TUME ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imeamuru Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku na Mbunge wa Mukurweini John Kaguchia kuondoa matamshi yao yaliyodaiwa kuchochea mgawanyiko wa kikabila na kisiasa.
Maagizo hayo yalitolewa huku joto la kisiasa likizidi kupanda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Katika maamuzi mawili yaliyotolewa jana, Mwenyekiti wa NCIC Askofu Kepha Omae alisema matamshi ya Bw Ruku huko Tharaka Nithi yalihusu lawama za kikabila, huku ya Bw Kaguchia katika mkutano wa kisiasa Kieni, Nyeri, yakihusisha kutisha wananchi kwa misingi ya misimamo yao ya kisiasa.
Kwa Bw Ruku, NCIC ililenga matamshi aliyotoa akiwa Kiang’ondi, Tharaka Nithi mwezi Julai.
Tume ilisema Waziri huyo alikataa eneo la Mlima Kenya Mashariki kuchukuliwa kama “trela” ya Wakikuyu na pia akazungumzia madai kuwa baadhi ya watu wa Mlima Kenya Magharibi wanaamini Kenya ni yao.
NCIC pia ilikosoa matumizi ya majina ya kikabila katika mjadala kuhusu maendeleo na uteuzi wa watu serikalini.
“Kurejelea kwa jamii zao, madai kwamba watu wa Mlima Kenya Magharibi walifikiri Kenya ni yao na matumizi ya majina ya kikabila yalibadilisha malalamishi ya kitaasisi kuwa lawama za kikabila,” alisema Askofu Omae.
Bw Ruku alikiri kutoa matamshi hayo alipofika mbele ya NCIC Septemba 1, lakini akasema Katiba inalinda kutambua jamii na madai ya usawa katika maendeleo na uteuzi wa watu serikalini.
Alikanusha kuwa alikuwa na chuki dhidi ya watu wa jamii moja na akasema kauli yake kuhusu “kukanyaga shingo” ilikuwa lugha ya kisiasa iliyomaanisha kumshinda mpinzani kisiasa, wala si kumdhuru kimwili.
Hata hivyo, NCIC ilisema wadhifa wake kama Waziri wa Serikali ulimpa ushawishi mkubwa na hivyo alipaswa kuwa mwangalifu zaidi.
Tume imemwamuru Ruku kuondoa hadharani, kwa Kiswahili na Kiingereza, madai kwamba Wakikuyu wanaamini Kenya ni mali yao au wanawajibika kwa ukosefu wa usawa katika maendeleo na uteuzi.
Kwa upande wa Kaguchia, NCIC ilisema matamshi yake katika mkutano wa Kieni Agosti yalivuka mipaka ya ushawishi wa kisiasa na kuwa vitisho kwa wananchi.
Tume ilisema mbunge huyo aliwataka wafuasi wa Rais William Ruto, aliowataja kama wafuasi wa “Kasongo”, kutambuliwa, kufuatiliwa na kutolewa chini ya vitanda vyao.
Bw Kaguchia alikamatwa Agosti 3 baada ya kuonekana katika kipindi cha Kiririmbi cha Inooro TV na baadaye kushtakiwa katika Mahakama ya Milimani kwa kosa la kutoa matamshi yanayoweza kuvuruga amani.
Alipoitwa na NCIC, alipinga tafsiri ya Kiingereza ya matamshi yake ya Kikuyu, akitaka rekodi ya hotuba hiyo ichezwe na kutafsiriwa kwa Kikuyu.
NCIC ilisema matamshi hayo yalikuwa na hatari ya kusababisha vitisho, kutengwa kwa watu na kudhoofisha ushiriki wa kisiasa kwa amani.
Kaguchia ameagizwa kuomba msamaha hadharani na kutoa taarifa ya kusahihisha matamshi yake kwa Kikuyu, Kiswahili na Kiingereza, kwa kiwango kinacholingana na uenezaji wa hotuba yake ya awali.
Adhabu ya pamba: NCIC yaamuru Ruku, Kaguchia kuomba msamaha

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…