyoro.
Alimshutumu Bw Gachagua kwa kuongoza kampeni ya kumchafua, akidai kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakimfikishia ujumbe kutoka kwa Bw Gachagua Amerika ukiwaelekeza jinsi ya kumkosoa.
Bw Gachagua mwenyewe amekuwa akiwaonya viongozi wa upinzani kuhusu watu anaodai wamepandikizwa na Rais Ruto katika vyama vyao ili kuvuruga umoja wao.
Dkt Matiang’i pia amewahi kupinga madai kwamba anafanya kazi ya kudhoofisha upinzani kutoka ndani. Alisema shutuma hizo ni mbinu ya kukwepa kujadili masuala muhimu. “Watu wanapokosa hoja, huamua kutumia matusi na majina ya kudhalilisha,” akasema mnamo Agosti.
Dkt Matiang’i aliteuliwa hivi majuzi kuwa kiongozi wa chama cha Jubilee, akimrithi rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Bw Methu alisema anamwamini kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, akidai wameonyesha msimamo thabiti wa kutaka Rais Ruto aondoke madarakani.
Hata hivyo, alionyesha kutokuwa na uhakika kuhusu Dkt Matiang’i, akisema urafiki wake wa kisiasa na Bw Nyoro umeibua maswali kuhusu uaminifu wake.
Usuhuba wa Matiang’i na Nyoro waibua maswali

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…