MFULULIZO wa ajali za helikopta nchini unapaswa kuwaamsha usingizini wenye mamlaka husika. Hatua za dharura zinahitajika ili kuzuia maafa zaidi.
Kila mwaka, takribani ajali tano za helikopta huripotiwa nchini, hali inayozua maswali mazito kuhusu usalama wa usafiri huu wa angani na utekelezaji wa sheria zinazousimamia.
Ajali ya hivi karibuni iliyohusisha Katibu wa Wizara ya Mazingira, Dkt Festus Ng’eno, na abiria wengine wanne inapaswa kuwa onyo la mwisho kwa serikali.
Ingawa waliokuwa ndani ya ndege hiyo walinusurika, rubani alijeruhiwa vibaya huku helikopta hiyo iliyotua katika uwanja wa Kericho Golf Club ikiharibika pakubwa.
Kisa hicho hakifai kutazamwa kama tukio moja pekee. Mwezi Agosti, ajali nyingine ya helikopta iliripotiwa Samburu, miezi michache baada ya Mbunge wa Emurua Dikirr, Yohana Ng’eno, kufariki katika ajali ya helikopta mwezi Februari mwaka huu.
Matukio haya yanadhihirisha umuhimu wa kuchunguza kwa kina sababu za ajali hizo na kuhakikisha hatua za kuzuia kurudiwa kwa makosa zinachukuliwa.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba uchunguzi umekuwa ukifanywa na ripoti kutolewa zikiwa na mapendekezo ya kuimarisha usalama wa usafiri wa angani.
Hata hivyo, ikiwa mapendekezo hayo hayatekelezwi kikamilifu, uchunguzi ukibaki kuwa shughuli ya kuwasahaulisha waathiriwa na Wakenya kwa jumla maafa hayo tu.
Serikali inapaswa kueleza hatua zilizochukuliwa kutokana na ripoti hizo na kwa nini ajali zinaendelea kutokea.
Ripoti kadhaa zimebaini kuwa baadhi ya helikopta zinazotumiwa nchini ni kuukuu na zinahitaji kuondolewa kwenye huduma au kufanyiwa marekebisho makubwa.
Ikiwa hali hii imethibitishwa na ukaguzi wa kitaalamu, hakuna sababu ya kuruhusu ndege hizo kuendelea kubeba abiria huku zikihatarisha maisha yao.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) inapaswa kukagua helikopta zote, kuthibitisha ubora wa matengenezo yake na kusimamisha mara moja zile zisizokidhi viwango vya usalama.
Aidha, uchunguzi unapaswa kuangazia mafunzo na uzoefu wa marubani, ratiba za matengenezo, hali ya hewa na mifumo ya usimamizi wa safari.
Wamiliki na waendeshaji wa helikopta wanaokiuka kanuni wanapaswa kuwajibishwa bila upendeleo. Matokeo ya uchunguzi na utekelezaji wa mapendekezo yake pia yawekwe wazi kwa umma, bila kuathiri taratibu halali za uchunguzi.
Serikali haipaswi kusubiri ajali nyingine imeze maisha ya viongozi au raia wasio na hatia ndipo ichukue hatua.
Ni wakati mwafaka wa kutekeleza ripoti hizo kwa dhati.
Hatua za sasa zitaamua ikiwa usafiri wa helikopta nchini utakuwa salama au utaendelea kuwa chanzo cha hofu na majonzi
TAHARIRI: Ajali hizi za helikopta zimezidi sasa, serikali ichukue hatua hara

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…