MITANDAO ya kijamii imefurika jumbe za kutatanisha zinazohusisha wanawake “wakiwaanika” wanawake wenzao kwa wanachoita ‘kuwaibia” wanaume wao.
Kila uchao, ni nadra kukosa kukumbana na picha ya mwanamke aliyechapishwa na mwanamke mwenzake akimmiminia cheche za matusi yasiyoweza kutamkika.
Sehemu kubwa ya visa hivi vinahusisha wanawake waliopevuka kiumri wenye watoto kadhaa wanaowaanika wenzo wakiwashutumu kwa kusababisha waume zao kuwatekeleza watoto waliozaa nao.
Katika juhudi za kulipiza kisasi na kuwafedhehesha wanawake wanaochumbiana na waume zao, baadhi ya wanawake husika hata huambatisha madai kuwa washindani wao wanaugua maradhi ya zinaa wakiwatahadharisha wengine wajiepushe nao.
Ajabu ni kwamba, mwanamme ambaye ni mhusika mkuu anayezozaniwa katu hachapishwi wala jina lake kutajwa popote.
Katika kisa cha majuzi, mwanamke ambaye ni mama wa watoto saba amemwanika mwanamke anayemtaja kuwa rafikiye wa miaka mingi kwa ‘kuwaibia’ watoto wake baba yao.
Katika juhudi bayana za kumwaibisha mshindani wake, anachapisha picha yake na kutaja umri wake kuwa 55 japo anaonekana mchanga.
Baadhi ya wanawake wanampa moyo wakimweleza alivyo mrembo kuliko rafikiye aliyegeuka adui huku wakiwalaani marafiki wanawake!
Wengine wanakanusha kuwa mwanamme mtu mzima na akili zake timamu anaweza kuibiwa wakimtaka achapishe pia picha ya mwanamme husika wakihoji alifanya hivyo kwa hiari.
Matukio haya yanadhihirisha uhalisia wa kutamausha kuhusu wanawake wanavyohiari kupigana, kuchukiana na kulaumiana badala ya badala ya kukabili mhusika mkuu mwanamme anayesababisha masaibu yao.
Haihitaji mtaalam au mshauri nasaha kukueleza kuwa mwanamme mwenye akili razini anachagua kwa hiari ama kuchepuka au kuwa mwaminifu kwa mkewe na kutunza watoto waliojaaliwa pamoja.
Wanandoa waliofunga pingu za maisha wana mkataba kati yao na endapo yeyote kati yao ataenda kinyume ahadi zao basi ndiye anayepaswa kulaumiwa wala sio mwanamke au mwanamke anayechepuka nao ambao hawafahamu ndewe wala sikio kuhusu ahadi au pandashuka walizopitia.
Ni kinaya kisichoelezeka na aibu kwa wanawake katika karne hii kuumbuana na kuwalaani wanawake wenzao huku wakimwacha mwanamme aliyeamua mwenyewe kuvunja mkataba wa ndoa au mahusiano nao kustarehe wakimsawiri kama mhasiriwa wa kuhadaiwa, kupotoshwa na kuibiwa na mwanamke mwenzao.
Mwanamme ‘haibiwi’ na mwanamke mwingine, huchagua kwa hiari kuchepuka

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…