IRINGA: BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeingia kwa kishindo mkoani Iringa kutoa elimu kwa umma kuhusu mikopo salama, baada ya ripoti ya uchunguzi kubaini kuwepo kwa ongezeko la mikopo kandamizi isiyo rasmi maarufu kama “mikopo umiza” au “kimangala”. Mikopo hiyo imeelezwa kudumaza maendeleo ya kiuchumi ya wakazi wa mkoa huo. Ripoti hiyo iliyofanyika kati ya…
DAR ES SALAAM: WATANZANIA wanaendelea kuelimishwa namna ya kukabiliana na huduma za dharura kwa wagonjwa wanaokutana na changamoto mbalimbali za kiafya, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) anaeleza. Dk Evelyne Mapunda ametoa kauli hiyo leo Julai 1, 2025 akiwa katika banda la MUHAS viwanja vya…
MATUMIZI sahihi ya viuatilifu ndiyo chachu kufikia uzalishaji unaotarajiwa kupatikana katika zao la korosho nchini na hii ni kutokana na uwepo wa baadhi ya magonjwa yanayoathiri zao hilo yakiwemo ‘bright’ na ‘ubwiriunga.’ Wanasema watalaamu mbalimbali wa kilimo cha korosho na kusisitiza kuwa, ili kukabiliana na changamoto ya magonjwa dhidi ya zao hilo, elimu ni muhimu…
Kutokana na uchumi mgumu unaoendelea kushuhudiwa nchini, wazazi wengi wamekuwa wakilemewa kumudu karo ya kuwasomesha watoto wao. George Wasonga, 57 afisa wa polisi amekuwa na kibarua kuwalipia watoto wake karo chuoni. Kama mzazi amekuwa akijituma sana kuhakikisha wanatimiza kiu chao cha kupata elimu ya juu ili wajitegemee siku za baadaye. Nuru ilimwaangazia Wasonga wiki hii baada ya dua yake kutimia na akashinda Sh11 milioni kwenye ubashiri wa Sportpesa Midweek Jackpot. “Nimekuwa nikipambana sana kuwasomesha watoto wangu na nia yangu imekuwa wasikose chochote maishani ili nao wawe na msingi wa kusaka kujizimbulia riziki siku zijazo,”akasema Wasonga, akiwa mwingi wa furaha baada ya kushinda hela hizo nyingi alizokiri zitasaidia kubadilisha maisha yake. Alikuwa akiongea mtaa wa Shauri moyo viungani mwa jiji la Nairobi alipopokezwa hundi kutokana na ushindi wake ambao sasa unaashiria mwanzo wa ufanisi na maisha mazuri. “Kupitia mapenzi ya mwenyezi Mungu sasa mambo yataimarika na wanangu watasoma na kufikia viwango vya juu vya elimu nchini. Sasa sina shaka kwa sababu kila kitu wanachohitaji, nitawatimizia,” akaongeza. Kando na kuwasomesha wanawe, afande huyo tayari ameweka mikakati ya kupanua biashara zake kisha kufanyia nyumba yake ukarabati. Wasonga amekuwa akibashiri mechi na Sportpesa tangu 2016 na amewahi kushinda Sh15,000 mapema mwaka huu. Hata baada ya kushinda Sh11 milioni kuwahi bonasi ya 12 kwenye Mega Jackpots ameapa kuwa ataendelea kushiriki huku akilenga Mega Jackpot. Jumamosi hii Mega Jackpot ilikuwa imefika Sh420,655,592. “Kwa wengine wanaobashiri jikazeni kwa sababu dua yenu itatimia. Nami nitaendelea kwa sababu nalenga fedha za juu zaidi kwenye Mega Jackpot,” akasema.
RAIS William Ruto jana aliwateua makamanda wapya wa Jeshi na Kikosi cha Jeshi la wana Anga kisha kuwaidhinisha maafisa 21 wapandishwe vyeo katika huduma ya jeshi. Mabadiliko hayo yalitangazwa kufuatia mapendekezo kutoka kwa Baraza la Ulinzi ambalo ni taasisi ya juu zaidi ya kufanya maamuzi yanayohusu Jeshi la Ulinzi Nchini (KDF). Meja Jenerali David Kipkemboi Ketter alipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali na kuteuliwa Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu. Ni hatua kuu kwa taaluma ya Luteni Jenerali Ketter katika KDF kwa kuwa 2023 alikuwa miongoni mwa maafisa wa jeshi waliotunukiwa na rais. Wakati huo alipandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Naibu Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu. Luteni Jenerali Ketter amechukua nafasi ya Luteni Jenerali David Kimaiyo Chemwaina Tarus, ambaye amepelekwa katika Chuo Kikuu cha Ulinzi Kenya ili kuhudumu kama naibu chansela. Hadi uteuzi wake mpya, Luteni Jenerali Ketter alihudumu vilevile kama Naibu Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi aliyesimamia wafanyakazi na mipangilio. Hatua ya kumtaja Luteni Jenerali Ketter kama Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu ina maana ndiye mtu wa tatu kwenye foleni ya kuwa mkuu wa jeshi nchini. Hii ni kwa kufuata mzunguko wa kuyatoa mamlaka kwenye uteuzi wa mkuu wa jeshi, kulingana na sheria zilizowekwa na Jenerali Mstaafu Daudi Tonje. Wengine katika daraja hilo ni pamoja na Luteni Jenerali Tarus na Luteni Jenerali Juma Shee Mwinyikai (Kamanda wa Chuo cha Kitaifa kuhusu Mafunzo ya Ulinzi). Uteuzi wa kuwa mkuu wa jeshi nchini, hata hivyo, unazingatia masuala mengine, ukiwemo umri. Jenerali Charles Kahariri anatoka kikosi cha jeshi la wanamaji naye Jenerali Francis Ogolla aliyeaga dunia Aprili mwaka jana, alitoka kikosi cha Jeshi la Anga.
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuweka nguvu zaidi katika utoaji wa huduma na elimu kwa umma kuhusu sheria ya usimamizi wa mazingira, ili kuhakikisha utunzaji wa mazingira unakuwa endelevu nchini. Mhandisi Masauni ametoa agizo…
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Nsajigwa Kabigi, wametembelea banda la Tume ya Madini katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayohitimishwa leo viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. Katika ziara hiyo, viongozi hao wamejionea namna Tume ya Madini inavyoshiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwa…
MAMILIONI ya wanafunzi wa shule za msingi na upili wataelekea nyumbani wiki hii kwa likizo fupi huku walimu wakuu wakikita kambi Mombasa kwa warsha yao ya kila mwaka kujadili masuala tata kuhusu elimu. Wanafunzi hao watakuwa likizoni kuanzia Juni 25, 2025 hadi Juni 29, 2025 na kurejea shuleni kwa wiki nyingine tatu kumaliza silabasi na kujitayarisha kwa mitihani ya kufunga muhula wa pili. Walimu hao wakuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Muungano wao wa kitaifa Willie Kuria alisema warsha hiyo itajumuisha zaidi ya walimu 9,000 ambao watakongamana katika ukumbi wa Sheikh Zayed Mombasa. Mwaka huu, walimu hao watajadili namna ya kukumbatia mifumo ya elimu na matayarisho ya shule zao kupokea wanafunzi wa Gredi ya 10. Wanafunzi milioni 1.2 walioko Gredi 9 wanaendelea na uchaguzi wa masomo yao na shule mbalimbali wanazotaka kujiunga nazo hapo mwakani baada ya kupewa mtihani wa kutathmini elimu yao ya shule ya msingi (KJSEA). Walimu wa shule za kitaifa pia wanatakiwa kujitayarisha kuhusu namna wanafunzi wa kutwa watajiunga na shule zao. Hii ni baada ya Wizara ya Elimu kutangaza kuwa shule za kitaifa zitatakiwa kuwa na wanafunzi wa kutwa ili kuhakikisha wanafunzi wote milioni 1.2 wanajiunga na shule za upili. Awali, walimu wakuu walipinga mfumo huu wakisema itakuwa hatari hasa kwa masuala ya kudumisha nidhamu na hata wanafunzi wa kutwa kutumiwa kuingiza dawa za kulevya shuleni. Masuala mengine ambayo yatajadiliwa ni pamoja na ufadhili wa masomo ya bure nchini. “Waziri wa Fedha John Mbadi ataeleza kuhusu ufadhili wa masomo nchini. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Mombasa, Prof Laila Abubakar, atajadili kuhusu namna ya kukumbatia teknolojia katika shule za upili,” alisema Bw Kuria. Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Dkt Nancy Gathungu, naye atazungumzia namna ya kulinda fedha za elimu huku Tume ya Kuwaajiri wa Walimu Nchini (TSC) ikitwikwa jukumu la kueleza kuhusu nafasi ya walimu katika kusaidia wanafunzi kuchagua masomo ya shule za sekondari. Waziri wa Afya, Bw Aden Duale, ataeleza kuhusu afya ya wanafunzi shuleni. Mnamo Juni 25, Naibu Rais Prof Kithure Kindiki atafungua rasmi kongamano hilo ambalo litahudhuriwa pia na wageni tofauti akiwemo Mwenyekiti wa TSC Dkt Jamleck Muturi, Gavana wa Mombasa Bw Abdulswamad Nassir, Waziri wa Elimu Bw Julius Ogamba. Ufadhili wa masomo umesalia donda sugu nchini huku walimu wakuu wakilalamika kwa kusema serikali imepunguza bajeti. Hata hivyo, kamati ya bunge inayosimamia elimu ikiongozwa na mwenyekiti wake Bw Julius Melly alisema bajeti hiyo inatosha kuhakikisha elimu inapigwa jeki.
TIMU ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia wilayani Ilala imebaini katika Kata ya Pugu baadhi ya wanawake wanazaa na waume za watu na kujihesabia haki kuwa nao ni wake halali ilihali ndoa ya awali ya mwanaume huyo haijavunjwa kisheria. Hivyo mwito wao ni kuwa elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili wawe na…
KAZI ya ualimu imegeuka tamu chungu kwa maelfu ya walimu ambao wamekwama kwenye daraja moja kwa miaka mingi huku wakilazimika kushuhudia walimu wenzao wachanga wakiwapita na kupandishwa vyeo. Licha ya kutumia hela nyingi kujiendeleza kielimu, kutuma maombi ya kupandishwa vyeo mara kadhaa na kuitwa kuhojiwa, idadi kubwa ya walimu wamebaki na machungu dhidi ya mfumo wanaohisi umewasaliti. Kulingana na alama za TSC, kiwango cha chini zaidi ni B5 na cha juu zaidi ni D5. Gredi b5 ni kiwango cha kuingilia huduma ya kufunza katika shule ya msingi kinachofuatiwa na C1 (mwalimu wa shule ya msingi), C2 (mwalimu wa kiwango cha juu II), C3 (mwalimu wa kiwango cha juu I), C4 (naibu mwalimu mkuu II) na C5 (mwalimu mkuu). Kisha kulingana na daraja ya walimu wakuu kuna D1 (mwalimu mkuu wa kiwango cha juu) D2 (naibu mwalimu mkuu II), D3 (mwalimu mkuu), D4(mwalimu mkuu wa daraja ya juu) na D5 (mkuu wa walimu wakuu). Mwalimu kutoka Nakuru kwa jina Simon Karanja aliye katika daraja la C2 alisimulia kuhusu taaluma yake ambayo imemwacha na machungu na majuto chungunzima. Huku akiwa amebakisha mwaka mmoja tu astaafu, alisimulia safari yake katika TSC ambayo haijamwachia sababu yoyote ya kutabasamu. “Nimekwamba katika kiwango cha P1 kwa miaka 27, licha ya kuhudhuria mahojiano tele ambapo nilipokea barua baada ya nyingine za kukataliwa,” anaeleza. “Ni baada ya tu ya kuandikia barua afisi ya Malalamishi ya Umma, Spika wa Bunge la Kitaifa, Wakili Mkuu, na hata rais, ambapo kitu kilisonga.” “Afisi ya Malalamishi ya Umma ilijibu na punde baadaye nikapandishwa cheo. Lakini maji yalishamwagika.” Akiwa mwaka wake wa tatu katika Daraja la Kazi C2, Bw Karanja anasema amepoteza imani na haki katika TSC na kuamini kwamba sehemu kubwa ya kupandishwa cheo husukumwa kisiasa. Hisia zake zimekaririwa na wengine wengi kote nchini akiwemo Naibu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msinyi ya Kayole, Dismus Omollo, ambaye amekwama katika Daraja la Kazi C4 kwa miaka 19 (tangu 2006) licha ya kutuma maombi ya kupandishwa cheo mara tatu. Bi Berline Langat, mwalimu wa C1 jijini Nairobi amekwama katika kiwango hicho hicho tangu 2014 (miaka 11) huku kusahihisha kila siku vitabu vya wanafunzi 80 katika kipindi cha dakika 35 kukimlemea kimwili na kihisia. Bi Florence Wanjiru ambaye amekwama katika Daraja la Kazi c2 tangu 2015 (miaka 10) anasema ualimu ni taaluma ya kujitolea mhanga bila kuzawadiwa, baada ya kuhojiwa mara tatu pasipo mafanikio. Hisia zake zinarejelewa na Lenah Chebet, mwalimu kutoka Bomet akisema “nilijiunga na huduma hii 2010, nikakwama B5 hadi 2020 (miaka 10) ambapo katika shughuli ya kuwapandisha vyeo walimu wote kwa jumla nilipanda C1 na kukwama hapo hadi leo hii.”
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na taasisi nyingine za elimu, kusimamia na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu ili kuendelea kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa. Majaliwa alisema hayo alipomwakilisha…
MWANZA: TAKRIBANI wadau wa elimu 200 wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kidigitali wa udhibiti ubora wa elimu mkoani Mwanza, wakasema matarajio yao ni kuleta kasi ya uwazi na uwajibikaji katika sekta ya elimu. Matarajio mengine ni kupunguza matumizi ya karatasi, hatua itakayochochea utunzaji wa mazingira pia, wamesema washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa…
MOROGORO; Wananchi Mkoa wa Morogoro wamejitokeza kupata huduma za kibingwa na bobezi bure katika maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislam (MUM). Huduma hizo zinatolewa na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), ambapo madaktari bingwa na wabobezi wanatoa huduma ya ushauri na matibabu kwa wananchi wa mji wa Morogoro na…
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ujio wa shule za amali pamoja na ufundi zenye michepuo ya ufundi, kilimo, muziki na fani mbalimbali unakwenda kutatua changamoto ya ajira hasa kwa vijana. Alisema serikali imeamua kubadilisha mwelekezo wa elimu nchini kwa kuanzisa shule hizo ambazo lengo lake kubwa ni kuhakikisha mtoto akihitimu elimu ya sekondari awe na…
IRINGA: Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga, amewataka Watanzania kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 2025 unazaa viongozi watakaotoa kipaumbele kwa sekta ya michezo, sanaa na elimu ili kuibua vipaji vya vijana kitaifa na kimataifa. Akizungumza katika hafla ya kufunga mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yaliyofanyika katika shule ya sekondari Lugalo mjini…
DAR ES SALAAM: TIMU ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imewafikia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiluvya wilayani Ubongo Dar es Salaam na kuwaelimisha masuala mbalimbali ikiwemo jinsi ya kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia. Akizungumza leo Juni 18,2025 shuleni hapo, mwanasheria katika timu hiyo, Nipael Ezekiel aliwaambia wanafunzi hao kuwa wanapaswa…
SIMIYU: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema jumla ya Sh bilioni 23.98 zimetolewa kwa ajili ya kuiendeleza sekta ya elimu wilayani Meatu mkoani Simiyu katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita. Akizungumza na wananchi wa Meatu mkoani humo katika Kiwanja cha Stendi ya Mabasi Meatu kwenye muendelezo wa ziara yake ya siku…
ARUSHA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amewaagiza maofisa manunuzi na wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali nchini kutoa elimu ya zabuni kwa makundi maalum, vijana na wanawake ili waweze kuomba zabuni na kujikwamua kiuchumi. Ridhiwani ametoa agizo hilo jijini Arusha kwenye kufunga kongamano la 9 la ununuzi wa lililoandaliwa…
DAR ES SALAAM: Zaidi ya Wanafunzi 150 Kutoka Chuo cha United African University Of Tanzania (UAUT) kilichopo Dar es salaam wamepewa mafunzo maaalumu ya Akili Unde (AI) lengo likiwa ni kuendana na mabadiliko ya Tehama ya dunia ya sasa. Prof Rwekaza Mukandala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema mafunzo hayo yaliyoanza Juni 9…
Ikiwa wewe ni mzazi wa kijana, tayari unajua kuwa mwanao wa kiume au wa kike hutumia saa nyingi kila siku akiwa katika vifaa vya kiteknolojia vya aina mbalimbali. Kile ambacho huenda hujui ni kwamba kutumia muda mrefu kwenye michezo ya video au mara kwenye kompyuta kunaweza kuathiri uwezo wa kijana wako kupata usingizi mzuri usiku. Kulingana na watafiti kutoka Centers for Disease Control and Prevention, vijana wanaotumia saa mbili au zaidi kila siku kwenye kompyuta kwa shughuli zisizo za masomo au kucheza michezo ya video hawapati usingizi wa kutosha ikilinganishwa na wenzao wanaotumia muda mchache kwenye vifaa vya elektroniki. Zaidi ya hayo, wanafunzi wa shule ya upili wanaofanya mazoezi kila siku wana nafasi kubwa zaidi ya kupata usingizi mzuri usiku ikilinganishwa na wale wasiokuwa na shughuli nyingi za kimwili. Matokeo ya utafiti huu uliohusisha vijana zaidi ya 15,000 yalichapishwa katika jarida la American Journal of Preventive Medicine. Vijana wanahitaji usingizi wa muda gani? Wataalamu wanapendekeza kuwa mwanafunzi wa shule ya upili anahitaji kati ya saa 8 hadi 9 za usingizi kila usiku. Hata hivyo, vijana wengi hulala kwa saa 5 – 6 au chini ya hapo. Ingawa kutofanya mazoezi na kutumia muda mwingi kwenye vifaaa vya dijitali kunaweza kuathiri usingizi, kuna pia maelezo ya kisaikolojia. Katika kipindi cha ujana, homoni inayoitwa melatonin,inayozalishwa kwenye ubongo,huzalishwa usiku wa manane zaidi ikilinganishwa na wakati wa utotoni. Kwa nini usingizi ni muhimu — hasa kwa vijana? Usingizi una faida muhimu kwa watu wa rika zote. Katika ujana, ukosefu wa usingizi unaweza kuchangia matatizo ya kusoma shuleni, kudhoofika kwa kinga ya mwili, hasira, na hata msongo wa mawazo. Unaweza kufanya nini? Ingawa huwezi kumlazimisha kijana wako ahisi usingizi kabla ya kuwa tayari, unaweza kuongeza uwezekano wa kupata usingizi mzuri mara tu atakapoweka kichwa chake kwenye kitanda kwa kuweka mipaka ya matumizi ya vifaa vya dijitali. Ingawa vijana na teknolojia huenda pamoja, ni muhimu kuweka mipaka ya busara inayofaa kwa familia yako. Zungumza na kijana wako kuhusu mipaka unayoweka, na eleza kwa nini hili ni muhimu kwa afya na ustawi wake. Kuna faida nyingi za kuwa na vijana wanaoelewa teknolojia, hivyo hakuna haja ya kuacha kabisa! Lenga kuwa na usawa wa kiafya kati ya muda wa kuvitumia na shughuli nyingine. Badilisha mazingira Vijana wengi wana kifaa kimoja au zaidi cha kielektroniki katika chumba chao cha kulala. Wengine wana zaidi ya vinne. Vifaa hivi vinaweza kuwa visumbufu na kuchochea akili. Hamisha baadhi ya vifaa vya teknolojia kwenye chumba kingine ili chumba cha kulala kitumiwe kwa kulala pekee. Himiza kijana wako kufanya kazi za shule zinazohusiana na kompyuta mapema jioni. Kujifunza kusimamia muda kutaboresha usingizi na pia kutasaidia mtoto wako kufanikiwa shuleni.
RAIS William Ruto ameapa kutopeana mamlaka kwa kiongozi yeyote aliye upinzani kwa sasa akisema wote wamechanganyikiwa na hawana ajenga kwa nchi. Rais Ruto amesema Upinzani wanatafuta kitu kimoja tu, yaani kumwondoa mamlakani bila mipango yoyote mahsusi kwa manufaa ya Wakenya na maendeleo kwa nchi. Nimeona ajenda yao kuu ni ‘Ruto must go’. Hakuna kingine. Sasa, ‘Ruto must go’ itasaidiaje Wakenya wanaokumbwa na changamoto za matibabu, elimu na matatizo mengine? akauliza alipohudhuria ibada ya kanisa katika Shule ya Kivaywa, Lugari.
MAAFISA ugani walioajiriwa kupitia programu ya kilimo ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) Mkoani Mtwara wameeleza mkakati wao wa kufanikisha lengo la serikali kuzalisha korosho tani 700,000 mwaka 2025/2026. Maafisa hao waliajiriwa na Bodi ya Korosho Nchini (CBT) kupitia programu ya BBT ili kutoa huduma za kilimo, elimu na mbinu za kisasa kwa wakulima wa korosho…
MIAKA mitatu tangu Rais William Ruto aingie madarakani, sekta ya elimu ya juu nchini Kenya inakumbwa na mzozo mkubwa unaotishia ustawi wake. Kati ya ahadi sita kuu alizotoa kuhusu elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya kati katika kampeni yake ya uchaguzi mkuu wa 2022, ni moja tu iliyotekelezwa kikamilifu: kuidhinisha Open University of Kenya. Ahadi tano zilizobaki — ikiwemo kuanzisha Baraza la Kitaifa la Ujuzi na Ufadhili litakalounganisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB), TVET na Hazina ya Vyuo Vikuu; ujenzi wa vyuo vya TVET katika maeneo bunge 52; na kuanzisha mpango wa kitaifa wa mafunzo kwa wahitimu, bado hazijatekelezwa au zimekwama kutokana na changamoto za kisheria, kifedha au mipango. Ahadi yenye utata zaidi ni kuhusu mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya juu ulioanzishwa miezi michache baada ya Rais Ruto kuapishwa. Mfumo huu uligawanya wanafunzi katika makundi matano ya uhitaji wa kifedha, kuanzia kundi la kwanza (wenye mahitaji makubwa zaidi) hadi kundi la tano (walio na mahitaji madogo zaidi na kutoa ufadhili kulingana na uhitaji. Mfumo huu umekosolewa kwa kukosa uwazi na ushirikishaji katika hatua za kuundwa kwake. Rais aliteua kamati maalum kuupitia upya lakini ripoti yake haijatangazwa hadharani. Mahakama Kuu pia imesema unakiuka Katiba, jambo lililozua sintofahamu zaidi.Wakati huo huo, sekta ya elimu ya juu inakumbwa na nakisi kubwa ya kifedha. Kulingana na Waziri wa Elimu Julius Ogamba, vyuo vikuu 23 vya umma vimetangazwa kufilisika. Kwa jumla vinadaiwa madeni ya jumla ya Sh72.2 bilioni huku Chuo Kikuu cha Nairobi kikiongoza kwa deni la zaidi ya Sh13 bilioni. Vyuo vingine vilivyo na madeni makubwa ni Kenyatta, Moi na Technical University of Kenya.Ukosefu wa fedha si tatizo pekee. Mwanauchumi Dkt Samuel Nyandemo anasema usimamizi mbovu na uongozi dhaifu umechangia zaidi matatizo haya.Anapendekeza kupitiwa upya mfumo wa ufadhili, kushirikiana na sekta ya kibinafsi, na kurekebisha karo ili kuziba pengo la kifedha.Wakati huo huo, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB) pia inakabiliwa na mgogoro. Bajeti yake ya sasa ya Sh41.1bilioni dhidi ya Sh76.3 bilioni zinazohitajika kufanikisha mfumo mpya wa ufadhili, na kuacha pengo la Sh35.1 bilioni.Mgogoro huu pia umelemaza shughuli za vyuo vikuu. Chuo Kikuu cha Moi kilifungwa kwa miezi mitatu kutokana na migomo ya wafanyakazi na kucheleweshwa kwa mishahara. Serikali ililazimika kuingilia kati kwa kutoa Sh2.9 bilioni ili kurejesha hali ya kawaida. Hata hivyo, hatua kama hizi za dharura haziwezi kutatua matatizo ya kimsingi yaliyo katika mfumo.Mwezi Mei 2025, Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei alitangaza marufuku ya miradi mipya katika vyuo 23 vilivyo katika hali ya kufilisika. Ukaguzi wa kina wa kifedha unaendelea ili kubaini matumizi mabaya ya rasilmali.Waziri Ogamba, alipozungumza na kamati ya bunge mwezi Machi, alikiri kuwa hali ya hatari ya kifedha kwenye vyuo vikuu na kuhusisha changamoto hizo na kucheleweshwa kwa bajeti na uongozi mbovu.
KOROGWE: KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ali ussi amewataka wakandarasi waliopewa kazi za miradi ya kimkakati ya maendeleo kuitekeleza kwa viwango vyenye ubora hatua ambayo inalenga kujibu changamoto za wananchi. Kauli hiyo ameitoa wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Amani katika eneo la…
IRINGA: WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, amesema kuwa Tanzania ipo katika mchakato wa mageuzi makubwa ya teknolojia, ambapo serikali imejizatiti kuhakikisha elimu ya Tehama inakuwa nyenzo muhimu ya maendeleo kwa vijana wa kitanzania hususan walioko mashuleni. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara za kompyuta katika Shule ya Sekondari Nyalumbu, wilayani Kilolo…
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameitaka mikoa na wadau wa elimu kuendelea kuongeza tahasusi katika shule za kidato cha tano hususani za masomo ya sayansi. Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano, vyuo vya elimu…
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza kuwachagua wanafunzi 214,141 wenye sifa za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka wa masomo 2025. Idadi hiyo inajumuisha wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalumu na kwamba uchaguzi huo umezingatia vigezo vya ufaulu, sera ya elimu,…
Katika kipindi cha miaka minne, bajeti ya mikopo ya elimu imepanda kutoka shs bilioni 464 (2020/2021) hadi shs bilioni 787 (2024/2025). Kwa mwaka mpya wa masomo wa 2025/2026, bajeti iliyoidhinishwa imefikia shs bilioni 916.7, ikiwa ni ishara ya dhamira ya Serikali ya kuwekeza zaidi katika elimu. Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.…
SERIKALI imetangaza kuwa miongozo ya mikopo ya elimu kwa mwaka wa masomo 2025/2026 itapatikana katika lugha za Kiingereza na Kiswahili kwenye tovuti za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz*) na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (*www.heslb.go.tz). Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ametoa tangazo hilo…
MTWARA: MAOFISA ugani 569 mkoani Mtwara wanatarajia kupatiwa mafunzo kuhusu matumizi sahihi na salama ya viuatilifu vya zao la korosho katika msimu wa kilimo mwaka 2025/2026. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele, Bakari Kidunda amesema uzalishaji wa korosho umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ambapo moja…
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kutekeleza mikakati endelevu ili kuwapa fursa viongozi wapya na wabobezi kuonesha uwezo na ubunifu katika taasisi za elimu ya juu. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo ya viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne…
DAR ES SALAAM: HUDUMA ya afya ya kinywa na meno nchini imeendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali baada ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kupokea mashine mbili za huduma hiyo kutoka kwa Taasisi ya Foshan DYM Medical Instrument CO.,LTD ya China. Akizungumza leo Juni 4, 2025 jijini Dar es Salaam, Ferdinand Machibya,…
ARUSHA: SERIKALI imeanzisha mfumo wa kidigiti wa udhibiti ubora wa shule kwa viongozi wa elimu ili kuongeza ufanisi, uwazi, uwajibikaji na kuimarisha ukusanyaji, uchambuzi na utoaji wa mrejesho wa tathmini za shule kwa wizara na wadau wa elimu. Aidha, mfumo huo pia utawezesha utunzaji na uchakataji wa taarifa kwa urahisi na kwa wakati hivyo ni…
ARUSHA: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ‘Vodacom’ na Taasisi ya Twaweza wamesaini mkataba wa makubaliano kuwezesha walimu kutoa mbinu kwa wanafunzi kwa ajili ya kuwezesha ongezeko la ufaulu shuleni. Akisaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu na Uboreshaji Mitaala, Angela Katabazi kwa niaba ya Mkurugenzi wa TET Dk,…
TUME ya Kuajiri Walimu (TSC) imemteua Eveleen Mitei kama Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji huku Dkt Nancy Macharia, ambaye anatazamiwa kustaafu Juni 30, 2025 akianza likizo yake. Dkt Macharia alitangaza kuwa ameanza likizo yake ya mwisho, akiondoka rasmi kabla ya kustaafu kwake Juni 30, 2025. Kuondoka kwake kunaashiria mwisho wa uongozi wake katika Tume hiyo, ambapo alihudumu katika nyadhifa mbalimbali na kusimamia mageuzi makubwa ya sekta ya elimu nchini Kenya. "Ninaendelea na likizo kuanzia leo Juni 1, 2025, nikisubiri kustaafu kwangu kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu mnamo Juni 30, 2025, baada ya kuitumikia Tume katika nyadhifa mbalimbali. Wakati huo huo, kumbuka kuwa Tume imemteua Bi Eveleen Mitei, kuwa kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume wakati akisubiri uteuzi wa mrithi wangu." Haya yanajiri baada ya Mahakama ya Ajira na Mahusiano mjini Mombasa kutoa maagizo ya muda ya kusimamisha shughuli ya kuajiri Afisa Mkuu Mtendaji mpya wa TSC. Hatua hii ilichukuliwa kujibu ombi lililowasilishwa na mkazi wa Mombasa, Thomas Mosomi Oyugi, ambaye anadai shughuli ya kuajiri watu imekumbwa na ukiukaji wa katiba na inatawaliwa na vigezo vya ubaguzi. Katika ombi hilo, mlalamishi alidai kuwa mchakato mzima wa kuajiri haufuati katiba na kwamba unatawaliwa na ubaguzi. Katika notisi iliyochapishwa katika MyGov mnamo Mei, TSC ilialika waliohitimu kutuma maombi ya kazi. Jukumu hilo linahusisha kusimamia mwelekeo wa kimkakati wa tume na kusimamia shughuli zake za kila siku. Mkurugenzi Mtendaji ajaye atahudumu kwa muda wa miaka mitano kulingana na Kifungu cha 16 cha Sheria ya TSC. Pia wanatakiwa kutimiza matakwa ya Sura ya 6 ya Katiba na kuwa na uzoefu wa angalau miaka kumi katika sekta ya elimu, utawala na usimamizi, utawala wa umma, rasilimali au usimamizi wa fedha.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Juni 03 ni mgeni rasmi katika jukwaa la vijana na mazingira linalofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jukwaa hilo la vijana na mazingira lina malengo ya kuwaunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya mazingira pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya…
WANAFUNZI wa Gredi ya Tisa watajiunga na shule za sekondari mwaka ujao kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa kuwasajili wanafunzi maarufu kama KEMIS. Serikali imebuni mfumo huo wa kieletroniki kuhakikisha wanafunzi wote walioko Gredi ya Tisa wanajiunga na shule za sekondari. Katibu katika Wizara ya Elimu Prof Julius Bitok alitangaza kuwa wanafunzi milioni 1.2 walioko Gredi ya Tisa watajiunga na Gredi ya 10 katika shule za sekondari mwakani. Mfumo huo wa kieletroniki uliovumbuliwa wiki iliyopita jijini Nairobi utanakili wanafunzi wote nchini kwanzia chekechea, shule za msingi, shule za upili, taasisi za kiufundi na vyuo vikuu. “Tutatumia mfumo mpya wa KEMIS kuhakikisha wanafunzi wote walioko Gredi ya Tisa wanajiunga na Gredi ya 10 bila yeyote kuachwa nyuma. Tunatarajia wanafunzi 1.2 milioni wajiunge na shule za upili na kila kitu kiko tayari,” akasema Profesa Bitok. Akiongea kwenye sherehe za kutuza wanafunzi bora katika shule ya upili ya Baringo, Prof Bitok alisema kila mtoto atapata nafasi katika shule za sekondari. Hii ni licha ya kuwa na shule chache za sekondari nchini. Kulingana na takwimu katika wizara yake kuna shule 10,000 za sekondari na wazazi wameanza kueleza wasiwasi wao huku idadi ya wanafunzi ikiwa kubwa ikilinganishwa na shule za sekondari. Wazazi wanahofu kuwa huenda kukawa na msongamano mkubwa katika shule za sekondari. Prof Bitok alisema Rais William Ruto amewekeza katika sekta ya elimu na kuhakikisha inapokea bajeti kubwa. “Rais ameipa kipaumbele sekta ya elimu, anataka kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora ndio maana serikali yake imeweka kila mikakati ya kuhakikisha watoto wote wanajiunga na shule za sekondari bila changamoto zozote,” alisema Prof Bitok. Awali wizara hiyo ilikuwa ikitumia mfumo wa NEMIS kuchukua takwimu ya wanafunzi katika shule za umma ndiposa itume mgao wa fedha za elimu ya bure. Hata hivyo, KEMIS sasa itachukua nafasi ya NEMIS. “Mfumo huu utasaidia pakubwa kufuatilia maendeleo ya mtoto akiwa chekechea hadi pale atakapoachia ama kumalizia masomo yake,” akaongeza Profesa Bitok. Haya yanajiri siku kadhaa baada ya Kamati ya Bunge inayosimamia Elimu ikiongozwa na mwenyekiti wake Julius Melly kuunga mkono mfumo huo akiitaka wizara hiyo kuhakikisha inanakili wanafunzi wote kote nchini. “Lazima mfumo huu wa kieletroniki ufanye kazi, awali washikadau katika sekta ya elimu walikuwa wanalalamika kuhusu NEMIS wakisema siyo wanafunzi wote walinakiliwa. Tunataka KEMIS ifanye kazi vizuri,“ akasema Bw Melly. Kwa muda wa miaka mitatu sasa walimu wakuu wamekuwa wakilalamika kuhusu mfumo wa NEMIS ambao ulizuia wanafunzi wengi kukosa mgao wa fedha za elimu ya bure. Ili unakiliwe kwenye NEMIS lazima uwe na cheti cha kuzaliwa, hata hivyo wanafunzi wengi hawana stakabadhi hiyo huku walimu wakuu wakiisihi serikali kunakili vidole badala ya cheti hicho.
MOROGORO: WAKULIMA wa vijiji vinne vya Mkoa wa Morogoro wameanzisha miradi ya uchakataji maziwa yanayotokana na mbegu za soya kwa lengo la kuongeza wigo mpana unywaji maziwa kwenye jamii na kwa wanafunzi wa shule za msingi. Mratibu wa Mradi wa Ushirikiano kati ya Mkoa wa Morogoro na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Waziri Mahimbo…
IRINGA: Sekta ya usafirishaji nchini imezidi kupata mwelekeo mpya baada ya Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT) kuzindua rasmi ofisi yake ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mjini Iringa, tukio lililoambatana na mkutano wa mwaka wa usafiri na usafirishaji uliowakutanisha wadau muhimu serikalini na binafsi. Uzinduzi huo uliambatana na utoaji wa elimu kwa wanachama na…
Serikali imetangaza mpango wa kuajiri walimu 40,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2026 ili kuimarisha uwiano kati ya walimu na wanafunzi katika shule za umma. Katibu wa Elimu ya Msingi, Julius Bitok, amesema walimu 24,000 wataajiriwa mwaka huu na walimu wengine 16,000 kuanzia mwaka ujao. Hii ni sehemu ya ahadi ya serikali kuajiri walimu 116,000 katika kipindi cha miaka mitano. Kamati ya Bunge kuhusu Elimu imeshauri Sh1.3 bilioni zitolewe katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 ili kubadilisha walimu wanagenzi 20,000 kuwa wa kudumu kuanzia Julai. Awali, Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) ilieleza kuwa haikuwa imetengewa fedha za kuajiri walimu hao baada ya muda wao kumalizika. TSC imesema kuna upungufu mkubwa wa walimu 98,261 nchini, hali inayotarajiwa kuwa mbaya zaidi ifikapo 2026 wakati shule za sekondari pevu zitakapoanzishwa. Aidha, kuna walimu 343,485 waliosajiliwa lakini bado hawajaajiriwa, wakiwemo walimu wa shule za msingi, sekondari na wale wa chekechea. Waziri wa Elimu Julius Ogamba ameeleza kuwa uajiri wa walimu unategemea bajeti, upatikanaji wa fedha na nafasi zilizopo. Alisisitiza kuwa mpango wa mafunzo kwa walimu wasio na ajira umeimarisha ujuzi wa vitendo kwa walimu 94,300. Katika miaka ya fedha 2022/2023 hadi 2024/2025, walimu 68,313 waliajiriwa kufundisha katika shule za msingi, wakiwemo wa kudumu na wa kandarasi. Hata hivyo, idadi ya walimu katika shule za msingi za umma ilipungua kwa asilimia 3.2 mwaka 2024, licha ya ongezeko la wanafunzi katika shule zote. Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Shule ya Baringo, Katibu wa Elimu ya Msingi, Julius Bitok, alitangaza kuwa serikali itaajiri 24,000 walimu mwaka huu na 16,000 zaidi mwaka ujao, ili kutimiza ahadi ya kuajiri walimu 116,000 ndani ya miaka mitano chini ya mpango wa Kenya Kwanza. Mwaka jana, walimu wa shule ya msingi walioajiriwa kwa kandarasi 39,550 walibadilishwa kuwa wa kudumu, na wengine 8,378 walihamishiwa kufundisha shule za sekondari msingi. Kulingana na Ripoti ya Uchumi ya 2025, usajili wa wanafunzi umeongezeka katika viwango mbalimbali vya elimu: Wanafunzi wa chekechea waliongezeka hadi milioni 2.914 mwaka 2024 kutoka milioni 2.885 mwaka 2023. Shule za msingi na sekondari msingi idadi ya wanafunzi iliongezeka kwa asilimia 3.2 hadi kufikia wanafunzi 10,733,300 mwaka 2024. Katika shule za sekondari idadi ya wanafunzi iliongezeka kwa asilimia 5.2 hadi wanafunzi 4,321,600 mwaka huo huo. Hata hivyo, idadi ya walimu katika shule za msingi za umma ilipungua kwa asilimia 3.2 hadi 212,602 mwaka 2024. Kwa upande mwingine, walimu katika shule za sekondari za umma na vyuo vya walimu waliongezeka kutoka 125,563 mwaka 2023 hadi 130,818 mwaka 2024.
ARUSHA: MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Za Kulevya (DCEA) Kanda yaa Kaskazini kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro wametoa elimu na kuunda mikakati ya pamoja kudhibiti dawa za kulevya. Kwa mujibu wa Ofisa Elimu Jamii kutoka DCEA, Shabani Miraji amesema lengo ni kushirikisha viongozi hao ni kuhamasisha…
MOROGORO: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imebaini utekelezaji hafifu usiokidhi viwango miradi 12 ya maendeleo ikiwemo ujenzi, afya na elimu yenye thamani ya Sh bilioni 1.26. Mkuu wa Takukuru mkoa huo ,Pilly Mwakasege amesema hayo kupitia taarifa yake kwa waandishi wa habari ambayo iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu…
CHUO Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimefanya kongamano lake la nne la kimataifa likiwaleta pamoja wataalamu, watafiti, wanataaluma na wadau kutoka ndani na nje ya nchi. Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Method Samwel amesema lengo la kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili lilikuwa ni kuwasilisha tafiti bunifu, kubadilishana uzoefu na kujadili masuala muhimu ya…
TANGA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Tanga imebaini mapungufu katika miradi ya maendeleo 12 ya maji, afya na elimu yenye thamani ya Sh bilioni 5.4. Akitoa taarifa ya utendajikazi wa taasisi hiyo katika kipindi Januari hadi Machi mwaka huu leo Mei 30, 2025, Naibu Mkuu wa Taasisi hiyo mkoani hapa, Marium…
DAR ES SALAAM: WAFANYAKAZI kutoka taasisi mbalimbali wametakiwa kupata elimu namna ya kudhibiti vihatarishi katika maeneo ya kazi ili kutimiza majukumu yao katika mazingira yenye usalama. Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk Jerome Materu amekiri kuwa maeneo mengi ya kazi kuna vihatarishi ila wanaweza wasione athari…
JUMLA ya wanafunzi 156,201 wamenufaika na ufadhili wa elimu kuanzia sekondari hadi shule ya upili kupitia Mpango wa ufadhili wa kwa wanafunzi wa kike chini ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali CAMFED Tanzania. Akizungumza leo Mei 29 Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa CAMFED, Nasikiwa Duke, amesema shirika hilo limelenga kusaidia watoto wa kike wanaotoka mazingira…
DAR ES SALAAM– TIMU ya mchezo wa Rugby au Raga ya DAR Leopards inatarajia kuumana na Les Gaulois de Nairobi kutoka Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kujenga mahusiano. Pambano hilo litafanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Jumamosi ya Mei 31, 2025. Akizungumza na Dailynews Digital, Katibu Mkuu wa Chama…
WAZAZI wa watahiniwa wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa mwaka huu sasa wamepata afueni baafa ya Bunge la Kitaifa kutenga Sh5.9 bilioni za mitihani hiyo katika shule za msingi, shule za sekondari msingi na sekondari pevu. Hii ni kufuatia kilio kutoka kwa wadau mbalimbali na Wakenya kwa ujumla baada ya makadirio ya awali ya bajeti kutotengea Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) fedha za kugharamia mitihani ya kitaifa katika shule zote. Mitihani hiyo itakayoanza kufanywa Novemba mwaka huu ni Mtihani wa Kitaifa wa Gredi ya Sita (KPSEA), Mtihani wa Kitaifa wa Sekondari Msingi (KJSEA) na Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE). Sasa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu imependekeza kutengwa kwa Sh5.9 bilioni kutoka mgao wa idara zingine ili kufadhili mitihani ya kitaifa. Pendekezo hilo sasa liko mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Bajeti (BAC). Haya yanajiri baada ya Waziri wa Fedha John Mbadi kutangaza kuwa serikali itaangalia upya mfumo wa usimamizi wa mitihani ya kitaifa na wale ambao serikali inapasa kuwalipa ada za mitihani ya kitaifa. “Tunapendekeza ugavi wa Sh5.9 bilioni za kugharamia usimamizi wa mitihani ya kitaifa, pesa ambazo hazikuwa zimetengwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026,” kamati hiyo ikasema kwenye ripoti yake kuhusu bajeti hiyo ya mwaka ujao wa kifedha. Pesa hizo zitapatikana kutoka mgao wa fedha za matumizi ya kawaida za Sekondari ya Msingi (Sh2 bilioni), Shule za Sekondari (Sh3 bilioni) na Shule za Msingi (Sh900 milioni). Bajeti ya jumla inayohitaji kufadhili mitihani ya kitaifa ya KPSEA, KJSEA na KCSE ni Sh12.58 bilioni. Makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa bungeni mwezi Aprili yalionyesha kuwa sekta ya elimu ilipunguziwa kima cha Sh62 bilioni. Vitengo mbalimbali katika sekta hiyo viliathirika kinyume na ilivyopendekezwa katika Taarifa ya Sera Kuhusu Bajeti (BPS). Kwa mfano, kulingana na makadirio hamna pesa zilizotengewa mitihani ya kitaifa na usimamizi wa mitihani hiyo ambayo kwa jumla inahitaji Sh12.5 bilioni. Aidha, Sh1.8 bilioni zilipunguzwa katika mgao wa kufadhili masomo katika shule za msingi za umma huku Sh21.85 bilioni zikiondolewa kwenye mgao wa fedha za kufadhili elimu katika shule za upili. Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu Julius Melly alikuwa ameapa kuwa kamati yake haingeandaa ripoti ya bajeti hadi fedha za mitihani zirejeshwe. IMETAFSIRIWA NA CHARLES WASONGA
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa, Riziki Shemdoe ameutaka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA), kuandaa wahitimu watakaojiajiri na kuajiri wengine badala ya kusubiri kuajiriwa kama ilivyo hivi sasa. Prof Shemdoe ametoa kauli hiyo mjini Morogoro wakati akifungua kikao kilichokutanisha wadau wa kujadili rasimu ya mitaala mitano inayohuishwa na 12…