Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anapania kujenga vuguvugu jipya la kisiasa linalozingatia Katiba, uwajibikaji na uchumi unaowajali wananchi, huku akijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 2027.
Chama chake kipya, The Equitable Party (TEP), kinatarajiwa kubadilishwa jina na kuitwa Linda Mwananchi Movement kufuatia uamuzi wa Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) mnamo Oktoba 8, 2026.
Mbali na jina, chama hicho kinapanga kubadilisha katiba yake, rangi rasmi, nembo na kuhamisha makao makuu yake. Hatua hizo zinaashiria juhudi za Bw Sifuna kujijenga upya baada ya kutengana na ODM alikohudumu kama katibu mkuu kwa karibu miaka kumi.
Hata hivyo, msimamo wake kuhusu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua mwaka 2024 unaweza kuibua maswali anapojaribu kuunganisha upinzani dhidi ya Rais William Ruto.
Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi Ijumaa, Bw Sifuna alitetea jukumu lake katika mchakato huo, akisema haupaswi kuzuia viongozi waliokuwa na tofauti kushirikiana katika uchaguzi ujao.
Alipoulizwa jinsi atakavyoshirikiana na Bw Gachagua, ambaye sasa anaongoza chama cha DCP, alisema: “Tayari nilimuondoa madarakani kwa makosa yake. Kwa hivyo, hamuwezi kuniuliza maoni yangu kuhusu makosa ambayo tayari nilimwadhibu.”
Bw Gachagua ametangaza kuwa yuko tayari hata kuwa naibu wa Bw Sifuna ikiwa upinzani utaamua kuwa seneta huyo ndiye anayefaa zaidi kumshinda Rais Ruto. Hata hivyo, amewahi kuwakashifu viongozi wa Mlima Kenya walioshiriki kumuondoa madarakani, akiwataja kuwa wasaliti.
Bw Sifuna hakutaja chama atakachoungana nacho wala kueleza namna mgombea mmoja wa upinzani atakavyochaguliwa. Alisema mazungumzo hayo bado hayajafika wakati wake.
“Subirini kwanza. Mazungumzo hayo yatafanyika baadaye sana,” aliwaambia wanahabari.
Wakili Nelson Osiemo alisema Bw Sifuna atalazimika kueleza jinsi uamuzi wake kuhusu Gachagua unavyoendana na misingi ya kisiasa anayotaka kuweka mbele katika vuguvugu lake jipya.
Bw Sifuna anasisitiza kuwa uwajibikaji na kuheshimu Katiba lazima viwe msingi wa uongozi. Alisema utendaji wa rais haupaswi kupimwa kwa miradi inayoonekana pekee, bali pia kwa namna serikali inavyofuata sheria.
Akizungumzia deni la taifa na matumizi ya fedha za umma, alisisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikishaji wa wananchi na ukopaji unaofuata sheria.
“Hauwezi kusema kwamba kwa sababu umejenga uwanja mzuri wa Talanta, basi tukupigie makofi. Hapana. Tunataka uwazi,” alisema.
Msimamo huo unajiri baada ya miezi kadhaa ya migogoro ndani ya ODM kuhusu ushirikiano wake na serikali jumuishi pamoja na mwelekeo wa chama hicho baada ya kifo cha Raila Odinga.
Bw Sifuna alisema alijaribu kupatanisha makundi hasimu lakini akahitimisha kuwa uongozi wa chama ulikuwa ukielekea upande ambao hangeweza kuutetea. Alikosoa ushirikiano wa ODM na UDA akisema unatishia uhuru wa chama, na pia akapinga mchakato wa kuondolewa kwake kama katibu mkuu.
Hata hivyo, alisema hana kinyongo na aliyekuwa wenzake na anaiachia hatima ya ODM kwa wapigakura.
Alisema timu yake pia inatayarisha sera za kupunguza matumizi mabaya ya fedha za serikali na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi. Katika elimu, anataka data sahihi za wanafunzi, shule na walimu ili kuimarisha usimamizi wa fedha, huku katika afya akipendekeza hospitali zilipwe madai halali kwa wakati na hatua zichukuliwe dhidi ya madai ya ulaghai.
Alisema manifesto ya vuguvugu hilo inaandaliwa kwa usaidizi wa wataalamu na itakaguliwa kabla ya kuchapishwa.
Bw Sifuna alisema ataruhusu wapigakura kuamua mustakabali wa ODM katika uchaguzi wa Agosti 11, 2027.
Sifuna afichua mikakati yake kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…