Funza mtoto kupumzika akuze utulivu na kuongeza motisha

Katika ulimwengu wa sasa ambao tekinolojia inaendelea kukua kwa kasi, watoto wengi wamezama katika vifaa vya kielektroniki kama simu, michezo ya video, na televisheni.
Ingawa teknolojia ina faida zake katika kufundisha na burudani, ni muhimu kutambua umuhimu wa kumpa mtoto muda wa kupumzika bila kutumia vifaa hivyo.
Tafiti mbalimbali, ikiwemo ile iliyofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Southern California, zimeonyesha kuwa akili ya binadamu huwa katika hali ya kipekee wakati mtu anapokuwa ametulia na kuzama ndani ya fikra zake.
Hali hii ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya uwezo wa kujitambua, maadili, uwezo wa kujifunza, na kumbukumbu.
Watoto wanapopewa muda wa kuwa kimya na kutafakari bila usumbufu wa dijitali au kelele, wana nafasi ya kujiendeleza kiakili na kihisia. Muda huu unawasaidia kufikiria kuhusu maisha yao, kuota ndoto, na kuelewa vyema hisia zao wenyewe. Tafakari ya aina hii huchangia katika kukuza utulivu wa ndani, kuongeza motisha, na hata kuboresha utendakazi wao.
Katika mfano wa maisha ya kila siku, mzazi mmoja aliamua kuondoka na mwanawe wa miaka tisa bila kifaa chake cha mchezo wa video kwenda safari fupi. Ingawa awali mtoto huyo alionekana kuwa na wasiwasi, baadaye alianza kuangalia mazingira ya nje na kufurahia mandhari ya kawaida — jambo ambalo mara nyingi linasahaulika watoto wakizama katika dijitali kwa muda mwingi. Mzazi huyo alichukulia hiyo kuwa fursa nzuri mtoto kuwa peke yake na mawazo yake, hali inayochochea ubunifu na tafakari ya ndani.
Manufaa ya kupumzisha akili sio tu kwa watoto wa shule. Hata watoto wadogo wanaofikia umri wa kuanza kujifunza wanaweza kufaidika kwa kuwa mbali na vifaa bebe vya dijitali kwa muda. Hii inawasaidia kukuza uwezo wa kuzingatia, kuvumbua njia za kuburudika wao wenyewe, na kukuza ustawi wa kihisia.
“Watoto wanapofundishwa namna ya kutafakari na kujitambua, wana uwezo mkubwa wa kupunguza wasiwasi, kukuza ari ya kujifunza, na hata kufaulu katika mitihani” asema mtaalamu wa malezi Debbie Glaussier akiandika katika jarida la Psychology Today.
Anasema wazazi, walimu na walezi wote wanapaswa kutambua kuwa si kila wakati mtoto anatakiwa kuwa na kifaa cha kielektroniki mkononi. Muda wa kutulia, kutazama mazingira, au hata kuwaza tu kwa mbali bila shughuli yoyote maalum ni muhimu kwa afya ya akili na maendeleo ya mtoto. Ni muda usio na gharama yoyote, lakini wenye thamani kubwa kwa mustakabali wa watoto wetu.