WABUNGE sasa wanapanga kuondoa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika usimamizi au kusikiliza migogoro inayotokana na mchujo ndani ya vyama vya kisiasa, wakisema hatua hiyo itaongeza uhuru wa vyama hivyo.
Wakati wa kujadili Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa mwaka 2024, wabunge walisisitiza kuwa vyama vya kisiasa ni taasisi huru zenye haki ya kusimamia shughuli zao za ndani bila kuingiliwa na IEBC.
Wanataka Sheria ya Uchaguzi ifanyiwe marekebisho ili kuondoa mamlaka ya IEBC kushughulikia migogoro ya uteuzi wa wagombea ndani ya vyama na jukumu hilo lihamishiwe Mahakama ya Kutatua Migogoro ya Uchaguzi.
Kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 88 inapatia IEBC jukumu la kusimamia au kuendesha kura za maamuzi na uchaguzi.
Aidha, Ibara ya 88(4)(e) inaeleza kuwa tume hiyo ina wajibu wa kushughulikia migogoro ya uchaguzi, ikiwemo inayotokana na uteuzi wa wagombea, isipokuwa kesi za uchaguzi na migogoro inayozuka baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Hata hivyo, wabunge wanasema kuhusika kwa IEBC katika mchujo wa vyama kunadhoofisha uhuru wa vyama vya kisiasa.Kwa mujibu wao, uamuzi wa kumpa mwanasiasa tiketi ya moja kwa moja au kupitia mchujo ni haki ya chama husika pekee.
Kwa msingi huo, wanadai IEBC haipaswi kuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamishi yanayotokana na maamuzi hayo.Pia walieleza kuwa kushiriki kwa IEBC katika michakato ya vyama ni sawa na kuingilia masuala ya ndani ya vyama vya kisiasa. Hoja nyingine iliyotolewa ni uwezekano wa mgongano wa maslahi.
Walisema baadhi ya vyama hupatia IEBC jukumu la kusimamia mchujo kutokana na uwezo wake wa kiteknolojia na kiutawala. Hivyo, si sahihi kwa tume hiyo hiyo kusikiliza migogoro inayotokana na uchaguzi ambao imesimamia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria, George Murugara, alisema wabunge wanataka jukumu la IEBC katika kusuluhisha migogoro ya uteuzi lifutwe kabisa.
“Tunataka kuondoa jukumu la IEBC katika kushughulikia migogoro inayotokana na uteuzi wa wagombeaji. Migogoro hiyo ishughulikiwe na Mahakama ya Kutatua Migogoro ya Uchaguzi,” alisema Murugara.
Mbunge wa Ugenya, David Ochieng’, alisema Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa inapaswa kuimarisha vyama ili viweze kusimamia shughuli zao kwa uhuru.
“IEBC haina kazi katika uteuzi wa ndani ya vyama. Vyama ni kama vilabu. Kama chama kinaamua kunipa tiketi ya moja kwa moja, hilo ni suala lake. Kwa nini IEBC ihusike?” alihoji.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wanawake wa Baringo, Florence Jematiah, alisema hana tatizo IEBC kusaidia vyama visivyo na uwezo wa kusimamia uchaguzi wa mchujo.
Hata hivyo, alionya kuwa matatizo huibuka pale tume hiyo hiyo inapolazimika kusikiliza migogoro inayotokana na mchujo iliyoendesha.
Kulingana na Mpango wa Uchaguzi wa 2025-2027 uliozinduliwa Mei, vyama vyote vinavyokusudia kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027, vinapaswa kukamilisha mchujo na kutatua migogoro yote ifikapo Mei 9, 2027.
Ratiba hiyo pia inaeleza kuwa wagombea wasioridhika na namna vyama vyao vilivyoshughulikia malalamishi yao watakuwa na hadi Juni 12, 2027 kuwasilisha kesi kwa IEBC, ambayo itatakiwa kutoa uamuzi ndani ya siku 10.
Wabunge wataka IEBC ijitenge na mchujo vyamani

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…