POLISI wamemkamata Kassim Abdi Sebo, anayeshukiwa kuongoza genge lililolaumiwa kutekeleza wizi kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi uliofanyika Homa Bay Agosti 16.
Abdi alikamatwa Alhamisi usiku pamoja na wanaume wengine saba wanaodaiwa kuwazuia maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kutekeleza majukumu yao.
Maafisa waliokuwa wamejihami na kufunika nyuso zao walimzingira Abdi katika kituo cha mabasi cha Homa Bay mjini.
Amekuwa akitoroka polisi tangu mahakama ya Homa Bay ilipotoa kibali cha kukamatwa kwake Agosti 14, baada ya maafisa kuandaa mashtaka kadhaa.
Ripoti ya OB inaonyesha mashtaka hayo yanahusu madai ya kushambulia mtu na kumjeruhi kinyume na Kifungu cha 251 cha Sheria ya Adhabu.
Kamanda wa DCI kaunti ya Homa Bay, Jimmy Kisobo, alisema Abdi anakabiliwa na mashtaka matatu huku uchunguzi ukiendelea na huenda yakaongezwa.
“Kuna kesi nyingine nyingi tunazochunguza kutokana na yaliyotokea. Tukipata ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuhusika kwa Abdi, tutamshtaki pia kwa makosa hayo. Kwa sasa, tayari tuna kesi tatu dhidi yake” alisema.
Kisobo alisema Abdi anahusishwa na visa vya vurugu vilivyoripotiwa katika kaunti hiyo kabla ya mkutano wa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.
Abdi analaumiwa kuhusika katika wizi wa kutumia nguvu baada ya kundi la vijana kudaiwa kuvamia Hoteli ya Tourist na kuiba mali.
“Kundi hilo hilo lilichoma mkahawa ulio Koduogo na kuwanyanyasa watu waliokuwa hapo wakipata chakula,” alisema Kisobo.
Alisema mshukiwa pia anatuhumiwa kuwatuma vijana wanaomuunga mkono kuchoma vibanda na kuharibu magari katika eneo hilo.
Watu kadhaa waliripotiwa kushambuliwa katika mkahawa huo.
Abdi alikamatwa Alhamisi usiku baada ya kukwepa majaribio kadhaa ya polisi ya kumtia mbaroni.
“Tulikuwa tukimtafuta na kwa bahati nzuri, jana usiku tulimpata mjini na kumkamata pamoja na wengine saba waliowazuia polisi kutekeleza majukumu yao kisheria,” alisema Kisobo.
Baada ya kukamatwa kwa Abdi, vijana wanaomuunga mkono walizua ghasia, kupora biashara mjini na kufunga barabara.
Vijana hao waliendelea na vitendo hivyo Ijumaa asubuhi.
“Ninawaomba wakome wanachofanya. Wanavunja sheria,” alisema Kisobo.
Kamanda huyo wa DCI alionya kuwa wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvunja sheria mjini watakamatwa..
Washukiwa saba waliokamatwa pamoja na Abdi ni Achiando Victor Odhiambo, 26; Isaac Masika Muliro, 30; Oyege Moses Geoffrey, 27; Geoffrey Njore, 25; Odhiambo Wesley Arnold, 26; Joseph Kobila, 28; na Alfred Nyagiro Aliwa, 26.
Anayeshukiwa kuongoza genge lililotibua mkutano wa Sifuna Homa Bay anyakwa

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…