Top headlines and developing stories from Tanzania, Kenya, Uganda and the wider region, gathered from the leading local and international newsrooms and updated throughout the day.
By Dickson Omobola “Mayday, mayday”! Those are the words associated with pilots experiencing distress with their planes during flight and the words are usually uttered to air traffic controllers for help.The crash of a Nigerian Air Force, NAF, ATR-42 aircraft, a twin-engine turboprop configured for intelligence, surveillance and reconnaissance, ISR, operations, has raised fresh questions […]
By Adeola Badru The National Association of Nigerian Students (NANS) has raised concerns over the safety of students and other commuters using the Owo–Benin, Akure–Owo and Ilesa roads, urging improved attention to federal road infrastructure across the South-West. The association expressed the concerns after its nationwide federal roads project tour, during which its delegation inspected […]
Raila Odinga alikuwa zaidi ya kiongozi wa chama cha ODM. Kwa wanasiasa waliotembea naye kwa miaka mingi, alikuwa mshauri, rafiki, mzalendo na mwavuli uliowapa nafasi watu wenye misimamo tofauti kufanya kazi pamoja. Mwaka mmoja baada ya kifo chake, viongozi waliokuwa karibu naye wanakumbuka ujasiri wake, uwezo wake wa kujenga miungano na alivyoshawishi mijadala ya kisiasa na kuathiri mwelekeo wa serikali. Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi anasema kifo cha Raila kilikuwa pigo kubwa kwake, kwani alipoteza mtu aliyekuwa amesafiri naye kwa miaka mingi kisiasa. Wandayi alipokea habari za kifo cha Raila asubuhi ya Oktoba 15, 2025, akiwa ndani ya ndege kuelekea Kitui kuungana na Rais William Ruto katika ziara ya maendeleo. Alipigiwa simu na mtu aliyewafahamu wote wawili, kisha akapigiwa na Seneta Oburu Oginga, aliyethibitisha habari hizo za kusikitisha. Wandayi anasema Raila hakuwa tu kiongozi wa chama, bali pia rafiki, mshauri na dira yake ya kisiasa. Anakumbuka kuwa alipoamua kujiunga na Baraza la Mawaziri la Rais Ruto Agosti 2024, alifanya hivyo akiwa na imani kuwa Raila alikuwa amemuunga mkono. Uamuzi huo ulimfanya aachane na wadhifa wa Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, ambao ulimpa nafasi muhimu ya kuongoza upinzani bungeni. Kwa Wandayi, hatua hiyo ilikuwa ishara ya imani ambayo Raila alikuwa nayo kwake. Anasema kifo cha Raila kilifichua changamoto ya urithi wa kisiasa ndani ya ODM, huku viongozi wakishindania nafasi ya kuongoza chama. “Raila hakuwa mwanasiasa wa kawaida. Alikuwa na uwezo wa kusoma mikondo ya kisiasa, kuweka ajenda ya taifa na, muhimu zaidi, kujenga miungano,” anasema Wandayi. Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Kitaifa John Mbadi anakumbuka mazungumzo yake ya mwisho na Raila katika Nairobi Club, siku chache kabla ya kiongozi huyo kusafiri kwenda India kwa matibabu. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohamed na aliyekuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Mbadi alikuwa amewasilisha hali ya uchumi katika mkutano wa mwisho wa wabunge uliohudhuriwa na Raila. Walikutana tena kujadili uchumi na fedha za kaunti, huku Raila akimtaka Mbadi kushauriana na Profesa Hiroyuki Hino kuhusu madeni ya nchi. “Hakikisha Ruto anafanikiwa, nasi tutakusaidia,” Mbadi anakumbuka Raila akimwambia. Mbadi anasema Raila alitaka Rais Ruto afanikiwe katika mipango yake, ikiwemo Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) na mradi wa nyumba za gharama nafuu. Anamtaja Raila kama mzalendo aliyekuwa tayari kuweka kando azma yake binafsi kwa maslahi ya nchi. Pia alikosoa serikali ikikosea na kuisifu ikifanya jambo linalofaa. Hata hivyo, viongozi hao wanakiri kuwa ODM inakabiliwa na changamoto ya kudumisha umoja bila kiongozi huyo. Mbadi anataka viongozi washauriane zaidi na kuhakikisha chaguzi za mchujo zinafanyika kwa uwazi. Wandayi anasema chama kinapaswa kuimarisha taasisi zake, kuheshimu maoni tofauti na kuzuia azma za kibinafsi kusigeuka kikwazo cha maendeleo. Kwao, urithi wa Raila hauishii katika ODM. Maisha yake yalihusishwa na mapambano ya demokrasia ya vyama vingi, mageuzi ya Katiba, ugatuzi na uhuru wa kisiasa. Ingawa hayupo tena, Wandayi anasema kizazi cha sasa kitahukumiwa kwa namna kitakavyotumia nafasi ya kisiasa aliyoisaidia kuunda.
Nairobi, Kisumu, Busia na Mandera ni miongoni mwa kaunti zilizo katika hatari kubwa ya kukumbwa na athari za mvua ya El Niño, kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Kukabiliana na Majanga (NDOC). Kati ya kaunti 18 zinazokabiliwa na uwezekano wa majanga kutokana na utabiri wa mvua nyingi kuliko kawaida, serikali imetambua kaunti hizo nne kuwa miongoni mwa zinazoweza kuathirika zaidi. Wakati huohuo, takriban watu milioni 1.5 wanatarajiwa kuathiriwa na mvua hiyo, huku serikali ikikadiria kuwa watu 500,000 wanaweza kulazimika kuhama makazi yao. Mkurugenzi wa NDOC, Kanali David Samoei, alisema serikali imepatia kaunti hizo nne kipaumbele na inaendeleza hatua za kuzuia au kupunguza athari za majanga yanayoweza kutokea. Alisema serikali imekuwa ikijiandaa tangu Idara ya Hali ya Hewa nchini itoe tahadhari kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua nyingi kuliko kawaida katika kipindi cha Oktoba, Novemba na Desemba. “NDOC imeangazia zaidi Nairobi na kufanya mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga. Kaunti ya Kisumu pia huenda ikaathirika zaidi kutokana na Mto Nyando, na kwa sasa tunafanya kazi katika kingo za mto huo,” alisema Kanali Samoei. Aliongeza kuwa Busia huenda ikaathirika kutokana na Mto Nzoia na eneo la Budalangi, ambako maafisa wa serikali wanaendelea na maandalizi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Rasilimali za Maji. “Mandera inaweza kukumbwa na changamoto iwapo barabara inayounganisha Mandera na Wajir itafunikwa na maji ya mafuriko,” alisema. Kanali Samoei alisema serikali imejiandaa vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na El Niño na hatua za usalama zinazopaswa kuchukuliwa. Alisema NDOC imeratibu vituo vya uokoaji na makazi salama na serikali za kaunti, ambavyo vitatumika iwapo majanga yatatokea. “Tunathibitisha kuwa Idara ya Hali ya Hewa imekuwa ikitoa utabiri sahihi katika siku za hivi karibuni. Kwa hivyo, tulichukulia tahadhari yake kwa uzito na kuanza maandalizi. “Tumeendesha mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga katika maeneo ya Nairobi, Garissa na Naivasha. Lengo letu ni kuhakikisha hakuna maisha yatakayopotea katika kipindi hiki kwa kuchukua hatua mapema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa idara hiyo,” alisema. Kanali Samoei alikuwa akizungumza katika kongamano la siku tatu lililofanyika Nakuru, lililowaleta pamoja wataalamu na wadau kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na majanga. Waliohudhuria ni pamoja na mashirika ya kibinafsi, taasisi na mashirika ya serikali pamoja na wasomi, ambao walitarajiwa kubadilishana mawazo kuhusu maandalizi ya kukabiliana na majanga. Baada ya kongamano hilo, washiriki wataadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari za Majanga (IDDRR) Oktoba 13. Kanali Samoei aliwahakikishia wananchi kuwa serikali inachukua hatua za kulinda usalama wao, huku akiwashauri kufuata miongozo itakayotolewa mara kwa mara na kamati ya usimamizi. “Serikali imetenga rasilimali za kutosha kukabiliana na majanga hayo, huku ikitarajia pia kupata msaada kutoka kwa washirika na sekta ya kibinafsi iwapo kutatokea tatizo,” alisema. Naibu Gavana wa Nakuru, David Kones, aliyeshiriki kongamano hilo, alisema serikali ya kaunti imekuwa ikielimisha wakazi kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za kuzuia majanga kuanzia ngazi ya familia.
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anapania kujenga vuguvugu jipya la kisiasa linalozingatia Katiba, uwajibikaji na uchumi unaowajali wananchi, huku akijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Chama chake kipya, The Equitable Party (TEP), kinatarajiwa kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kufuatia uamuzi wa Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) mnamo Oktoba 8, 2026. Mbali na jina, chama hicho kinapanga kubadilisha katiba yake, rangi rasmi, nembo na kuhamisha makao makuu yake. Hatua hizo zinaashiria juhudi za Bw Sifuna kujijenga upya baada ya kutengana na ODM alikohudumu kama katibu mkuu kwa karibu miaka kumi. Hata hivyo, msimamo wake kuhusu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua mwaka 2024 unaweza kuibua maswali anapojaribu kuunganisha upinzani dhidi ya Rais William Ruto. Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi Ijumaa, Bw Sifuna alitetea jukumu lake katika mchakato huo, akisema haupaswi kuzuia viongozi waliokuwa na tofauti kushirikiana katika uchaguzi ujao. Alipoulizwa jinsi atakavyoshirikiana na Bw Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha DCP, alisema: “Tayari nilimuondoa madarakani kwa makosa yake. Kwa hivyo, hamuwezi kuniuliza maoni yangu kuhusu makosa ambayo tayari nilimwadhibu.” Bw Gachagua ametangaza kuwa yuko tayari hata kuwa naibu wa Bw Sifuna ikiwa upinzani utaamua kuwa seneta huyo ndiye anayefaa zaidi kumshinda Rais Ruto. Hata hivyo, amewahi kuwakashifu viongozi wa Mlima Kenya walioshiriki kumuondoa madarakani, akiwataja kuwa wasaliti. Bw Sifuna hakutaja chama atakachoungana nacho wala kueleza namna mgombea mmoja wa upinzani atakavyochaguliwa. Alisema mazungumzo hayo bado hayajafika wakati wake. “Subirini kwanza. Mazungumzo hayo yatafanyika baadaye sana,” aliwaambia wanahabari. Wakili Nelson Osiemo alisema Bw Sifuna atalazimika kueleza jinsi uamuzi wake kuhusu Gachagua unavyoendana na misingi ya kisiasa anayotaka kuweka mbele katika vuguvugu lake jipya. Bw Sifuna anasisitiza kuwa uwajibikaji na kuheshimu Katiba lazima viwe msingi wa uongozi. Alisema utendaji wa rais haupaswi kupimwa kwa miradi inayoonekana pekee, bali pia kwa namna serikali inavyofuata sheria. Akizungumzia deni la taifa na matumizi ya fedha za umma, alisisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikishaji wa wananchi na ukopaji unaofuata sheria. “Hauwezi kusema kwamba kwa sababu umejenga uwanja mzuri wa Talanta, basi tukupigie makofi. Hapana. Tunataka uwazi,” alisema. Msimamo huo unajiri baada ya miezi kadhaa ya migogoro ndani ya ODM kuhusu ushirikiano wake na serikali jumuishi pamoja na mwelekeo wa chama hicho baada ya kifo cha Raila Odinga. Bw Sifuna alisema alijaribu kupatanisha makundi hasimu lakini akahitimisha kuwa uongozi wa chama ulikuwa ukielekea upande ambao hangeweza kuutetea. Alikosoa ushirikiano wa ODM na UDA akisema unatishia uhuru wa chama, na pia akapinga mchakato wa kuondolewa kwake kama katibu mkuu. Hata hivyo, alisema hana kinyongo na aliyekuwa wenzake na anaiachia hatima ya ODM kwa wapigakura. Alisema timu yake pia inatayarisha sera za kupunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi. Katika elimu, anataka data sahihi za wanafunzi, shule na walimu ili kuimarisha usimamizi wa fedha, huku katika afya akipendekeza hospitali zilipwe madai halali kwa wakati na hatua zichukuliwe dhidi ya madai ya ulaghai. Alisema manifesto ya vuguvugu hilo inaandaliwa kwa usaidizi wa wataalamu na itakaguliwa kabla ya kuchapishwa. Bw Sifuna alisema ataruhusu wapigakura kuamua mustakabali wa ODM katika uchaguzi wa Agosti 11, 2027.
Juhudi za Kalonzo Musyoka kubadilisha jina na muundo wa muungano wa Azimio la Umoja kuwa The Ukombozi Alliance (TUA) zinaweza kumweka katika nafasi nzuri ya kuwania urais kwa tiketi ya upinzani au kumtenga na viongozi wengine kuelekea uchaguzi wa 2027. Kalonzo, ambaye anaongoza chama cha Wiper, amekuwa mstari wa mbele katika kuunda upya muungano huo baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyekuwa kiongozi wake. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wanapinga kujiunga na TUA, wakisema wanataka kuhifadhi utambulisho wa vyama vyao na kuunda muungano mpya. Chama cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna vimeonyesha kusitasita kujiunga na TUA. Bw Sifuna alisema chama chake kipya, The Equitable Party, kinapanga kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu miungano. “Kwa sasa chama changu kinafanyiwa mabadiliko makubwa. Tuna miundo ya kuweka na makataa ya Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Kisiasa ya kuzingatia. Mazungumzo kuhusu miungano yatakuja baadaye,” alisema. Kalonzo naye amewataka wabunge wa Wiper walioonekana kushirikiana na Bw Sifuna kuzingatia shughuli za chama chao. Alitaja Mbunge wa Kaiti Joshua Kimilu na mwenzake wa Wundanyi Danson Mwashako. Hali hii inaashiria ushindani wa kutafuta uungwaji mkono mashinani na udhibiti wa vyama huku viongozi wakijaribu kuungana kumuondoa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu ujao. Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema chama hicho hakina haraka ya kujiunga na TUA, akisema upinzani unahitaji mawazo mapya. Alisema baadhi ya wanasiasa waliounga mkono mgombea wa Azimio katika uchaguzi wa 2022 walipata hasara kisiasa katika maeneo yao, na hawako tayari kujitolea tena kwa mpangilio kama huo. Hata hivyo, viongozi wa Democratic Party Justin Muturi na wa DAP-K Eugene Wamalwa wameunga mkono TUA kama chombo kinachoweza kumshinda Rais Ruto. Wote wamekuwa wakifanya kampeni pamoja na Kalonzo, ambaye wanamchukulia kama mgombeaji anayefaa kupewa tiketi ya urais. Mzozo huo unatokana na kipengele cha makubaliano ya muungano ambacho awali kilionekana kumpa kiongozi wa chama nafasi ya moja kwa moja kuwa mgombea urais. Washirika wa Kalonzo wanasema kipengele hicho kimebadilishwa na sasa wanachama wote wanaweza kuwania tiketi hiyo. Kalonzo pia amesisitiza kuwa kujiuzulu kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama mwenyekiti wa baraza la muungano hakujasababisha pengo la uongozi ndani ya TUA. Kuna juhudi za kumshawishi Bw Gachagua achukue nafasi ya Bw Kenyatta ili kuvutia DCP kujiunga na muungano huo. Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye anahusishwa na Linda Mwananchi, pia ametajwa kama anayeweza kupewa nafasi hiyo ili kuvutia wafuasi wa Nyanza. Hata hivyo, Mbunge wa Gatanga Edward Muriu, mshirika wa Bw Gachagua, alisema DCP inataka kwanza kuimarisha uungwaji mkono wake kabla ya kujadiliana na vyama vingine kuunda muungano mkubwa. Mchambuzi wa siasa Profesa David Monda alisema TUA inaweza kuwa vigumu kupata uungwaji mkono wa kutosha bila kuwashirikisha Kalonzo, Sifuna, Gachagua na aliyekuwa Waziri wa utawala wa ndani Fred Matiang’i katika mpangilio mmoja. Alisema viongozi hao wanapaswa kuungana ili kumshinda Rais Ruto au kuhatarisha kushindwa kila mmoja akigombea urais kivyake. Wanaounga mkono TUA wanataka muungano huo uige mfano wa National Rainbow Coalition (Narc), uliomuingiza Mwai Kibaki mamlakani mwaka 2002. Chini ya mfumo huo, vyama havikuvunjwa lakini viliunga mkono mgombea mmoja wa urais na ajenda ya pamoja. Lengo ni kuzuia upinzani kugawanyika na kumpa Rais Ruto nafasi ya kushinda uchaguzi wa 2027.
KAULI ya Rais William Ruto kwamba wakulima wadogo wa chai wanapata wastani wa Sh56 kwa kilo ya majani imezua hasira, huku wakulima wakisema madai hayo hayaakisi hali halisi mashambani. Wakati huo huo, Mahakama Kuu Nairobi imewapa wakulima wa chai kutoka Nyamira na Kisii ruhusa ya kuwasilisha kesi ya mapitio ya uamuzi kuhusu malipo ya pili ya chai ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026, maarufu kama bonasi. Wanadai kuna ubaguzi, hesabu zisizoeleweka na ukiukaji wa Sheria ya Chai ya 2021. Wakulima katika kaunti za Nandi, Kericho, Bomet na Nakuru pia wameandamana kupinga bonasi ya kati ya Sh12.50 na Sh22 kwa kilo, ikilinganishwa na Sh50 zinazolipwa na baadhi ya viwanda eneo la Mlima Kenya. Rais Ruto alitoa kauli hiyo Alhamisi katika mkutano na wananchi wakati wa Kongamano la Mabadiliko ya Kilimo na Mifumo ya Chakula linalofanyika Nairobi. Alisema mageuzi katika sekta ya chai yameongeza mapato ya wakulima kutoka Sh34 kwa kilo miaka mitatu iliyopita hadi wastani wa Sh56 sasa. Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Chai nchini, Willy Mutai, alithibitisha takwimu hizo. Hata hivyo, mtaalamu wa kilimo na msemaji wa Chama cha Wakulima Wadogo wa Chai, Joseph Rono, alisema Rais anapaswa kupewa taarifa sahihi kuhusu malipo wanayopokea wakulima. “Huenda Rais alikuwa na nia njema kulingana na taarifa alizopewa. Lakini kuwaambia wakulima wanalipwa wastani wa Sh56, ilhali malipo ya majani ni Sh26 na bonasi wastani wa Sh17, na kufanya jumla kuwa kati ya Sh41 na Sh43 kwa kilo, ni kupotosha,” alisema. Aliuliza tofauti ya Sh13 kwa kilo inayotajwa na Rais inaenda wapi, akisema haionekani katika akaunti za wakulima wala stakabadhi zao za malipo. Alexander Rono, anayepeleka majani katika kiwanda cha Tirgaga, Bomet, alisema Shirika la Maendeleo ya Chai Kenya (KTDA) lilipandisha bei ya majani kutoka Sh23 hadi Sh26 kwa kilo mwezi Aprili, baada ya miaka miwili bila mabadiliko. Sekta hiyo ina takriban wakulima wadogo 700,000. Ukaguzi wa malipo ulionyesha viwanda vingi magharibi mwa Bonde la Ufa hulipa kati ya Sh22 na Sh26 kwa kilo, huku vile mashariki mwa bonde hilo vikilipa wastani wa Sh30. KTDA imekuwa ikihimiza viwanda kulipa angalau Sh26 kwa kilo. Tofauti hiyo inahusishwa kwa kiasi na ubora wa uchumaji. Mahakama Kuu ya Milimani imewaagiza wakulima wa Nyamira na Kisii kuwasilisha kesi yao kamili ndani ya siku saba, huku upande wa pili ukipewa siku 21 kujibu. Jaji Nabil Orina alitoa ruhusa ya kuwasilisha kesi dhidi ya Bodi ya Chai, KTDA Management Services, Waziri wa Kilimo na Mwanasheria Mkuu. Wakulima wanapinga tofauti inayodaiwa kufikia asilimia 470 katika bonasi kati ya viwanda vya mashariki na magharibi mwa Bonde la Ufa. Kwa mfano, viwanda vya Chebut na Kaptumo hulipa Sh12.50 kwa kilo, huku Rukuriri kikilipa Sh50. Katika kaunti ya Nandi, wakulima wa Chebut na Kaptumo waliandamana Kapsabet Alhamisi wakitaka mabadiliko ya uongozi wa viwanda na malipo bora. Kaptumo ililipa bonasi ya Sh12.50 kwa kilo kwa mwaka wa kifedha wa 2025/2026, kutoka Sh13 mwaka uliotangulia. “Bonasi inapaswa kuwa sawa katika maeneo yote yanayolima chai,” alisema Richard Rono, mkulima wa Chebut. Rukuriri iliyoko Mlima Kenya ililipa bonasi ya juu zaidi ya Sh50 kwa kilo, huku Momul magharibi mwa Bonde la Ufa ikilipa Sh34, kutoka Sh32.50 awali. Wakulima wanataka serikali na KTDA kutafuta masoko mapya na kupunguza kutegemea masoko yale yale ya nje ya nchi. Wanasema pia kupanda kwa gharama za pembejeo, usafirishaji na mafuta kunapunguza faida yao. John Tiony, mkulima kutoka Kapkangani, alisema serikali inapaswa kuongeza juhudi za kutafuta masoko mbadala ili wakulima wapate mapato bora. Chai ni mojawapo ya bidhaa kuu zinazoletea Kenya fedha za kigeni na chanzo muhimu cha mapato kwa familia nyingi. Hata hivyo, wakulima wanaonya kuwa gharama ya uzalishaji inapozidi mapato, wengi wanaweza kung'oa mimea yao ya chai. Taarifa za Vitalis Kimutai, Ruth Mbula na Barnabas Bii.
RAIS William Ruto amependekeza Kenya ipanue vyanzo vya maziwa kwa kujumuisha ngamia, mbuzi na kondoo baada ya upungufu wa maziwa ya ng’ombe kusababisha bei kupanda hadi Sh85 kwa lita katika baadhi ya maeneo. Rais alisema ukame wa hivi majuzi umeathiri uzalishaji wa maziwa, hivyo kuna haja ya kutafuta njia mbadala ili kukidhi mahitaji ya wananchi. “Tunahitaji kupanua vyanzo vyetu vya maziwa kutoka kwa ngamia, kondoo, mbuzi na hata nyati,” alisema Dkt Ruto na akawachekesha waliohudhuria mkutano alipotaja nyati. Akizungumza Ijumaa katika kufungwa kwa kongamano la siku tatu la Mabadiliko ya Kilimo na Mifumo ya Chakula 2026, lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Nairobi, Rais alimwagiza Katibu wa Mifugo Jonathan Mueke kuharakisha utafiti wa mifugo bora ya ngamia ili kuongeza uzalishaji. Alisema jamii za wafugaji zinahitaji kuungwa mkono kwa kuwa zina mifugo hiyo na maarifa yanayoweza kusaidia kukuza biashara ya maziwa ya ngamia, ambayo pia yana soko mijini. Ukaguzi wa Taifa Leo ulibaini kuwa lita moja ya maziwa ilikuwa ikiuzwa hadi Sh85 katika maeneo ya Kasarani, Githurai, Zimmerman, Kayole, Buruburu na Embakasi. Zimmerman, bei ilikuwa imepanda kutoka Sh75 hadi Sh85. Hata hivyo, Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe alipuuza madai ya uhaba mkubwa wa maziwa, akisema ni kupungua kwa ugavi.
WIZARA ya Elimu imepiga marufuku wanasiasa na watu wengine wenye nia ya kutoa misaada kutembelea shule na kuwagawia wanafunzi zawadi, ikionya kuwa huenda shughuli hizo zikatumiwa kujinufaisha kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Waziri wa Elimu Julius Ogamba alisema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia misaada shuleni kama njia ya kujipatia umaarufu na kuendeleza maslahi yao binafsi. Alisema ziara hizo pia huvuruga ratiba ya masomo na kuhatarisha haki za watoto, hasa pale picha zao zinapopigwa na kusambazwa mitandaoni bila idhini ya wazazi au walezi. Bw Ogamba alisema agizo hilo linatumika kote nchini, ingawa linatekelezwa kaunti moja baada ya nyingine. Katika barua iliyotumwa kwa maafisa wa elimu Nyamira, wakuu wa shule za upili, wizara ilisema baadhi ya watu wamekuwa wakitembelea shule, kutoa misaada midogo kisha kupiga picha na wanafunzi. “Tumeshuhudia watu wanaojitolea kutembelea shule na kuruhusiwa kuvuruga shughuli za masomo, kupiga picha na video za wanafunzi kwa sababu tu wametoa mchango mdogo,” ilisema barua iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Elimu Nyamira, Joshua Kaga. Wizara ilionya kuwa shule hazipaswi kutumiwa na wanasiasa kujitafutia umaarufu wakati wa msimu wa kampeni. Akizungumza katika Shule ya Upili ya Senator Kebaso wakati wa maandalizi ya mtihani wa KCSE, Bw Kaga alisema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwapa wanafunzi mikate na soda, kisha kuchapisha picha zao mitandaoni. Alisema tabia hiyo inakiuka miongozo ya elimu na huenda ikavunja sheria zinazolinda faragha za watoto. Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa Nyamira wamedai kuwa agizo hilo linalenga kuwazuia wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakiwapa wanafunzi chakula.
MALAWI: Timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) nchini Tanzania imehitimisha kambi ya matibabu ya kibingwa nchini Malawi, ambapo wagonjwa 64 wamefanyiwa upasuaji na wengine 49 kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa matibabu zaidi. Kambi hiyo imefanyika chini ya ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Malawi katika sekta ya afya,…
SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna, amesema kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga kimebadilisha maisha yake kisiasa na kibinafsi, akilazimika kuwa mwangalifu zaidi kuhusu usalama wake, anakoenda na hata chakula na vinywaji anavyotumia. Sifuna, ambaye anamchukulia Raila kama mlezi, mshauri na mlinzi wake wa kisiasa kwa zaidi ya miaka 10, alisema sasa anakabiliwa na majukumu mazito ya kuongoza vuguvugu lake huku kukiwa na mzozo ndani ya ODM na kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wake wa kisiasa. Akizungumza katika kikao na wanahabari jijini Nairobi Ijumaa, Oktoba 9, seneta huyo alisema anahisi pengo kubwa tangu kiongozi huyo wa muda mrefu wa ODM afariki. “Binafsi, namkosa mshauri wangu,” alisema Sifuna. Alisema Raila alipokuwa hai, wanachama wa ODM walijua kuwa masuala magumu yalipoibuka, kiongozi huyo angeweza kuingilia kati na kutoa mwelekeo. “Baba alipokuwepo, mzigo wa uwajibikaji haukuwa mzito kama ulivyo sasa kwa sababu tulijua hata kunapokuwa na masuala magumu ndani ya chama, si wewe pekee uliyetakiwa kufanya uamuzi,” alisema. Aliongeza kuwa Raila angewaambia waache suala tata kwake alishughulikie. “Sasa ni wewe. Unatarajiwa kutoa mwelekeo kwa chama,” alisema. Sifuna alisema amekuwa akijaribu kupatanisha makundi hasimu ndani ya ODM, hata kwa kuhudhuria mikutano katika makazi ya viongozi wa chama. Hata hivyo, juhudi hizo hazikuzuia kuondolewa kwake katika wadhifa wa katibu mkuu. Mzozo huo ulitokana na tofauti kuhusu mwelekeo wa chama na uhusiano wake na utawala wa Rais William Ruto. Sifuna na washirika wake wanataka ODM idumishe utambulisho wake wa kisiasa badala ya kufifia ndani ya mpango wa ushirikiano na serikali. Mnamo Septemba, Baraza la Kutatua Migogoro ya Vyama vya Kisiasa liliunga mkono kuondolewa kwake baada ya hatua mpya za kinidhamu. Chama kilimlaumu kwa kukiuka misimamo rasmi na kujihusisha na shughuli za kisiasa bila idhini, madai aliyokataa. Sifuna, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi, alisema kuachana na ODM ni jambo gumu kihisia kwa sababu amekuwa mwanachama wa chama hicho na mfuasi wa Raila kwa muda mrefu. “Kwa kweli, huu ni wakati wenye hisia nyingi kwangu, lakini maisha yangu yote nimejua chama kimoja cha kisiasa na kiongozi mmoja,” alisema. Alitania kuwa ana fulana nyingi za rangi ya machungwa nyumbani na hajui atazifanyia nini. Alisema Raila alimkinga mara kwa mara alipokabiliwa na madai ya kuondolewa katika wadhifa wa katibu mkuu, aliohudumu kwa miaka minane. Kwa mujibu wa Sifuna, Raila aliamini viongozi vijana wanapaswa kuruhusiwa kueleza maoni yao, hata pale lugha yao ilipokuwa kali au kuwakwaza viongozi wengine. Bila ulinzi huo wa kisiasa, Sifuna sasa anasema analazimika kutetea misimamo yake huku akikabiliana na matokeo ya maamuzi yake. Pia amekuwa mwangalifu zaidi kuhusu usalama wake. “Unahitaji kuwa mwangalifu zaidi kuhusu unakoenda, unachokula na unachokunywa,” alisema. Alisimulia tukio ambapo mmoja wa wafanyakazi wake alimletea chupa ya maji wakati wa shughuli ya umma, lakini baadhi ya watu waliokuwa kwenye umati, ambao hawakumfahamu mwanamke huyo, nusura wamvamie. Sifuna alisema tukio hilo lilionyesha hali ya wasiwasi inayomzunguka na umuhimu wa watu walio karibu naye kutambulika kwa wafuasi wake. Hata hivyo, hakutoa ushahidi huru unaomhusisha mtu yeyote na njama ya kumdhuru. Licha ya changamoto hizo, alisema ametiwa moyo na mapokezi ambayo timu yake imepata katika maeneo yanayohusishwa na ODM. Alisema siku za mwanzo zilikuwa ngumu kwa sababu kundi lake lilikabiliwa na matusi na kukosolewa, lakini sasa wanataka kuendelea kueleza msimamo wao kwa wananchi. Kuhusu mipango yake ya 2027, Sifuna alisema anataka kujenga uongozi unaozingatia mahitaji ya wananchi na unaosikiliza maoni ya wataalamu. Alikiri kuwa hana majibu ya kila suala, hasa katika uchumi na taaluma nyingine maalumu. “Mimi ni wakili,” alisema, akisisitiza kuwa nchi inahitaji viongozi wanaoweza kusikiliza wataalamu na kutumia mapendekezo yao kufanya maamuzi. Sifuna pia alisema hana kinyongo binafsi na waliotofautiana naye ndani ya ODM. “Nimewasamehe wote walionitukana au kuniita majina. Hayo yamepita,” alisema.
POLISI wamemkamata Kassim Abdi Sebo, anayeshukiwa kuongoza genge lililolaumiwa kutekeleza wizi kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi uliofanyika Homa Bay Agosti 16. Abdi alikamatwa Alhamisi usiku pamoja na wanaume wengine saba wanaodaiwa kuwazuia maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutekeleza majukumu yao. Maafisa waliokuwa wamejihami na kufunika nyuso zao walimzingira Abdi katika kituo cha mabasi cha Homa Bay mjini. Amekuwa akitoroka polisi tangu mahakama ya Homa Bay ilipotoa kibali cha kukamatwa kwake Agosti 14, baada ya maafisa kuandaa mashtaka kadhaa. Ripoti ya OB inaonyesha mashtaka hayo yanahusu madai ya kushambulia mtu na kumjeruhi kinyume na Kifungu cha 251 cha Sheria ya Adhabu. Kamanda wa DCI kaunti ya Homa Bay, Jimmy Kisobo, alisema Abdi anakabiliwa na mashtaka matatu huku uchunguzi ukiendelea na huenda yakaongezwa. “Kuna kesi nyingine nyingi tunazochunguza kutokana na yaliyotokea. Tukipata ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuhusika kwa Abdi, tutamshtaki pia kwa makosa hayo. Kwa sasa, tayari tuna kesi tatu dhidi yake” alisema. Kisobo alisema Abdi anahusishwa na visa vya vurugu vilivyoripotiwa katika kaunti hiyo kabla ya mkutano wa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Abdi analaumiwa kuhusika katika wizi wa kutumia nguvu baada ya kundi la vijana kudaiwa kuvamia Hoteli ya Tourist na kuiba mali. “Kundi hilo hilo lilichoma mkahawa ulio Koduogo na kuwanyanyasa watu waliokuwa hapo wakipata chakula,” alisema Kisobo. Alisema mshukiwa pia anatuhumiwa kuwatuma vijana wanaomuunga mkono kuchoma vibanda na kuharibu magari katika eneo hilo. Watu kadhaa waliripotiwa kushambuliwa katika mkahawa huo. Abdi alikamatwa Alhamisi usiku baada ya kukwepa majaribio kadhaa ya polisi ya kumtia mbaroni. “Tulikuwa tukimtafuta na kwa bahati nzuri, jana usiku tulimpata mjini na kumkamata pamoja na wengine saba waliowazuia polisi kutekeleza majukumu yao kisheria,” alisema Kisobo. Baada ya kukamatwa kwa Abdi, vijana wanaomuunga mkono walizua ghasia, kupora biashara mjini na kufunga barabara. Vijana hao waliendelea na vitendo hivyo Ijumaa asubuhi. “Ninawaomba wakome wanachofanya. Wanavunja sheria,” alisema Kisobo. Kamanda huyo wa DCI alionya kuwa wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvunja sheria mjini watakamatwa.. Washukiwa saba waliokamatwa pamoja na Abdi ni Achiando Victor Odhiambo, 26; Isaac Masika Muliro, 30; Oyege Moses Geoffrey, 27; Geoffrey Njore, 25; Odhiambo Wesley Arnold, 26; Joseph Kobila, 28; na Alfred Nyagiro Aliwa, 26.
Juhudi za Kalonzo Musyoka kubadilisha jina na muundo wa muungano wa Azimio la Umoja kuwa The Ukombozi Alliance (TUA) zinaweza kumweka katika nafasi nzuri ya kuwania urais kwa tiketi ya upinzani au kumtenga na viongozi wengine kuelekea uchaguzi wa 2027. Kalonzo, ambaye anaongoza chama cha Wiper, amekuwa mstari wa mbele katika kuunda upya muungano huo baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyekuwa kiongozi wake. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wanapinga kujiunga na TUA, wakisema wanataka kuhifadhi utambulisho wa vyama vyao na kuunda muungano mpya. Chama cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna vimeonyesha kusitasita kujiunga na TUA. Bw Sifuna alisema chama chake kipya, The Equitable Party, kinapanga kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu miungano. “Kwa sasa chama changu kinafanyiwa mabadiliko makubwa. Tuna miundo ya kuweka na makataa ya Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Kisiasa ya kuzingatia. Mazungumzo kuhusu miungano yatakuja baadaye,” alisema. Kalonzo naye amewataka wabunge wa Wiper walioonekana kushirikiana na Bw Sifuna kuzingatia shughuli za chama chao. Alitaja Mbunge wa Kaiti Joshua Kimilu na mwenzake wa Wundanyi Danson Mwashako. Hali hii inaashiria ushindani wa kutafuta uungwaji mkono mashinani na udhibiti wa vyama huku viongozi wakijaribu kuungana kumuondoa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu ujao. Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema chama hicho hakina haraka ya kujiunga na TUA, akisema upinzani unahitaji mawazo mapya. Alisema baadhi ya wanasiasa waliounga mkono mgombea wa Azimio katika uchaguzi wa 2022 walipata hasara kisiasa katika maeneo yao, na hawako tayari kujitolea tena kwa mpangilio kama huo. Hata hivywameunga mkono TUA kama chombo kinachoweza kumshinda Rais Ruto. Wote wamekuwa wakifanya kampeni pamoja na Kalonzo, ambaye wanamchukulia kama mgombeaji anayefaa kupewa tiketi ya urais. Mzozo huo unatokana na kipengele cha makubaliano ya muungano ambacho awali kilionekana kumpa kiongozi wa chama nafasi ya moja kwa moja kuwa mgombea urais. Washirika wa Kalonzo wanasema kipengele hicho kimebadilishwa na sasa wanachama wote wanaweza kuwania tiketi hiyo. Kalonzo pia amesisitiza kuwa kujiuzulu kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama mwenyekiti wa baraza la muungano hakujasababisha pengo la uongozi ndani ya TUA. Kuna juhudi za kumshawishi Bw Gachagua achukue nafasi ya Bw Kenyatta ili kuvutia DCP kujiunga na muungano huo. Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye anahusishwa na Linda Mwananchi, pia ametajwa kama anayeweza kupewa nafasi hiyo ili kuvutia wafuasi wa Nyanza. Hata hivyo, Mbunge wa Gatanga Edward Muriu, mshirika wa Bw Gachagua, alisema DCP inataka kwanza kuimarisha uungwaji mkono wake kabla ya kujadiliana na vyama vingine kuunda muungano mkubwa. Mchambuzi wa siasa Profesa David Monda alisema TUA inaweza kuwa vigumu kupata uungwaji mkono wa kutosha bila kuwashirikisha Kalonzo, Sifuna, Gachagua na aliyekuwa Waziri wa utawala wa ndani Fred Matiang’i katika mpangilio mmoja. Alisema viongozi hao wanapaswa kuungana ili kumshinda Rais Ruto au kuhatarisha kushindwa kila mmoja akigombea urais kivyake. Wanaounga mkono TUA wanataka muungano huo uige mfano wa National Rainbow Coalition (Narc), uliomuingiza Mwai Kibaki mamlakani mwaka 2002. Chini ya mfumo huo, vyama havikuvunjwa lakini viliunga mkono mgombea mmoja wa urais na ajenda ya pamoja. Lengo ni kuzuia upinzani kugawanyika na kumpa Rais Ruto nafasi ya kushinda uchaguzi wa 2027.
RAIS William Ruto ameeleza kutoridhishwa na utabiri wa hali ya hewa nchini, akizua mjadala kuhusu uwezo wa wataalamu kutabiri kwa usahihi wakati ambao mvua kubwa ya El Niño itaanza. Akizungumza Alhamisi, Oktoba 8, katika kongamano la Kilimo na Utoshelevu wa Chakula katika uwanja wa Jamhuri, Nairobi, Rais alisema muda wa kuanza kwa mvua hiyo umekuwa ukibadilishwa mara kwa mara. “Wale wanaohusika walituambia mvua itanyesha Agosti, lakini ikaahirishwa hadi Septemba, sasa ni Oktoba,” alisema. Aliongeza: “Kusubiri mvua hii ni kama kubahatisha. Hujui itanyesha lini,” alisema. “Tunasubiri El Niño, lakini hatujui itafika lini.” Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Ruto kuhoji utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kenya (KMSA). Mnamo Oktoba 2023, alitilia shaka tahadhari kuhusu El Niño iliyokuwa ikitarajiwa kusababisha mafuriko makubwa. Wakati huo, aliyekuwa Mkurugenzi wa KMSA, David Gikungu aliwaomba Wakenya radhi kwa mkanganyiko kuhusu utabiri, lakini akasisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa mvua nyingi. Mvua ilizofuata ilisababisha maafa makubwa. Kufikia Desemba 20, 2023, mafuriko ya mvua ya El Niño yalikuwa yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 174 na zaidi ya watu 500,000 kuhama makazi yao, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). Kaunti 38 kati ya 47 ziliathiriwa na mafuriko baada ya mito kuvunja kingo, mafuriko ya ghafla na maporomoko ya ardhi. Maeneo yaliyoathirika zaidi yalijumuisha Mandera, Garissa, Tana River, Wajir, Isiolo na Meru. Mtaalamu wa hali ya hewa, Fred Njehu wa Greenpeace Africa alisema utabiri wa kisayansi hutegemea hali na mifumo ya kihistoria, ambayo inaweza kubadilika kadri hali ya hewa inavyoendelea. “Utabiri wa matukio makali ya hali ya hewa huwa si sahihi kwa asilimia 100,” alisema. Alieleza kuwa utabiri wa mvua nyingi haumaanishi kila kaunti itakumbwa na mafuriko, wala kuchelewa kwa mvua hakumaanishi tahadhari iliyotolewa awali haina umuhimu. Njehu alisema badala ya viongozi na wataalamu kubishana kuhusu nani aliye sahihi, wanapaswa kuangazia ushahidi wa kisayansi na hatua za kujiandaa. Alisema taasisi za kisayansi zina wajibu wa kutoa ushauri kuhusu hatari za hali mbaya ya hewa, huku viongozi wa kisiasa wakitarajiwa kuhakikisha kuna fedha, sera na mipango ya kukabiliana na majanga. Kaimu Mkurugenzi wa KMSA Edward Muriuki alisema El Niño hutokana na ongezeko la joto la maji ya bahari katika maeneo ya kati na mashariki mwa Bahari ya Pacific, jambo linaloweza kubadilisha mifumo ya hali ya hewa duniani. Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema kuna uwezekano wa karibu asilimia 100 wa El Niño kuendelea hadi Februari 2027. Shirika hilo linaonya kuwa huenda ikawa mojawapo ya matukio makubwa zaidi tangu 1950. Hata hivyo, athari zake hutofautiana kulingana na maeneo na mifumo mingine ya hali ya hewa. Bw David Samoei wa Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Kukabiliana na Majanga alisema serikali sasa inalenga maandalizi ya msimu wa mvua ya Oktoba, Novemba na Desemba badala ya kubishana iwapo mafuriko yatatokea. “Hatuzungumzi tena kuhusu iwapo kutakuwa na mafuriko. Tunachojadili ni hatua tunazopaswa kuchukua katika msimu wa Oktoba, Novemba na Desemba,” alisema. Serikali imesema imeanzisha uratibu wa mashirika mbalimbali kutathmini hatari na kupanga hatua za kukabiliana na mafuriko. Pia, mazoezi ya kujaribu mifumo ya uokoaji yanafanywa ili kubaini mapungufu. Wataalamu wanasema mamlaka ya hali ya hewa inapaswa kueleza mabadiliko ya utabiri kwa uwazi, huku serikali ikiwekeza katika wataalamu, teknolojia, ukusanyaji wa data na ufadhili wa kutosha. Wanasema mawasiliano bora kati ya wataalamu, wanahabari na viongozi ni muhimu ili wananchi waelewe tahadhari na kuchukua hatua mapema.
The National Agency for Food and Drug Administration and Control, (NAFDAC), has warned that the continued circulation and misuse of banned pesticides in Nigeria pose serious threats to public health, raising concerns over the detection of pesticide residues above permitted safety limits in some samples of beans
"Many Nigerians have called INEC to sanction political parties and candidates or some politicians who, in their campaigns, incite the public or raise matters that are not issue-based. We have been told to go on campaigns based on issues. What are you going to do about the people attacking personality or insulting individuals? Up till now, I have not heard that INEC has been able to call or draw the attention of the vice presidential candidate of the ADC, Rotimi Amaechi, to this," the minister said.
Persistent sadness, fear, hopelessness, low self-esteem, excessive talking or silence, social withdrawal and confusion about oneself are among the signs of mental health problems that require professional assessment, a psychologist has said. Other possible signs include insomnia or excessive sleeping, stress and unusual skin sensations, such as feeling that insects are crawling on the body. Speaking on October 9, 2026, during celebrations to mark World Mental Health Day, a psychologist at Mbeya Zonal Referral Hospital, Mr Batana Mwamboneke, said mental health conditions had many symptoms but could be treated with appropriate professional support. He said stigma remained a major barrier, with many people reluctant to acknowledge that they were experiencing mental health problems. He added that changes in feelings and behaviour could help indicate when someone needed professional assessment. “When mental health suffers, every aspect of life is affected. In my 12 years of experience, I have seen conditions that require the attention of psychologists rather than simply visiting doctors. We need to work together to address these challenges,” he said. Mr Mwamboneke said people with mental health conditions had previously been confined indoors because of misconceptions, but specialised facilities were now helping to address the problem. He added that excessive anger leading to inappropriate behaviour could also signal a problem, while mental health difficulties could affect relationships and marriages. “The mind works through the brain, just as a phone relies on its systems and internet connection. Some aspects can be seen, while others cannot,” he said. Meanwhile, Ms Maimuna Tangu, reporting on a mental health awareness and well-being project implemented by Shalom Development Organisation (SHADO), said 20 people had received support over seven months. She said the Simama CBR project had helped improve public understanding of mental health and enabled people to access counselling and psychological support. “Since the project began, we have provided education, counselling, awareness campaigns encouraging people to seek help and initiatives to combat stigma. This has improved understanding of professional support, the challenges people face and the harm caused by stigma,” she said. Ms Tangu said the project continued to face challenges, including limited public awareness, harmful cultural misconceptions and inadequate resources to reach communities. She called for greater cooperation between stakeholders and health facilities. A Mbeya resident, Ms Agynes Mwakyusa, said mental health problems affected many people, although some were unwilling to acknowledge them because the signs were not always immediately apparent. “When we see people killing one another, violence increasing and harmful misconceptions, particularly those related to witchcraft, we should also consider whether mental health problems may be involved. Experts should continue educating and reaching out to communities,” she said. Ms Mwakyusa urged people from all educational backgrounds to help raise awareness, identify those who needed support and encourage them to seek professional assistance. “Everyone has a role to play in helping communities remain safe, but individuals must also be willing to recognise that they may have a problem and seek help,” she said.
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk Bashiru Ally Kakurwa, amezindua maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) inayolenga kufanya utafiti kuhusu ongezeko la asidi baharini na athari zake kwa viumbe hai, hatua inayotarajiwa kuimarisha msingi wa kisayansi wa maendeleo endelevu ya uchumi wa buluu nchini. Uzinduzi wa maabara hiyo…
KIGOMA: RAIS wa Baraza la Maaskofu Mashariki mwa Afrika (AMECEA), Askofu Gervas Nyaisonga, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya, amewataka Watanzania wenye changamoto za macho kupata matibabu kutoka kwa wataalamu wenye taaluma badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao, amesema, matibabu yao hayaaminiki. Askofu Nyaisonga alitoa kauli hiyo wakati akizindua jengo…
Lagos State Government has raised concerns over the impact of social media and foreign influences on children’s mental health, calling for stronger preventive measures and improved parental guidance to protect young people.
JUHUDI za kampuni moja kuingiza nchini tani 540,000 za mahindi kutoka Zambia zimekumbwa na mzozo wa kisheria huku maswali yakiibuka kuhusu jinsi ilivyoidhinishwa na iwapo zilihusishwa na mpango wa serikali wa kuagiza mahindi. Kesi iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa inalenga kusimamisha uagizaji wa takriban magunia milioni sita ya mahindi, kila moja likiwa na uzani wa kilo 90. James Mwikabi ameomba mahakama isimamishe mpango huo, akidai serikali imeanza kuwezesha uagizaji kabla kuhalalishwa. Katika kesi yake anataka mahakama itoe amri ya muda ya kuzuia serikali, maafisa wake au taasisi zake kuidhinisha, kuwezesha, kusafisha au kutoa mahindi hayo bandarini. "Mahakama hii itoe amri ya muda ya kuzuia utekelezaji, kuwezesha, kuidhinisha au kuachilia takriban tani 540,000 za mahindi yanayopendekezwa kuagizwa na kampuni ya Baita Trading Company Limited,” anasema Mwikabi katika kesi yake. Pia anataka serikali ifichue iwapo kampuni hiyo imepewa sehemu ya mgao wa mpango wa kitaifa wa kuagiza mahindi au kupewa msamaha wa ushuru, punguzo la kodi au upendeleo mwingine wa kisheria.Mnamo Oktoba 5, Mahakama Kuu ya Mombasa ilitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kuamuru stakabadhi za kesi ziwasilishwe kwa Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe na mwenzake wa Fedha John Mbadi. Stakabadhi hizo zinapaswa kuwasilishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya (KRA), Mwanasheria Mkuu, Mamlaka ya Bandari Kenya na Baita Trading Company Limited, miongoni mwa washtakiwa wengine. “Baada ya kusoma kesi hii, nimeridhika kwamba ni ya dharura na hivyo imethibitishwa kuwa la dharura,” mahakama ilisema. Mwikabi anasema kesi yake si dhidi ya uagizaji wa mahindi au biashara halali ya kimataifa, bali inahusu jinsi mamlaka ya umma ilivyotumika kuwezesha mpango huo. Anataka serikali ieleze iwapo Baita ilipewa sehemu ya mpango wa serikali wa kuagiza mahindi na ikiwa iliahidiwa msamaha wa ushuru, punguzo la kodi au upendeleo wa forodha. Kwa mujibu wa Mwikabi, serikali ilitangaza Agosti 19 kuwa ingewezesha kuingizwa nchini kwa takriban magunia milioni 25 ya mahindi ya kilo 90 ili kukabiliana na upungufu uliotarajiwa, kuongeza upatikanaji na kuzuia bei kupanda.Mnamo Agosti 28, Baita ilitangaza kuwa ilikuwa tayari kununua mahindi kwa wingi kutoka Zambia kuyaleta nchini. Baadaye kampuni hiyo ilidaiwa kufanya makubaliano na Food Reserve Agency ya Zambia ya kununua na kusafirisha nchini tani 540,000 za mahindi. Kiasi hicho ni sawa na magunia milioni sita na kinawakilisha sehemu kubwa ya mahitaji yaliyotangazwa na serikali.Mwikabi anataka serikali kutoa tathmini iliyotumika kuamua kiasi cha mahindi kitakachoagizwa, ikiwemo tathmini ya chakula, uchumi na uzalishaji wa ndani. Anasema mahakama haiombwi kuamua bei ya mahindi, bali kuchunguza iwapo maslahi ya wakulima, usalama wa chakula na soko la ndani yalizingatiwa.
Watu wanne walifariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya lori kugonga magari na pikipiki kadhaa mjini Meru Alhamisi jioni. Kamanda wa Polisi wa Imenti Kaskazini, Bashir Hassan, alisema ajali hiyo ilitokea dakika chache kabla ya saa tatu usiku, breki za lori hilo lililokuwa likielekea Nkubu zilipofeli. Alisema lori hilo liligonga magari mawili barabarani, kisha likagonga pikipiki mbili na matatu zilizokuwa zimeegeshwa kando ya barabara kabla ya kupinduka. “Lori lilikuwa likiteremka mlima breki zilipofeli. Wanaume watatu na mwanamke mmoja walifariki papo hapo. Waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Meru,” alisema Bw Hassan. Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Bernard Murithi, alisema watu 21 walipelekwa hospitalini. Kati yao, 10 walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani, huku 11 wakilazwa kwa matibabu zaidi. Alisema hali yao ilikuwa shwari. Mashahidi walisema lori hilo lililokuwa limebeba simiti lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kutoka Makutano. Dereva alijaribu kuwaonya watumiaji wa barabara kwa kupiga honi kabla ya kugonga magari na watu waliokuwa kando ya barabara. Mkazi Frank Mwongera alisema baadhi ya waathiriwa walinaswa chini ya lori hilo.
DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetwaa tuzo nne katika Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST), zikitambua mchango wake katika kuboresha mawasiliano kwa umma, kampeni za uelimishaji na usimamizi wa mawasiliano wakati wa changamoto. Tuzo hizo zilitolewa Oktoba 8, 2026, ambapo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa…
MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) ameidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya washukiwa watano wanaodaiwa kuhusika na kifo cha wakili maarufu Mathew Kyalo Mbobu. Washukiwa hao ni mwanasiasa Rose Mbithe Mulwa, watoto wake Chris Mulwa na Angela Mulwa pamoja na maafisa wawili wa polisi, Julius Kipkoech Cheruiyot na Kennedy Kipkemei Borboroi. Wawili hao, Cheruiyot na Borboroi, walifikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza katika Mahakama Kuu ya Kibera, lakini hawakujibu mashtaka hayo baada ya kuamriwa kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili katika Hospitali ya Mbagathi. Jaji Kavedza pia aliamuru Rose na Angela, wanaozuiliwa katika gereza la wanawake la Lang’ata, pamoja na Chris anayezuiliwa rumande Nairobi, wafikishwe kortini. Washukiwa wote wanatarajiwa kujibu mashtaka ya mauaji Oktoba 27, 2026, baada ya ripoti za uchunguzi huo kuwasilishwa kortini. Mbobu, ambaye alikuwa wakili, mhadhiri wa chuo kikuu na mwandishi, aliuawa Septemba 9, 2025 alipokuwa akiendesha gari kuelekea nyumbani kupitia Barabara ya Magadi karibu na Shule ya Brookhouse International.
AFRIKA inaendelea kuagiza dawa nyingi zinazotumiwa na wananchi wake kutoka nje ya bara hilo, hali inayozifanya nchi kama Tanzania kuwa katika hatari ya kukumbwa na changamoto za upatikanaji wa dawa kutokana na utegemezi wa minyororo ya kimataifa ya usambazaji, licha ya serikali mbalimbali kuongeza juhudi za kuimarisha uzalishaji wa dawa ndani ya nchi. Changamoto hiyo…
Tanzania inakabiliwa na changamoto inayoongezeka ya kuhakikisha uendelevu wa programu muhimu za afya, huku mabadiliko katika ufadhili wa Marekani yakifichua hatari za kutegemea kwa kiasi kikubwa fedha za nje katika huduma za kinga na matibabu ya VVU, huduma za maabara na huduma za afya zinazotolewa katika jamii. Kwa zaidi ya miongo miwili, programu zinazoungwa mkono…
By Henry Umoru ABUJA — The Obidient Movement has faulted the Federal Government’s 30-day petrol discount initiative, questioning the figures used to calculate fuel-related interventions and accusing the government of failing to provide sufficient transparency in the management of the petroleum sector. The movement said the temporary discount raised questions about the government’s position on […]
One of the mothers of the 20 prospective National Youth Service Corps (NYSC) members abducted in Imo State has recounted how she struggled to raise ₦3 million as ransom while fearing for her child’s life. The distraught mother said she ran from place to place to raise the money before eventually sending someone to deliver […]
WABUNGE sasa wanapanga kuondoa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika usimamizi au kusikiliza migogoro inayotokana na mchujo ndani ya vyama vya kisiasa, wakisema hatua hiyo itaongeza uhuru wa vyama hivyo. Wakati wa kujadili Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa mwaka 2024, wabunge walisisitiza kuwa vyama vya kisiasa ni taasisi huru zenye haki ya kusimamia shughuli zao za ndani bila kuingiliwa na IEBC. Wanataka Sheria ya Uchaguzi ifanyiwe marekebisho ili kuondoa mamlaka ya IEBC kushughulikia migogoro ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama na jukumu hilo lihamishiwe Mahakama ya Kutatua Migogoro ya Uchaguzi. Kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 88 inapatia IEBC jukumu la kusimamia au kuendesha kura za maamuzi na uchaguzi. Aidha, Ibara ya 88(4)(e) inaeleza kuwa tume hiyo ina wajibu wa kushughulikia migogoro ya uchaguzi, ikiwemo inayotokana na uteuzi wa wagombea, isipokuwa kesi za uchaguzi na migogoro inayozuka baada ya kutangazwa kwa matokeo. Hata hivyo, wabunge wanasema kuhusika kwa IEBC katika mchujo wa vyama kunadhoofisha uhuru wa vyama vya kisiasa.Kwa mujibu wao, uamuzi wa kumpa mwanasiasa tiketi ya moja kwa moja au kupitia mchujo ni haki ya chama husika pekee. Kwa msingi huo, wanadai IEBC haipaswi kuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamishi yanayotokana na maamuzi hayo.Pia walieleza kuwa kushiriki kwa IEBC katika michakato ya vyama ni sawa na kuingilia masuala ya ndani ya vyama vya kisiasa. Hoja nyingine iliyotolewa ni uwezekano wa mgongano wa maslahi. Walisema baadhi ya vyama hupatia IEBC jukumu la kusimamia mchujo kutokana na uwezo wake wa kiteknolojia na kiutawala. Hivyo, si sahihi kwa tume hiyo hiyo kusikiliza migogoro inayotokana na uchaguzi ambao imesimamia. Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria, George Murugara, alisema wabunge wanataka jukumu la IEBC katika kusuluhisha migogoro ya uteuzi lifutwe kabisa. “Tunataka kuondoa jukumu la IEBC katika kushughulikia migogoro inayotokana na uteuzi wa wagombeaji. Migogoro hiyo ishughulikiwe na Mahakama ya Kutatua Migogoro ya Uchaguzi,” alisema Murugara. Mbunge wa Ugenya, David Ochieng’, alisema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa inapaswa kuimarisha vyama ili viweze kusimamia shughuli zao kwa uhuru. “IEBC haina kazi katika uteuzi wa ndani ya vyama. Vyama ni kama vilabu. Kama chama kinaamua kunipa tiketi ya moja kwa moja, hilo ni suala lake. Kwa nini IEBC ihusike?” alihoji. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wanawake wa Baringo, Florence Jematiah, alisema hana tatizo IEBC kusaidia vyama visivyo na uwezo wa kusimamia uchaguzi wa mchujo. Hata hivyo, alionya kuwa matatizo huibuka pale tume hiyo hiyo inapolazimika kusikiliza migogoro inayotokana na mchujo iliyoendesha. Kulingana na Mpango wa Uchaguzi wa 2025-2027 uliozinduliwa Mei, vyama vyote vinavyokusudia kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027, vinapaswa kukamilisha mchujo na kutatua migogoro yote ifikapo Mei 9, 2027. Ratiba hiyo pia inaeleza kuwa wagombea wasioridhika na namna vyama vyao vilivyoshughulikia malalamishi yao watakuwa na hadi Juni 12, 2027 kuwasilisha kesi kwa IEBC, ambayo itatakiwa kutoa uamuzi ndani ya siku 10.
Tanzania imeweka lengo la kujenga uwezo wa ndani wa kuzalisha dawa na bidhaa za afya na hatimaye kuwa kitovu cha uzalishaji wa dawa kwa Afrika Mashariki, lakini utegemezi mkubwa wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje unaendelea kuwa changamoto kubwa kwa sekta ya afya na viwanda nchini. Serikali imelenga kufikisha uzalishaji wa ndani hadi asilimia 80 ya…
TABORA: KALIUA District in Tabora Region is targeting the production of one million tree seedlings to help restore degraded forests and reduce pressure on natural forest reserves caused by tree cutting and charcoal production. The seedlings are being raised at a Tanzania Forest Services Agency (TFS) nursery established in September 2026 under the Miombo Collaborative…
Kwa miaka kadhaa, Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) umekuwa nguzo muhimu katika mwitikio wa Tanzania dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), ukisaidia matibabu, kinga, huduma za maabara, programu za kijamii, mifumo ya taarifa na watumishi wa afya. Ushirikiano huo umeiwezesha Tanzania kupanua upatikanaji wa huduma muhimu za kuokoa…
GAVANA wa Nairobi, Johnson Sakaja, aliingia ofisini mwaka wa 2022 akiwa na ahadi kubwa ya kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sambamba Nairobi lakini miaka minne baadaye takwimu za matumizi ya fedha za umma zinaibua swali iwapo jiji hilo limetimiza lengo hilo. Bw Sakaja alipokuwa akihutubu wakati wa kuapishwa kwake Agosti 2022, alikumbuka maisha yake ya utotoni Ngara na jinsi alivyoshangaa kuona baadhi ya mitaa ikiwa safi, yenye barabara nzuri na iliyopangwa huku mingine ikiwa katika hali mbaya.Alisema akiwa na umri wa miaka saba aliwahamasisha watoto wenzake kuandamana wakitaka mazingira yao yaimarishwe. “Nilijifunza kuwa eneo hilo halikuwa na watu bora zaidi; walikuwa wamejipanga, walikuwa na hisia za jamii, walichagua uongozi mzuri na mambo yakawa sambamba,” alisema. Hata hivyo, ripoti za matumizi zinaonyesha Nairobi bado inakabiliwa na changamoto kubwa za maendeleo. Katika miaka minne ya uongozi wa Bw Sakaja, kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2026, serikali ya kaunti ilitumia Sh125 bilioni.Kati ya fedha hizo, Sh15.4 bilioni pekee, sawa na asilimia 12.36, zilitumika kwa miradi ya maendeleo huku Sh109.5 bilioni zikitumika katika shughuli za kawaida. Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma inataka angalau asilimia 30 ya matumizi ya kaunti yaelekezwe kwa maendeleo.Hii ina maana kuwa Nairobi ilipaswa kutumia takriban Sh37.5 bilioni kwa maendeleo, tofauti ya zaidi ya Sh22 bilioni ambazo zingetumika kujenga barabara, hospitali, masoko na miradi mingine. Kituo cha Centre for Economic Governance (CEG), kinasema Nairobi ni miongoni mwa kaunti zinazofanya vibaya zaidi katika matumizi ya fedha za maendeleo.Changamoto hiyo pia imeonekana katika miradi iliyokwama. Kufikia Juni, Nairobi ilikuwa na miradi 57 iliyokwama ya thamani ya zaidi ya Sh2 bilioni.Miongoni mwa hiyo ni jengo la matibabu la Sh256 milioni katika Hospitali ya Mbagathi, ukumbi wa kijamii wa Mwiki wa thamani ya Sh76 milioni na wodi ya uzazi ya Sh30 milioni katika Kituo cha Afya cha Umoja 1. Mdhibiti wa Bajeti, Margaret Nyakang’o, alisema miradi hiyo ilikwama kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wakandarasi kuondoka kwa kukosa malipo. Wakati huo huo, zaidi ya nusu ya Sh125 bilioni zilizotumiwa na serikali ya Sakaja zilienda kwa mishahara na marupurupu.Takriban Sh63.3 bilioni zilitumika kwa mishahara, sawa na asilimia 50.65 ya matumizi yote. Ukaguzi pia umeibua maswali kuhusu mfumo wa malipo wa kaunti. Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilitaja Sh1.9 bilioni zilizotolewa kutoka akaunti ya mishahara bila kaunti kueleza zilitumika vipi.Aidha, Sh840.4 milioni zilizotajwa kama gharama za wafanyakazi zilikosa stakabadhi muhimu za kuthibitisha waliolipwa.Idadi ya wafanyakazi wa kaunti pia imeongezeka kutoka 13,354 mwaka 2023 hadi 19,258 Juni 2025. Katika sekta ya taka, kaunti ilitumia Sh1.7 bilioni mwaka 2024/25, huku data nyingine ya City Hall ikionyesha matumizi ya Sh3 bilioni. Mkaguzi Mkuu alisema malipo ya Sh361 milioni hayakuwa na stakabadhi za kutosha kuthibitisha huduma zilizotolewa. Nairobi pia ilitumia Sh2.6 bilioni kwa mawakili wa nje mwaka 2024/25, licha ya kuwa na zaidi ya mawakili 100 katika idara yake ya sheria. Ofisi ya Bajeti ya Bunge pia iliorodhesha Nairobi miongoni mwa kaunti zilizofanya vibaya katika matumizi ya rasilimali za umma.Nairobi inachangia karibu theluthi moja ya uchumi wa Kenya, ikiwa na shughuli za kiuchumi zenye thamani ya Sh4.1 trilioni mwaka 2024. Bw Sakaja sasa anaingia mwaka wa mwisho wa muhula wake wa kwanza huku akitakiwa kukabiliana na changamoto za mishahara, miradi iliyokwama, taka na matumizi ya fedha za umma ambazo zinaendelea kuathiri huduma kwa wakazi.
By Rosemary Iwunze Claims paid by insurance companies rose by 0.1 per cent, year-on-year, YoY to N346.87 billion in the first half of 2026, H1’26, from N346.59 billion in the corresponding period of 2025. The rise in claims payment was in spite of a 1.8 per cent YoY decline in Gross Premium Written, GPW, raising […]
MAHAKAMA Kuu imebatilisha uamuzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) wa kuacha kumshtaki Waziri na aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuhusu madai ya ufisadi wa Sh56.7 milioni. Jaji Benjamin Musyoki alisema ODPP ilikiuka taratibu na Katiba ilipobadilisha uamuzi wake wa awali wa kumshtaki Oparanya bila kuhusisha Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), iliyokuwa imefanya uchunguzi. Jaji alitangaza uamuzi wa ODPP wa Julai 8, 2024 kuwa batili na kuamuru uamuzi huo uondolewe. “Ni baada tu ya EACC kuchunguza ushahidi huo unaodaiwa kuwa mpya ndipo ODPP ingekuwa na mamlaka ya kikatiba kufanya uamuzi kuhusu suala hilo,” alisema Jaji Musyoki. EACC ilikuwa imependekeza Oparanya ashtakiwe kwa makosa ya kula njama ya kutenda ufisadi, mgongano wa kimaslahi, kutumia vibaya mamlaka na ulanguzi wa pesa. Uchunguzi huo ulihusisha madai kwamba Oparanya alipokea Sh56.74 milioni kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni zilizopata kandarasi kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Kakamega wakati wa uongozi wake kati ya 2013 na 2022. EACC ilisema baadhi ya pesa hizo zilitumika kununua mali katika mtaa wa Karen, Nairobi. Awali, ODPP ilikuwa imekubaliana na pendekezo la EACC la kumshtaki Oparanya mnamo Desemba 18, 2023. Hata hivyo, baada ya mawakili wa Oparanya kuomba mapitio ya uamuzi huo Julai 3, 2024, ODPP iliamuru faili hiyo ifungwe, ikisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhakikisha ana hatia EACC ilipinga uamuzi huo na baadaye ikasisitiza pendekezo lake la kumshtaki Oparanya, ikisema haikuhusishwa katika mchakato wa kupitia upya faili ya kesi. Mwanaharakati wa haki Fredrick Mulaa ndiye aliyewasilisha suala hilo mahakamani, akipinga uamuzi wa ODPP. EACC iliunga mkono kesi hiyo, ikisema uchunguzi wake ulionyesha kulikuwa na msingi wa kumshtaki Oparanya. Tume hiyo ilisema ilichunguza kandarasi 60 zilizotolewa kwa kampuni sita na Kaunti ya Kakamega za thamani ya zaidi ya Sh2.2 bilioni. Aidha, EACC ilikuwa imepata amri ya kuzuilia Sh28.9 milioni zilizoshukiwa kuwa mapato ya ufisadi. Jaji Musyoki alisema ingawa ODPP ina mamlaka ya kuamua iwapo mtu atashtakiwa, mamlaka hayo hayaipatii haki ya kuchukua nafasi ya EACC katika uchunguzi. “Taasisi ya kikatiba au kisheria haifai kutumia mamlaka au busara zake kiholela bila kuzingatia maslahi ya washiriki wengine katika suala linalohusika,” alisema. Jaji alisema mwongozo wa ODPP wa 2019 kuhusu uamuzi wa kushtaki unahitaji mwendesha mashtaka kushauriana na mpelelezi anapoamua kutowasilisha mashtaka. “Ni wazi kwamba barua ya ODPP ya Julai 8, 2024 iliandikwa bila kushauriana na EACC,” alisema. Aliongeza kuwa ODPP ilivuka mipaka kwa kupokea ushahidi uliodaiwa kuwa mpya na kuamua yenyewe kupitia upya uamuzi wa kumshtaki Oparanya bila kuhusisha EACC. Hata hivyo, mahakama ilikataa ombi la kubatilisha uteuzi wa Oparanya kuwa Waziri. Jaji alisema Bunge lilimkagua na kuidhinisha uteuzi wak na mahakama haikupewa ushahidi wa kuonyesha kuwa mchakato wa kikatiba ulikiukwa.
KIONGOZI wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, amethibitisha kuwa ranchi iliyopo jimbo la Texas nchini Amerika ambayo imezua mijadala mitandaoni ni mali yake binafsi na kwamba ataishi hapo kwa siku 15 zaidi baada ya kukamilisha ziara yake ya kisiasa nchini humo. Bw Gachagua, aliondoka Kenya mnamo Agosti 26, anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya siku 50 nchini Amerika mjini Boston mnamo Oktoba 10. Hata hivyo, badala ya kurejea nyumbani mara moja, ataelekea katika ranchi hiyo kwa kile chama chake kimetaja kuwa ni mkutano maalum wa kupanga mikakati ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Ranchi hiyo ilivutia hisia za umma mwishoni mwa Septemba baada ya Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya kusambaza picha na video mitandaoni akiwa pamoja na Bw Gachagua katika eneo hilo. Akizungumzia kuhusu mali hiyo, Bw Gachagua alisema ranchi hiyo ni yake na akaiita “Wamunyoro Texas”, akiilinganisha na makazi yake maarufu ya Wamunyoro nchini Kenya. “Ndiyo, mali hiyo ni yangu. Ni Wamunyoro yangu nyingine ya faragha,” alisema. Kauli hiyo inafanana na matamshi aliyotoa Septemba 26 alipokutana na Wakenya wanaoishi Texas. Wakati huo alisema alifurahia wageni kukutana katika makazi hayo badala ya hoteli ili kuunda mazingira ya kifamilia na ya karibu zaidi. Picha zilizochapishwa na Bw Gachagua zinaonyesha nyumba kubwa ya ghorofa moja iliyojengwa kwa matofali mekundu, ikiwa katikati ya eneo pana lenye nyasi zilizopambwa vizuri. Pia kuna sehemu za kuketi nje, farasi na ng’ombe wa aina ya Texas Longhorn wanaonekana ndani ya ranchi hiyo iliyozungushiwa ua. Gari dogo la matumizi ya ndani ya ranchi pia linaonekana likiwa na maandishi “Wamunyoro Texas” na “Riggy G”. Mbunge Salasya alisema aliguswa na mafanikio ya Gachagua baada ya kutembelea ranchi hiyo. “Nilimwambia natamani siku moja niwe na mali kama hii. Aliniambia siri ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya kifedha na kumwamini Mungu,” alisema. Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa DCP, John Methu, Bw Gachagua amezuru miji mitano tofauti tangu aanze shughuli za kisiasa nchini Amerika. Baada ya kupumzika kwa siku kumi, alifanya mikutano Spokane, Washington, Portland, Oregon, Kansas City, Missouri na baadaye Texas kabla ya kuelekea Boston. Methu alisema kipindi atakachotumia katika ranchi hiyo kitahusisha mikutano na washirika wa kisiasa, wataalamu na marafiki wa kimataifa kujadili mikakati ya chama hicho. Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na ujenzi wa miungano ya kisiasa, uteuzi wa mgombea wa pamoja wa urais dhidi ya Rais William Ruto mwaka 2027 na mapendekezo ya kufufua uchumi wa Kenya. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kupunguza kutegemea mikopo, kuunganisha mashirika ya umma, kupanua wigo wa kodi na kuongeza mapato ya serikali za kaunti. Mratibu wa DCP nchini Amerika, Joseph Warui, alisema mikutano hiyo pia itatumika kutathmini zaidi ya vikao 80 vya umma na vya faragha ambavyo Bw Gachagua amehudhuria wakati wa ziara yake. Aliongeza kuwa washiriki watajadili hali ya uchumi, haki za binadamu na mustakabali wa kisiasa wa Kenya. Hata hivyo, tarehe rasmi ya kurejea kwa Bw Gachagua nchini Kenya bado haijatangazwa. Chama chake kimesema taarifa hiyo itatolewa baadaye baada ya kukamilika kwa shughuli zote alizopanga nchini humo.
MADAKTARI na wauguzi wanane waliomhudumia mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu hatua ya kupelekwa karantini katika jengo lile lile la hospitali ya Nairobi Hospital ambako mgonjwa huyo alitibiwa na baadaye kufariki dunia. Katika taarifa ya pamoja, wahudumu hao wa afya walisisitiza kuwa hawapingi maagizo ya karantini wala ufuatiliaji wa kiafya unaohitajika kufuatia kisa hicho. Hata hivyo, wanahoji utaratibu unaotumika kwa sasa wakisema hauzingatii viwango tofauti vya hatari ya maambukizi kwa watu waliohusika. Kwa mujibu wao, kila mtu aliyewasiliana na mgonjwa huyo anaonekana kushughulikiwa kana kwamba alikuwa katika kiwango sawa cha hatari ya kuambukizwa virusi vya Ebola, jambo ambalo wanasema si sahihi kimatibabu. “Tunaelewa uzito wa kisa hiki na tunakubali kushirikiana kikamilifu na hatua za kulinda afya ya umma. Hata hivyo, tunataka tathmini ya hatari ifanywe kulingana na kiwango halisi cha kila mtu,” walisema. Wahudumu hao walifichua kuwa mwanzoni waliarifiwa kuwa wangekamilisha siku 21 za ufuatiliaji na kujitenga nyumbani chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Baadaye, hata hivyo, walipewa maagizo ya kuhamia katika jengo la East Wing la Hospitali ya Nairobi ili kuendelea na karantini yao. Walisema jengo hilo ndilo lililotumika kumhudumia mgonjwa wa Ebola kabla ya kifo chake, jambo ambalo limezua maswali kuhusu usalama wao. “Tungependa kujua kama eneo hilo limesafishwa kikamilifu na kuthibitishwa rasmi kuwa salama kwa matumizi. Pia tunataka kufahamu sababu za kitaalamu zilizosababisha eneo hilo lichaguliwe kuwa kituo cha karantini,” walieleza. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mgonjwa huyo awali alitengwa katika chumba maalum ndani ya kitengo cha dharura kabla ya kuhamishwa kituo cha East Wing. Nairobi Hospital imesema kituo hicho kiko mbali na majengo mengine ya hospitali, kina lango lake maalum na wafanyakazi wake wa kujitegemea. Hata hivyo, wahudumu hao wanasisitiza kuwa walimhudumia mgonjwa huyo wakiwa wamevaa vifaa vyote vya kujikinga vinavyopendekezwa katika visa vya Ebola. Aidha, hakuna aliyeripoti kuwa na hitilafu kwenye mavazi hayo ya kinga wala kuhusika katika mtagusano wa moja kwa moja usio na kinga. Kwa msingi huo, wanataka tathmini ya kibinafsi ya hatari ifanywe kwa kila mhudumu badala ya kuwekewa viwango sawa na watu waliokuwa na mtagusano wa karibu na mgonjwa bila vifaa vya kujikinga. Walinukuu miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inayotaka wahudumu wa afya wanaohusika katika matibabu ya wagonjwa wa Ebola kutathminiwa kulingana na kiwango halisi cha hatari ya kila mmoja. Miongozo hiyo inaeleza kuwa wahudumu waliokuwa na vifaa sahihi vya kujikinga hawapaswi kuchukuliwa sawa na watu waliokutana na mgonjwa bila kinga. “Kuwa karibu na mgonjwa pekee si kipimo sahihi cha hatari. Kinachopaswa kuangaliwa ni aina ya mtagusano na matumizi ya vifaa vya kujikinga,” walisema. Pia wamepinga uwezekano wa kuwekwa pamoja katika karantini na watu waliotangamana zaidi na mgonjwa huyo. Kwa maoni yao, wahudumu waliotumia mavazi kamili ya kinga hawapaswi kushughulikiwa sawa na watu waliokuwa na mtagusano wa moja kwa moja bila ulinzi wa kutosha. Iwapo karantini ya taasisi itaendelea kutumika, wanapendekeza watu watenganishwe kulingana na viwango vya hatari walivyokumbana navyo. Pia wanataka kila mhusika apewe chumba chake binafsi chenye choo, huduma bora za matibabu, chakula cha kutosha, maji safi na vifaa vingine muhimu. Mbali na hilo, wahudumu hao wanataka usaidizi wa kisaikolojia na ufuatiliaji wa afya kazini kwa wote waliohusika katika kushughulikia mgonjwa huyo. Wanasema kazi yao iliwaweka katika mazingira hatari na hivyo wanapaswa kupewa fidia au marupurupu maalum ya mazingira hatari. Katika barua ya ndani ya hospitali hiyo Oktoba 6, Mkurugenzi Mkuu Dkt Felix Osano alisema wafanyakazi waliotambuliwa kuwa walitangamana na mgonjwa huyo wawasiliane moja kwa moja ili kubaini kiwango cha hatari walichokuwa nacho. Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), Dkt Davji Atellah, alisema wahudumu wa afya waliokuwa wamevaa vifaa vya kujikinga hawapaswi kuwekwa pamoja na watu waliotagusana moja kwa moja na mgonjwa bila kinga. Alisisitiza kuwa madaktari na wauguzi waliokuwa mstari wa mbele katika kuokoa maisha ya mgonjwa huyo wanastahili kulindwa na kupewa mazingira salama wakati wa karantini. Hata hivyo, Dkt Atellah alisema watu wanaotambuliwa kuwa katika hatari ya kuambukizwa Ebola wanapaswa kufuatiliwa kwa karibu ili kuzuia uwezekano wa kusambaza maambukizi kwa wengine.
DODOMA: Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na Kongamano la 26 la SACCOS Afrika (SACCA Congress – 2026), linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 11 hadi 16, 2026. Ameyasema hayo leo, Oktoba 8, 2026, jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano hilo litakalowakutanisha…
CHINA: “Tanzania should assess development not only by the number of projects completed, but also by how those projects improve peoples lives, says” Dr Komba. Dr Komba, a member of the CCM Political Committee in China, said infrastructure completion and expenditure of allocated funds should be assessed alongside improvements in services, livelihoods and economic opportunities.…
Transfoma nne kubwa zimeanza kusafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda katika vituo vya kupoza umeme vya Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovoti 400 wa Iringa–Kisada–Mbeya–Tunduma–Sumbawanga (TAZA), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange. Usafirishaji huo unalenga kuwezesha kukamilika kwa mradi na kuanza…
MAREHEMU Raila Odinga Alhamisi alikumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kupigania mageuzi ya kisiasa, uhuru wa kidemokrasia na ushirikishaji wa wananchi. Wasomi, wanahabari na wadau wa siasa waliokutana katika Chuo Kikuu cha Daystar walisema mchango wa Raila kwa demokrasia utakumbukwa na vizazi vijavyo kwa miaka mingi. Katika kongamano la kumbukumbu la RAO2026 lililodumu kwa siku mbili, washiriki walitafakari safari ya kisiasa ya Raila, kuanzia miaka ya kuzuiliwa gerezani na kupambana akiwa upinzani hadi nafasi yake katika kujenga miungano ya kisiasa, kupigania mageuzi ya katiba na kushiriki katika siasa za kitaifa. Askofu mteule wa Kanisa la Anglikana Kenya, Dayosisi ya Garissa, Dkt Francis Omondi, alimtaja Raila kama kiongozi aliyefaulu kuunganisha makundi mbalimbali ya kisiasa na mtetezi wa utawala wa kidemokrasia barani Afrika. “Ni wachache wameacha alama kubwa katika safari ya Kenya kuelekea demokrasia kama Raila Odinga,” alisema Dkt Omondi. Alieleza kuwa mchango wa Raila haupaswi kupimwa kwa nafasi za uongozi alizoshikilia au uchaguzi aliogombea, bali kwa juhudi zake za kuimarisha demokrasia, utawala wa katiba na ushirikishaji wa kisiasa. Kwa mujibu wake, kukamatwa, kufungwa gerezani na kuandamwa kisiasa baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 1982 hakukumvunja moyo waka kumfanya akate tamaa, bali kulimfanya kuwa nembo ya mapambano ya kidemokrasia. Mkurugenzi Mkuu wa Nation Media Group, Geoffrey Odundo, alisema maisha ya kisiasa ya Raila yalijengwa juu ya kujitolea na kujinyima kwa manufaa ya taifa. “Alivumilia mengi na alipigania demokrasia na uhuru wetu. Tunapaswa kujiuliza tuko tayari kujitolea kiasi gani kwa manufaa ya jamii,” alisema. Bw Odundo pia alikumbuka uhusiano wa karibu ambao Raila alikuwa nao na wananchi wa kawaida, hasa wakazi wa Kibera, akisema kila alipokabili changamoto za kisiasa au alipokuwa na ujumbe mpya kwa wafuasi wake, angeenda moja kwa moja kwa wananchi. “Uhusiano wake na wananchi ulikuwa wa kipekee sana,” alisema. Washiriki wa kongamano pia walitambua mchango wake katika kupigania uhuru wa vyombo vya habari unaofurahiwa nchini leo. Katika ujumbe wake, Dkt Ida Odinga alisema Raila alichangia kwa kiasi kikubwa safari ya Kenya kuelekea demokrasia na kuhamasisha mamilioni ya watu Afrika na duniani kote. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Daystar, Profesa Laban Ayiro, alisema Raila atasalia kuwa mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika historia ya demokrasia ya Kenya, huku maisha yake ya kisiasa yakiendelea kuchochea mijadala kuhusu haki, mageuzi ya taasisi na utawala bora.
DAR ES SALAAM: THE Chama Cha Mapinduzi (CCM) National Executive Committee (NEC) Secretary for Economic and Financial Affairs, Jamal Kassim Ali, has called on the CCM Dar es Salaam Region to review the party’s contracts and investment projects, saying some existing agreements do not provide sufficient benefits to the party. Jamal made the remarks on…
DAR ES SALAAM: TANZANIA has today, October 8, 2026, joined countries around the world in commemorating Eye Health Day, with citizens urged to raise awareness about the importance of protecting eye health and seeking early intervention for vision problems. The Ministry of Health said eye health is an essential part of an individual’s overall health…
MANYARA: NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Methew, amezitaka Mamlaka za Maji mkoani Manyara kuhakikisha zinakamilisha miradi ya maji iliyofikia hatua za mwisho kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi mipya. Mhandisi Methew ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Manyara, iliyohitimishwa jana, Oktoba 7, 2026, akisisitiza umuhimu wa kutumia fedha…
MANYARA: Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Hanang’ kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo. Mhandisi Kundo ameelekeza mamlaka za maji mkoani Manyara kuhakikisha ifikapo 2030 Kila kijiji katika wilaya ya Hanang kinafikiwa huduma ya…
DODOMA: THE Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA) has presented an update on the implementation of recommendations raised by the Controller and Auditor General (CAG) for the 2024/25 financial year before the Parliamentary Public Accounts Committee (PAC) in Dodoma. During the meeting chaired by Acting Committee Chairperson Beng’i Issa, TAWA Board of Directors Chairperson Major General…
KALAMBO, Rukwa: CCM Youth Wing (UVCCM) Deputy Chairperson, Rehema Sombi (MNEC), is expected to officially launch CCM Youth Week today, October 8, 2026, in Kalambo District, Rukwa Region. The UVCCM Youth Week is scheduled to run until October 14, 2026, bringing together young people from different parts of the country to explore common opportunities, share…
TUME ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imeamuru Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku na Mbunge wa Mukurweini John Kaguchia kuondoa matamshi yao yaliyodaiwa kuchochea mgawanyiko wa kikabila na kisiasa. Maagizo hayo yalitolewa huku joto la kisiasa likizidi kupanda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Katika maamuzi mawili yaliyotolewa jana, Mwenyekiti wa NCIC Askofu Kepha Omae alisema matamshi ya Bw Ruku huko Tharaka Nithi yalihusu lawama za kikabila, huku ya Bw Kaguchia katika mkutano wa kisiasa Kieni, Nyeri, yakihusisha kutisha wananchi kwa misingi ya misimamo yao ya kisiasa. Kwa Bw Ruku, NCIC ililenga matamshi aliyotoa akiwa Kiang’ondi, Tharaka Nithi mwezi Julai. Tume ilisema Waziri huyo alikataa eneo la Mlima Kenya Mashariki kuchukuliwa kama “trela” ya Wakikuyu na pia akazungumzia madai kuwa baadhi ya watu wa Mlima Kenya Magharibi wanaamini Kenya ni yao. NCIC pia ilikosoa matumizi ya majina ya kikabila katika mjadala kuhusu maendeleo na uteuzi wa watu serikalini. “Kurejelea kwa jamii zao, madai kwamba watu wa Mlima Kenya Magharibi walifikiri Kenya ni yao na matumizi ya majina ya kikabila yalibadilisha malalamishi ya kitaasisi kuwa lawama za kikabila,” alisema Askofu Omae. Bw Ruku alikiri kutoa matamshi hayo alipofika mbele ya NCIC Septemba 1, lakini akasema Katiba inalinda kutambua jamii na madai ya usawa katika maendeleo na uteuzi wa watu serikalini. Alikanusha kuwa alikuwa na chuki dhidi ya watu wa jamii moja na akasema kauli yake kuhusu “kukanyaga shingo” ilikuwa lugha ya kisiasa iliyomaanisha kumshinda mpinzani kisiasa, wala si kumdhuru kimwili. Hata hivyo, NCIC ilisema wadhifa wake kama Waziri wa Serikali ulimpa ushawishi mkubwa na hivyo alipaswa kuwa mwangalifu zaidi. Tume imemwamuru Ruku kuondoa hadharani, kwa Kiswahili na Kiingereza, madai kwamba Wakikuyu wanaamini Kenya ni mali yao au wanawajibika kwa ukosefu wa usawa katika maendeleo na uteuzi. Kwa upande wa Kaguchia, NCIC ilisema matamshi yake katika mkutano wa Kieni Agosti yalivuka mipaka ya ushawishi wa kisiasa na kuwa vitisho kwa wananchi. Tume ilisema mbunge huyo aliwataka wafuasi wa Rais William Ruto, aliowataja kama wafuasi wa “Kasongo”, kutambuliwa, kufuatiliwa na kutolewa chini ya vitanda vyao. Bw Kaguchia alikamatwa Agosti 3 baada ya kuonekana katika kipindi cha Kiririmbi cha Inooro TV na baadaye kushtakiwa katika Mahakama ya Milimani kwa kosa la kutoa matamshi yanayoweza kuvuruga amani. Alipoitwa na NCIC, alipinga tafsiri ya Kiingereza ya matamshi yake ya Kikuyu, akitaka rekodi ya hotuba hiyo ichezwe na kutafsiriwa kwa Kikuyu. NCIC ilisema matamshi hayo yalikuwa na hatari ya kusababisha vitisho, kutengwa kwa watu na kudhoofisha ushiriki wa kisiasa kwa amani. Kaguchia ameagizwa kuomba msamaha hadharani na kutoa taarifa ya kusahihisha matamshi yake kwa Kikuyu, Kiswahili na Kiingereza, kwa kiwango kinacholingana na uenezaji wa hotuba yake ya awali.
RUKWA: Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (MNEC), Rehema Sombi anatarajiwa kuzindua rasmi Wiki ya Vijana wa CCM leo, Oktoba 8, 2026 Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa. Wiki hiyo ya UVCCM inatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 14, 2026, ikiwa na lengo la…
MBIO za kumtafuta mgombeaji atakayepeperusha bendera ya upinzani dhidi ya Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027 zinageuka vita vya kizazi, huku vijana wakitaka kuchukua nafasi ya viongozi waliotawala siasa kwa miongo kadhaa. Kwa upande mmoja kuna Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, wabunge Ndindi Nyoro (Kiharu) na Babu Owino (Embakasi East), Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. Kwa upande mwingine kuna vigogo kama Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front, Martha Karua wa People’s Liberation Party, Rigathi Gachagua wa Democracy for the Citizens Party (DCP) na Gavana wa Siaya James Orengo. Pia kuna kundi la wataalamu na vigogo waliotoka nje ya siasa za kawaida za uchaguzi akiwemo aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i, mfanyabiashara Jimi Wanjigi na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga. Hali hii imefanya kambi ya upinzani kuwa na wagombea wengi hata kabla ya vyama kuanza rasmi mchakato wa kumteua mgombea mmoja wa urais. Wachambuzi wanasema mjadala huu hauhusu umri pekee bali pia uzoefu wa kisiasa, mtandao wa kitaifa, uungwaji mkono wa maeneo, taaluma na uwezo wa kuvutia kizazi kipya cha wapigakura. Mjadala huo umeonekana zaidi kupitia Seneta Sifuna ambaye amezindua The Equitable Party (TEP), inayotarajiwa kubadilishwa jina kuwa Linda Mwananchi Movement. Kundi lake linasukuma tiketi inayowapa vijana nafasi kubwa, jambo linaloweza kuathiri mazungumzo ya kuunda muungano mpana wa upinzani. Mbunge Babu Owino ameunga mkono azma hiyo akisema wakati umefika kwa vijana kuongoza. “Vijana wa nchi hii huambiwa kila mara kuwa wao ni viongozi wa kesho. Sasa tunasema sisi ni viongozi wa leo na wakati wetu umefika,” alisema. Hata hivyo, juhudi za vijana zinakabiliwa na ukweli kwamba vyama mbalimbali vya upinzani vina watu wanaotaka kuwania urais. Seneta wa Kitui Enoch Wambua, mshirika wa Bw Musyoka, amesema anaendelea kumuunga mkono kiongozi huyo wa Wiper, ingawa hakufunga mlango wa ushirikiano na mrengo wa Sifuna. “Ukiangalia kwa karibu, Linda Mwananchi ina watu kutoka vyama mbalimbali vya Muungano wa Upinzani. Timu hizi mbili zina lengo moja la kuhakikisha Rais Ruto anahudumu kwa muhula mmoja,” alisema. Wakati huohuo, DCP ya Bw Gachagua imeibua mvutano na \Bw Nyoro. Katibu Mkuu wa DCP John Methu alishambulia People’s Progressive Party (PPK), akiitaja kama wilibaro ndogo na kudai inalenga kuwachanganya wapigakura na kupunguza ushawishi wa DCP eneo la Mlima Kenya. Mchambuzi wa siasa Javas Bigambo alisema Bw Nyoro ana haki ya kuwania urais. “Mkenya yeyote anaweza kuwania nafasi yoyote,” alisema, akiongeza kuwa hakuna mwanasiasa au chama chenye haki ya siasa za eneo fulani. Kwa upande wake, Dkt Matiang’i ametoa wito kwa wanasiasa wa upinzani kutotafsiri ushindani wao kama uadui. “Kenya yetu ni demokrasia ya vyama vingi. Hata sisi Jubilee tunataka kiti hicho cha urais na wengine pia wanakitaka, lakini sisi si maadui,” alisema. Bw Musyoka anajipanga kama mmoja wa vigogo wanaotaka kuunganisha makundi mbalimbali ya upinzani, huku Bw Gachagua akijikita zaidi katika kuunganisha Mlima Kenya chini ya DCP. Bi Karua na Bw Orengo pia wameonyesha nia ya kuwania urais. Wataalamu wanasema changamoto kubwa kwa vijana ni kubadilisha umaarufu na ushawishi wa mitandao ya kijamii kuwa mtandao wa mashinani unaohitajika katika uchaguzi wa urais. Wakati huo huo, wagombea kama Dk Matiang’i, Bw Wanjigi na Bw Maraga wanajaribu kutumia rekodi zao za kitaaluma, utawala na utumishi wa umma kama njia mbadala ya siasa za kawaida. Seneta wa Busia Okiya Omtatah naye anajikita katika mageuzi ya Katiba, utawala wa sheria na kupunguza mamlaka makubwa ya urais. Mchambuzi Dismas Mokua anasema vita hivyo huenda visitatuliwe na umri wa wagombea bali uwezo wao wa kuunda muungano mpana unaovuka misingi ya kikabila, maeneo na vyama.