MANYARA: Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Hanang’ kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.
Mhandisi Kundo ameelekeza mamlaka za maji mkoani Manyara kuhakikisha ifikapo 2030 Kila kijiji katika wilaya ya Hanang kinafikiwa huduma ya maji.
Kundo amesema hayo wilayani Hanang’, mkoani Manyara, wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ambapo amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara kuhakikisha wananchi hawatembei zaidi ya kilomita mbili kufuata huduma ya maji, kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu na makazi yao.
Amezielekeza mamlaka za maji mkoani Manyara kuhakikisha ifikapo 2030 Kila kijiji katika wilaya ya Hanang kinafikiwa huduma ya maji.
Alisema mkoa wa Manyara bado vijiji 55 vimebaki kutokuwa na huduma rasmi ya maji safi na salama ambapo katika wilaya ya Hanang bado vijiji 20 pekee ambavyo vimebaki kutokuwa na miundombinu rasmi.
”Hakuna nchi itaendelea bila kujali sekta ya maji,maji ni uhai ni siasa na ni afya yetu pamoja na nguvu kazi ya taifa” Aliongeza kuwa
”Maji ni uchumi, uwekezaji ambapo kupitia uwepo wa maji shughuli mbalimbali zitafanyika,” alisema Mhandisi Kundo.
Aliwahimiza wananchi wa kijiji cha Mulbadaw kulinda miundombinu ya maji ikiwemo vyanzo vya maji ili iwe endelevu itakayosaidia vizazi vijavyo.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Hanang wameishukuru serikali na kwamba kwa muda mrefu walikuwa wakimfuata huduma ya maji kwa kutembea zaidi ya kilomita 5.
Serikalu yaahidi maji safi vijiji vyote Hanang

This story was originally published by Habari Leo.
Read the full story at Habari LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…