USHINDANI wa ugavana wa Mombasa katika uchaguzi wa 2027 unatarajiwa kupima uwezo wa vyama vya upinzani kuungana dhidi ya Rais William Ruto ili kudhibiti nyadhifa muhimu za uongozi katika kaunti hiyo.
Kiongozi wa Jubilee Party, Fred Matiang’i, ametangaza kuwa chama hicho kitawasilisha wagombea katika nyadhifa zote za uchaguzi katika eneo la Pwani 2027, huku vyama vya upinzani vikiendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kuwa na mgombea mmoja wa urais.
Hatua hiyo inaiweka Jubilee katika ushindani wa moja kwa moja na Wiper, ambapo Mbunge wa Nyali, Mohamed Ali, anapanga kuwania ugavana wa Mombasa kupitia tiketi ya chama hicho.
Mbunge wa zamani wa Kisauni, Bw Ali Mbogo, pia anawania kiti hicho cha Gavana Abdulswamad Nassir wa ODM kupitia tiketi ya Jubilee.
Awali, kinara wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Bw Rigathi Gachagua, alikuwa ametangaza kumuunga mkono Bw Ali, bila kujali iwapo atawania kiti hicho kwa tiketi ya DCP au Wiper.
Dkt Matiang’i alisema Jubilee tayari kina watu wanaotaka kuwania nyadhifa mbalimbali Pwani, lakini hakutaja baadhi yao kwa sababu bado wanahudumu serikalini akisema huenda wakaandamwa iwapo watatambuliwa kabla ya kujiuzulu.
“Tuna wagombea wengi ambao wanataka kuwania viti vya kisiasa kupitia chama chetu katika eneo hili. Tuna wagombea watatu katika kila kiti cha kisiasa huku Pwani, kwa hivyo tutafanya uteuzi ili kumpata mgombea bora zaidi,” alisema.
Jubilee pia imekuwa ikiandaa mikutano ya mashinani inapojitayarisha kwa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC). Dkt Matiang’i alichukua uongozi wa chama hicho kutoka kwa Rais mstaafu Bw Kenyatta mwezi uliopita.
Alisema Jubilee imewasilisha kanuni zake za uteuzi kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na inajiandaa kufanya uteuzi wa wagombea kote nchini.
Dkt Matiang’i pia alitetea uamuzi wake wa kuacha kazi katika Benki ya Dunia na kurejea nchini Kenya, akisema vijana wa Kenya, hasa kizazi cha Gen Z, walimtafuta wakitumia mtandao wa kijamii kabla ya kurejea kwake.
“Nilipigiwa simu na vijana wa Gen Z kabla sijarejea hapa kutoka Benki ya Dunia. Jambo hilo lilikuwa kila mahali, kwenye mitandao ya kijamii,” alisema.
Alipuuza madai kwamba kurejea kwake katika siasa kulifadhiliwa na Bw Kenyatta.
“Hapana. Mkitaka kuuliza kuhusu mfadhili, wafadhili wangu ni wananchi wa Kenya,” alisema.
Dkt Matiang’i alijiunga na Benki ya Dunia baada ya kuondoka serikalini 2022 na kurejea Kenya mwaka 2025 na kutangaza azma yake ya kuwania urais. Jubilee imemuidhinisha kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa 2027.
Alisema kampeni yake inaungwa mkono na wakenya wa kawaida, wakiwemo wanaochanga fedha kwa ajili ya shughuli zake.
“Urais unahitaji fedha nyingi, lakini mnajua kuwa azma yangu ya kuwania urais ni tofauti. Niliitwa kuja kuwatumikia Wakenya. Ni wao wanaofadhili kampeni zangu. Wananichangia fedha kwa ajili ya kampeni zangu, huku wengine wakinipatia fedha za mafuta ya gari,” alisema.
Dkt Matiang’i alisema anawania urais kwa sababu anaamini Kenya inahitaji kiongozi mwenye uzoefu katika utumishi wa umma na utaalamu katika kusimamia Idara za serikali.
“Nina uzoefu katika utumishi wa umma baada ya kuhudumu katika wizara mbali mbali. Nimefanya kazi kwa karibu na rais wa zamani na ninaamini mimi ndiye mgombea anayefaa zaidi kuchukua uongozi wa nchi hii,” alisema.
Alisema atakabiliana na ufisadi, ubadhirifu wa rasilimali za umma, ushuru wa juu, ukosefu wa usalama na siasa za kikabila.
Pia alikosoa sera za elimu za utawala wa Kenya Kwanza, hasa mfumo mpya wa ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu, akidai kuwa baadhi ya wanafunzi wameshindwa kuendeleza masomo kutokana na changamoto za ufadhili.
Jubilee yalenga kiti cha ugavana Mombasa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…