GAVANA wa Nairobi, Johnson Sakaja, aliingia ofisini mwaka wa 2022 akiwa na ahadi kubwa ya kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sambamba Nairobi lakini miaka minne baadaye takwimu za matumizi ya fedha za umma zinaibua swali iwapo jiji hilo limetimiza lengo hilo.
Bw Sakaja alipokuwa akihutubu wakati wa kuapishwa kwake Agosti 2022, alikumbuka maisha yake ya utotoni Ngara na jinsi alivyoshangaa kuona baadhi ya mitaa ikiwa safi, yenye barabara nzuri na iliyopangwa huku mingine ikiwa katika hali mbaya.Alisema akiwa na umri wa miaka saba aliwahamasisha watoto wenzake kuandamana wakitaka mazingira yao yaimarishwe.
“Nilijifunza kuwa eneo hilo halikuwa na watu bora zaidi; walikuwa wamejipanga, walikuwa na hisia za jamii, walichagua uongozi mzuri na mambo yakawa sambamba,” alisema.
Hata hivyo, ripoti za matumizi zinaonyesha Nairobi bado inakabiliwa na changamoto kubwa za maendeleo. Katika miaka minne ya uongozi wa Bw Sakaja, kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2026, serikali ya kaunti ilitumia Sh125 bilioni.Kati ya fedha hizo, Sh15.4 bilioni pekee, sawa na asilimia 12.36, zilitumika kwa miradi ya maendeleo huku Sh109.5 bilioni zikitumika katika shughuli za kawaida.
Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma inataka angalau asilimia 30 ya matumizi ya kaunti yaelekezwe kwa maendeleo.Hii ina maana kuwa Nairobi ilipaswa kutumia takriban Sh37.5 bilioni kwa maendeleo, tofauti ya zaidi ya Sh22 bilioni ambazo zingetumika kujenga barabara, hospitali, masoko na miradi mingine.
Kituo cha Centre for Economic Governance (CEG), kinasema Nairobi ni miongoni mwa kaunti zinazofanya vibaya zaidi katika matumizi ya fedha za maendeleo.Changamoto hiyo pia imeonekana katika miradi iliyokwama.
Kufikia Juni, Nairobi ilikuwa na miradi 57 iliyokwama ya thamani ya zaidi ya Sh2 bilioni.Miongoni mwa hiyo ni jengo la matibabu la Sh256 milioni katika Hospitali ya Mbagathi, ukumbi wa kijamii wa Mwiki wa thamani ya Sh76 milioni na wodi ya uzazi ya Sh30 milioni katika Kituo cha Afya cha Umoja 1.
Mdhibiti wa Bajeti, Margaret Nyakang’o, alisema miradi hiyo ilikwama kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wakandarasi kuondoka kwa kukosa malipo.
Wakati huo huo, zaidi ya nusu ya Sh125 bilioni zilizotumiwa na serikali ya Sakaja zilienda kwa mishahara na marupurupu.Takriban Sh63.3 bilioni zilitumika kwa mishahara, sawa na asilimia 50.65 ya matumizi yote.
Ukaguzi pia umeibua maswali kuhusu mfumo wa malipo wa kaunti. Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilitaja Sh1.9 bilioni zilizotolewa kutoka akaunti ya mishahara bila kaunti kueleza zilitumika vipi.Aidha, Sh840.4 milioni zilizotajwa kama gharama za wafanyakazi zilikosa stakabadhi muhimu za kuthibitisha waliolipwa.Idadi ya wafanyakazi wa kaunti pia imeongezeka kutoka 13,354 mwaka 2023 hadi 19,258 Juni 2025.
Katika sekta ya taka, kaunti ilitumia Sh1.7 bilioni mwaka 2024/25, huku data nyingine ya City Hall ikionyesha matumizi ya Sh3 bilioni. Mkaguzi Mkuu alisema malipo ya Sh361 milioni hayakuwa na stakabadhi za kutosha kuthibitisha huduma zilizotolewa.
Nairobi pia ilitumia Sh2.6 bilioni kwa mawakili wa nje mwaka 2024/25, licha ya kuwa na zaidi ya mawakili 100 katika idara yake ya sheria. Ofisi ya Bajeti ya Bunge pia iliorodhesha Nairobi miongoni mwa kaunti zilizofanya vibaya katika matumizi ya rasilimali za umma.Nairobi inachangia karibu theluthi moja ya uchumi wa Kenya, ikiwa na shughuli za kiuchumi zenye thamani ya Sh4.1 trilioni mwaka 2024.
Bw Sakaja sasa anaingia mwaka wa mwisho wa muhula wake wa kwanza huku akitakiwa kukabiliana na changamoto za mishahara, miradi iliyokwama, taka na matumizi ya fedha za umma ambazo zinaendelea kuathiri huduma kwa wakazi.
Serikali ya Sakaja yafyonza Sh125 bilioni miradi ikikwama

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…