Wenyeviti wa vijiji waomba msaada wa kisheria endelevu

Habari Leo
Published: Apr 25, 2025 11:13:53 EAT   |  Educational

WENYEVITI wa vijiji vya Mtukula, Byeju, Nkerenge vilivyopo Kata Mtukula, Wilaya ya Missenyi wameishukuru serikali kwa kuona elimu…

The post Wenyeviti wa vijiji waomba msaada wa kisheria endelevu appeared first on HabariLeo.

WENYEVITI wa vijiji vya Mtukula, Byeju, Nkerenge vilivyopo Kata Mtukula, Wilaya ya Missenyi wameishukuru serikali kwa kuona elimu ya kisheria inafaa kuwafikia wananchi wote wa vijijini wilayani Missenyi.

Timu ya wataalamu wanaoratibu kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia wilayani Missenyi imefanya mafunzo na utatuzi wa migogoro wa kisheria katika vijiji hivyo ambapo wenyeviti wengi wa vijiji wamekuwa wakitimiza wajibu wao wa kutoa huduma kwa wananchi lakini mara nyingi wamejikuta wakivunja sheria bila kujua.

Oscar Evarsta, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtukula amesema kampeni hii ni muhimu na serikali imefikiria mbali sana na kuona mahitaji  ya sasa ya wananchi kwani wenyeviti wanaongoza  wananchi lakini asilimia  kubwa ya wenyeviti hawajui sheria.

Ametoa wito kwa timu hiyo kuomba mafunzo ya sheria kuwa endelevu  ili kupunguza changamoto za uvunjifu wa sheria  ambazo zimekuwa zikijitokeza na kuondoa changamoto za familia nyingi kupelekana mahakamani kwani  wakiwa na elimu ya kutosha migogoro mingi itasuruhishwa kifamilia   bila kupoteza muda mahakamani.

Mwenyekiti kijiji cha Byeju, Patrick Deogratias  Kata Mtukula amesema wenyeviti wamekuwa kama sehemu ya mahakama ndogo hivyo wanasukuhisha migogoro ya ndoa ,ardhi, ugomvi,wizi  na wakati mwingine wanahusika kuvunja sheria kwa kuwalinda wapiga kura wao.

Ameipongeza  elimu ya kisheria ambayo imeongeza uelewa juu ya maswala  ya ardhi, kuandika wosia , kupata hati miliki ambapo alidai kuwa pamoja na  serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo  swala la kupita vijiji vya pembezoni  na kutoa elimu pamoja na kutatua migogoro imeongeza morali ya wananchi kuendelea kuipenda serikali yao.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Tawi la Mtukula  ameipongeza serikali ya awamu ya 6 kutoa elimu hiyo ya kisheria na kuomba kuwa endelevu kwani vijiji vingi vinavyopakana na mipaka  ya nchi nyingine vinakumbana na uvunjifu mkubwa wa Sheria.

Amesema uwepo wa kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imeongeza imani kubwa katika chama hicho kwani kupitia kampeinu hiyo ameshuhudia wananchi wasio na uwezo wanasaidika na kutatuliwa changamoto zao hivyo kama kampeini hiyo itakuwa endeleavu wananchi wengi watasaidika na kupunguza kwenda kupanga foleni mahakamani .

Taaarifa iliyotolewa na mratibu wa kampeini ya msaada wa kisheria Wilaya ya Missenyi, Maxmillan Fransis imeeleza kuwa tayari vijiji 30 vya Wilaya ya Missenyi vimefikiwa na kampeini ya msaada wa kisheria  na tayari Wizara ya Katiba na Sheria imeongeza siku 5 wilayani humo kwa ajili ya wananchi kuongezewa elimu zaidi ya kisheria na kutatua changamotoo za kisheria zilizojitokeza.

“Waziri wa Katiba na Sheria alifungua kampieni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia  Aprili 14 hadi 23 mkoani Kagera ikiwemo Wilaya ya Missenyi lakini baada ya kuona bado kuna uhitaji wa elimu hiyo na wananchi wanauhitaji wa  kutatuliwa changamoto zao za kisheria hawana uwezo wa kuwalipa mawakili wameongeza siku 5 nyingine za Kuwahudumia Wanachi hivyo wilaya ya Missenyi tutafikia  vijiji 45 hadi kufikia Aprili 28,” amesema Fransis.

The post Wenyeviti wa vijiji waomba msaada wa kisheria endelevu appeared first on HabariLeo.