MAHAKAMA Kuu imebatilisha uamuzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) wa kuacha kumshtaki Waziri na aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuhusu madai ya ufisadi wa Sh56.7 milioni.
Jaji Benjamin Musyoki alisema ODPP ilikiuka taratibu na Katiba ilipobadilisha uamuzi wake wa awali wa kumshtaki Oparanya bila kuhusisha Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), iliyokuwa imefanya uchunguzi.
Jaji alitangaza uamuzi wa ODPP wa Julai 8, 2024 kuwa batili na kuamuru uamuzi huo uondolewe.
“Ni baada tu ya EACC kuchunguza ushahidi huo unaodaiwa kuwa mpya ndipo ODPP ingekuwa na mamlaka ya kikatiba kufanya uamuzi kuhusu suala hilo,” alisema Jaji Musyoki.
EACC ilikuwa imependekeza Oparanya ashtakiwe kwa makosa ya kula njama ya kutenda ufisadi, mgongano wa kimaslahi, kutumia vibaya mamlaka na ulanguzi wa pesa.
Uchunguzi huo ulihusisha madai kwamba Oparanya alipokea Sh56.74 milioni kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni zilizopata kandarasi kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Kakamega wakati wa uongozi wake kati ya 2013 na 2022.
EACC ilisema baadhi ya pesa hizo zilitumika kununua mali katika mtaa wa Karen, Nairobi.
Awali, ODPP ilikuwa imekubaliana na pendekezo la EACC la kumshtaki Oparanya mnamo Desemba 18, 2023.
Hata hivyo, baada ya mawakili wa Oparanya kuomba mapitio ya uamuzi huo Julai 3, 2024, ODPP iliamuru faili hiyo ifungwe, ikisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhakikisha ana hatia
EACC ilipinga uamuzi huo na baadaye ikasisitiza pendekezo lake la kumshtaki Oparanya, ikisema haikuhusishwa katika mchakato wa kupitia upya faili ya kesi.
Mwanaharakati wa haki Fredrick Mulaa ndiye aliyewasilisha suala hilo mahakamani, akipinga uamuzi wa ODPP.
EACC iliunga mkono kesi hiyo, ikisema uchunguzi wake ulionyesha kulikuwa na msingi wa kumshtaki Oparanya.
Tume hiyo ilisema ilichunguza kandarasi 60 zilizotolewa kwa kampuni sita na Kaunti ya Kakamega za thamani ya zaidi ya Sh2.2 bilioni.
Aidha, EACC ilikuwa imepata amri ya kuzuilia Sh28.9 milioni zilizoshukiwa kuwa mapato ya ufisadi.
Jaji Musyoki alisema ingawa ODPP ina mamlaka ya kuamua iwapo mtu atashtakiwa, mamlaka hayo hayaipatii haki ya kuchukua nafasi ya EACC katika uchunguzi.
“Taasisi ya kikatiba au kisheria haifai kutumia mamlaka au busara zake kiholela bila kuzingatia maslahi ya washiriki wengine katika suala linalohusika,” alisema.
Jaji alisema mwongozo wa ODPP wa 2019 kuhusu uamuzi wa kushtaki unahitaji mwendesha mashtaka kushauriana na mpelelezi anapoamua kutowasilisha mashtaka.
“Ni wazi kwamba barua ya ODPP ya Julai 8, 2024 iliandikwa bila kushauriana na EACC,” alisema.
Aliongeza kuwa ODPP ilivuka mipaka kwa kupokea ushahidi uliodaiwa kuwa mpya na kuamua yenyewe kupitia upya uamuzi wa kumshtaki Oparanya bila kuhusisha EACC.
Hata hivyo, mahakama ilikataa ombi la kubatilisha uteuzi wa Oparanya kuwa Waziri.
Jaji alisema Bunge lilimkagua na kuidhinisha uteuzi wak na mahakama haikupewa ushahidi wa kuonyesha kuwa mchakato wa kikatiba ulikiukwa.
Jaji afuta uamuzi wa kuondolea Oparanya mashtaka ya ufisadi

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…