Bunifu Muhas majawabu changamoto za afya

Habari Leo
Published: Apr 25, 2025 12:51:01 EAT   |  Educational

DAR ES SALAAM: SERIKALI imesema inaunga mkono bunifu mbalimbali za afya zinazofanyika Chuo Kikuu na Sanyansi Shirikishi (Muhas)…

The post Bunifu Muhas majawabu changamoto za afya appeared first on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: SERIKALI imesema inaunga mkono bunifu mbalimbali za afya zinazofanyika Chuo Kikuu na Sanyansi Shirikishi (Muhas) ili kupata majawabu mapya ya changamoto za afya.

Akizungumza leo Aprili 25, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Peter Msofe amesema wiki ya ubunifu iliyoanzishwa na chuo hicho italeta majawabu mapya ya changamoto za afya.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Msofe amesema serikali imetengeneza miongozi ya matumizi ya akili unde katika taasisi zake za elimu ya juu.

“Tunajua pia kuna taratibu zinafanyika kupitia wizara inashughulika na mawasiliano kwa ajili ya kutumia akili undu,”amesema Prof Msobe.

Aidha, Makamu Mkuu wa Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema waliona umuhimu mkubwa wa kuanzisha wiki ya ubunifu kwa kuwakaribisha wananchi 300 kufanya vipimo mbalimbali.

Amesema lengo kuhakikisha masuala ya bunifu yanaimarishwa ambapo baadhi ya wanafunzi bunifu zao zimejikita kutafuta changamoto za magonjwa na kuhakikisha bidhaa au njia zinakuwa gharama nafuu.

“Vilevile tumeona bunifu kwenye vifaa tiba, tumeona pia dawa asili, vijana wanatengneza bunifu kuboresha zile bidhaa za maji, vidonge, lakini tumeona vitakasa mikono kama sabuni,”amesema Prof Kamuhabwa.

Clara Mcharo, mwanafunzi wa udaktari mwaka wa nne Muhas akizungumza kuhusu bunifu yake amesema uwiano kati ya wakunga na wagonjwa hauko sawa, hivyo bunifu yake inalenga kutatua changamoto hiyo.

“Unakuta baadhi ya maeneo mkunga mmoja anatakiwa ahudhurie wagonjwa 1,000 inauwa mzigo kuhakikisha wagonjwa wanaangaliwa, hivyo tumeleta mfumo ambao utasaidia hao wakungwa kuwaangalia wagonjwa wengi kwa muda mmoja,” amesema mwanafunzi huyo.

Katika Wiki ya Ubunifu ya Muhas kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa huduma za bure za kupima magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi, kama sehemu ya mchango wake katika kukuza ubunifu unaolenga kuboresha afya ya jamii.

Wiki ya Ubunifu, ya Kwanza ya Muhas ambayo ilianza rasmi Aprili 22, 2025 imemalizika leo inalenga kuonyesha miradi mbalimbali ya ubunifu kutoka kwa wanafunzi, watafiti na wadau wa sekta ya afya – yote yakiwa na lengo la kuleta suluhisho bunifu kwa changamoto zinazokabili jamii.

The post Bunifu Muhas majawabu changamoto za afya appeared first on HabariLeo.