TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) inapanga kuongeza zaidi ya vituo 9,000 vya kupigia kura kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027.
Kwa sasa pendekezo la IEBC la kuongeza idadi ya wapigakura katika kila kituo kutoka 700 hadi 1,000 linakabiliwa na upinzani katika Bunge la Kitaifa.
Stakabadhi rasmi ya IEBC iliyowasilishwa bungeni inaonyesha kuwa vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kuongezeka kutoka 46,229 vilivyotumika katika uchaguzi wa 2022 hadi 55,393.
Hii inatokana na lengo la tume kusajili wapigakura wapya milioni 6.3 kabla ya uchaguzi ujao.
Hata hivyo, wabunge wanapinga pendekezo la kuongeza idadi ya wapigakura kwa kila kituo, wakitaka idadi ya sasa ya wapigakura 700 idumishwe.
Pendekezo hilo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa 2024 liliidhinishwa na Seneti mnamo Disemba 2024, lakini limekumbana na upinzani katika Bunge la Kitaifa.
IEBC inakadiria kuhitaji vifaa 59,959 vya kielektroniki vya Kiems kwa shughuli za uchaguzi, vikiwemo vifaa 3,959 vitakavyotengwa kwa mafunzo ya maafisa wa uchaguzi katika maeneobunge.
Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, alisema maeneo ya vituo vipya yataamuliwa baada ya zoezi la usajili wa wapigakura kukamilika.
“Vituo vipya vitaanzishwa katika maeneo ambako vituo vya sasa vya kupigia kura na usajili wa wapigakura vinazidi wapigakura 700,” akasema Bw Ethekon, akiongeza kuwa umbali na haja ya kusongeza vituo karibu na wapigakura pia zitazingatiwa.
Kifungu cha 38A cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza kuwa idadi ya wapigakura katika kila kituo haipaswi kuzidi 700 ili kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa njia huru.
Hata hivyo, Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria ya Bunge la Kitaifa inapinga pendekezo la kuongeza idadi hiyo.
“Mimi lazima nikiri kuwa tuna tatizo kidogo kuhusu kifungu hiki na vifungu vingine. Tutapendekeza marekebisho wakati mswada huu utakapowasilishwa kusomwa kwa mara ya tatu,” akasema Mbunge wa Tharaka George Murugara, ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.
Bw Ethekon alisema tume itahifadhi sajili ya sasa ya wapigakura milioni 22.3 na kuongeza wapya milioni 6.3, na hivyo kufikisha jumla ya milioni 28.63.
Mchakato wa kuhakiki na kuthibitisha sajili hiyo utafanywa miezi sita kabla ya uchaguzi wa 2027.
IEBC sasa inaachana na matumizi ya takwimu za sensa kuweka malengo ya usajili, ikipendelea takwimu kutoka Idara ya Usajili wa Watu na Idara ya Huduma za Uhamiaji kuhusu vitambulisho vya taifa na pasipoti zilizotolewa.
Tume inasema mfumo wa zamani haukuwa sahihi wala rahisi kuthibitishwa, kwa kuwa takwimu za sensa zinajumuisha watu wasiostahili kupiga kura, wakiwemo wasio raia na wakimbizi.
Badala yake, IEBC itatumia mfumo wa idadi ya watu wanaostahili kujiandikisha kama wapigakura, kwa kuzingatia barua zinazohitajika kisheria.
Katiba, chini ya Ibara ya 83, inahitaji raia kuwa na kitambulisho cha taifa au pasipoti halali ya Kenya ili kusajiliwa kama mpigakura.
Ili kufikia lengo lake, tume itaendeleza usajili katika afisi zote 290 za maeneobunge, vituo vya Huduma Center, wadi, taasisi za elimu ya juu na Wakenya wanaoishi ughaibuni.
IEBC inasema mikakati hiyo itasaidia kuweka malengo halisi, kutumia rasilimali kwa ufanisi na kuhakikisha Wakenya wengi zaidi wanapata nafasi ya kujiandikisha kupiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.
IEBC yalenga kuongeza vituo 9,000 vya kupiga kura kuelekea 2027

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…