Nairobi, Kisumu, Busia na Mandera ni miongoni mwa kaunti zilizo katika hatari kubwa ya kukumbwa na athari za mvua ya El Niño, kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Kukabiliana na Majanga (NDOC).
Kati ya kaunti 18 zinazokabiliwa na uwezekano wa majanga kutokana na utabiri wa mvua nyingi kuliko kawaida, serikali imetambua kaunti hizo nne kuwa miongoni mwa zinazoweza kuathirika zaidi.
Wakati huohuo, takriban watu milioni 1.5 wanatarajiwa kuathiriwa na mvua hiyo, huku serikali ikikadiria kuwa watu 500,000 wanaweza kulazimika kuhama makazi yao.
Mkurugenzi wa NDOC, Kanali David Samoei, alisema serikali imepatia kaunti hizo nne kipaumbele na inaendeleza hatua za kuzuia au kupunguza athari za majanga yanayoweza kutokea.
Alisema serikali imekuwa ikijiandaa tangu Idara ya Hali ya Hewa nchini itoe tahadhari kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua nyingi kuliko kawaida katika kipindi cha Oktoba, Novemba na Desemba.
“NDOC imeangazia zaidi Nairobi na kufanya mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga. Kaunti ya Kisumu pia huenda ikaathirika zaidi kutokana na Mto Nyando, na kwa sasa tunafanya kazi katika kingo za mto huo,” alisema Kanali Samoei.
Aliongeza kuwa Busia huenda ikaathirika kutokana na Mto Nzoia na eneo la Budalangi, ambako maafisa wa serikali wanaendelea na maandalizi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Rasilimali za Maji.
“Mandera inaweza kukumbwa na changamoto iwapo barabara inayounganisha Mandera na Wajir itafunikwa na maji ya mafuriko,” alisema.
Kanali Samoei alisema serikali imejiandaa vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na El Niño na hatua za usalama zinazopaswa kuchukuliwa.
Alisema NDOC imeratibu vituo vya uokoaji na makazi salama na serikali za kaunti, ambavyo vitatumika iwapo majanga yatatokea.
“Tunathibitisha kuwa Idara ya Hali ya Hewa imekuwa ikitoa utabiri sahihi katika siku za hivi karibuni. Kwa hivyo, tulichukulia tahadhari yake kwa uzito na kuanza maandalizi.
“Tumeendesha mazoezi ya kujiandaa kukabiliana na majanga katika maeneo ya Nairobi, Garissa na Naivasha. Lengo letu ni kuhakikisha hakuna maisha yatakayopotea katika kipindi hiki kwa kuchukua hatua mapema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa idara hiyo,” alisema.
Kanali Samoei alikuwa akizungumza katika kongamano la siku tatu lililofanyika Nakuru, lililowaleta pamoja wataalamu na wadau kujadili namna ya kujiandaa kukabiliana na majanga.
Waliohudhuria ni pamoja na mashirika ya kibinafsi, taasisi na mashirika ya serikali pamoja na wasomi, ambao walitarajiwa kubadilishana mawazo kuhusu maandalizi ya kukabiliana na majanga.
Baada ya kongamano hilo, washiriki wataadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari za Majanga (IDDRR) Oktoba 13.
Kanali Samoei aliwahakikishia wananchi kuwa serikali inachukua hatua za kulinda usalama wao, huku akiwashauri kufuata miongozo itakayotolewa mara kwa mara na kamati ya usimamizi.
“Serikali imetenga rasilimali za kutosha kukabiliana na majanga hayo, huku ikitarajia pia kupata msaada kutoka kwa washirika na sekta ya kibinafsi iwapo kutatokea tatizo,” alisema.
Naibu Gavana wa Nakuru, David Kones, aliyeshiriki kongamano hilo, alisema serikali ya kaunti imekuwa ikielimisha wakazi kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za kuzuia majanga kuanzia ngazi ya familia.
El Niño: Wakenya milioni 1.5 wako hatarini katika maeneo haya

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…