JUHUDI za kampuni moja kuingiza nchini tani 540,000 za mahindi kutoka Zambia zimekumbwa na mzozo wa kisheria huku maswali yakiibuka kuhusu jinsi ilivyoidhinishwa na iwapo zilihusishwa na mpango wa serikali wa kuagiza mahindi.
Kesi iliyowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Mombasa inalenga kusimamisha uagizaji wa takriban magunia milioni sita ya mahindi, kila moja likiwa na uzani wa kilo 90.
James Mwikabi ameomba mahakama isimamishe mpango huo, akidai serikali imeanza kuwezesha uagizaji kabla kuhalalishwa.
Katika kesi yake anataka mahakama itoe amri ya muda ya kuzuia serikali, maafisa wake au taasisi zake kuidhinisha, kuwezesha, kusafisha au kutoa mahindi hayo bandarini.
"Mahakama hii itoe amri ya muda ya kuzuia utekelezaji, kuwezesha, kuidhinisha au kuachilia takriban tani 540,000 za mahindi yanayopendekezwa kuagizwa na kampuni ya Baita Trading Company Limited,” anasema Mwikabi katika kesi yake.
Pia anataka serikali ifichue iwapo kampuni hiyo imepewa sehemu ya mgao wa mpango wa kitaifa wa kuagiza mahindi au kupewa msamaha wa ushuru, punguzo la kodi au upendeleo mwingine wa kisheria.Mnamo Oktoba 5, Mahakama Kuu ya Mombasa ilitaja kesi hiyo kuwa ya dharura na kuamuru stakabadhi za kesi ziwasilishwe kwa Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe na mwenzake wa Fedha John Mbadi.
Stakabadhi hizo zinapaswa kuwasilishwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya (KRA), Mwanasheria Mkuu, Mamlaka ya Bandari Kenya na Baita Trading Company Limited, miongoni mwa washtakiwa wengine.
“Baada ya kusoma kesi hii, nimeridhika kwamba ni ya dharura na hivyo imethibitishwa kuwa la dharura,” mahakama ilisema.
Mwikabi anasema kesi yake si dhidi ya uagizaji wa mahindi au biashara halali ya kimataifa, bali inahusu jinsi mamlaka ya umma ilivyotumika kuwezesha mpango huo.
Anataka serikali ieleze iwapo Baita ilipewa sehemu ya mpango wa serikali wa kuagiza mahindi na ikiwa iliahidiwa msamaha wa ushuru, punguzo la kodi au upendeleo wa forodha.
Kwa mujibu wa Mwikabi, serikali ilitangaza Agosti 19 kuwa ingewezesha kuingizwa nchini kwa takriban magunia milioni 25 ya mahindi ya kilo 90 ili kukabiliana na upungufu uliotarajiwa, kuongeza upatikanaji na kuzuia bei kupanda.Mnamo Agosti 28, Baita ilitangaza kuwa ilikuwa tayari kununua mahindi kwa wingi kutoka Zambia kuyaleta nchini.
Baadaye kampuni hiyo ilidaiwa kufanya makubaliano na Food Reserve Agency ya Zambia ya kununua na kusafirisha nchini tani 540,000 za mahindi.
Kiasi hicho ni sawa na magunia milioni sita na kinawakilisha sehemu kubwa ya mahitaji yaliyotangazwa na serikali.Mwikabi anataka serikali kutoa tathmini iliyotumika kuamua kiasi cha mahindi kitakachoagizwa, ikiwemo tathmini ya chakula, uchumi na uzalishaji wa ndani.
Anasema mahakama haiombwi kuamua bei ya mahindi, bali kuchunguza iwapo maslahi ya wakulima, usalama wa chakula na soko la ndani yalizingatiwa.
Mpango wa kuingiza magunia milioni 6 ya mahindi nchini wapingwa kortini

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…