Kampeni Mama Samia yaondoa mfumo wanawake kutomiliki ardhi Korogwe

Habari Leo
Published: Apr 12, 2025 07:08:57 EAT   |  Educational

TANGA: LICHA  ya serikali na wadau mbalimbali kutoa elimu ya kuondoa mfumo dume wa wanawake kupata haki ya…

The post Kampeni Mama Samia yaondoa mfumo wanawake kutomiliki ardhi Korogwe appeared first on HabariLeo.

TANGA: LICHA  ya serikali na wadau mbalimbali kutoa elimu ya kuondoa mfumo dume wa wanawake kupata haki ya kumiliki ardhi hali ni tofauti katika kijiji cha Magunga Mziha wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Wanawake katika kijiji hicho hawana haki ya kumiliki ardhi. Hayo yamebainika baada ya timu ya kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia legal Aid  kuwajengea uwelewa wa kisheria kuhusu haki ya wanawake kumiliki ardhi.

Wanawake katika kijiji hicho walikuwa hawa haki ya kumiliki ardhi hata pale wazazi au wenzawao wanapofariki na umiliki ulikuwa unakwenda kwa wanaume pekee.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwajengea uwezo wa masuala ya sheria na haki za binadamu wananchi hao walisema kuwa kutokana na elimu ya kisheria waliyoipata imewasaidia kubadilisha dhana ya mfumo dume waliyokuwa nayo

Mtendaji wa kijiji hicho, Hussein Mwanyoka amesema kutokana na kukosa uwelewa wa kisheria wanawake katika eneo hilo walikuwa hawawezi kumiliki ardhi hata eneo dogo kwani walioneka wao ni watu ambao wanategemea kufanyiwa maamuzi tu.

“Hapa kwetu tulimchukulia mwanamke ni muolewa tuu hivyo hana haki ya kumiliki ardhi hata kama ni mali ya mzazi wake tulikuwa tunawamilisha wanaume pekee lakini leo kampeni hii imetusaidi kufahamu na tutaanza kubadilika kutoka sasa,” amesema Mwanyoka

Hata hivyo wakili kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Gloria Baltazari amesema kampeni hiyo imekuja maalum kutoa uwelewa kuhusu masuala ya sheria lakini na kutatua changamoto za kisheria ambazo zinawakabili wananchi.

The post Kampeni Mama Samia yaondoa mfumo wanawake kutomiliki ardhi Korogwe appeared first on HabariLeo.