MWANAFUNZI wa Mwaka wa Tatu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Nairobi ameamrishwa na mahakama kufidia dereva wa Nabii David Owuor kitita cha Sh7.5 milioni baada ya kupatikana na hatia ya kumtusi kupitia ukurasa wake wa Facebook. Hakimu mkuu wa Eldoret Dennis Mikoyan alimpata na hatia Kevin Ndung’u ya kukiuka sheria za uhalifu wa mtandao na dhuluma za mtandao ya mwaka wa 2018. Mahakama iliamuru Benard Kagia ambaye ni mmoja wa madereva wa Nabii Owour wa kanisa la Repentance and Holiness kufidiwa pesa hizo kutokana na matusi kutoka kwa Bw Ndung’u, mtumiaji wa mitandao ya kijamii miaka mitatu iliyopita. Sehemu ya jumbe hizo ilimtaja mlalamishi kama mwanaume ambaye hakuwa na uwezo wa kumudu matakwa ya familia yake, Vile vile mahakama iliambiwa kuwa Ndung’u alimtaja Kagia kama asiye na maadili, madai ambayo yalimfanya mkewe kumtema. Akitoa hukumu hakimu alibainaisha kuwa matamshi hayo yalikuwa ya kudhalilisha na kudunisha mlalamishi. “Ni bayana kuwa mlalamishi anastahili fidia kutokana na madhara ya matusi husika hivyo basi mshtakiwa hana budi kulipa sh7, 512, 700 kama fidia,” mahakama iliamuru. Punde baada ya uamuzi huo kulitokea sarakasi kortini pale mshtakiwa alilamika kuwa pesa hizo ni nyingi na hangeweza kuzilipa huku akitaka muda wa siku 30 kushauriana na wazazi wake kubaini uwezo wa kuzilipa.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinatoa elimu ya uwekezaji kwa watu mbalimbali wakiwamo mabalozi wanaokwenda kuwakilisha Tanzania nje ya nchi. Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani TIC, Felix John amesema hayo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika kongamano kuhusu nafasi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika kufanikisha Dira…
MOROGORO: KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa, Riziki Shemdoe ameutaka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA),kuandaa wahitimu watakaoweza kujiajiri na kuajiri wengine badala ya kusubiria kuajiriwa. Profesa Shemdoe ametoa kauli hiyo mjini Morogoro wakati akifungua kikao kilichokutanisha wadau wa kujadili rasimu ya mitaala mitano inayohuishwa na mitaala 12 mipya…
MKURUGENZI wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema ingawa deni la taifa linaongezeka, uchumi wa nchi ni himilivu. Kafulila amesema wastani wa deni la serikali kwenye uchumi ni takribani asilimia 47. Kafulila ameyasema hayo katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam…
HUENDA walimu wa shule za upili wakaitisha mgomo muhula huu endapo Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) haitaandaa majadiliano kuhusu makubaliano ya nyongeza ya mishahara maarufu kama CBA kabla ya kusomwa kwa bajeti ya kitaifa mwezi ujao. Walimu wanachama wa Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET) wamesema watalemaza shughuli za masomo iwapo TSC haitaongea nao ndani ya siku saba zijazo. Mwenyekiti wa Kuppet Omboko Milemba na Naibu Katibu Mkuu Moses Nthurima wamesema ni lazima TSC iwaite kujadili nyongeza ya mshahara. “Baada ya kila miaka minne, walimu huwa na mazungumzo na mwajiri wao na kutengeneza makubaliano mapya ya nyongeza ya mishahara na masuala mengine tata yanayowaathiri. Mwaka jana KUPPET iliwasilisha matakwa yao kwa mwaajiri, miezi ssaba imeisha bila mkutano kufanyika,” akasema Bw Milemba. Mbunge huyo wa Emuhaya alisema mkutano huo unapaswa kufanyika kabla ya kupitishwa kwa bajeti mpya. “Sababu nyongeza ya misharaha inafaa kuwekwa kwenye bajeti inayotarajiwa kusomwa mwezi ujao. Bunge la Kitaifa limeshaanza kutengeneza bajeti na hii ina maana ya kwamba walimu watakosa nyongeza ya mishahara kuwekwa kwenye bajeti itakayosomwa,” akaongoza. Waziri wa Fedha Bw John Mbadi alisema huenda bajeti hiyo ikasomwa Juni 12. Bw Nthurima alisema TSC iliwaahidi kwamba itawaita kwenye mkutano kujadili makubaliano ya nyongeza ya mshahara mwaka wa kifedha 2025/2026. Wakiongea kwenye mkutano wa Kuppet huko Mtwapa, Kaunti ya Kilifi, Bw Nthurima alisema makubaliano ya nyongeza ya mishahara yanatarajiwa kufika kikomo mnamo Juni. Wakuu wa Kuppet wamekuwa wakikutana Kilifi kwa siku mbili kujadili masuala ya muungano wao. “TSC inajikokota sana, tuna wasiwasi kama muungano huenda bajeti ikasomwa bila ya kutilia maanani makubaliano yetu ya nyongeza ya mishahara. Tunatoa makataa ya siku saba kuitwa kwenye meza kujadili suala hili,” akasema Bw Nthurima. Chama cha Walimu Nchini (KNUT) nacho kilikuwa kinatarajia kutia saini makubaliano ya nyongeza ya mishahara na TSC kabla ya kustaafu kwa aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji Nancy Macharia ambaye nafasi yake ishatangazwa. Akiwaaga walimu wakuu wa shule za upili za umma mwezi uliopita, Bi Macharia aliwaambia mazungumzo kuhusu CBA hasa nyongeza ya mshahara yameanza. Bi Macharia alisema wameweka mikakati kabambe kukabiliana na migomo ya mara kwa mara kwenye sekta ya elimu. Matakwa ya Knut ni kuongezwa marupurupu, mishahara, uajiri wa walimu kukabiliana na uhaba mkubwa uliopo, walimu kuruhusiwa kuchukua likizo ya siku 90 kugombea viti vya kisiasa miongoni mwa masuala mengine.
HASIRA zimezidi miongoni mwa walimu wa shule za umma sio tu kufuatia kucheleweshwa kwa mgao wa muhula wa pili wa mwaka 2025, bali kiasi cha pesa ambazo shule zao zilitumiwa. Walimu wakuu wengi sasa wanaonya kuwa shughuli za masomo na za ziada zitalemazwa kabisa iwapo hali haitarekebishwa. Baadhi ya wakuu wa shule walishangazwa na kiasi kidogo cha fedha walizopokea, wengine wakisema ni cha kuchekesha.Kwa mfano, baadhi ya shule zilipokea kati ya Sh87 hadi Sh4,000, kiasi kilichoshangaza walimu na wazazi wa shule hizo. “Nilipokea taarifa ya benki kwamba Sh87 pekee ndizo zilitumwa kwenye akaunti ya shule. Nilipofuatilia akaunti, nilibaini ni kweli. Hakutakuwa na shughuli shuleni katika muhula wa pili. Tumeonywa tusiombe msaada kutoka kwa wazazi. Naheshimu hilo. Lakini lazima tuseme. Hatupaswi kufa kimya tukijaribu kusimamia shule bila pesa,” alilalamika mkuu mmoja wa shule ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu ya hofu ya kuadhibiwa. Mwalimu mwingine alitaka Bunge kumhoji Waziri wa Elimu kueleza kwa nini kiasi kidogo cha fedha kilitolewa kwa shule.“Bunge lijue. Wizara itolewe jasho. Wanafunzi wetu wana haki. Wazazi wana haki. Sisi pia tuna haki. Bajeti si maneno, ni pesa. Tutafunza bila chochote?” alisema mwalimu huyo. Kilio hicho kilirudiwa na shule nyingine ndogo ya umma inayoendelea kuangamia kwa kukosa miundombinu, walimu wa kutosha, na fedha muhimu hali inayoathiri ubora wa elimu kwa wanafunzi. Bw Mark Onyango, mkuu wa shule ya msingi na sekondari ya Ng’op Ngeso katika eneobunge la Seme, Kisumu, alisema shule hiyo inapambana kuendelea kuwepo huku changamoto zikizidi. Shule hiyo iliyoanzishwa miaka ya 1980, kwa sasa ina wanafunzi 125 katika shule ya msingi na 33 wa sekondari msingi. Tangu alipoteuliwa Juni 2022, Bw Onyango amekuwa akikabiliana na majengo duni, upungufu wa walimu na ukosefu mkubwa wa vifaa vya kufunza. “Madarasa yetu mengi ni mabovu, kuna mashimo sakafuni na madirisha yaliyovunjika yenye nyaya hatari. Hatuna madarasa ya kutosha kwa JSS, na wanafunzi wa darasa la saba hawana sehemu nzuri ya kusomea,” alisema. Shule ina walimu sita tu wa shule ya msingi na mmoja wa JSS licha ya kuwa na madarasa mawili, la saba na la nane. Hali hiyo imesababisha walimu wa shule ya msingi kufundisha pia JSS, hali inayowalemaza na kuathiri ubora wa elimu. Licha ya changamoto hizi, fedha zilizotumiwa shule zimeshangaza zaidi. “Tulipokea Sh4,155 pekee kwenye akaunti ya shule. Sasa tunatarajiwa kutumia pesa hizo kwa shughuli zote ikiwemo kuimarisha miundomisingi. Sijui kwa nini Wizara inatutesa namna hii,” alisema. Mgao wa shule hugawanywa katika sehemu mbili: ada za masomo na matumizi ya kawaida ya shule. “Akaunti ya matumizi ya kawaida huendesha mishahara ya wafanyakazi wa mkataba, ukarabati, kulipia umeme, shughuli za ziada, usafiri wa ndani, miongoni mwa mahitaji mengine. Hatujui tuanzie wapi,” aliongeza.Katika muhula wa pili mwaka 2024, shule ilipokea Sh14,808 kwa matumizi ya kawaida na Sh11,520 kwa ada ya masomo ya shule ya msingi. Kwa upande wa JSS, shule ilipokea Sh302,108 kwa matumizi ya kawaida na Sh24,449 kwa ada ya masomo muhula wa pili wa 2024. Kulingana na Bw Onyango, bajeti ya mwaka huu inaonyesha tofauti kubwa kati ya mahitaji halisi na fedha walizopokea. Kwa mfano, shule inahitaji Sh1,048,543 kwa mwaka, lakini katika muhula wa kwanza ilipokea Sh147,340 pekee na kulazimika kukopa au kutegemea wahisani. “Tulilazimika kuajiri mwalimu mmoja wa JSS kwa fedha zetu, tukimlipa Sh10,000 kwa mwezi. Mlinzi wa usiku analipwa Sh6,000. Bajeti yetu inakuwa ngumu mno,” alisema. Mnamo Mei 20 2025 Wizara ya Elimu ilitoa Sh22.03 bilioni kama mgao wa muhula wa pili baada ya kuchelewa kwa wiki tatu. Waziri wa Elimu Julius Ogamba alisema kuwa fedha hizo zilitolewa kusaidia shughuli za masomo na kupunguza matatizo ya kifedha yanayokumba shule nyingi tangu mwanzo wa muhula. Hata hivyo, hakufafanua kiwango kilichotengwa kwa kila mwanafunzi au kama kiasi hicho kinajumuisha fedha ambazo hazikutolewa katika muhula wa kwanza. Pia hakuelezwa wazi iwapo fedha hizo ni sehemu ya asilimia 30 ya mgao inayopaswa kutolewa kwa muhula wa pili.
MWANASAIKOLOJIA ameelezea kwa kina madhila ya kiakili waliyopitia watoto waliokolewa kutoka kwa mauaji ya Shakahola miaka mitatu tangu waokolewe kutoka kwenye dhehebu hatari lililoongozwa na mhubiri tata, Paul Nthenge Mackenzie. Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkuu Nelly Chepchirchir katika Mahakama ya Watoto ya Tononoka, Dkt Florence Mueni, alieleza hali ya kusikitisha ya msongo wa mawazo waliobeba watoto hao tangu waokolewe. Dkt Mueni alisema watoto hao walionesha dalili kali za kiwewe zilizosababishwa na njaa ya muda mrefu, kutengwa, kufundishwa imani potovu, na kupoteza jamaa zao wa karibu. “Wanaota ndoto za kutisha mara kwa mara na mawazo ya kushuhudia watu wakifa. Walieleza kwa huzuni wanapokumbuka masaibu hayo, ikiwemo kufungwa kwenye mti,” alisema Dkt Mueni akimrejelea baadhi ya wanusurua. Dkt Mueni alikuwa miongoni mwa timu ya wataalamu wa afya ya akili waliojitolea kuwasaidia watoto 13 waliokolewa kutoka msitu wa Shakahola baada ya kupitia mateso makubwa chini ya uongozi wa Mackenzie. Alisema watoto walieleza kuwa walizuiwa kuomboleza vifo vya wapendwa wao waliokufa kwa njaa. Wengi walipatwa na huzuni nzito na msongo wa mawazo wa muda mrefu. Mvulana mmoja alishuhudia kaka yake akifariki mbele yake—tukio lililoacha makovu ya ndani yasiyofutika. “Baadhi ya watoto walionesha hofu, hasira, aibu, na kupoteza hamu ya vitu walivyovipenda hapo awali,” alisema mtaalamu huyo akiongozwa na Kiongozi wa mashtaka Jami Yamina, Betty Rubia, miongoni mwa wengine. Aliongeza kuwa njaa na kutengwa kwa muda mrefu kulisababisha mwitikio wa ‘kuporomoka’—hali ambapo mwili unazima unapohisi hatari kubwa. Watoto wengi mwanzoni walikuwa waoga kupindukia, hasa jina la Mackenzie lilipotajwa. “Hofu yao ilikuwa kubwa sana, jambo lililodhihirisha athari za kina alizowaachia. Hata hivyo, baada ya miezi kadhaa ya tiba na msaada wa kisaikolojia, wengi wao walianza kupona na kurejea shule na hata hali ya kawaida,” alisema. Mkuu wa Upelelezi Kigen Sawe na Sajenti Livingstone Lihanda kutoka Kitengo cha Uchunguzi wa Kisayansi cha DCI waliwasilisha picha na video za kutisha kutoka eneo la tukio, ikiwemo vibanda vya kufungiwa, mali zilizoachwa, na makazi ya muda. Afisa Mkuu wa Watoto, Sebastian Muli Muteti, alieleza jinsi walivyowaokoa watoto waliokuwa dhaifu, wameshushwa lishe, na wenye majeraha. Timu yake ilipata watoto wanne wakiwa ndani ya msitu wakiwa na mavazi machafu na alama za kupigwa. “Watoto hao walieleza mateso waliyopata kutoka kwa walinzi wa Mackenzie waliokuwa wakiwapiga na kuwaweka kifungoni,” alisema. Mahakama pia ilisikia ushahidi kutoka kwa wakuu wa shule wawili waliothibitisha kutoweka kwa wanafunzi waliokuwa wamepelekwa Shakahola. Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mtopanga, Bw Omari Omari, alisema msichana mmoja alitoweka mwaka wa 2018. Bw Mathew Maroko Samoita kutoka shule ya kibinafsi Kisauni, alisema mwanafunzi wa Darasa la Tatu aliondolewa na wazazi wake ambao sasa wanakabiliwa na mashtaka. Watoto hao baadaye walitoa ushahidi dhidi ya walezi wao, wakidai waliteswa na kunyimwa haki ya elimu huku wakilazimishwa kufuata mafundisho ya dhehebu hilo. Paul Mackenzie na wenzake wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo ukatili kwa watoto, mateso ya kisaikolojia, na kuwanyima watoto haki zao za masongo ya msingi.
KUANZIA mwaka ujao, wazazi watalazimika kulipia ada za mitihani kwa watoto wao, hatua inayomaliza rasmi msamaha wa ada uliokuwa ukifurahiwa na watahiniwa tangu ulipoanzishwa miaka kumi iliyopita. Serikali itagharamia ada za mitihani kwa watahiniwa watakaotambuliwa kuwa wahitaji kupitia mpango wa utathamini wa hali ya maisha unaofanana na ule tata wa ufadhili wa elimu ya juu ulioanzishwa mwaka 2023. Iwapo utatekelezwa, wazazi watalazimika kulipia gharama za mitihani ya Kenya Primary School Education Assessment (KPSEA), Kenya Junior School Education Assessment (KJSEA) na Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE). Mitihani hii yote inasimamiwa na Baraza la Mitihani la Kenya (KNEC). Waziri wa Hazina ya Taifa na Mipango ya Kiuchumi John Mbadi aliambia Taifa Leo katika mahojiano maalum kuwa serikali itatumia mfumo wa ruzuku ya malengo ambao utawanufaisha tu wanafunzi ambao hawana uwezo wa kugharamia mitihani hiyo. Hata hivyo, hakufafanua ni njia gani wanafunzi hao watatambuliwa. “Wizara ya Elimu lazima ije na vigezo vya kuwatambua wanaoweza kulipa ada za mitihani. Kwa mfano, kama mtoto wako anasoma katika shule ya kibinafsi ambapo unalipa Sh300,000 kwa muhula au Sh1 milioni kwa mwaka, kwa kweli huwezi kulipa ada ya mtihani ya Sh5,000? Kwa nini ulazimishe walipa kodi—ambao baadhi yao hawana hata uwezo wa kujikimu—kugharamia mtihani wa mtoto wako?” alisema Bw Mbadi. Msamaha wa ada ya mitihani ulianzishwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta mwaka 2015 kwa wanafunzi wa shule za umma, na mwaka 2017 ukafaidi shule za kibinafsi. Msamaha huo ulilenga kuhakikisha wanafunzi wote wanafanya mitihani ya kitaifa na kuendeleza sera ya asilimia 100 ya uhamisho kutoka daraja moja hadi jingine. Serikali ilitenga Sh4 bilioni kugharimia mitihani hiyo mwanzoni, lakini katika miaka miwili iliyopita imekuwa ikitenga Sh5 bilioni kila mwaka. Wakati huo, watahiniwa wa mtihani wa KCPE waliokuwa wakilipa Sh800, huku wale wa KCSE wakilipa ada ya msingi ya Sh2,700 na Sh400 kwa kila somo. Mpango huu mpya ni mabadiliko makubwa ya sera kutoka mfumo wa sasa wa msamaha wa ada kwa wote, unaowezesha wanafunzi wote katika shule za umma na kibinafsi kufanya mitihani bila gharama yoyote. Bw Mbadi alisema uamuzi huo umechukuliwa kwa misingi ya uwajibikaji wa kifedha na usawa katika matumizi ya pesa za walipa kodi. Alikanusha ripoti kuwa Hazina ya Taifa haijatenga fedha kwa mitihani mwaka huu. Waziri alieleza kuwa bajeti ya mitihani ya kitaifa kwa mwaka huu ipo na Baraza la Mawaziri tayari limeidhinisha. “Kutakuwa na utaratibu wa kutoa fedha hizo. Kwa hiyo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Wazazi wasikate tamaa,” alisema Bw Mbadi. Aliongeza kuwa kuanzia mwaka ujao, wanafunzi wote hawatakuwa na uhakika wa kupata msaada wa serikali. Katika miaka ya hivi karibuni, KNEC imekuwa ikikumbwa na changamoto za kifedha kulipa maafisa wanaohusishwa na mitihani kutokana na ongezeko la idadi ya watahiniwa tangu msamaha huo uanze. “Lazima tuchunguze upya gharama hii na tujiulize, kwa nini tuwalipie ada ya mtihani wanafunzi wote, hata wale wa shule za kibinafsi? Tunapaswa kusaidia tu wale wasioweza kugharamia,” alisema Bw Mbadi. Tangu mwaka 2015, serikali imekuwa ikigharamia mitihani ya KCPE, KCSE, na hivi majuzi tathmini mbalimbali chini ya mfumo mpya wa elimu (CBC), jambo lililosaidia kupunguza mzigo wa kifedha kwa familia wakati gharama ya maisha inaendelea kupanda.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendesha bonanza kwa wanafunzi wa baadhi ya shule za sekondari mkoani Mtwara kwa lengo la kuendeleza uhusiano na ujirani mwema. Akizungumza wakati wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha shirika hilo Marie Msellem amesema TPDC lengo ni…
KUNA mapinduzi ya kimya yanayoendelea miongoni mwa wanawake wa Kenya huku wakichagua wanyama kipenzi badala ya kupata watoto. Hii ni kinyume kabisa na tamaduni za jadi ambazo zilimchukulia mwanamke kuwa hajakamilika ikiwa hana mtoto. Siku hizi, wanawake wengi wanafanya maamuzi ya makusudi ya kutokuwa mama, si kwa sababu hawawezi kupata watoto, bali kwa sababu hawataki. Badala ya watoto, wanakumbatia paka na mbwa. Badala ya chupa za watoto, nguo na vinyago, wanawekeza katika chakula cha wanyama, vifaa vya kuondoa manyoya, na mabakuli ya kulishia. Wanyama wao wanapendwa, wanatunzwa, na kwa njia nyingi, wanachukuliwa kama watoto. Jane Njeri, mwenye umri wa miaka 43, ni mhadhiri wa chuo kikuu na mama wa paka tisa. Alipokuwa mdogo, alitarajia kuolewa akiwa na umri wa miaka 25 na kupata watoto watatu au wanne. Lakini maisha yalichukua mkondo tofauti. “Ni uamuzi niliofanya kwa muda. Baada ya masomo yangu ya chuo kikuu, nilihusiana na watu wachache lakini sikufanikiwa. Nilirudi kusoma nikapata Shahada ya Uzamili, kisha Shahada ya Uzamivu. Mahusiano hayakuwa kipaumbele tena,” anasema. Akiwa mhadhiri, anashuhudia changamoto nyingi wazazi wanazopitia kulea watoto. Anasema watoto wanahitaji nguvu nyingi na mara nyingine huleta hasira kuliko furaha. “Nimeamua kuwa sawa na maisha yangu bila watoto, na hali yangu ya maisha ni nzuri,” anasema. Mama yake hapendezwi na uamuzi wake na mara nyingi humwambia, “Laiti ungelipenda mama yako kama unavyowapenda paka wako.” Jane hutumia takribani Sh10,000 kwa mwezi kwa paka wake, na hadi Sh30,000 ikijumuisha gharama za matibabu. Eva Mutua, wakili, ana mbwa watatu: Max, Joe, na Ruby.Mbwa hawa walimsaidia kupona baada ya kufiwa na mama yake. “Walikuja maishani mwangu polepole na kunisaidia kuponya huzuni yangu,” anasema. Eva alipanga maisha yake mapema – alitarajia kuwa ameolewa na kupata watoto kabla ya kufikisha miaka 32. Lakini baada ya kusoma India na kuishi Uingereza, mahusiano yake hayakufaulu. “Nilijikuta sina mtu sahihi wa maisha na nilifanya amani na hali hiyo,” asema. Tofauti na Jane, mama yake Eva alimwelewa na hakumpa presha. “Watu walimwambia anilazimishe kupata mtoto, lakini alisema, ‘Nitabaki kumlea mimi huyo mtoto.’” Eva huwachukulia mbwa wake kama watoto wake wa kweli. “Ninawavalisha na ninawapeleka kuoshwa.” Aliomba Mungu kabla ya kuamua kutopata watoto. “Niliomba Mungu anipe mtu wa maisha ambaye naweza kupata naye watoto. Hilo halikutokea na nikaomba nguvu za kuikubali hali hiyo kwa amani.” Stephen Karimi, mwanasaikolojia, anasema kuchagua wanyama badala ya watoto kunasababishwa na sababu za kihisia, kiuchumi na hata kibaolojia. “Hauwezi kuchukua nafasi ya kipekee ambayo mtoto huleta, lakini unaweza kupata uhusiano wa karibu kupitia wanyama vipenzi” asema. Anabainisha kuwa tafiti zinaonyesha kuwa wanyama hupunguza upweke, na hisia hasi maishani. “Wanyama ni chanzo cha msaada wa kihisia na walinzi wa upendo.” Hata hivyo, anaonya kwamba wanyama hawawezi kuchukua kabisa nafasi ya mtoto wa binadamu.
DAR ES SALAAM: SERIKALI inakusudia kujizatiti kuongeza mitaala zaidi ya elimu ya afya ili kuzalisha wataalamu wa afya, lakini pia kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kufanya tafiti na kutoa huduma za afya. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo leo Mei 23, katika uzinduzi wa Awamu ya Pili ya…
MOROGORO: CHUO Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepata miradi tisa ya utafiti katika nyanja mbalimbali yenye kugharimu zaidi ya Sh bilioni 3.8 kwa kipindi cha Oktoba 2024/2025. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema hayo mbele ya mkuu wa chuo hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati wa mahafali…
DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kuanza kutoa mafunzo maalum ya kitaalamu kwa wakufunzi wa mazoezi ya viungo (gym instructors) na wasimamizi wa kumbi za mazoezi (fitness managers),ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja wanaopelekwa kufanya mazoezi kwa sababu za kitabibu. IIrene Mzokolo akifafanua namna vifaa vya…
SERIKALI kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) inatarajia kutumia zaidi ya Shs bilioni 3 kutekeleza ujenzi wa jengo jipya la Taaluma katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU). Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi katika Chuo…
BARAZA la Kitaifa la Mtihani Kenya (Knec) mwezi ujao litatoa mtihani wa ustadi kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na mtaala mpya wa Umilisi na Utendaji (CBC) ili kupima uwezo wao wa kufanya Mtihani wa Kenya Junior Secondary Education Assessement (KJSEA). Afisa mkuu mtendaji wa Knec, Dkt David Njengere alisema mtihani huo utafanywa mtandaoni. Mtihani huo unalenga watoto waliotoka nchi za kigeni au wale ambao wanasoma chini ya mifumo mingine ya elimu. 'Hii inalenga watoto waliotoka nchi za kigeni na ambao wanataka kufanya mtalaa wa CBC. Tofauti na kasumba kwamba elimu inayozingatia ujuzi na uwezo sio maarufu, tuna watoto wengi sana kutoka nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Uingereza, Australia, Canada, Amerika wanaotaka kujiunga na mfumo huo wa CBC,' alisema Dkt Njengere. Kwa mujibu wa ratiba na maelekezo ya mtihani wa mchujo wa 2025, watahiniwa watapewa somo la hisabati, Kiingereza, sayansi jumuishi na Kiswahili. Watahiniwa wote waliolengwa waliosajiliwa lazima waripoti katika vituo vyao vilivyoteuliwa mnamo Juni 9, 2025, kwa maelekezo ya majaribio ya mtandaoni kabla ya mtihani halisi. Dkt Njengere alisema watahiniwa hao watapewa matokeo na hati za matokeo mara baada ya kumaliza mtihani. Hizi zitatiwa saini ipasavyo na wakurugenzi wa elimu wa kaunti ndogo (SCDE) kwa madhumuni ya usajili wa KJSEA. Majaribio yatawekewa muda na hakuna muda wa ziada utakaoruhusiwa. Muda anaochukua mtahiniwa kusoma maswali utakuwa sehemu ya muda uliopangwa isipokuwa pale ambapo maelekezo maalum yanaonyesha vinginevyo.
MTWARA: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mndimba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wakawe waadilifu katika mapambano dhidi ya rushwa. Kiongozi huyo ametoa ushauri huo leo Mei 22, 2025 wakati Mwenge wa Uhuru ulipozindua bweni la wanafunzi la shule hiyo…
MWANAFUNZI ameshtaki Shule ya St Bakhita, Nairobi, akidai kuwa taasisi hiyo ilishindwa kumlinda baada ya kudaiwa kuadhibiwa na mwalimu mnamo Machi, jambo lililosababisha jeraha kwenye sikio lake. Kupitia kwa baba yake, mwanafunzi huyo ambaye jina lake limefichwa kwa ulinzi wake, alisema alifinywa na mwalimu wake wa Kiswahili Machi 19, tukio ambalo limemwacha na mshtuko na woga. Baba huyo ameshtaki shule hiyo, bodi ya wakurugenzi, mwalimu mkuu James Ogweno pamoja na Bw Fredrick Manyasa, mwalimu anayedaiwa kumjeruhi mwanafunzi huyo. Bw G.O. alisema katika stakabadhi za mahakama kuwa “shambulio hilo lilikuwa la makusudi na lililenga kumdhuru mtoto huyo.” “Mlalamishi anadai kuwa mtoto huyo anaonekana wazi kuwa amepatwa na mshtuko, anaogopa, amejitenga na hulia bila kukoma kila mara anaposikia jambo lolote linalohusiana na shule,” alisema Bw G.O. Kesi hiyo itatajwa Juni 17 mahakama itoe mwelekeo. G.O. alisema shule hiyo ilishindwa kutekeleza wajibu wake wa kumlinda mtoto huyo dhidi ya mateso au adhabu ya kinyama na udhalilishaji, pamoja na kuhakikisha mazingira mazuri kwa mtoto huyo kama mwanafunzi. Alisema tukio hilo limemfanya mtoto huyo kuomba ahamishwe na kutafuta usaidizi wa ushauri nasaha. “Mtoto anahudhuria vikao vya ushauri nasaha ili kusaidia hali yake ya kihisia,” alisema baba huyo. Mlalamishi anadai kuwa haki na uhuru wa mtoto huyo zilikiukwa, ikiwemo uhuru dhidi ya mateso, adhabu ya kikatili, na udhalilishaji. Anadai fidia ya jumla na maalum, ikiwa ni pamoja na Sh18,618 zilizotumika kwa matibabu na gharama nyinginezo. “Tunaomba mahakama itoe tamko kuwa vitendo dhidi ya mtoto huyo vilikuwa kinyume cha Katiba, haramu, vya kudhalilisha na vya kikatili, na hivyo basi washitakiwa wawajibike,” alisema G.O. Anataka pia agizo kutoka kwa mahakama kuamuru shule hiyo kulipia gharama za matibabu ya sasa na ya baadaye hadi mtoto huyo apone kabisa katika hospitali atakayochagua. Mzazi huyo alieleza kuwa shule hiyo ilijitolea kumpatia mtoto huyo huduma za ushauri nasaha na msaada wa kihisia bila malipo yoyote.
DAR ES SALAAM: WANANCHI zaidi ya 120 wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika kambi ya siku mbili inayoendea kituo cha magonjwa ya moyo Kampasi ya Mloganzila, Dar es Salaam. Kambi hiyo imeandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS ). Akizungumza katika eneo hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Cha…
WAKULIMA wa uyoga wangali wanatumia mbinu asilia kukuza zao hilo, ambalo ni chanzo mbadala cha virutubisho vya protini. Uyoga ni jamii ya kuvu (fungi) inayokua ardhini, kwenye miti, au sehemu zenye unyevunyevu, na inajulikana kwa muundo wa kipekee ulio kama kofia juu ya kikonyo. Kuboresha ukuzaji, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kimezindua mfumo mpya kusaidia kuongeza mazao na kutunza mazingira. Chini ya teknolojia, Smart Mushroom Farming, wakulima sasa wanaweza kuzalisha kuvu kwa njia ya kiotomatiki – mtambo unaotumika kunyunyizia uyoga maji, kupulizia dawa na hata kudhibiti kiwango cha joto, unyevuunyevu na vigezo vingine muhimu. [caption id="attachment_172538" align="aligncenter" width="300"] Dkt Lawrence Nderu mwasisi wa JHUB Africa, JKUAT akionyesha jinsi mtambo mpya wa kukuza uyoga hufanya kazi. Picha|Sammy Waweru[/caption] Chini ya mradi – Smart Mushroom Farming Initiative, mradi huo, kituo cha utafiti cha JKUAT, ndicho JHUB Africa, mwasisi wake Dkt Lawrence Nderu anasema mfumo huo utasaidia kuboresha ukuzaji. “Ni ukuzaji kwa njia ya kiotomatiki kuboresha kilimo cha uyoga,” akasema Dkt Nderu, wakati wa uzinduzi wa mradi huo JKUAT, Juja, Kaunti ya Kiambu majuzi. Mpango huo, aidha, unalenga kufanikisha kilimo endelevu na kulinda misitu kwa sababu mfumo unaotumika unahitaji kiwango kidogo tu cha ardhi. Wakulima wengi wa uyoga wanalazimika kukata miti ili kuukuza. [caption id="attachment_172539" align="aligncenter" width="300"] Maafisa wa JKUAT na Mushroom & wakikagua uyoga unaoendelea kukua chini ya mfumo wa Smart Mushroom Farming. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kwenye mahojiano ya kipekeee na Akilimali, Dkt Nderu ambaye pia ni mwenyekiti wa Kitengo cha Uchakataji wa Taarifa kwa Kutumia Kompyuta, JKUAT, alisema teknolojia hiyo inayotumika Korea Kusini inawezesha wakulima maeneo ya miji kukuza uyoga kwenye mabustani yao, hivyo basi kuzuia ukataji na uharibifu wa miti. “Uzinduzi wa kilimo cha uyoga kwa njia ya kisasa ni mojawapo ya mbinu kuangazia ajenda ya usalama wa chakula, kuboresha mazingira na kulinda misitu Kenya,” Dkt Nderu akaelezea. Uyoga, bidhaa mbadala ya nyama, huliwa kwenye hoteli na mikahawa mingi ya kifahari Nairobi, Nakuru, Mombasa, Kisumu, na Eldoret, na inaendelea kuwa maarufu kwenye menu. Watu wanazidi kuwa makini na wanachokula, kwa sababu ya maradhi yanayohusishwa na afya. Kupitia mfumo wa Smart Mushroom Farming, wakulima hawahitaji kukata miti. [caption id="attachment_172540" align="aligncenter" width="300"] Dkt Lawrence Nderu mwasisi wa JHUB Africa na mfanyakazi JKUAT kwenye chumba cha kuzalisha uyoga JKUAT. Picha|Sammy Waweru[/caption] Shukran kwa JHUB Africa na ushirikiano wake na Mush &, kampuni kutoka Korea Kusini, na Korea International Cooperation Agency (KOICA), chini ya mpango wa teknolojia hiyo bunifu kukuza na kuboresha kilimo cha uyoga. “Ni mfumo unaodhibiti kiwango cha joto, unyevuunyevu, hewa, Kaboni, na mwangaza hivyo kupunguza gharama ya uzalishaji,” akasema Jihyun Jung, Afisa Mkuu Mtendaji Mush &. Mfumo huo, unashirikisha teknolojia ya kuunganisha mtambo kudhibiti huduma kwa simu ya mkono, ndiyo rununu, hivyo mkulima anaweza kujua jinsi ‘shamba’ lake la uyoga linavyoendelea hata akiwa mbali nalo. [caption id="attachment_172541" align="aligncenter" width="300"] Jihyun Jung, Afisa Mkuu Mtendaji Mush & akielezea kuhusu mfano wa kisasa kuzalisha uyoga. Picha|Sammy Waweru[/caption] “Huduma zote zinaendeshwa kutoka eneo moja,” Jihyun akaongeza, akisisitiza kwamba ni mfumo endelevu kuboresha kilimo cha uyoga na kulinda na kudumisha mazingira. JHUB Africa, tayari imeanza kuhamasisha wakulima, Dkt Nderu akidokeza kuwa wakulima wapatao 400 kutoka Kiambu na Machakos wamepata mafunzo. Mradi huo ni wa bajeti ya Sh29.82 milioni. Kaunti ya Kiambu pekee, alifichua kwamba wanalenga kufikia wakulima 60, 000. Mradi huo wa miezi 15, unalenga kusambaza mbegu za uyoga (spawn) maeneo mbalimbali nchini, kutoa mafunzo kuhimiza ukumbatiaji wa zao hilo kwa njia ya kidijitali, ili kuongeza kiwango cha mazao na kulinda mazingira. [caption id="attachment_172542" align="aligncenter" width="300"] Mbegu za uyoga - maarufu kama spawns kwenye mifuko. Picha|Sammy Waweru[/caption]
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Agha Khan Foundation, leo imepanda miti zaidi ya 200 katika eneo la Makao Makuu ya TET, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya taasisi hiyo.
IRINGA: WALIMU wa shule za msingi Manispaa ya Iringa wameanza kupatiwa mafunzo ya siku tatu kuhusu mbinu mpya ya kufundisha Kiingereza kwa kutumia mfumo wa Jolly Phonics. Mfumo huo unaolenga kuwasaidia wanafunzi wa darasa la kwanza kujifunza kusoma na kuandika kwa ufanisi zaidi. Akizungumza katika mafunzo hayo yanayofanyika katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Mratibu wa…
DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kimeandaa Kambi Maalum ya Afya ya Moyo kuanzia Mei 21 hadi Mei 22, 2025 ambapo wananchi watapata fursa ya kufanyiwa uchunguzi wa awali wa viashiria vya moyo, uchunguzi wa visababishi vya magonjwa ya moyo. Pia watapata elimu na ushauri kuhusu afya ya…
MRADI wa Kilimo na Lishe Tanzania (NOURISH -Tanzania), umeandaa siku ya wakulima katika wilaya 10 za mikoa mitano nchini kwa lengo la kuwaelimisha wakulima kuhusu kilimo cha tija ili kuleta mapinduzi kwenye sekta hiyo. Akizungumza katika kijiji cha Nghumbi, Halmashauri ya Kongwa, mkoani Dodoma, Ofisa wa Mradi wa NOURISH, Theophil Tarimo amesema wamelenga kutoa elimu…
MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa rai kwa viongozi wa mikoa kwa kushirikiana na taasisi za misitu na utafiti waanzishe bustani za mimea zinakazosaidia vijana kutafiti na kutengeneza dawa. Dk Mpango alitoa rai hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) katika viwanja vya chuo hicho mkoani Iringa jana.…
MTOTO wa hayati Cleopa Msuya, Job Msuya amesema Januari 4, mwaka huu katika siku ya kuzaliwa, baba yake alieleza nia yake ya kujengewa Chuo Kikuu Mwanga kinachohusu mambo ya Bioteknolojia au Teknolojia ya Habari (IT). Job alisema hayo alipozungumza kwa niaba ya familia wakati wa ibada ya maziko ya baba yao Usangi wilayani Mwanga mkoani…
MAELFU ya wananchi wake kwa waume wa Wilaya ya Mwanga na maeneo ya jirani wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Mwanga, Cleopa Msuya kwenye Uwanja wa Cleopa Msuya mjini Mwanga mkoani Kilimanjaro. Kwa heshima ya alama aliyoiweka katika sekta ya elimu, shule za msingi na sekondari za maeneo ya…
GEITA: IDADI ya wanafunzi wanaosoma Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi (ASEP) katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeongezeka kutoka wanafunzi 105 mwaka 2021 hadi kufikia 176 Aprili mwaka 2025. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 71 wa Elimu ya Sekondari Nje ya Mfumo Rasmi ndani ya kipindi cha miaka minne sawa…
Katika ulimwengu wa sasa ambao tekinolojia inaendelea kukua kwa kasi, watoto wengi wamezama katika vifaa vya kielektroniki kama simu, michezo ya video, na televisheni. Ingawa teknolojia ina faida zake katika kufundisha na burudani, ni muhimu kutambua umuhimu wa kumpa mtoto muda wa kupumzika bila kutumia vifaa hivyo. Tafiti mbalimbali, ikiwemo ile iliyofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Southern California, zimeonyesha kuwa akili ya binadamu huwa katika hali ya kipekee wakati mtu anapokuwa ametulia na kuzama ndani ya fikra zake. Hali hii ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya uwezo wa kujitambua, maadili, uwezo wa kujifunza, na kumbukumbu. Watoto wanapopewa muda wa kuwa kimya na kutafakari bila usumbufu wa dijitali au kelele, wana nafasi ya kujiendeleza kiakili na kihisia. Muda huu unawasaidia kufikiria kuhusu maisha yao, kuota ndoto, na kuelewa vyema hisia zao wenyewe. Tafakari ya aina hii huchangia katika kukuza utulivu wa ndani, kuongeza motisha, na hata kuboresha utendakazi wao. Katika mfano wa maisha ya kila siku, mzazi mmoja aliamua kuondoka na mwanawe wa miaka tisa bila kifaa chake cha mchezo wa video kwenda safari fupi. Ingawa awali mtoto huyo alionekana kuwa na wasiwasi, baadaye alianza kuangalia mazingira ya nje na kufurahia mandhari ya kawaida — jambo ambalo mara nyingi linasahaulika watoto wakizama katika dijitali kwa muda mwingi. Mzazi huyo alichukulia hiyo kuwa fursa nzuri mtoto kuwa peke yake na mawazo yake, hali inayochochea ubunifu na tafakari ya ndani. Manufaa ya kupumzisha akili sio tu kwa watoto wa shule. Hata watoto wadogo wanaofikia umri wa kuanza kujifunza wanaweza kufaidika kwa kuwa mbali na vifaa bebe vya dijitali kwa muda. Hii inawasaidia kukuza uwezo wa kuzingatia, kuvumbua njia za kuburudika wao wenyewe, na kukuza ustawi wa kihisia. “Watoto wanapofundishwa namna ya kutafakari na kujitambua, wana uwezo mkubwa wa kupunguza wasiwasi, kukuza ari ya kujifunza, na hata kufaulu katika mitihani” asema mtaalamu wa malezi Debbie Glaussier akiandika katika jarida la Psychology Today. Anasema wazazi, walimu na walezi wote wanapaswa kutambua kuwa si kila wakati mtoto anatakiwa kuwa na kifaa cha kielektroniki mkononi. Muda wa kutulia, kutazama mazingira, au hata kuwaza tu kwa mbali bila shughuli yoyote maalum ni muhimu kwa afya ya akili na maendeleo ya mtoto. Ni muda usio na gharama yoyote, lakini wenye thamani kubwa kwa mustakabali wa watoto wetu.
SINGIDA: MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ametoa wiki mbili kwa wajenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali Kitukutu kumaliza maeneo yote ambayo hayajakamilika. Shule hiyo inayojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 1.6 ipo katika kijiji cha Kitukuu kata ya Ulemo mkoani humo. DC Mwenda ametoa agizo hilo mara baada ya jana…
KUPUNGUZA uzani si jambo rahisi kwa wengi hasa kwa sababu mara nyingi huhusisha kufanya mazoezi. Kwa hivyo, kuna baadhi ya watu ambao wamelazimika kutumia njia za mkato ili kupunguza uzani, na katika harakati hizo kuhatarisha afya na maisha yao. Ikiwa wewe ni mmoja wao, haina haja ya kufanya hivyo. Badala yake, sasa waweza anza kula vyakula vitakavyokusaidia kupunguza huo uzani unaokusumbua. Baadhi ya vyakula vinavyosaidia kupunguza uzani ni pamoja na: Maji Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tokyo, unapokula vyakula vilivyo na viwango vya juu vya maji kama vile matunda na mboga unashiba upesi na hivyo kukuepusha usile chakula kingi. Brokoli Mboga hizi zina viwango vya juu vya nyuzi na madini ya calcium, viungo muhimu katika ukuzaji wa misuli. Kabeji Mboga hii ina kiwango cha juu cha kemikali za kusfisha mwili kama vile vitamin C, mbali na kuimarisha hali ya kinga mwilini. Koliflawa Sawa na mboga zingine, koliflawa ina viwango vya juu vya virutubisho vya vitamini C na folate. Inapoliwa ikiwa bichi au ikipikwa kwa muda mfupi basi unaongeza uwezo wake wa kusafisha damu. Balungi Tunda hili lina viwango vya juu vya vitamini C, folic acid, na potassium. Saladi Kwa kawaida chakula hiki huwa na kiwango cha juu cha B vitamins, folic acid, na manganese, virutubisho muhimu vinavyodhibiti viwango vya sukari kwenye damu na ni muhimu kusaidia kuimarisha kinga mwilini. Figili Mboga hizi zina viwango vya juu vya madini ya potassium, folic acid, sulfur na kemikali za kusafisha mfumo wa mwili na hivyo kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Spinachi Mboga hizi zina viwango vya juu vya madini ya chuma, folic acid, na vitamin K. Kadhalika zina viwango vya juu vya kemikali za kupambana na maradhi. Unapoandaa chakula hiki hakikisha haukipiki kwa muda mrefu.
KATIKA moja ya kauli zake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere amewahi kunukuliwa akisema, “Uandishi wa habari ni nyenzo muhimu katika kujenga taifa lenye umoja na maendeleo, vyombo vya habari vinapaswa kuwa na jukumu la kutoa elimu kwa umma, kuhamasisha maendeleo na kuimarisha uzalendo”. Hakuna ubishi kuhusu kauli hii ya Mwalimu Nyerere, kutokana na ukweli…
KAUNTI ya Turkana sasa imechukua nafasi ya kwanza kama kaunti yenye mzigo mkubwa zaidi wa malaria nchini Kenya, kulingana na takwimu mpya kutoka kwa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Turkana imebadilika kutoka kuwa eneo la milipuko ya msimu hadi kuwa eneo la malaria ya kudumu, na visa vya ugonjwa huo vimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 65 wakati wa misimu ya mvua tangu mwaka wa 2017. Kwa kiwango cha maambukizi cha asilimia 39 kilichorekodiwa mwaka uliopita—ambacho ni mara sita zaidi ya wastani wa kitaifa wa asilimia 6—kaunti hiyo sasa imeorodheshwa kuwa eneo lenye mzigo mkubwa wa malaria chini ya Mkakati wa Kitaifa wa Malaria. Katibu katika Idara ya Afya ya Umma na Viwango vya Kitaalamu, Bi Mary Muthoni, alieleza kuwa mvua kubwa inayonyesha Turkana huwafanya wakazi wengi kuwahifadhi wagonjwa nyumbani kutokana na hali mbaya ya hewa, hali inayotishia maisha. Mwaka wa 2017, Turkana ilishuhudia mlipuko mbaya zaidi ambapo zaidi ya watu 45,000 walipatikana na maambukizi ya malaria ndani ya mwezi mmoja pekee. Eneo la Turkana Magharibi lilirekodi asilimia 65 ya visa hivyo. Bi Muthoni alisema hali hii mpya imeifanya Turkana kuwa eneo muhimu la kuanzisha mkakati wa kudhibiti malaria kwa watoto wa umri mdogo kupitia mpango wa Seasonal Malaria Chemoprevention (SMC)—ambapo dawa za kuzuia malaria hutolewa kila mwezi wakati wa msimu wa maambukizi. Katika mwaka wa 2024, awamu ya kwanza ya mpango huo ililenga eneo la Turkana ya Kati ambalo lilikuwa na visa 102,000 vya malaria, huku asilimia 60 ya maambukizi hayo yakitokea kati ya Mei na Septemba. Mpango wa SMC ulizinduliwa mwezi Juni 2024 kwa msaada wa Catholic Relief Services (CRS) na unahusisha utoaji wa dawa aina ya sulfadoxine-pyrimethamine pamoja na amodiaquine (SP+AQ) kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Dawa hizo hutolewa mlango kwa mlango na wasambazaji wa kujitolea wa jamii. Bi Muthoni aliongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi yanachangia ongezeko la malaria Turkana kwa kuongeza maeneo ya maji yaliyosimama, ambayo ni mbu wanaoeneza ugonjwa huo huzaana. Utafiti wa hivi karibuni kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown nchini Amerika unaonyesha kuwa malaria imekuwa ikisambaa hadi maeneo ya juu zaidi barani Afrika kila mwaka kutokana na ongezeko la joto. Kutokana na hali hiyo, mwaka 2012, WHO ilipendekeza SMC kama njia bora ya kuzuia malaria kwa watoto katika maeneo yenye milipuko ya msimu. Mwaka jana, watoto 38,585 walio chini ya miaka mitano walipewa dawa hizo katika mizunguko mitano tofauti. Asilimia 71 (27,206) ya watoto hao walikamilisha mizunguko yote mitano ya tiba hiyo.
MASOMO katika shule 2,400 za chekechea katika kaunti ya Nakuru hayatalipiwa ikiwa Gavana Susan Kihika atatekeleza pendekezo la hoja iliyopitishwa na bunge la kaunti ya Nakuru. Hoja hiyo iliyodhaminiwa na Diwani wa Shabab David Wathiai ilipitishwa kwa kauli moja na madiwani wote wiki jana. Madiwani hao walisema wanataka kuhakikisha watoto wote wanapata elimu ya msingi. Wazazi wamekuwa wakilipa karo ya kati ya Sh200 na Sh3,500 kila muhula kama karo kwa watoto wao wanaosomea katika shule za chekechea. “Masomo ya chekechea ni muhimu katika ukuaji wa binadamu. Hii ndio maana tunataka kuondoa ada zote zinazotozwa wanafunzi. Hatua hii inalandana na hitaji la Katiba kwamba elimu ya msingi itolewe kwa watoto wote bila malipo,” akaeleza Bw Wathiai. Endapo Gavana Kihika ataidhinisha uamuzi huo wa Bunge la Kaunti ya Nakuru, serikali yake itatenga pesa za kufanikisha utekelezaji wa sera hiyo. “Tumepitisha mswada huo na sasa tunataka Gavana Susan Kihika atekeleze pendekezo lake kwamba shule zote za chekechea zitoe elimu bila malipo. Bunge la Kaunti linaweza pia kutenga fedha za kufanikisha utekelezaji wa pendekezo hilo hatua ambayo itafanyika kila mwaka,” Bw Wathiai akasema. Diwani wa London Benard Gatuso alisema hoja kama hiyo ilikuwa inahitajika kupitishwa mapema na bunge hilo. “Karo inayolipwa katika shule za chekechea zinazoweza kuonekana kama kidogo, lakini ni mzigo mkubwa kwa wazazi wakati huu ambapo uchumi umezorota. Kwa kupitisha hoja hii, tumewawezesha watoto wetu kupata elimu ya msingi kwa urahisi,” akasema Bw Gatuso.
SHULE zinafunguliwa wiki hii kwa muhula wa pili, huku walimu wakuu wakitoa wito kwa serikali kutoa fedha bila kuchelewa ili kuepuka misukosuko inayoshuhudiwa mara kwa mara wakati wa muhula huu mrefu zaidi wa kalenda ya masomo. Katika muhula huu, serikali pia inatarajiwa kutangaza uteuzi wa wanafunzi watakaojiunga na shule za Sekondari Pevu mwaka ujao. Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari (KESSHA), Bw Willy Kuria, ameitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha pesa zinazotengewa wanafunzi ni 22,000 na zitumwe kwa shule mapema ili kusaidia kupanga shughuli za ziada ambazo hutawala muhula huu. “Hali ilikuwa mbaya sana, tulikaribia kufunga shule kabla ya wakati kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Tunapofungua shule, Sh2,300 za muhula wa kwanza hazikutolewa ili kuwa Sh11,000. Tafadhali toeni pesa hizo kabla ya kutuma pesa za muhula wa pili,” alisihi Bw Kuria. Mkuu huyo wa shule ya upili ya Murang’a alisema ukosefu wa fedha umesababisha shule nyingi kukosa kushiriki katika shughuli za ziada, jambo ambalo hufanya wanafunzi kusababisha ghasia. “Muhula huu huwa na shughuli nyingi za ziada. Wakikosa kushiriki, hiyo huwa dalili ya matatizo. Mara nyingi tunakosa kushiriki katika shughuli hizo kwa sababu ya ukosefu wa fedha,” alieleza. Bw Kuria alisema muhula wa pili ni mrefu na muhimu zaidi kwa sababu walimu hujitahidi kukamilisha silabasi. “Ni muhula wenye shughuli nyingi unaoamua ikiwa watahiniwa watafaulu au kufeli mitihani yao ya kitaifa,” alibainisha. Aliongeza: “Ni muhula ambapo ghasia kama migomo hutokea kwa sababu ya mitihani ya majaribio. Wanafunzi wengine huwa hawajajiandaa na hivyo kuzua fujo. Wakuu wa shule wanapaswa kuwa macho.” Muhula huo unaanza Aprili 28 na utaendelea kwa wiki 14 hadi Agosti 1. Kwa mujibu wa ratiba ya mwaka wa masomo 2025, wanafunzi watapata mapumziko ya katikati ya muhula kwa siku tano kuanzia Juni 25 hadi Juni 29. Shule zitafungwa tena mwezi Agosti kwa wiki tatu, kuanzia Agosti 4 hadi Agosti 22, kabla ya muhula wa tatu kuanza.Katika mahojiano na Taifa Leo, Waziri wa Elimu Bw Julius Ogamba alihakikishia kuwa atahakikisha fedha zinatumwa shuleni kwa wakati.
NDOTO ya Michelle Omondi ya kumaliza masomo yake upili katika Shule ya Wasichana ya Pangani nusura ikatizwe kutokana na ukosefu wa karo. Michelle, 15 anatoka familia maskini lakini sasa anaweza kufurahi baada ya shirika moja lisilo la kiserikali kumsaidia na kumpa udhamini wa masomo.Tineja huyo ni kati ya wasichana na wanawake 1, 544 ambao SHOFCO imewalipia karo ili wamalize masomo ya shule ya upili katika Kaunti ya Nairobi.“Kuna wakati ambapo nilifikiria ningeacha masomo na kuanza kusaka vibarua vya kusaidia familia yangu. Kulipiwa karo kumenisaidia sana na kunipa matumaini ya kusaka maisha bora,” akasema Michelle.Bi Maureen Isinga, mzazi katika Shule ya Wasichana ya Huruma, naye alisema mwanawe alikuwa na deni la karo lakini sasa anaweza kutabasamu baada ya Shofco kumlipia deni hilo na kugharimia elimu yake yote.“Hawajamlipia tu karo, pia wamelipa deni la awali ambalo lilikuwa likinisumbua. Sasa nitamakinika kusaka karo kwa watoto wangu wawili,” akasema Bi Isinga wakati Shofco ilizindua utoaji udhamini wa karo Nairobi.Wanafunzi kutoka kaunti mbalimbali ndogo ambao wanatoka familia maskini na ni werevu walinufaika kwa kulipiwa karo.Wakati wa hafla hiyo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Shofco , Bw Kennedy Odede, alisema shirika hilo lina imani kuwa kupitia elimu, maisha ya familia nyingi maskini yataimarika.“Elimu inastahili kuwa haki na wasichana hawa wameonyesha ari na bidii masomoni licha ya kutatizwa na karo. Tunawekeza kwenye taaluma yao ya baadaye kupitia ufadhili huu ambao tunawapa,” akasema Bw Odede.Kati ya 1, 544 walionufaika, 159 walikuwa wasichana waliojifungua watoto na wamerejelea masomo ili kutimiza ndoto zao za kupata elimu.Shofco inalenga kuwasaidia zaidi ya wasichana 11,000 maskini kwa kuwapa udhamini wa masomo kote nchini.