RAIS William Ruto ameeleza kutoridhishwa na utabiri wa hali ya hewa nchini, akizua mjadala kuhusu uwezo wa wataalamu kutabiri kwa usahihi wakati ambao mvua kubwa ya El Niño itaanza.
Akizungumza Alhamisi, Oktoba 8, katika kongamano la Kilimo na Utoshelevu wa Chakula katika uwanja wa Jamhuri, Nairobi, Rais alisema muda wa kuanza kwa mvua hiyo umekuwa ukibadilishwa mara kwa mara.
“Wale wanaohusika walituambia mvua itanyesha Agosti, lakini ikaahirishwa hadi Septemba, sasa ni Oktoba,” alisema.
Aliongeza: “Kusubiri mvua hii ni kama kubahatisha. Hujui itanyesha lini,” alisema. “Tunasubiri El Niño, lakini hatujui itafika lini.”
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Ruto kuhoji utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kenya (KMSA). Mnamo Oktoba 2023, alitilia shaka tahadhari kuhusu El Niño iliyokuwa ikitarajiwa kusababisha mafuriko makubwa.
Wakati huo, aliyekuwa Mkurugenzi wa KMSA, David Gikungu aliwaomba Wakenya radhi kwa mkanganyiko kuhusu utabiri, lakini akasisitiza umuhimu wa kujiandaa kwa mvua nyingi.
Mvua ilizofuata ilisababisha maafa makubwa. Kufikia Desemba 20, 2023, mafuriko ya mvua ya El Niño yalikuwa yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 174 na zaidi ya watu 500,000 kuhama makazi yao, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).
Kaunti 38 kati ya 47 ziliathiriwa na mafuriko baada ya mito kuvunja kingo, mafuriko ya ghafla na maporomoko ya ardhi. Maeneo yaliyoathirika zaidi yalijumuisha Mandera, Garissa, Tana River, Wajir, Isiolo na Meru.
Mtaalamu wa hali ya hewa, Fred Njehu wa Greenpeace Africa alisema utabiri wa kisayansi hutegemea hali na mifumo ya kihistoria, ambayo inaweza kubadilika kadri hali ya hewa inavyoendelea.
“Utabiri wa matukio makali ya hali ya hewa huwa si sahihi kwa asilimia 100,” alisema.
Alieleza kuwa utabiri wa mvua nyingi haumaanishi kila kaunti itakumbwa na mafuriko, wala kuchelewa kwa mvua hakumaanishi tahadhari iliyotolewa awali haina umuhimu.
Njehu alisema badala ya viongozi na wataalamu kubishana kuhusu nani aliye sahihi, wanapaswa kuangazia ushahidi wa kisayansi na hatua za kujiandaa.
Alisema taasisi za kisayansi zina wajibu wa kutoa ushauri kuhusu hatari za hali mbaya ya hewa, huku viongozi wa kisiasa wakitarajiwa kuhakikisha kuna fedha, sera na mipango ya kukabiliana na majanga.
Kaimu Mkurugenzi wa KMSA Edward Muriuki alisema El Niño hutokana na ongezeko la joto la maji ya bahari katika maeneo ya kati na mashariki mwa Bahari ya Pacific, jambo linaloweza kubadilisha mifumo ya hali ya hewa duniani.
Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limesema kuna uwezekano wa karibu asilimia 100 wa El Niño kuendelea hadi Februari 2027. Shirika hilo linaonya kuwa huenda ikawa mojawapo ya matukio makubwa zaidi tangu 1950.
Hata hivyo, athari zake hutofautiana kulingana na maeneo na mifumo mingine ya hali ya hewa.
Bw David Samoei wa Kituo cha Kitaifa cha Operesheni za Kukabiliana na Majanga alisema serikali sasa inalenga maandalizi ya msimu wa mvua ya Oktoba, Novemba na Desemba badala ya kubishana iwapo mafuriko yatatokea.
“Hatuzungumzi tena kuhusu iwapo kutakuwa na mafuriko. Tunachojadili ni hatua tunazopaswa kuchukua katika msimu wa Oktoba, Novemba na Desemba,” alisema.
Serikali imesema imeanzisha uratibu wa mashirika mbalimbali kutathmini hatari na kupanga hatua za kukabiliana na mafuriko. Pia, mazoezi ya kujaribu mifumo ya uokoaji yanafanywa ili kubaini mapungufu.
Wataalamu wanasema mamlaka ya hali ya hewa inapaswa kueleza mabadiliko ya utabiri kwa uwazi, huku serikali ikiwekeza katika wataalamu, teknolojia, ukusanyaji wa data na ufadhili wa kutosha.
Wanasema mawasiliano bora kati ya wataalamu, wanahabari na viongozi ni muhimu ili wananchi waelewe tahadhari na kuchukua hatua mapema.
El-Nino: Ruto akejeli na kutilia shaka utabiri wa hali ya hewa nchini

This story was originally published by Taifa Leo.
Read the full story at Taifa LeoRelated stories
NewsIcoT yatakiwa kuongeza wataalamu ujenzi
MOROGORO: Serikali imesema itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), ili kutayarisha wataalamu wengi wenye ujuzi na umahiri watakaoweza kujiajiri na kuajirika kikamilifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi, Aisha Amour amesema hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa mafundi sanifu na wataalamu wa kada mbalimbali…
NewsKampuni za Amerika zashinda zabuni kuchimba madini Kwale
MUUNGANO wa kampuni nne za Amerika umeshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji na uchakataji wa madini-adimu na niobium katika eneo la Mrima Hill, Kaunti ya Kwale, ambayo thamani yake inakadiriwa kuzidi Sh6 trilioni. Waziri wa Madini Hassan Joho alitangaza Frontier Minerals Consortium kuwa mshindi wa zabuni hiyo ya matrilioni ya fedha baada ya mchakato wa tathmini na ukaguzi wa ununuzi kukamilika. Ushindi huo unaipa Amerika nafasi muhimu katika sekta ya madini ya kimkakati nchini Kenya, huku ikiendelea kushindana na China kudhibiti upatikanaji na uchakataji wa madini hayo duniani. Kampuni zinazounda muungano wa ushirika huo ni Frontier Minerals LLC, Bunker Hill Mining Corp, ReElement Technologies na American Resources Corporation. Kila kampuni ina utaalamu wake katika uchimbaji, upatikanaji wa madini adimu, uchakataji na usafishaji wa madini muhimu kwa viwanda vya kisasa. Madini ya niobium katika Mrima Hill hutumika katika utengenezaji wa vifaa vya anga, huku madini-adimu yakihitajika katika magari ya umeme, vifaa vya kielektroniki, mitambo ya upepo, silaha za kisasa na teknolojia ya Akili-Unde. Kampuni ya ReElement Technologies tayari imevutia uwekezaji wa serikali ya Amerika wa Dola milioni 25 (takriban Sh3.2 bilioni) uliotangazwa mnamo Julai 2026 kusaidia uwekaji wa vifaa katika kiwanda chake cha kusafisha madini adimu katika jimbo la Indiana, Amerika. Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za Amerika kupunguza kutegemea China, ambayo inaongoza duniani katika uchakataji wa madini hayo. Kampuni saba ziliorodheshwa kushindania mradi huo mnamo Julai, zikiwemo kampuni mbili za China, miungano miwili ya kampuni kutoka Amerika, muungano wa Australia na ubia wa Kenya na Uingereza. Kampuni za China baadaye zilijiondoa. Joho alisema kushinda zabuni hakumaanishi kampuni hiyo inaweza kuanza uchimbaji mara moja. Inapaswa kwanza kupata leseni zinazohitajika, kutekeleza masharti ya kisheria na kushirikisha jamii ya eneo hilo. Serikali pia imesisitiza kuwa madini hayo hayapaswi kuuzwa yakiwa ghafi, bali yaongezwe thamani nchini kupitia viwanda vya uchakataji. Muungano huo umesema utajenga uwezo wa kuchakata madini nchini, hatua inayoweza kuunda nafasi za ajira na kuongeza mapato. Kwa Kenya, mradi huo unatoa fursa ya kupanua uchumi ambao kwa muda mrefu umetegemea kilimo na utalii. Mapato ya sekta ya madini yalipungua kutoka Sh35 bilioni mwaka 2022 hadi Sh20.3 bilioni mwaka jana, hasa kutokana na kufungwa kwa migodi ya madini ya titanium katika Kaunti ya Kwale. Hata hivyo, mafanikio ya mradi wa Mrima Hill yatategemea uwekezaji, masharti ya leseni na namna jamii zitakavyoshirikishwa na kunufaika.
News2027: ACF warns of emerging political violence, urges restraint
…Forum urges Tinubu, governors to ensure fairness to opposition By Ibrahim Hassan-Wuyo The Arewa Consultative Forum (ACF) has raised concerns over emerging signs of political violence ahead of the 2027 general elections, urging political leaders, security agencies and Nigerians to embrace restraint and protect democratic values. The forum warned that provocative demonstrations, stone-throwing, abusive chants […]
NewsUtatu haki jinai watakiwa kuimarisha ushirikiano
ARUSHA: Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za haki jinai, kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo ili kujenga imani ya wananchi kwa Serikali. Johari amesema hayo leo jijini Arusha…