DC Mwenda atoa wiki mbili sekondari ikamilike

SINGIDA: MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ametoa wiki mbili kwa wajenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali Kitukutu kumaliza maeneo yote ambayo hayajakamilika. Shule hiyo inayojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 1.6 ipo katika kijiji cha Kitukuu kata ya Ulemo mkoani humo. DC Mwenda ametoa agizo hilo mara baada ya jana …
SINGIDA: MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda ametoa wiki mbili kwa wajenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali Kitukutu kumaliza maeneo yote ambayo hayajakamilika.
Shule hiyo inayojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 1.6 ipo katika kijiji cha Kitukuu kata ya Ulemo mkoani humo.
DC Mwenda ametoa agizo hilo mara baada ya jana Mei 8, kutembelea mradi wa ujenzi wa shule hiyo unaotekelezwa na serikali kupitia SEQUIP.
“Tupo nyuma yaradi hakikisheni ndani ya wiki mbili zijazo mnamaliza maeneo yote ambayo yapo nyuma kama vile karakana ili mradi uishe kwa haraka watoto waweze kuingia,” ameagiza DC Mwenda.