Kidato cha sita Nanyamba wafundwa udanganyifu mitihani

WANAFUNZI wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Dinyecha iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara…
The post Kidato cha sita Nanyamba wafundwa udanganyifu mitihani appeared first on HabariLeo.
WANAFUNZI wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari ya Dinyecha iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara kujiepusha na udanganyifu wa mitihani kwani walimu wamewaandaa vizuri na wanapaswa kujiandaa vizuri pia. Mitihani hiyo itafanyika Mei 5, 2025.
Hayo yamejiri wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita katika shule hiyo yaliyofanyika na kwamba bado safari yao ya elimu hawajakamilisha hivyo wanapoelekea kufanya mitihani hiyo kikubwa ni kufanya ibada ya kumuomba Mwenyezi Mungu ili awape wepesi kwenye mitihani yao na siyo kinyume na hapo.
Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota amewapongeza wahitimu hao kwa jitihada za kuwakikisha wanafikia hatua hiyo pia wazazi waliyoweka moyo wa imani na uwekezaji huo uliyofanywa kwa kutowahamisha wanafunzi shuleni hapo kutokana na ile dhana kuwa mtwara hakufikiki, hakutakuwa na walimu na mengine hivyo kupelekea wazazi wengi kuhamisha watoto wao kuwapeleka mikoa mingine.
‘’Niwashukuru wale wazazi ambao mlijenga imani na kama mnavoona matokeo ya mwaka jana wahitimu wetu walifanya vizuri sana na wenyewe hawa wahitimu wa sasa wanasema divisheni one ni lazima kwao, nina uhakika kwa uwekezaji na jitihada ambazo walimu wamezifanya na walizoonyesha wanafunzi kwa mapenzi ya Mungu watafanya vizuri katika matihani yao,’’amesema Chikota.
Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa anaoufanya kwenye sekta ya elimu ikiwemo shule hiyo kwani wana shule zingine kama hizio ambazo kwa sekta ya elimu ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga miundombinu hiyo ili kuhakikisha kizazi cha Tanzania kinatapata elimu inayostahili ili waweze kupambana na maisha ya wakati wa sasa.
Mkuu wa shule hiyo, Mwajuma Mnayahe amesema awali wahitimu hao walikuwa 594 lakini sasa wanaohitimu 215 kwasababu wengi wao walihamia shule zingine huku akiishukuru serikali kwa kuleta miundombinu bora ya shule yenye thamani ya Sh bilioni 1.2 na kueleza moja ya changamoto inayoikabili shule ikiwemo uzio.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Hapiphania Severine ameipongeza serikali kwa kujenga shule mbalimbali za kidato cha tano na cha sita nchi mzima bila kuangalia sehemu maalum huku akieleza moja ya changamoto inayowakabili wanafunzi hao ikiwemo gari la kuwawezesha kwenye safari za kimasomo kwenye mitihani ya ujirani mwema.
The post Kidato cha sita Nanyamba wafundwa udanganyifu mitihani appeared first on HabariLeo.