KIONGOZI wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, amethibitisha kuwa ranchi iliyopo jimbo la Texas nchini Amerika ambayo imezua mijadala mitandaoni ni mali yake binafsi na kwamba ataishi hapo kwa siku 15 zaidi baada ya kukamilisha ziara yake ya kisiasa nchini humo.
Bw Gachagua, aliondoka Kenya mnamo Agosti 26, anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya siku 50 nchini Amerika mjini Boston mnamo Oktoba 10. Hata hivyo, badala ya kurejea nyumbani mara moja, ataelekea katika ranchi hiyo kwa kile chama chake kimetaja kuwa ni mkutano maalum wa kupanga mikakati ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Ranchi hiyo ilivutia hisia za umma mwishoni mwa Septemba baada ya Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya kusambaza picha na video mitandaoni akiwa pamoja na Bw Gachagua katika eneo hilo.
Akizungumzia kuhusu mali hiyo, Bw Gachagua alisema ranchi hiyo ni yake na akaiita “Wamunyoro Texas”, akiilinganisha na makazi yake maarufu ya Wamunyoro nchini Kenya.
“Ndiyo, mali hiyo ni yangu. Ni Wamunyoro yangu nyingine ya faragha,” alisema.
Kauli hiyo inafanana na matamshi aliyotoa Septemba 26 alipokutana na Wakenya wanaoishi Texas. Wakati huo alisema alifurahia wageni kukutana katika makazi hayo badala ya hoteli ili kuunda mazingira ya kifamilia na ya karibu zaidi.
Picha zilizochapishwa na Bw Gachagua zinaonyesha nyumba kubwa ya ghorofa moja iliyojengwa kwa matofali mekundu, ikiwa katikati ya eneo pana lenye nyasi zilizopambwa vizuri. Pia kuna sehemu za kuketi nje, farasi na ng’ombe wa aina ya Texas Longhorn wanaonekana ndani ya ranchi hiyo iliyozungushiwa ua.
Gari dogo la matumizi ya ndani ya ranchi pia linaonekana likiwa na maandishi “Wamunyoro Texas” na “Riggy G”.
Mbunge Salasya alisema aliguswa na mafanikio ya Gachagua baada ya kutembelea ranchi hiyo.
“Nilimwambia natamani siku moja niwe na mali kama hii. Aliniambia siri ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya kifedha na kumwamini Mungu,” alisema.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa DCP, John Methu, Bw Gachagua amezuru miji mitano tofauti tangu aanze shughuli za kisiasa nchini Amerika. Baada ya kupumzika kwa siku kumi, alifanya mikutano Spokane, Washington, Portland, Oregon, Kansas City, Missouri na baadaye Texas kabla ya kuelekea Boston.
Methu alisema kipindi atakachotumia katika ranchi hiyo kitahusisha mikutano na washirika wa kisiasa, wataalamu na marafiki wa kimataifa kujadili mikakati ya chama hicho. Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na ujenzi wa miungano ya kisiasa, uteuzi wa mgombea wa pamoja wa urais dhidi ya Rais William Ruto mwaka 2027 na mapendekezo ya kufufua uchumi wa Kenya.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kupunguza kutegemea mikopo, kuunganisha mashirika ya umma, kupanua wigo wa kodi na kuongeza mapato ya serikali za kaunti.
Mratibu wa DCP nchini Amerika, Joseph Warui, alisema mikutano hiyo pia itatumika kutathmini zaidi ya vikao 80 vya umma na vya faragha ambavyo Bw Gachagua amehudhuria wakati wa ziara yake. Aliongeza kuwa washiriki watajadili hali ya uchumi, haki za binadamu na mustakabali wa kisiasa wa Kenya.
Hata hivyo, tarehe rasmi ya kurejea kwa Bw Gachagua nchini Kenya bado haijatangazwa. Chama chake kimesema taarifa hiyo itatolewa baadaye baada ya kukamilika kwa shughuli zote alizopanga nchini humo.
Wamunyoro Texas iliyopo Amerika ni mali yangu, Gachagua

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…