MADAKTARI na wauguzi wanane waliomhudumia mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Kenya wameeleza wasiwasi wao kuhusu hatua ya kupelekwa karantini katika jengo lile lile la hospitali ya Nairobi Hospital ambako mgonjwa huyo alitibiwa na baadaye kufariki dunia.
Katika taarifa ya pamoja, wahudumu hao wa afya walisisitiza kuwa hawapingi maagizo ya karantini wala ufuatiliaji wa kiafya unaohitajika kufuatia kisa hicho. Hata hivyo, wanahoji utaratibu unaotumika kwa sasa wakisema hauzingatii viwango tofauti vya hatari ya maambukizi kwa watu waliohusika.
Kwa mujibu wao, kila mtu aliyewasiliana na mgonjwa huyo anaonekana kushughulikiwa kana kwamba alikuwa katika kiwango sawa cha hatari ya kuambukizwa virusi vya Ebola, jambo ambalo wanasema si sahihi kimatibabu.
“Tunaelewa uzito wa kisa hiki na tunakubali kushirikiana kikamilifu na hatua za kulinda afya ya umma. Hata hivyo, tunataka tathmini ya hatari ifanywe kulingana na kiwango halisi cha kila mtu,” walisema.
Wahudumu hao walifichua kuwa mwanzoni waliarifiwa kuwa wangekamilisha siku 21 za ufuatiliaji na kujitenga nyumbani chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Baadaye, hata hivyo, walipewa maagizo ya kuhamia katika jengo la East Wing la Hospitali ya Nairobi ili kuendelea na karantini yao.
Walisema jengo hilo ndilo lililotumika kumhudumia mgonjwa wa Ebola kabla ya kifo chake, jambo ambalo limezua maswali kuhusu usalama wao.
“Tungependa kujua kama eneo hilo limesafishwa kikamilifu na kuthibitishwa rasmi kuwa salama kwa matumizi. Pia tunataka kufahamu sababu za kitaalamu zilizosababisha eneo hilo lichaguliwe kuwa kituo cha karantini,” walieleza.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, mgonjwa huyo awali alitengwa katika chumba maalum ndani ya kitengo cha dharura kabla ya kuhamishwa kituo cha East Wing. Nairobi Hospital imesema kituo hicho kiko mbali na majengo mengine ya hospitali, kina lango lake maalum na wafanyakazi wake wa kujitegemea.
Hata hivyo, wahudumu hao wanasisitiza kuwa walimhudumia mgonjwa huyo wakiwa wamevaa vifaa vyote vya kujikinga vinavyopendekezwa katika visa vya Ebola. Aidha, hakuna aliyeripoti kuwa na hitilafu kwenye mavazi hayo ya kinga wala kuhusika katika mtagusano wa moja kwa moja usio na kinga.
Kwa msingi huo, wanataka tathmini ya kibinafsi ya hatari ifanywe kwa kila mhudumu badala ya kuwekewa viwango sawa na watu waliokuwa na mtagusano wa karibu na mgonjwa bila vifaa vya kujikinga.
Walinukuu miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inayotaka wahudumu wa afya wanaohusika katika matibabu ya wagonjwa wa Ebola kutathminiwa kulingana na kiwango halisi cha hatari ya kila mmoja. Miongozo hiyo inaeleza kuwa wahudumu waliokuwa na vifaa sahihi vya kujikinga hawapaswi kuchukuliwa sawa na watu waliokutana na mgonjwa bila kinga.
“Kuwa karibu na mgonjwa pekee si kipimo sahihi cha hatari. Kinachopaswa kuangaliwa ni aina ya mtagusano na matumizi ya vifaa vya kujikinga,” walisema.
Pia wamepinga uwezekano wa kuwekwa pamoja katika karantini na watu waliotangamana zaidi na mgonjwa huyo.
Kwa maoni yao, wahudumu waliotumia mavazi kamili ya kinga hawapaswi kushughulikiwa sawa na watu waliokuwa na mtagusano wa moja kwa moja bila ulinzi wa kutosha.
Iwapo karantini ya taasisi itaendelea kutumika, wanapendekeza watu watenganishwe kulingana na viwango vya hatari walivyokumbana navyo. Pia wanataka kila mhusika apewe chumba chake binafsi chenye choo, huduma bora za matibabu, chakula cha kutosha, maji safi na vifaa vingine muhimu.
Mbali na hilo, wahudumu hao wanataka usaidizi wa kisaikolojia na ufuatiliaji wa afya kazini kwa wote waliohusika katika kushughulikia mgonjwa huyo. Wanasema kazi yao iliwaweka katika mazingira hatari na hivyo wanapaswa kupewa fidia au marupurupu maalum ya mazingira hatari.
Katika barua ya ndani ya hospitali hiyo Oktoba 6, Mkurugenzi Mkuu Dkt Felix Osano alisema wafanyakazi waliotambuliwa kuwa walitangamana na mgonjwa huyo wawasiliane moja kwa moja ili kubaini kiwango cha hatari walichokuwa nacho.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), Dkt Davji Atellah, alisema wahudumu wa afya waliokuwa wamevaa vifaa vya kujikinga hawapaswi kuwekwa pamoja na watu waliotagusana moja kwa moja na mgonjwa bila kinga.
Alisisitiza kuwa madaktari na wauguzi waliokuwa mstari wa mbele katika kuokoa maisha ya mgonjwa huyo wanastahili kulindwa na kupewa mazingira salama wakati wa karantini.
Hata hivyo, Dkt Atellah alisema watu wanaotambuliwa kuwa katika hatari ya kuambukizwa Ebola wanapaswa kufuatiliwa kwa karibu ili kuzuia uwezekano wa kusambaza maambukizi kwa wengine.
Madaktari, wauguzi waliohudumia mgonjwa wa Ebola waeleza sababu ya kukataa karantini

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…