Juhudi za Kalonzo Musyoka kubadilisha jina na muundo wa muungano wa Azimio la Umoja kuwa The Ukombozi Alliance (TUA) zinaweza kumweka katika nafasi nzuri ya kuwania urais kwa tiketi ya upinzani au kumtenga na viongozi wengine kuelekea uchaguzi wa 2027.
Kalonzo, ambaye anaongoza chama cha Wiper, amekuwa mstari wa mbele katika kuunda upya muungano huo baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyekuwa kiongozi wake.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani wanapinga kujiunga na TUA, wakisema wanataka kuhifadhi utambulisho wa vyama vyao na kuunda muungano mpya.
Chama cha DCP kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na vuguvugu la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna vimeonyesha kusitasita kujiunga na TUA.
Bw Sifuna alisema chama chake kipya, The Equitable Party, kinapanga kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu miungano.
“Kwa sasa chama changu kinafanyiwa mabadiliko makubwa. Tuna miundo ya kuweka na makataa ya Tume ya Uchaguzi na Msajili wa Vyama vya Kisiasa ya kuzingatia. Mazungumzo kuhusu miungano yatakuja baadaye,” alisema.
Kalonzo naye amewataka wabunge wa Wiper walioonekana kushirikiana na Bw Sifuna kuzingatia shughuli za chama chao. Alitaja Mbunge wa Kaiti Joshua Kimilu na mwenzake wa Wundanyi Danson Mwashako.
Hali hii inaashiria ushindani wa kutafuta uungwaji mkono mashinani na udhibiti wa vyama huku viongozi wakijaribu kuungana kumuondoa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.
Naibu kiongozi wa Jubilee Jeremiah Kioni alisema chama hicho hakina haraka ya kujiunga na TUA, akisema upinzani unahitaji mawazo mapya.
Alisema baadhi ya wanasiasa waliounga mkono mgombea wa Azimio katika uchaguzi wa 2022 walipata hasara kisiasa katika maeneo yao, na hawako tayari kujitolea tena kwa mpangilio kama huo.
Hata hivyo, viongozi wa Democratic Party Justin Muturi na wa DAP-K Eugene Wamalwa wameunga mkono TUA kama chombo kinachoweza kumshinda Rais Ruto. Wote wamekuwa wakifanya kampeni pamoja na Kalonzo, ambaye wanamchukulia kama mgombeaji anayefaa kupewa tiketi ya urais.
Mzozo huo unatokana na kipengele cha makubaliano ya muungano ambacho awali kilionekana kumpa kiongozi wa chama nafasi ya moja kwa moja kuwa mgombea urais. Washirika wa Kalonzo wanasema kipengele hicho kimebadilishwa na sasa wanachama wote wanaweza kuwania tiketi hiyo.
Kalonzo pia amesisitiza kuwa kujiuzulu kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama mwenyekiti wa baraza la muungano hakujasababisha pengo la uongozi ndani ya TUA.
Kuna juhudi za kumshawishi Bw Gachagua achukue nafasi ya Bw Kenyatta ili kuvutia DCP kujiunga na muungano huo. Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye anahusishwa na Linda Mwananchi, pia ametajwa kama anayeweza kupewa nafasi hiyo ili kuvutia wafuasi wa Nyanza.
Hata hivyo, Mbunge wa Gatanga Edward Muriu, mshirika wa Bw Gachagua, alisema DCP inataka kwanza kuimarisha uungwaji mkono wake kabla ya kujadiliana na vyama vingine kuunda muungano mkubwa.
Mchambuzi wa siasa Profesa David Monda alisema TUA inaweza kuwa vigumu kupata uungwaji mkono wa kutosha bila kuwashirikisha Kalonzo, Sifuna, Gachagua na aliyekuwa Waziri wa utawala wa ndani Fred Matiang’i katika mpangilio mmoja.
Alisema viongozi hao wanapaswa kuungana ili kumshinda Rais Ruto au kuhatarisha kushindwa kila mmoja akigombea urais kivyake.
Wanaounga mkono TUA wanataka muungano huo uige mfano wa National Rainbow Coalition (Narc), uliomuingiza Mwai Kibaki mamlakani mwaka 2002. Chini ya mfumo huo, vyama havikuvunjwa lakini viliunga mkono mgombea mmoja wa urais na ajenda ya pamoja.
Lengo ni kuzuia upinzani kugawanyika na kumpa Rais Ruto nafasi ya kushinda uchaguzi wa 2027.
Dalili Kalonzo anarukwa na vinara wa upinzani kuhusu Ukombozi Alliance

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…