MTANGAZAJI wa zamani wa habari kwenye runinga, Esther Arunga, ameondoa rasmi jina la ukoo la Quincy Timberlake, mwanamume ambaye wakati mmoja alimtangaza kwa fahari kuwa mumewe.
Miaka 16 baada ya kutumia jina la “Timberlake” wakati wa sakata iliyozua mjadala mkubwa nchini Kenya, sasa amerejelea jina alilokulia.
Katika notisi iliyochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali mnamo Oktoba 9, mawakili wake walisema mteja wao, Esther Adongo Arunga, aliyekuwa akijulikana kama Esther Adongo Timberlake, ameachana rasmi na matumizi ya jina hilo la zamani.
Waliomba watu wote wamwite Esther Adongo Arunga pekee.
Hatua hiyo inafungua ukurasa mwingine katika maisha ya Esther na Quincy, ambao wamehusishwa na kesi za mahakamani katika mabara mawili.
Mnamo Machi 2010, Esther alikuwa ametangaza jijini Nairobi kwamba alikuwa amebadilisha jina lake baada ya kufunga ndoa na Quincy.
Kabla ya sakata hiyo, Esther alikuwa miongoni mwa watangazaji waliotambulika sana nchini. Alisoma Shule ya Upili ya Kenya High, akafanya kazi Capital FM na KTN, na kushinda tuzo ya Chaguo la Teeniez ya 2008 kama mtangazaji bora miongoni mwa vijana. Alikubaliwa kuwa wakili mnamo 2009.
Maisha yake yalibadilika mnamo 2009 alipojiunga na kanisa la Finger of God, lililoanzishwa na mwanamuziki Joseph Hellon. Februari 2010, watatu hao walitangaza kuunda chama cha PlaCenta, siku ambayo Esther alijiuzulu KTN.
Baadaye, polisi walivamia nyumba iliyohusishwa na kanisa hilo jijini Nairobi.
Esther na Quincy walihamia Australia kutafuta hifadhi ambapoJuni 18, 2014, mwanao wa miaka mitatu, Sinclair, alifariki. Esther alisema mtoto alikuwa ameanguka kwenye ngazi, lakini uchunguzi wa maiti ulionyesha alikufa kutokana na majeraha makubwa yasiyolingana na kuanguka.
Mnamo 2019, Esther alikiri kosa la kumsaidia mkosaji na kuhukumiwa kifungo cha miezi 10, lakini akaachiliwa kwa masharti kisha Septemba 2023, Quincy alikiri kosa la kuua bila kukusudia na akahukumiwa miaka 11 gerezani
Hata hivyo, muda aliokuwa amekaa rumande kabla ya hukumu ulihesabiwa, hivyo angeweza kukaa gerezani kwa muda usiozidi miaka miwili zaidi.
Notisi ya hivi karibuni inaonyesha anwani ya Esther kuwa Nairobi, hali inayozua uwezekano kuwa amerejea nchini.
Mtangazaji wa zamani Esther Arunga ataliki jina la aliyekuwa mumewe

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…